Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, October 1, 2018

Wazee Nchini Wataka Uwakilishi Bungeni Na Mabaraza Ya Madiwani

Na Ahmed Mahmoud Arusha
WAZEE wameiomba serikali kuhakikisha wanapata uwakilishi wa viti maalumu bungeni na mabaraza ya maidwani nchini ili kuweza kupaaza sauti zao sanjari na kutungiwa sheria kama yalivyo makundi mengine.

Akizungumza kwenye kilele cha siku ya wazee duniani Rais wa awamu ya pili Alhaji Ally Hassan Mwinyi amesema kuwa serikali ipo teyari na inaendelea kuhakikisha wazee wanapata huduma bora ikiwemo sheria hiyo.

Amewataka wazee hao kuwa na subira wakati mchakato wa kupata sheria ukiendelea sambamba na mapitio ya sheria hiyo kwani walipotoka na wanapoelekea na pazuri sana kuliko awali.

“Nawasihi sana muwe na subira wakati serikali ya awamu ya tano ikiendelea na mchakato huu wa wazee kupata sheria pamoja na suala la pensheni mliloomba kwenye risala yenu”alisema mwinyi.

Kwa upande wake waziri wa Afya wazee jinsia na watoto Ummy Mwalim alisema kuwa mchakato wa sheria umefikia mahali pazuri hivyo wanajipanga kuhakikisha mapitio ya sera ya wazee ya mwaka 2013 yanafanyiwa kazi kabla ya kuwa sheria.

Amesema kuwa masuala yote hayo yahitaji kufikiwa na kufanyiwa kazi na serikali ya wamu ya tano itahakikisha inaondoa kero zote wanazokumbana nazo wazee ikiwemo suala la matibabu.

“Nawasihi wazee wangu pindi mnapoenda kupata matibabu msiwahukumu wahudumu wa Afya wote bali msome jina la mhudumu huyo ili tuweze kudili nae na wataka wahudumu wote kuacha kutoa lugha zisizo na staha kwa wazee watakayefanya hivyo tutadili nae”alisema Ummy

Nae Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo alisema kuwa mkoa huo umejipanga kuhakikisha wazee wote zaidi wanapata huduma bora za afya na yeyote atakaye enda kinyume hatua mbali mbali za kisheria zitachukuliwa juu yake.

Amesema kuwa mkoa huo una jumla ya wazee zadi ya 90 elfu na kati yao 16 elfu wanapata huduma za afya na vitambulisho na mkoa umejipanga kuhakikisha wote wanafikiwa.
 
Mwisho……………………..
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )