Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, November 1, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 132 na 133 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
   
Mbele yangu kuna dada wa kizungu ameshika kioo kikubwa kiasi akijipamba nyusi zake, nikabahataika kupata upenyo mdogo wa kuangalia mtu aliye nyuma yangu, nikajikuta nikistuka baada ya kuona jamaa wawili wa kiarabu wenye ndevu nyingi wakiwa nao wamesimama kwenye hii foleni. Nikavuta kumbukumbu kwamba ni wapi nilipo waona jamaa hawa wawili. Kumbukumbu zangu zikaangukia katika kambi ya Al-Shabab, na mmoja kati ya hawa jamaa alikuwa ni mlinzi wa baba Hawa, sijafahamu ni wapi wanapo elekea ila mstari ambao nipo mimi sote tunapanda ndege moja, hapa ndipo nikaanza kupata wasiwasi mkubwa sana juu ya hawa jamaa kama hawapo hapa kwa ajili ya kutoroka basi wapo hapa kwa ajili yangu kwani mimi ndio muharibu mkubwa wa kambi yao.
           
ENDELEA   
Taratibu foleni ikazidi kusonge mbele, dada huyu wa kizungu akamaliza kujipamba uso wake na kurudisha kioo chake ndani ya pochi yake. Ikafika zamu yangu, nikakabidhi hati yangu ya kusafiria pamoja na begi langu, nikaliweka katika mkanda maalumu wa kukagulia mizigo.
“Karibu muheshimiwa”
Kijana huyu wa hapa uwanja wa ndege alizungumza huku akinikabidhi hati yangu ya kusafiria.
“Asante”
Nikachukua hati yangu ya kusafiria kisha, nikapiga hatua mbili mbele na kuchukua begi langu la mgongoni. Nikatembea kwa umakini hadi kwenye moja ya nguzo na kujibanza na kuwaangalia jamaa hawa. Nikawaona wakiwa wamesimama kwenye mlango maalumu wa kuelekea katika ndege. Kwa mauonekano wao hakuna hata mmoja ambaye ananifwatlia mimi. Taratibu nikaanza kupiga hatua hadi kwenye mlango wa ndege hii, nikajumuika na abiria wengine kuingia ndani.
 
“Karibu”   
Wafanyakazi wa shirika la hii ndege walitukaribisha kila abiria anaye ingia huku kila mmoja akionyesha tiketi yake. Nikaanza kutafuta herufi ya siti yangu ambayo na ‘J2’. Sikuchukua hata dakika moja nikawa nimefanikiwa kufika katika siti yangu, nikamkuta dada wa kizungu ambaye nilikuwa nimeongozana naye akiwa amesha kaa kwenye siti yake ambayo ni ‘J1”
“Mambo”
Dada huyu alinisalimia kwa lugha ya kingereza.
“Poa habari yako”
“Salama, ninaitwa Jane”
“Peter”
“Ahaa una jina kama la mdogo wangu wa mwisho”
“Yaaa tutakuwa tumefanana majina”
“Ninakwenda Nigeria wewe je?”
 
“Hata mimi pia ninakwenda Nigeria”
Nilizungumza huku nikiwatazama jamaa hawa wawili wakikaa kwenye siti zao ambazo zipo nyuma karibu na mlango wa kuelekea katika vyoo vilivyomo ndani ya hii ndege. Jane ni msichana mchangamfu sana kwani dakika kadhaa tangu nikae nae hapa amenizoea kwa haraka sana.
“Mimi ni dotka kutoka shirika la umoja wa mataifa, UN ninakwenda Nigeria kwenye semeni ya kidaktari wewe je?”
“Ahaa mimi ninakwenda kibiashara?”
“Labda biashara gani?”
Nikageuka nyuma na kuwaangalia jamaa hawa ambao hadi sasa hivi hawajanistulia kabisa. Jane na yeye akaangalia nyuma akitaka kuona nini ninacho kitazama mara kwa mara.
“Kuna tatizo?”
 
Jane aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.
“Hapana hakuna tatizo”   
“Unaonekana unawafwatilia sana wale jamaa, una wafahamu”
“Habari ndugu wasafiri karibuni katika ndege yetu. Tunakwenda kuianza safari dakika mbili mbeleni, tunawaomba muwezekufunga mikanda kwenye siti zetu tafahdali. Ninawatakia safari njema na Mungu atongoze”
Sauti ya kike ilisikika kupitia vipaza sauti vilivyomo humu ndani ya ndege, nikachukua  mkanda wa siti yangu na kujifunga vizuri kiuononi mwangu. Hata swali la Jane sikulikumbuka aliniuliza nini kwani akili yangu kwa sasa ipo juu ya hawa watu.
 
‘Lazima niawaue’
Nilizungumza kimoyo moyo kwani endapo nitawaacha hai watu hawa basi wanaweza kunigeukia mimi pale watakapo fahamu ukweli wote. Taratibu ndege ikaanza kuiacha ardhi huku abiria sote tukiwa kimya kila mmoja akimuomba Mungu wake kwa upande wake. Hadi ndege ilivyo tulia angani taartibu nikaanza kuona mtu mmoja baada ya mwengine akifungua mkanda wake.
“Huuu, hiili zoezi huwa silipendi sana”
Jane alizungumza huku akinitazama usoni mwangu
“Zoezi gani?”
“Zoezi la ndege kupaa au kutua, huwa ninapata mashaka sana na kuogopa”
“Hhaaha ila ni kawaida mbona”
“Yaa tangu nipo mtoto huwa sipendi ndege inavyo paa na kutua”
Nikatazama nyuma kidogo, nikamuona mmoja wa jamaa akifungua mkanda wake na kusimama. Nikamtazama Jane kisha nikajikoholesha taratibu.
 
“Ninakuja”
“Sawa”
Jane alizungumza huku akinitazama kwa macho ya mashaka kidogo, nikaanza kutembea katikati ya uwanzi ulio tengenisha siti hizi za pande mbele. Nikafika usawa wa siti aliuo kaa jamaa hawa, nikamtazama huyu mmoja kwa macho ya kuiba pasipo yeye kugundua lolote, nikaendelea kusonga mbele hadi kwenye vyoo vilivyomo humu ndani.
Nikausukuma mlango kwa nguvu na kuingia ndani, nikamkuta jamaa akiwa ameshika vipande vya bastola akiviunganisha, alipo niona akachomoa kisu mfukoni mwake, akajaribu kunirushia ngumi, ila nikaweza kumdhibiti kwa kumpiga kwa kutumia ubapande wa mkono wangu wa kulia ulio tua shingoni mwake na kumfanya awahi kulishika koo lake huku akijitahidi kupata pumzi. Nikampiga kabari moja nzito iliyo mfanya azidi kupoteza pumzi. 
 
Taratibu jamaa huyu akaanza kulainika na baada ya dakika moja, akawa ametebwereka kabisaa. Nikafungua moja ya mlango wa choo na kumkalisha kwenye choo cha kukaa kisha nikafunga choo hichi na kuweka kibao kidogo kilicho andikwa kwa maandishi ya rangi nyekundu ‘Choo kinafanyiwa matengenezo kwa muda’
Nikachukua begi ambalo lina silaha ambazo zinatakiwa kufungwa ili kukamilika, huku kuna mabomu sita ya machozi. Nikaiingiza bastola ndani ya begi aliyo kuwa ameanza kuifunga jamaa pamoja na kisu chake, kisha nikalifunga begi hili na kutoka katike eneo hili. Sikutaka kutoka na begi hili hadi walipo kaa abiria, nilicho kifanya ni kumuita muhudumu mmoja wa kike.
 
“Ndio kaka”
“Kwa jina ninaitwa Daniel, ninafanya kazi chini ya ofisi ya raisi wa Marekani bwana Donald Bush. Siku chache nyuma niliweza kuongoza oparesheni ya kuangamiza na kulifutilia mbali kundi la Al-Shabab na tulifanikiwa kuweza kumua mkuu wao. Sasa bado nipo kwenye oparesheni, na ndege yako leo hii ilitaka kwenda kutekwa na magaidi wachache walio salia, inavyo onyesha wanahitaji kulipiza kisasi kwa kile ambacho kimetokea siku chache zilizo pita”
 
Nikaanza kumuona dada huyu akianza kutetemeka mwili wake, naikamshika mkono na kumtuliza asitetemeke wala asizungumze neno lolote zaidi ya mimi nitakacho muambia.
“Ndani ya hii ndege yako kuna magaidi wawili wa Al-Shabab, mmoja nimedhibiti na mwingine bado yupo kwenye siti anasubiria mwenzake atoke ili waweze kufanya shambulizi, sasa ninacho hitaji kukuomba kwa sasa, wasiliana na rubani mkuuaombe kutua nchi yoyote kwa dharura ili kuwashusha hawa magaidi. Kumbuka hapa tunazungumzia roho za watu zaidi ya elfu mmoja tuliomo humu ndani ya hii ndege mukiwapa nafasi magaidi hawa, lolote linaweza kutokea sawa”
“Sawa”
“Na kama unahitaji udhibitisho wa kwamba kuna magaidi, silaha zao hizi hapa”
 
Nikafungua zipu ya begi kidogo na kumuonyesha dada huyu silaha zilizopo humu ndani, kwa haraka akachukua mkonga wa simu ya dharura uiliyopo kwenye moja ya ukuta humu ndani. Akameza mate kwa nguvu, ila kabla hajaminya batani yoyote, nikamshika mkono anao taka kuminya batani hizo.
“Ndani ya ndege hii hususani wafanyakazi wezako, kuna mmoja ni msaliti kwa maana silage hizi zimeingia hata kabla ya abiria kuingia na zimeweza kufichwa humu chooni, sasa unaweza kunieleza ni nani ambaye unaweza kumuhisi labda ana vijitabia hatarishi”
Dada huyu  akatingisha kichwa huku jasho likimwagika usoni mwake, nikamuachia mkono wake na kwa ishara nikamuomba ampigie rubani mkuu simu.
“Ndio mkuu, kuna tatizo”
“Kuna mtu anaitwa Daniel, anafanya akazi chini ya serikali ya Marekani, ameweza kukamata magaidi wawili weye silaha ndani ya hii ndege”
Dada huyu akanitazama kisha akautoa mkonga wa simu sikioni mwake na kunikabidhi mimi.
 
“Anahitaji kuzungumza na wewe”
Nikaupokea mkonga wa wasimu hii na kuuweka sikioni mwangu.
“Ndio rubabani?”
“Ni jambo gani ambalo unaweza kufanya hadi nikakuamini kwamba wewe ni mfanyakazi chini ya serikali ya Marekani na si gaidi?”
“Piga simu White House na uliza kwamba Dany ni nan? Hiyo ni moja mbili pasipo kukuvunjia heshima mkuu, hili ni tatizo linalo husu maelfu ya watu ndani ya ndege yako sasa ninakuomba kama utalizembea niwaachia magaidi hawa waanze kuua abiria mmoja baada ya mwengine na wewe utakuwa unafwata amri ya kila kitu watakacho kueleza na kumbuka kwamba hii lawama yote itakuwa juu yako, ninacho kuaomba, hakikisha kwamba unaomba kutua kwenye nchi yoyote tuwakabidhi hawa Magaidi kwenye vyombo vya usalama, ndege yoko ikaguliwe kisha safari hitaendelea na hii ni dharura”
 
Nilizungumza kwa msisitizo ambao nina amini kwamba umemfanya rubani wa hii ndege kunielewa.
“Nimekuelewa bwana Daniel”
“Nashukuru, gaidi mmoja bado yupo kwenye siti, nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kwamba ninamuwekea uangalizi”
“Sawa bwana Daniel ngoja niombe kutua chini kwa dharura”
“Sawa muheshimiwa rubani”
Nikakata simu kuurudisha mkonga wa simu kutoka sehemu nilipo utoa, nikamkabidhi begi muhudumu huyu.
“Hakikisha unalitafutia sehemu salama unaliweka”
 
“Sawa”
Nikaanza kutoka katika eneo hili huku nikijiweka sawa. Nikatazama watu walikaa kwenye siti za karibu na huyu gaidi, wengi wao wamelala. Nikapiga hatua za umakini na kukaa kwenye siti ya gaidi aliye kuwa ameondoka na kumfanya mwenzake kushangaa.
“Una nikumbuka?”
Nilimuuliza huku nikimtazama machoni gaidi huyu, msangao wake ukanipa nafasi ya kumpiga kisukusuku cha kustukiza kwenye pua yake na kumfanya aweweseke kwa maumivu makali. Taratibu nikampiga kabali iliyo mpelekea kutulia kimya, na zoezi hili hapakuwa na mtu yoyote wala aliye weza kushushudia hili tukio, nikamfunga mkanda gaidi huyu huku nikimuweka vizuri kwenye siti, kisha taratibu nikanyanyuka na kurudi kwenye siti yangu.
 
“Umechelewa?”
“Yaa kidogo tumbo langu linanisumbua sumbua”
“Ohoo pole, kwa nini usiombe msaada kwa wahudumu?”
“Hapana nipo vizuri kwa sasa”
“Kweli?”
“Yaa kweli”
Nilizungumza huku nikitabasamu. Jane akaka vizuri kwenye siti yake huku naye akionekana kuwa na furaha ila ana onekana ana jambo anahitaji kulizungumza.
“Una kitu unahitaji kuzungumza?”
“Ahaa…yaa ila naona kwa sasa sio muda sahihi”
“Kwa nini?”
“Ahaa unajua ile mtu unaamuona kwenye ndege tu alafu unakwenda kuzungumza hisia zako za moyo kwa haraka namna hii anaweza kukuona kwamba ni malaya”
Jane alizungumza kwa sauti ya chini kidogo.
 
“Inategemea lakini”
“Habari ndugu abiria, tunawaomba kufunga mikanda yenu iliyopo kwenye siti, na ndege yetu itatua katika kiwanja cha kimataifa cha Bole Addis Ababa nchini Ethiopia, tunawaomba radhi kwa usumbufu ulio jitokeza na asanteni”
Sauti ya rubani wa kiume ikasikika masikioni mwa kila mmoja, na kuwafanya watu wengine walio lala kustuka. Kila mmoja ambaye alifungua mkanda wake, taratibu akaanza kuufunga kiuonini mwake, akisubiria ndege hii kutua.
“Kuna nini kinacho endelea?”
Jane aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.
“Sifahamu kusema kweli”
“Inabidi waweze kutuarifu tujue kwamba kuna kitu gani ambacho kinaendelea, kwa maana hawawezi kusema kwamba wanatua Ethiopia wakati sio ratiba ya ndege hii”
“Naamini kuna tatizo ambalo wanahitaji kulilinda ili abiria wasichanganyikiewe ngoja tuone itakavyo kuwa”
 
“Taratibu ndege ikaanza jutua ardhini, kupitia kidoo cha dirisha pembeni ya Jane, tukaona kundi kubwa la askari wenye silaha wakiimarisha ulinzi ardhini hapa.
“Kuna tatizo”
Jane alizungumza huku akitazama askari hao.
“Unahisi kuna tatizo gani?”
Nilimuuliza Jane huku sote tukitazama nje ya uwanja huu wa ndege.
“Sijajua kwa kweli”
Taratibu ndege ikaanza kusimama, gari za polisi zinavyo washa ving’ora vyao tukaona jinsi vinavyo izunguka ndege hii. Mlango ukafunguliwa kwa haraka wanajeshi wenye bunduki wakaingia ndani ya ndege hii huku wakiwa na silaha mikononi mwao. Muhudumu ambaye nilimkabidhi begi lenye silaha, akawaongoza wanajeshi hawa hadi kwenye siti ya gaidi ambaye sasa hivi ndio anastuka, kwani sikumuua zaidi ya kumzimisha tu. Wanajeshi hawa wakamtoa gaidi mwengine ambaye alikuwa chooni huku wakimbeba.
 
“Mr Dany tunakuomba uongozane nasi”
Mwanajeshi mmoja alizungumza na kumfanya Jane kunikazia macho, nikamkonyeza huku nikifungua mkanda wa siti yangu niliyo kalia. Nikashuka kwenye ndege nikiw ana muhudumu huyu wa kike pamoja na askari wengine.
“Munatupelekea wapi afisi?”
“Tunahitaji kuwahoji maswali mawali matatu kisha mutaendelea na safari yenu”
“Sawa”
Nikiwa hapa uwanjani nikaona ndege nyingine ikitua huku ulinzi ukiendelea kuimarisha walinzi mkali. Nikaona gari sita za kifahari zikiisogelea gari hiyo huku zikiwa na bendera ya Ethiopia pamoja na Tanz.
“Kuna kiongozi gani anaye kuja?”
“Ni raisi wa Tanza K2, ana Ziara ya siku mbili hapa nchini Somalia”
Mwanajeshi huyu aliniambia, nikajukuta nikikaza macho yangu kwenye mlango wa kushukia abiria, nikaona walinzi wakianza kutangulia kushuka kisha akaanza kushuka K2 huku akiwa na furaha sana na akipunga mikono kwa wenyeji wake wlaio fika kumpokea katika hili eneo jambo lililo nitamanisha kwenda kumvamia na kumuua ili mradi nilipize kisasi kwa kila kitu kibaya alicho nifanyia katika maisha yangu.
                                                                                    
AISIIIII……….U KILL ME 133
   
“Dany......Dany”       
“Ndio afande”
 
Niliitika huku nikistuka kwani kwa sekunde kadhaa nilitingwa na mawazo mengi kichwani mwangu nikimfikiria K2.
“Ilikuwaje hadi ukafahamu kwamba watu hawa ni magaidi?”
“Niliwafwatilia nyendo zao tangu walivyo kuwa wamepanga foleni na nina ustadi mkubwa wa kuweza kumsoma mtu”
“Wewe labda ni nani?”
“Afande nimefanya kazi niliyoifanya, kikubwa wahojini hao magaidi nina imani wataweza kuwaeleza mengi na lengo la kuiteka ndege ilikuwa ni nini”
Nilizungumza kwa ujasiri huku nikimtazama afande huyu. Akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha akatingisha kichwa na kukubaliana nami kwa kile ambacho nimekizungumza.
“Ninaweza kwenda?”
“Ndio unaweza kwenda”
Nikaondoka katika eneo hili huku nikitazama gari za kifahari jinsi zinavyo ondoka katika eno hili. Nikaanza kupandisha kwenye ngazi za hii ndege na kurudi kwenye siti yangu niluyo kuwa nimekaa.
“Unaittwa Dany?”
Jane aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.
“Yaaa ni jina langu pia?”   
“Kwa nini uliniambia kwamba unaitwa Peter?”
“Naamini kila binadamu ana majina mawaili mawili si ndio?”
“Yaaa”
 
“Ok ukipenda unaweza kuniita Peter au Dany”
“Basi nitakuita Peter”
“Sawa”
Hatukuchukua muda mwingi katika uwanja huu wa ndege safari ya kueleka Nigeria ikaanza huku abiria wezangu kwa mara kadhaa walikuwa wakinitazama. Kadri muda ulivyo zidi kwenda ndivyo jinsi mazoea kati yangu na Jane yalivyo zidi kupamba moto. Kitu kikubwa ambacho ninajitahidi kukizuia katika mwili wangu ni hisia za mapenzi.
Baada ya masaa kadhaa tukafanikiwa kufika katika uwanja ndega wa Murtala Muhammed International(MMIA) Lagos nchini Nigeria, majira ya asubuhi.
“Una uwenyeji hapa Nigeria?”
Nilimuuliza Jane baada ya kutoka ndani ya uwanja huu wa ndege.
 
“Yaa nimesha wahi kufika, ila nimekuja kuchuliwa na shirika la kidaktari, kwa hiyo Mungu akibariki tunaweza kuonana”
“Sawa Jane”
Tukapena mikono na Jane kisha akaelekea kwenye gari aina ya Range Rover Sport na akaondoka eneo hili. Nikaanza kutazama eneo hili la uwanja, akanifwata kijana mmoja aliye valia kikoti maalumu lilicho andikwa dereva taksi.
“Unahitaji usafiri kaka?”
Nikamtazama kwa sekunde kadhaa kwenye macho yake, kisha nikatingisha kichwa na kumuambia ninahitaji. Tukaongozana na kuingia kwenye taksi yake aliyo isimamisha eneo maalumu ambalo kuna madera wengine ambao nao wamevalia sare za kufanana.
“Unaweza kunipeleka kwenye nyumba ya wageni ya bei raisi kabisa”
“Ndio ninaweza kukupeleka kuna nyumba nyingi za kawaida za kulala wageni”
“Napenda ambayo ipo katika mitaa mitaa ya watu wa maisha ya chini”
“Usijali kwa hilo kaka”
Safari ikazidi kusonga mbele, tukafanikiwa kufika katika mitaa iliyo jaa watu wa maisha ya chini, dereva akasimamisha gari mbele ya moja ya nyumba iliyo chakaa kiasi 
 
“Hii nyumba naamini itakufaa”
“Yaa tunaweza kushuka kwenda kuangalia”
“Yaa twende tu”
Tukashuka kwenye gari na kuingia katika nyumba hii ya kulala wageni, japo ninahitaji kuishi katika maisha ya kawaida sana ila hii nyumba ya kulala wageni inatisha, si kwa majengo yake tu ila ni kwa uchafu ambao unafanyika humu ndani. Watu wanafanya mapenzi kwenye kordo tea hii asubuhi ambayo watu wanatakiwa kuwa katika majukumu ya kufanya kazi.
“Kaka huna sehemu nyingine ambayo unaweza kunipeleka?”
“Si umehitaji sehemu ambayo ni ya bei rahisi, hii ndio ya bei rahisi”
“Hapana, ninakuomba tuondoke hili eneo, nipeleke katika hoteli nyi……”
Dada mmoja aliye shika ukuta huku mwanaume akiwa nyuma yake , akajaribu kunishika mkono wangu huku akiwa ameyalegeza macho, kwa haraka nikajikuta nikiiukwepesha mkono wangu kwa haraka huku nikiwa nimeikunja sura yangu.
“Tuondoke”
Nilizungumza huku nikitangulia kutoka nje huku nikiwa nimechoka kwa haya niliyo yaona humu ndani.
“Nipeleke hoteli yoyote ambayo ni kubwa sawa”
“Sawa bosi”
 
Safari ya kutafuta hoteli nzuri ikaanza, tukafanikiwa kupata hoteli iliyo tulia. Nikashuka kwenye gari, nikatoa noti ya dola mia na kumkabidhi dereva huyu.
“Nisubiri hapa nina baadhi ya mizunguko leo mjini”
“Sawa bosi”
Dereva huyu alizungumza kwa furaha, kwani ninaamini kwamba nimemlipa ujira ambao ni mkubwa sana kuliko hata pesa ambayo alitarajia mimi kumlipa. Nikaingia ndani na kusimama sehemu ya mapokezi .
“Habari dada?”   
“Salama tu za kwako?”
“Salama, ninahitaji kupata chumba”
Dada huyu akaanza kunitajia aina ya vyumba pamoja na bei zake. Nikalipia chumba cha bei ya kawaida kwa siku mbili, nikakabidhiwa funguo na  kuelekea chumbani kwangu, nikakichunguza chumba kizama kwa umakini sana nilipo hakikisha kwamba kina usalama wa kutosha, nikatoka kwenye chumba hichi huku nikiacha begi langu la nguo. Nikatoka na kuingia kwenye taksi, nikamuomba dereva anipeleke kwenye maduka ya simu.
Tukafika kwenye maduka ya simu, nikashuka kwenye gari, nikaingia kwenye moja ya duka simu, nikaanza kutafuta simu gani ni nzuri ambayo nitaweza kuitumia katika kazi yangu iliyo nileta hapa nchini Nigeria.
 
Nikanunua simu mbili, moja ikiwa ni iphone 6 huku nyingine ikiwa ni samsung note 4. Nikawaomba wanielekeze ni wapi ninapo weza kupata line za mitandao ya simu inayo tumika hapa hapa Nigeria, kwa bahati nzuri ndani ya duka hili kuna wakala wa moja ya mtandano. Nikampatia hati yangu ya kusafiria, akatoa nakala kisha akanirudishia.
“Itachukua muda gani dada?”
“Kama dakika tano hivi hadi kusajiliwa”
“Sawa”
Nikasubiri kwa dakika hizi tano wakawa wamemaliza kunihudumia. Niaweka salio la kutosha kisha nikatoka ndani ya duka hili. Nikaingia ndani ya gari na kumpigia simu meja.
“Ni mimi”
“Habari yako Dany?”
“Salama, nimefanikiwa kufika salama”
“Sawa hii ndio namba ambayo utakuwa unaitumia?”
“Ndio”
“Basi hakikisha unanunua kava ambazo zinazuia mawasiliano yako kunaswa na watu wa simu”
“Nitazipatia wapi meja”
“Uliza kwa hao wauzaji”
“Ngoja nijaribu”
“Sawa nitasubiria siku yako baada ya kuweza kupata hilo kava”
 
Nikashuka kwenye taksi na kurudi tena dukani, nikamfwata muhudumu aliye niuzia simu. Nikamtazama usoni kwa sekunde kadhaa.
“Samahani kwa usumbufu”
“Bila samahani”
“Kunakava fulani ambalo ukivalisha kwenye simu, basi mawasiliano unayo piga au kupigiwa yanakuwa salama je ninaweza kulipata”
Muhudumu huyu akanikazia macho huku akionekana anajiuliza maswali mengi sana kichwani mwake. Nikatoa noti ya dola mia na kumuwekea mezani kwake.
“Je ninaweza kulipata?”   
“Kwa nini unalihitaji, kwa maana kwa sheria ya hapa kuuza makava kama hayo unaweza kustakiwa na kupokonywa hata leseni ya usajili wa duka?”
“Ahaa mke wangu unajua ana wivu sana, sasa sihitaji afahamu nipo wapi?”
“Mke ndio anafanya ununue kava la simu yako kuto kunaswa na mawasiliano?”
 
“Yaaa, nisaidie kama unahitaji pesa nitakuongezea”
Kijana huyu akaka kimya akionekana kujishauri kichwani mwake, nikatoa noti ya dola mia nyingine na kumuwekea mezani. Akazichukua kwa pamoja na kuziingiza mfukoni mwake.
“Hembu simu yako?”
Nikatoa simu ya iphone 6, akaitazama kisha akaniomba nimsubiri. Nikaka eneo hilo kwa dakika kadhaa, baada ya muda akarudi akiwa kava hilo mikononi mwake.
“Ninakuomba uwe makini sana”
“Usijali, ila una uhakika wa kwamba hili ni kava halisi?”
“Ndio”
Nikalivisha kava hili kwenye simu yangu, kisha nikatoa dukani humu.
“Tunaelekea wapi bosi?”
“Turudi hotelini”
“Sawa”
Safari ya kurudi hotelini ikaanza, njia mzima nipo kimya huku nikifikiria ni kitu gani ambacho ninaweza kukifanya ili kazi yangu iende sawa. Tukafika hotelini, nikamlipa huyu dereva dola mia, kisha nikachukua namba yake na simu.
 
“Nitakupigia nikikuhitaji”
“Sawa bosi”
Moja kwa moja nikaingia chumbani kwangu, nikafunga mlango kwa ndani. Nikatoa simu na kumpigia meja.
“Mawasiliano kwa sasa yapo salama meja”
“Sawa hata mimi ninaona kwenye mtambo wangu hapa”
“Nahitaji kuzungumza na raisi”
“Sawa subiri kidogo niweze kumpigia, usikate simu”
“Sawa”
Nilizungumza huku nikiwa nimesimama pembeni ya dirisha langu nikitazama magorofa mengine yaliyopo karibu na hili gorofa.
“Dany unaweza kuzungumza sasa raisi yupo hewani”
“Muheshimiwa raisi habari yako?”
“Salama tu Dany nimeambiwa na meja kwamba umefika salama”
“Ndio muheshimiwa raisi nimefika salama, vipi mke wangu amefanikiwa kufika salama?”
 
“Ndio amefanikiwa kufika, na unaweza kuzungumza naye ndani ya muda mchache pale utakapo hitaji”
“Sawa nitashukuru sana muheshimiwa raisi. Ila muheshimiwa raisi kuna tukio liliweza kujitikeza njiani nilipo kuwa kwenye ndege”
“Jambo gani?”
“Kuna magaidi wawili wa Al-Shabab walihitaji kuiteka ndege ila niliweza kufanikiwa kuwadhibiti”
“Safi sana, ndio magaidi walio shushwa nchini Ethiopia?”
“Ndio hao muheshimiwa raisi”
“Nashukuru sana kwa kuweza kuwaokoa maelefu ya watu waliokuwa ndani ya hiyo ndege”
“Ni jukumu langu muheshimiwa raisi”
“Tena mke wako huyu hapa amesha fika ofisini kwangu unaweza kuzungumza naye”
“Dany”
Sauti ya Hawa ikanisisimua mwili mzima, moyo wangu ukajikuta ukijawa na furaha kubwa sana.
 
“Naa mke wangu”
“Umefika salama?”
“Ndio nimefanikiwa kufika, nahitaji kuanza kuianza kazi iliyo niletea huku”
“Kuwa makini mume wangu, na ninakuomba uweze kurudi salama”
“Usijali nitakurudi salama. Vipi unapata uangalizi mzuri katika hilo eneo?”
“Ndio tena raisi ameagiza watu wake, wananihudumia vizuri sana”
“Nafurahi kusikia hivyo mke wangu”
“Ninakupenda sana mume wangu, wewe ndio mwanaume wa maisha yangu”
“Hata wewe ndio mwanamke wa maisha yangu, nitakulinda kadri niwezavyo na nitahakikisha kwamba unajisifu kuwa na mwanaume kama mimi”
“Shukrani sana Dany wangu”
“Ok naomba umpatie simu muheshimiwa raisi”
“Sawa”
“Ndio Dany”
“Muheshimiwa raisi, ninahitaji kuianza kazi sasa”
“Mungu akutangulie katika hili”
 
“Shukrani sana”
Nikakata simu na kushusha pumzi taratibu, nikachukua rimoti na kuwasha tv, nikajitupa kitandani huku nikipangilia mipango ya jinsi gani ninaweza kumpata Yemi Okocha. Tangazo katika Tv hii likanifanya ninyanyuke kitandani na kukaa kitako. Yemi Okocha siku ya leo ana tamasha la kuchagua vijana wanao hitaji kujiunga kwenye maswala ya mavazi. Nikaandika eneo katika husika katika simu yangu kisha nikampigia dereva taksi, akaniahidi ndani ya dakika kumi atafika katika eneo hili. Nikasimama mbele ya kioo cha kabati kubwa lililopo hapa. Nikajitazama vizuri kuanzia chini hadi juu, nilipo ona nina vigezo kadhaa vya kuwa mwana mitindo nikashusha pumzi huku huku nikiwa nimejawa na furaha. Baada ya dakika kazaa simu yangu ikaita, nikaipokea.
“Bosi nimefika”
“Ninakuja”
Nikatoka chumbani kwangu na kufunga vizuri, nikashuka gorofani, nikaingia  kwenye gari nikamtajia jina la eneo ambalo ninahitaji kwenda.
 
“Tutachukua muda gani kufika”
“Hapo tutatumia dakika ishirini hadi kufika”
Ndani ya muda alio niambia dereva tukawa tumefika katika hoteli moja kubwa, nikakuta mlolongo wa vijana wakike na wakiume wakiwa wamepanga mistari kwa ajili ya kwenda kujisajili katika mashindano haya ya kutafuta wana mitindo, na mimi nikapanga mstari nikiwa ni mshirikia wa elfu moja na mia mbili. Muda ukazidi kwenda na foleni ikazidi kosogea, vijana walipo katika eneo hili wapo wengi wamependa, nikajitazama mweyewe nilivyo vaa na kimoyo moyo nikajishauri na kujiambia kwamba nina vigezo vya kuweza kushinda katika shindano hili.

==>>ITAENDELEA KESHO
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )