Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, November 3, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 136 na 137 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
  “Meneja?”   
Yemi Okocha alizungumza huku akimtazama meneja kwa macho ya mshangao. Kwnai hili lililo tokea hapa ni jambo lililo tushangaza sisi sote. Kwa haraka meneja akamkaba Yemi Okocha kabali kwa nyuma huku akitoa kisu kidogo mfukoni mwake na kumuwekea Yemi Okocha shingoni mwake.
“Mtu yoyote akinisogelea nitamuua jaji wenu”
Meneja alizungumza kwa msisitizo, walinzi wa Yemi wakabaki wakiwa ameduwaa tu wasijue ni nini cha kufanya kwa kitisho walicho patiwa na meneja huyu ambaye hadi sasa hivi tatujui lengo lake ni nini haswa.
   
ENDELEA           
“Unahitaji nini kutoka kwetu?”
Nilimuuliza meneja wa hii hoteli, akabaki akiwa ameduwaa duwaa huku akikaza kumkaba Yemi Okocha ambaye naye anaonekana kuto kujiweza kabisa katika swala la kupambana.
“Hilo halikuhusu”
Meneja alizungumza huku akianza kurudi nyuma nyuma kuelekea mlangoni huku akiwa amemshika Yemi Okocha. Nikataka kupiga hatu ili nimfwate Yemi ila akatishia kumkita kisu  cha shingo, ikanilazimu kusimama tu. Meneja akafungua mlango na kutoka chumbani huku, ikanibidi na mimi kutoka kwa haraka, nikamkuta meneja akiminya kitufe cha kufungulia lifti. Ilipo funguka, akamsukuma Yemi Okocha na yeye akaingia ndani na lifti ikajifunga. Kwa haraka nikamkimbilia Yemi chini alipo anguka. 
 
“Vipi umeumia?”
“Hapana”
Yemi alizungumza huku akikohoa kohoa. Nikamkanyanyua taratibu, nikatazama mshale ulipo juu ya mlango wa hii lifti unaonyesha kwamba lifti hii inaelekea juu gorofani.
“Muangalieni jaji mimi ninakuja”
Nilizungumza huku nikimuachia Yemi, nikaminya kitufe cha lifti nyingine.
“Calx naomba simu yako na ingia chumbani utaona simu yangu kitandani hapo tumia hiyo kunipigia na kuniambia kwamba lifti imesimama gorofa ya ngapi”
“Sawa Peter”
“Wapigieni simu polisi”
Nikaingia kwenye lifti na ikajifunga huku nikiwa nimeishika simu ya Yemi Calx. Nikaminya batani ya gorofa ya ishirini ambayo ndio ya mwisho kabisa ili hata kama hapo katikati kutakuwa na mabadiliko yoyote ninaweza kuminya batani ya gorofa husika na itasimama. Simu ikaita, nikaipokea kwa haraka na kuiweka sikioni.
 
“Peter amepanda hadi gorofa namba kumi na tisa”
“Poa”
Nikaminya batani ya gora namba kumi na tisa, sikumaliza hata dakika moja nikawa nimefanikiwa kufika, lifti ikafunguka na kutoka, kwenye kordo hii kumetulia sana, na hakuna mtu yoyote ambaye aliyopo kwenye hii kordo na vyumba vyote vimefungwa. Nikasikia vishindo vya miguu vikipandisha kwenye ngazi za kueleka gorofa inayo fwata. Nikaanza kuzipandisha ngazi hizi kwa kasi sana nikamuona meneja akijitahidi kupandisha ngazi hizi kwa kasi sana. Nikazidisha mwendo wa kupandisha ngazi hizi huku nikijitahidi kulikaza taulo langu mara kwa mara ili lisianguka. Meneja akazidi kukimbilia gorofa ya juu zaidi na akatokea juu kabisa ya gorofa. Meneja hakutaka kusimama zaidi ya kuzidi kukimbia kuelekea kwenye ukingo wa hili gorofa. 
 
“Meneja meneja”   
Nilimuita huku nikimkimbiza, akafika ukingoni mwa gorofa akasimama huku akinitazama. Kwa haraka nikaingia upande wa kurekodi video na kuanza kurekido tukio hili kwani sihitaji kuingia kwenye matatizo na serikali ya nchi hii.
“Niaembie meneja una tatizo gani meneja. Tafadhali simama hili swala tutalimaliza kiume hakuna chombo cha sheria ambacho kitakachoingilia”
Meneja huyu akabaki akitabasamu tu, akarudi hatua moja nyuma, na kumebaki usawa mdogo ambao akicheza vibaya basi anaanguka chini.
“Hujui unadili na watu wa aina gani”   
Meneja alizungumza kisha akajirusha kwenye hili gorofa nikakimbia kwa haraka hadi kwenye ukingo wa hili gorofa huku simu ya Calx ikiendelea kurekodi matukio haya, nikatazama chini na kumkuta meneja ndio akiangukia juu ya gari lililo simamishwa pembeni ya hii hoteli. Nikamvuta kwa karibu kutumia kamera ya hii simu, nikaona kichwa chake kilivyo pasuka kwa nyuma.
“Shitiii.”
 
Nilizungumza kwa hasira huku  nikikatisha kamera hii kuendelea kurekodi tukio hili. Nikawaona watu wakikusanyika katika gari hili, taratibu nikaanza kurudi ndani ya hili gorofa huku nikiwa nimekasirika sana. Nikarudi katika gorofani namba mbili kilipo chumba changu. Nikawakuta Yemi Okocha akiwa na baadhi ya maofisa wa polisi.
“Peter ni kitu gani kilicho tokea”
Nikamkabidhi Yemi simu huku nikimuwekea video niliyo irekodi. Yemi akaitazama, sura yake ikaonekana kujikunja kidogo, video ilipo isha akawakabidhi polisi mmoja ambaye naye pia aliitazama na kuwapatia wezake wawili.
“Yupo wapi Moses?”   
“Amesha chukuliwa na polisi anapelekwa kituoni”
“Calx na wezake?”
“Wapo katika chumba kingine, pamoja na walinzi wangu”
“Sawa sawa”
“Peter vaa nguo tuondoke katika hii hoteli tuelekee eneo salama”
“Peke yangu?”
“Tunaenda mimi na wewe, kesho washiriki wengine watakuja tutakapo kuwa”
 
“Sawa, ila kuna simu yangu kwa Calx ningeomba niweze kuichukua”
“Hii hapa ameniachia”
Yemi Okocha alizungumza huku akiitoa simu yangu mfukoni. Nikachukua suruali yangu na kuingia bafuni, nikavaa. Nikaitoa simu yangu nyingine mfukoni na kukuta ipo katika usalama mzuri. Nikamaliza kuvaa nguo zangu kisha nikatoka bafuni. Nikamalizia kuvaa viatu na tisheti yangu, nikamfwata Yemi sehemu alipo simama.
“Tayari jaji mkuu”
“Sawa twende zetu”
Tukawaacha polisi wawili humu ndani na kuongozana na polisi mmoja ambaye ndio alite kabidhiwa simu na Yemi. Tukashuka chini kabisa kwa kutumia lifti, tukatokea eneo la maegesho ya magari yaliyopo chini ya ardhi.
“Jaji walinzi wako wapo wapi?”
“Watawalinda washiriki wengine na sisi tunaelekea sehemu salama na huyu askari atatulinda”
“Tunaweza kuzungumza jaji mkuu”
“Ndio”
Tukasogea pembeni na kumuacha askari huyu akielekea kwenye gari la Yemi ambalo ni lina milango sita kama analo tumia raisi wa Marekani na baadhi ya matajiri wakubwa duniani.
 
“Kama nitakuwa ninakuvunjia heshima katika hili ninalo kwenda kulizungumza, ninakuomba unisamehe sana jaji mkuu”
“Zungumza tu Peter”
“Mimi ninaomba niweze kujivua katika haya maswala ya uwana mitindo”
Nilizungumza kwa ajili ya kumpima Yemi Okocha akili yake, japo ni jambo la hatari ambalo linaweza kuhatarisha ukaribu wangu naye ila inanibidi kufanya hivi ili hata kama ana maswali kadhaa ya kunihisi vibaya kichwani mwake, basi asipate majibu ya haraka haraka.
“Peter hicho kitu kwa sasa siwezi kukikubali kabisa, si kwajili ya hii kazi ila ni kwa ajili ya usalama wangu mimi mwenyewe”
“Kivipi jaji?”
“Peter, nimewaacha walinzi wangu kwa maana ninaona wanakula mishahara ya bure pasipo kufanya kazi ya aina yoyote. Wewe nimekujua leo ila umeonekana kujali usalama wangu kuliko wao, kwa hiyo nipo radhi kukulipa kiasi chochote cha pesa na uwe mlinzi wangu binafsi na nitakutaka wewe mwenyewe na sinto hitaji mlinzi mwengine binafsi”
 
Yemi alizuzungumza kwa msisitizo huku akinitazama usoni mwangu. Kimoyo moyo nikaanza kufurahia kwani mpango wangu unazidi kwenda vizuri.
“Ni bora wewe kunilinda kuliko kuacha kabisa maswala ya uwana mitindo”
“Hilo swala la kukulinda jaji mkuu mimi sina elimu nayo?”
“Hiyo hiyo ndogo uliyo kuwa nayo ndio ninayo ihitaji saawa Peter”
“Ninaomba unipe muda nifikirie”
“Sawa ila kwa sasa nitahitaji tuendelee nah ii safari”
Tukaingia kwenye gari na polisi huyu akawa na kazi ya kutuendesha. Yemi Okocha akachukua chupa ya pombe kali iliyomo ndani ya hili gari, akamimina kiasi kwenye glasi moja, akainywa yote kwa kasi huku akikunja sura yake na inaonyesha kwamba pombe hiyo ina kereketa sana kooni.
“Peter unatumia hii?”
“Hapana jaji huwa situmii kilevi”
“Kwel?”
“Yaaa”
“Hiyo itakuwa ni vizuri sana kwani walinzi wangu wale, ukiwapa pombe wanakunywa sasa kwa mfano kama leo kwa kile kililo jitokea, wamebaki wakiwa wamenitumbulia macho tu”
 
“Kwani walikuwa wamekunywa?”
“Wala sifahamu, ila wamezubaa kusema kweli.”
Sikutaka kuzungumza chochote kuepuka kuonekana kwamba imi ni mroho sana wa hiyo kazi. Tukatumia lisaa zima njani na tukafanikiwa kufika katika hoteli moja kubwa ambayo ipo pembezoni mwa bahari. Tukaagana na askari huyu na kuingia ndani ya hii hoteli.
“Mume wangu yupo humu”
“Umeolewa?”
“Yaa nimeolewa, na nina mtoto mmoja sema ninapenda kujiweka katika hali ya mazoezi ndio maana ukioniona huwezi kuamini kama nina mtoto”
Maeno ya Yemi yakanifanya nishushe macho yangu chini hadi kwenye mkono wake wa kushoto na kweli nikaona amevaa pete ya ndoa.
“Hongera kwakweli”
Nilizungumza huku nikitabasamu. Tukaingia kwenye lifti na taratibu tukaanza kuelekea juu.
 
“Peter kusema kweli wewe una roho ngumu”
“Kwa nini jaji?”
“Nimeshangaa kuona ulivyo mkata paja yule Moses, nilihisi kwamba unaweza kutania.
“Hahaaa unajua laiti nisinge fanya vile, mungenikuta na mimi ni maiti mule ndani”
“Kweli, ila natambua ni hasira uliyo kuwa nayo dhidi yake”
“Ndio”
Lifti ikafunguka katika gorofa namba tano, mlango ukafunguka na kuanza kufunguka. Tukafika kwenye moja ya chumba, Yemi akatoa kadi ya kufungulia mlango na akanikabidhi.
“Chumba chako ni hichi hapa, changu ni hichi hapa nina kadi yangu maalumu ambayo inafungua kila mlango wa hii hoteli”
“Ina maana hii hoteli ni mali yako?”
“Yaa hii ni hoteli ya mume wangu, chumba hicho hapo wanalala walinzi wangu na hichi ninalala mimi na mume wangu pale tunapo kuwa humu ndani”
 
“Sawa jaji mkuu nikutakie usiku mwema”
“Nawe pia Peter, ila zingatia kwa kile nilicho kueleza, naamini asubuhi utakuwa umenipatia jibu sahihi”
“Sawa jaji”
Nikafungua mlango huu na kuingia ndani na kuufunga kwa ndani. Nikawasha taa, chumba nilicho ingia ni kizui mara kumi ya chumba nilicho kuwa katika ile hoteli niliyo vamiwa. Uzuri wa chumba hichi, ni kikubwa sana, na kina huduma zote za nyumba ya wastani. Kuna sehemu ya jiko la kupikia, seble ndogo, choo chenye bafu ndani. Kitanda kimetengenezwa kwa muundo wa tairi kubwa. Nikakikalia kitanda hichi huku nikikiminya minya.
Nilipo hakikisha kwamba nimekagua chumba hichi vizuri, nikanyanyuka na kuelekea jikoni, nikafungua friji hili na kukuta likiwa limejaa vinywaji vingi. Nikachukua bia moja na kuifungua, nikaka kwenye kiti kirefu kilichopo hapa chumbani. Nikatoa simu aina ya iphone, taratibu nikaminya namba ya meja na kumpigia simu huku nikishusha mafunda kadhaa ya bia hii. Simu ya meja sikuipata hewani, ikanibidi kumpigia raisi Donald Bush moja kwa moja kwa namba yake ya mkononi. Simu yake ikaita na ikapokelewa.
 
“Ndio Dany”
“Habari yako?”
“Salama tu, vipi kuna hatua yoyote uliyo ipiga?”
“Ndio nipo naye kwa sasa na nimekuw amlinzi wake binafsi”
“Kazi nzuri, tena sana”
“Nashukuru muheshimiwa raisi. Hawa anaendeleaje?”
“Anaendelea vizuri, na kwasasa amekwenda Lass Vegacy na mwanagu wa kike”
“Ulinzi ni mzuri muhesimiwa?”
“Kwa hilo wala isitie shaka, yaani mwanangu ametokea kuwa rafiki mkubwa na mke wako hadi inafurahisha kwa kweli”
“Shukrani muheshimiwa r……..”
Mlango wa chumbani kwangu ukafunguliwa kwa nguvu.
“Badae muheshimiwa”
Nilizungumza kwa sauti ya chini huku nikikata simu na kuirudisha mfukoni mwangu, nikamuona Yemi Okocha akiingia huku analia na moja kwa moja akaka kwenye sofa na kujiinamia chini akizidi kuendelea kulia, kwa haraka nikanyanyuka kwenye kiti na kumfwata sehemua alipo kaa. Nikachuchumaa mbele yake na kumnyanyua taratibu uso wake.
 
“Kuna tatizo gani jaji”
“Ni…ni…memkuta mume wangu akiwa amelala na wasichana wawili kweliii”
Yemi Okocha alizungumza huku akizidi kulia kwa uchungu, mlango ukafunguliwa na akaingia mwanaume mrefu, huku akiwa amevalia suruali tu na hana tisheti yoyote juu yake.
“Mke wangu ninakuomba unisa…….”
Yemi Okocha kwa haraka akanishika mashavu yangu na kuanza kuninyonya lispi zangu huku machozi yakizidi kumchuruzika jambo lililo nifanya nibaki nimeduwaa kwa maana nimeingizwa kwenye kesi ambayo hainihusu kabisa.
                                                                                    
AISIIIII……….U KILL ME 137

    Nikastukia nikivutwa kwa nyuma na kuachanishwa na Yemi Okocha na nikaangukia pembeni. Mume wake akamnyanyua na kumtandika kofi zito la shavu lililo mrudisha Yemi Okocha chini. Kwa haraka nikanyanyuka na kumuwahi kumshika jamaa huyu kwa nyuma, huku nikijitahidi sana kumzuia asimpige Yemi.
 
Kutokana jamaa ana nguvu nyingi sana, akaniponyoka mikononi mwangu, akanigeukia na kunipiga kichwa kizito cha uso, nililicho nifanya nianguke chini pasipo msaada wa kuhiwahi. Kizunguzungu kikali kilicho nitawala baada ya kupigwa kichwa hichi, kikanifanya nilale chali kwa sekunde kadhaa.
“Niumeeeee”       
Nilisikia sauti ya Yemi Okocha akilia kwa uchungu, nikaka kitako, nikamuona mume wa Yemi akiwa amemkaba Yemi shingo yake, huku ameminya kwenye sofa na nisipo fanya msaada wowote basi ninaweza kushuhudia kifo cha Yemi mbele yangu. Nikajikaza kiume na kunyanyuka, nikamsogelea jamaa na kupiga kigoto cha mbavu na kumfanya kulegeza mikono yake kwenye koo la Yemi Okocha, akanigeukia huku akijaribu kurusha ngumi nzito. Jambo hili likanifanya nizidi kuwa makini sana, huku nikikwepa ngumi zake kwa ajili ya usalama wake kwa maana jamaa ananguvu nyingi sana na kamaa akinibahatisha kwa mara nyingine kunipiga basi nitajiweka katika hali mbaya hata ya kuuwawa. 
 
    Sikua na namna nyingine ya kufanya zaidi ya mimi kuanza kujilinda kwa kumzuia jamaa huyu kuwa kumpiga sehemu ambazo ziliweza kumpunguza kasi kila jinsi alivyo jaribu kunivamia. Kazi ya miguu yangu ni kurusha mateke yanayo tua kwenye mapaja yake kwa upande wa nyuma na kumnyong’onyeza. Zoezi hili likazaa matunda kwani jamaa alijikuta akipiga magoti chini pasipo kupenda kwani mapaja ya liishiwa nguvu na uwezo wa kuhimili mwili wake mkubwa.
“Mpumbavu wewee, ni nani aliye kupa ruhusua ya kumbusu  mke wangu”
Jamaa alizungumza huku akihema sana, jasho jingi likimwagika usoni mwake. Yemi akanyanyuka haraka kwenye sofa na kumrukia mume wake na kumuanguka chini. Akaanz akupiga makofi ya uso huku akimkwaruza na kucha. Hapa ndipo nilipo weza kuona hasiri ya Yemi, kwani bila ya huruma, akang’ata mumewe sikio aliye jitajidi kumtoa huku akipiga makofi ya mgongoni, ila Yemi hakuachia sikio hilo. Nilipo ona anaweza kumuumiza Yemi, ikanibidi kimshika mikono yake kwa nguvu na kumuacha Yemi amalizei anacho kifanya kwani baada ya dakika akatoka na kipande cha sikio kikiwa kinaning’inia mdomoni mwake na akakitema pembeni na kumfanya jamaa kupiga mayowe ya maumivu. Nikamuachia jamaa mikono yake na kumnyanyua Yemi Okocha na kumbeba kwa nguvu kwani bado alihitaji kumng’ata sikio la pili.
 
“Niache nimtie vilema malayaa huyu.”
Yemi alizungumza akijitahidi kujitoa mikononi mwangu, ila nikazidi kumkumbatia ili asiende kumvamia jaama ambaye kwa sasa amekaa kitako huku ameshika sikio lake lililo ng’ata akilia kwa uchungu sana.
“Malaya wewe, ulikuja kwangu ukiwa masikinii, leo nimekupa pesa, ku* na bado umenisaliti na malaya tuu wa hii hoteli na kuanzia hivi sasa nakuambia kwamba kila kitu ambacho ni changu nitakichukuaa, msen** wewe”
Yemi aliendelea kutukana huku akiendelea kujitahidi kujitoa mikononi mwangu.
 
“Peter niachee nikamuonyesheee msen... huyuuuuu. Awezi kulala na malaya ambao pesa, kula wanapata kutoka mikononi mwangu”
“Tulia Yemi, tulia adhabu uliyo mpa uliyo mpa inamtosha”
“Baado na nitakuwinda wewe. Nigeria yote hii utaiona chungu. Ku***** wewee”
Yemi aliendelea kufungulia kitabu chake cha matusi huku jasho likimwagika. Kusema kweli muwaone tu watu wakiwa wanacheka na kutabasamu, ila usije ukakutana na mtu wa aina hiyo akiwa katika kukasirika, hakika utajikuta ukiwa unaangukia pembeni.
Jamaa taratibu akanyanyuka huku akiyumba, huku sikio lake likiendelea kumvuja damu.
“Nitahakikisha ninakuua wewe malaya uliye msaidia mke wangu kunifanya hivi”
“Weeeee, weee mguse uonene. Nitamuambia baba yangu akunyoosheee. Na ninakuambia sasa kwamba huyu ndio ataichukua nafasi yako. Kwanza mwanaume gani usiye jiweze kwa chochote hadi usaidie na mwanamke.”
“Wewe ongea tuu, ila nitahakikisha huyo basha wako nina muua”
“Eheee ninaapa kwa jila la marehemu mama yangu, nitakuua hata kabla hujamgusa yeyee. Tena Peter niachie”
 
“Hapana Yemi”
Nikastulkia Yemi akining’ata mkono mwangu, nikajikuta nikimuachia kwa haraka akakimbilia sehemu yenye jiko, akachukua kisu kirefu na kuanza kukimbilia sehemua laipo simama mume wake. Mumewe kwa haraka wala hakuambiwa ni kitu gani kinacho kwenda kumtokea, kwani mlango alio uingilia aliufungua hata sikuona alipo elekea. Yemi akaufunga mlango kwa hasira huku akikikita kisu alicho kishika kwenye mlango.
“Hahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa”   
Yemi Okocha alipiga kelele huku akishika kichwa chake. Akaanza kubinua binua binua meza ya kioo iliyopo humu ndani akihitaji kuvunja kwa kuikanyaga jambo ambalo ni hatari kwani endapo kioo chochote kitamkata mguuni basi kutakuwa na zoezi la kuuguza kidonda. Nimamshika kiunoni mwake kwa nguvu na kuanza kumbebe juu juu.
“Peter niacheee ninahamu ya kuua mtuu”
“Achana na hilo swala Yemi, tahari imesha mpa kilema achana naye tafadhali”
 
“Peter nataka kuuaa, nataka kuuaaaaaaaaaaa………”
Yemi alizungumza huku akihema kwa nguvu, huku macho ameyatoa. Uzuri wake wote ukampotea usoni mwake. Nikamlaza kitandani kwa nguvu huku nikiendelea kumbana mikono na miguu yake ili asijaribu kunyanyuka.
“Peter, sawa nimetulia nimetulia naomba uniachie”
“Tafadhali niaahidi uto fanya kitu chochote cha kijinga”
“Ndio sinto fanya, nimesha rudi kwenye hali yangu ya kawaida”
Yemi alizungumza kwa upole. Taratibu nikamuachia Yemi Okocha huku nikikaa pembeni yake nikihema kwa kuchoka kwa maana ninatumia nguvu nyingi kumzuia mtu mwenye hasira kali. Gafla Yemi akashuka kitandani akaanza kukimbilia mlangoni, ikanibidi na mimi kunyanyuka kwa haraka, kabla hajakifikia kisu alicho kikita mlangoni nikawanikiwa kumuwahi kwa kumshika kiunoni mwake, nikamgeuza kwa hasira huku nikimtazama usoni mwake. Nikamsogeza kwa kasi hadi ukutani na kumgandamiza huku nikiwa nimeyang’ata meno yangu kwa hasira. 
 
“Si hitaji ujinga tenaa……”
Nilizungumza kwa hasira huku sauti nzito ikinitoka, jambo lililo mfanya Yemi kutulia kimya kwani nina imani hakutarajia kukutana na sura ya kutisha kama ninayo muonyesha.
“Umenielewa…….!!?”
Yemi akatingisha kichwa akisema kwamba amenielewa. Tukaendelea kutazamana kwa dakika kadhaa kisha nikamuachia. Nikachomoa kisu alicho kikita mlangoni, nikaanza kutembea kuelekea sehemu ya jiko na kumuacha Yemi akikaa chini taratibu huku akilia kwa uchungu sana. Nikarudisha kisu sehemu kilipo tolewa, nikaishika bia yangu na kuanza kuinywa kwa hasira huku nikimtazam Yemi anaye endelea kulia kwa hasira kali iliyo mtawala. Nikachukua bia nyingine kwenye friji, nikaifungua kifuniko chake kwa kutumia meno, nikaendelea kunywa. Nilipo ona kilio cha Yemi Okocha kinapungua, nikafungua friji na kuchukua chupa nyungine ya bia. Nikaanza kutembea kwa mwendo wa taratibu hadi sehemu alipo kaa. Nikaka pembeni yake huku nikimkabidhi bia hii niliyo kuja, akaitazama kwa sekunde kadhaa kisha akaichukua, akapiga funda moja na kuishika vizuri chupa hii.
“Mapenzi…..mapenziiiii. Nikitu kuzuri ila muda mwingine ni kitu kibaya”
 
Nilizungumza kwa sauti ya utaratibu, nikapiga fumba la bia, kisha taratibu nikashusha pumzi yangu huku nikimtazama Yemi usoni mwake.
“Mapenzi yalibadilisha maisha yangu na kuyafanya yawe mabaya kwa kiasi kikubwa. Mapenzi yalinifanya niwe mtu wa ajabu na muda mwingine nilichukiwa na kila mtu ambaye alinisikia pasipo kuniona na wala kunigundua mimi kwamba sina makosa yoyote katika kila jambo la uovu ambalo alilisikia”
“Una maaga gani?”
Yemi aliniuliza kwa sauti ya chini sana huku akinitazama usoni mwangu.
“Ni historia ndefu, ila kiufupi ni kwamba kwa sasa siyahitaji mapenzi, na wala siyatamani kwani madhara yake ni makubwa sana kama hivi uliyo yaona”
“Peter”
“Ndio”
“Samahani kwa kila kilicho tokea sikutarajia kama ninaweza kukuhusisha katika huu ugomvi ambao hauna tija yoyote kwako”
“Naelewa hakuna tabu na kuja kwako humu ndani ni kwamba uliniamini na ulitambua kwamba utakuwa upo kwenye mikono salama”
 
“Kweli wewe ni mtu wa tofauti sana, toafauti na watu nilio wahi kuwaona kwenye maisha yangu, upo tayari kuyahatarisha maisha yako kwa ajili ya mtu mwengine”
“Jukumu langu kwa sasa ni kukulinda wewe”
Nilizungumza kwa kujiamini huku nikimtazama Yemi Okocha usoni mwake, kimoyo moyo furaha inazidi kunitawala kwani mpango wa kumuweka Yemi Okocha karibu yangu unazidi kukomaa.
“Kweli Peter?”   
“Ndio, lazima mume wako atahitaji kulipiza kisasi kwa kile ulicho mfanyia, Kwa hiyo kitu kikubwa ni sisi kuwa makini sana kwa kila hatua ambayo tutaipiga”
“Nashukuru Peter kwa maneno yako ya ujasiri, nitakulipa kiasi chochote cha pesa utakacho kihitaji kwenye maisha yako”
“Sawa”
Yemi Okocha akasimama, akaipandisha suruali yake iliyo kuwa imeshuka kidogo, na kuyafanya makalio yake kujibana vizuri. Akaanza kutembea kuelekea kwenye friji, akachukua chupa za bia kumi na kuziweka kwenye kikapu kidogo cha plastiki, akarudi sehemu niliyo kaa akafungua chupa mbili na kunipatia moja kisha yeye akabaki na chupa moja.
“Peter”
“Ndiooo”
“Nataka tunywe tuleweeee. Tumsahau huyu mpumbavu”
“Sawa Yemi”
 
Tukaanza kunywa kwa kushindana, mchezo ulio tufanya tumalize bia hizi haraka sana, nikanyanyuka na kwenda kwenye friji, nikaongeza bia nyingine kumi na kurudi nazo, tukaendelea kunywa kwa mashindano, kadri muda unavyo zidi kwenda ndivyo jinsi nilivyo muona Yemi akipagawa kwa pombe kwani akaanza kufanya vituko vya kimapenzi.
Kwa mara kadhaa Yemi, akaninyonya lispi zangu huku akinisifia kwamba nina lispi nzuri. Sikuhitaji kuonyesha hisia zozote za mapenzi wala kumtamani kwani nimeweka ahadi kwa mke wangu Hawa kwamba nitajitahidi kuhakikisha kwamba ninalinda penzi lake.
Yemi akauweka mkono wa kushoto juu ya wangu, akaanza kupapasa papasa jambo lililo nifanya nianze kusisimka.
“Mmmmmm Peter”
“Eheee”
“Mimi ni bosi wako si ndioo”
Yemi alizungumza kwa sauti ya ulevi huku akiwa wamenilegezea macho yake.
“Ndio wewe ni bosi wangu”
“Kwani kuna ubaya wa sisi ku....
“Ndio wewe ni bosi wangu siwezi kufanya hivyo”
Nilizungumza kwa kujikaza tu, ila tayari jogoo wangu anasikiliazia maumivu ya kubanwa na nguo yangu ya ndani.
“Mmmmm, muongo. Kwa hiyo wewe unashindwa kuni...mimi kisa mimi ni bosi wako?”
“Ndio ninakuheshimu bosi wangu”
“Acha hizo, hembu shika hapa”
 
Yemi aliuchukua mkono wangu wa kulia na kuuweka kifuani mwake, akaanza kuushikisha ma..yake huku akinitazama usoni mwangu.
“Peter”
Yemi aliniita na nikajikuta nikishindwa kabisa kumjibu kutokana na kumeza funda la mate la kutamani sana kufanya anacho kihitaji Yemi Okocha.
“Peter, si nimekuita?”
“Yaa nimesikia bosi”
“Shika z.. langu hili liminye minye”
Yemi alizungumza huku akiusaidia mkono wangu kwa kushika na mkono wake katika kuminya ziwa lake la upande wa kulia. Yemi akashindwa kujizuia, na kujikuta akikaa kwenye mapaja yangu,
‘Hawa nisamehe, nipo kazini mama’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikikishika kiuno cha Yemi Okocha. Tukazidi  midomo yetu, nikajikaza taratibu huku nikinyanyuka chini na Yemi hakuendelea kuning’anga’ania mwili mwangu. Nikaanza kutemba hivyo hivyo kwa kujikaza hadi kwenye kitandaa, nikamvua Yemi
 

Nikajilaza pembeni huyu nikihema kwa nguvu kwani ni shuhuli kubwa, taratibu Yemi akajivuta na kulaza kichwa chake kifuani mwangu. Hatukuchukau hata dakika nyingi usingizi mzito ukatupitia.
“Baba umefwata nini chumbani kwangu!!”
Niliisikia sauti ya Yemi Okocha akizungumza kwa mshangao, nikahisi labda yupo usingizini.
“Huyu ndio aliye kufanya umsaliti mumeo”
Sauti nzito ya mwanaume ikanifanya nifumbua macho yangu, nikakutana na sura ya baba Yemi ambaye ni gaidi niliye tumwa kuja kumtafuta nchini hapa Ningeria, pembeni yake wamesimama wanajeshi wawili wakiwa na bunduki mkononi mwao, na mlangoni nikamuona mume wa Yemi Okocha akituzama kwa hasira kali huku Yemi naye amekaa pembeni yangu huku amejifunika kwa shuka kuficha maungo yake ya ndani.

==>>ITAENDELEA KESHO
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )