Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, October 8, 2018

Watumishi 11 wa Benki wanaswa na TAKUKURU

adv1
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU), leo imewafikisha mahakamani, Mwasibu Mwandamizi Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Bw. Isaya Philipo na watumishi 11 wa Benki ya CRDB kwa kosa la kuisababishia serikali hasara ya shilingi milioni 569,325.

Akizungumza katika ofisi za TAKUKURU jijini Dar es Salaam, Naibu Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kinondoni, Bw. Eugenius Benard Hazinamwisho, amesema watuhumiwa hao wanakabiriwa na makosa 404 ya ubadhirifu na ufujaji wa mali za serikali na fedha za Mamlaka ya Elimu nchini.

Ameibainisha kuwa makosa hayo yapo chini ya kifungu kinachozuia na kupambana na rushwa No.11 cha mwaka 2007 cha sheria na kanuni ya adhabu sura ya 16.

“Watuhumiwa wote kutoka TEA, na CRDB, Wamefikishwa mahakamani kwa wizi wa fedha za Mamlaka ya Elimu, katika makosa waliyoyafanya kati ya mwaka 2010 na 2013'', amesema Hazinamwisho.

Amefafanua kuwa baada ya uchunguzi kukamilika, wamebaini fedha hizo zilielekezwa katika kusaidia elimu nchini katika uboreshaji wa mitaala na miundombinu ya elimu.” amesema Hazinamwisho.

Aidha Bw, Hazinamwisho amewataka watumishi wote wa serikali na taasisi binafsi za fedha nchini kuheshimu nyadhifa zao katika kutekeleza majukumu pamoja na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu kwa kutojihusisha na vitendo vya rushwa na makosa ya jinai.

Hazinamwisho ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi hiyo juu ya taarifa za vitendo vya rushwa nchini.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )