Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, November 11, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 146 na 147 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA      
 
“Niliwaambia mmoja wenu akienda kinyume nami basi nitahakikisha kwamba ninawaua kwa mkono wangu mimi wenyewe, je kuna anaye weza kujitetea juu ya hilo”
Nilizungumza huku nikitoa bastola yangu kutoka sehemu nilipo ichomeka, na kumfanya mzee aliye nifokea baada ya kuingia ndani ya chumba walicho kuwepo, kuangua kilio kikali na kuzidi kuwatisha wezake ambao nao wote sura zao zimetawaliwa na woga kwani hakuna hata mmoja anaye jua hatima ya maisha yake kutoka kwangu.
   
ENDELEA   
“Ni kitu gani munaweza kunishauri nikawaelewa kwamba kati yenu hakuna msaliti?”
Niliwauliza wageni hawa, mzee akazidi kuendelea kulia kwa uchungu.
“Tuleni chakula”   
Nilizungumza huku nikiirudisha bastola yangu kiunoni nilipo itoa.
 
“Mume wangu nikuombe kitu”       
Yemi alizungumza huku akininong’oneza sikioni mwangu.
“Niambie tu mke wangu”   
“Waonee huruma, hembu tazama huyu mzee wa watu anavyo lia”
“Hahahaa, mke wangu huyo mzee mnafki unakumbuka kwenye msiba, uliweza kumuona hata mmoja wako akiangusha chozi?”
“Mmmm”
“Sasa inakuwaje hapa alie wakati wote hawa ni wanafki”
“Sasa unataka kuwaua kweli mume wangu?”
“Hapana nina watisha, nahitaji kuingia nao mikataba”
“Mikataba ya nini?”
“Ya kuhakikisha kwamba wanalete pesa nitakayo ihitaji kila mwezi, kwa maana kuna familia za hawa wanajeshi wanao kufa, je tunaziangalia vipi, nataka kulibadilisha hili jeshi, lisiwe ni jeshi la kigaidi tena, nahitaji liwe jeshi la amani na kuheshimiwa na watu duniani”
 
“Mmmm sawa mume wangu”
Mazungumzo yetu hapakuwa na mtu hata mmoja aliye weza kuyasikia kwa maana tunazungumza kwa sauti ya chini sana.
“Mzee jinsi unavyo endelea kulia ndivyo utakavyo wafanya wezako nao wafe”
Watu wote wakastuka huku wakinikodolea macho. Nikatabasamu kidogo ili kuwafanya waweze kupata hata uwezo wa kula hichi chakula. Tukaanza kula taratibu huku sauti za vijiko na uma ndio vinavyo sikika katika eneo hili.
“Nitahitaji kuingia mikataba na nyinyi. Mkataba huo utakufanya wewe kuondoka kwenye hili eneo salama salimi pasipo kuudhurika, ila ukikataa basi huto ondoka katika hili eneo na utachukua hukumu ambayo ameifanya K2 kwa watu wangu”
 
Watu wote wakaacha kula hata aliye karibia kukiingiza kijiko chenye chakula mdomoni alijikuta akikishusha na kukirudisha kwenye sahani na kunisikiliza kwa umakini.
“Kila momoja wenu ninahitaji ahakikishe kila mwisho wa mwenzi anaingiza kiasi cha dola milioni tano kwenye akaunti ya jeshi hili, naamini mulivuna pesa nyingi kwenye hili jeshi, sasa ni wakati wa nyinti kurudisha kile mulicho kivuna. Angalizo atakaye kwenda kinyume na makubaliano hayo, nitahakikisha ninaigeukia nchi yako na nitakacho kifahanya sihitaji kuzungumza kwa maana munaelewa hilo sawa”
 
Karibia wageni wote wakatingisha vichwa vyao, nikuita meja, akanisogelea, nikaanza kumpa maelekezo ya kutengeneza mikataba hiyo haraka iwezekanavyo.
“Sawa mkuu”
Meja akaondoka.
“Mume wangu jambo ulilo lifanya ni sahihi sana”
“Yaa ninahitaji wanajeshi wangu waishi maisha mazuri tofauti na hapo awali”
Hazikupita hata dakika kumi na tano meja akarudi akiwa ameshika karatasi, akanikabidhi nikazipitia kwa haraka haraka zote zipo sawa kama vile niliyo muagiza kufanya. Nikanyanyuka kwenye kiti changu na kuanza kumpitishia mgeni mmoja badaada ya mwengine.
 
“Usome mkataba vizuri na uelewe maelezo yake, chagua kufa ama kutuma pesa. Muna dakika tano”
Nikarudi na kukaa kwenye kiti changu, hapakuwa na mgeni yoyote aliye bisha mkataba wangu kwa maana wote wanapenda kuishia. Kila mmoja akasaini mkataba huu unao garimu mwaka mmoja tu na baada ya hapo mimi na wao tunaachana. Baada ya wageni kukabidhi mikataba niliyo wapa, sikuwa na jambo jengine zaidi ya kuwaruhusu kuondoka katika kambi hii.
*Mkuu”   
Martin alizungumza huku akinitazama usoni mwangu
“Ndio”
“Kuna kitu inabidi uone”
“Wapi?”
 
“Kwenye televishion”
Nikaongozana na Martin hadi kwenye ofisi yangu, nikaona taarifa inayo husiana na nchi ya Marekani kutuma vikosi vyake vya anga na ardhi kuja kusaidiana na nchi ya Nigeria katika kuhakikisha kwamba inafutilia mbali kundi la Boko Haramu. Nikaka kimya kwa sekunde kadhaa huku nikitafakari nini cha kufanya.
“Walitangaza kuhusiana na kiongozi wa hili kundi?”
“Hapana nina imani kifo cha mzee bado hakijafika masikioni mwa watu wengi”
“Sawa niitie makamanda wote wa vikosi, nahitaji kufanya nao kikao cha dharura”
“Sawa”
Japo nimechoka sana na muda umekwenda ila sina jinsi inaniladhimu kuhakikisha kwamba ninalinda jeshi langu na sifikirii hata kumpoteza mwanajeshi haya mmoja. Simu ya mezani ikaita kwa haraka nikaipokea.
“Genero Peter?”
“Mkuu tuna tatizo?”
“Tatizo gani?”
“Tupo huku porini ninaona kuna  majeshi yanajiandaa kutuvamia”
 
“Shiitiiii wapo mbali kiasi gani?”
“Kama mili moja hivi, kuna vijana wangu wamewaona”
“Muna silaha za kutosha?”
“Zipo ila ytutahitaji msaada wako mkuu, kwa maana wanaweza kutumia hata ndege kutumaliza”
“Usijali”
Nikakata simu na kushusha pumzi nyingi sana, ikiwa ni siku ya pili katika uongozi wa hili jeshi ila ninakutana na changamoto moja ambayo kusema kweli ni ngumu kuweza kuihimili kwa haraka. Wakaingia wanajeshi watano huku wakiwa wameongozana na meja.
“Naamini mumesikia au bado hajasikia, nchi ya Marekani imetuma jeshi lake hapa Nigeria na wanasaidiana na jeshi la Nigeria, na hadi ninavyo zungumza hivi sasa nimepata taarifa kwa wanajeshi walipo poroni, vikosi vya ardhi vinakuja sasa sijajua vikosi vya anga navyo vitafika hapa saa ngapi?”
Meja na wezake wakaonekana kushangaa sana, 
 
“Mkuu tumeanini kwamba ni lazima kutakuwa na msaliti kati ya wale wageni kwa maana kambi hii ni ngumu sana kuweza kujulikana”
“Ni kweli na hiyo imesha tokea na kwa sasa hatuna njia nyingine zaidi ya kujipanga na kuhakikisha kwamba tunawazuia hata kabla hawajaweza kufika huku”
“Mkuu tuna ndege za kivita kumi na tano ambazo kumi ni jeti zenye uwezo wa kufanya mashambulizi ya anga kwa anga, na tano ni ndege kubwa zenye uwezo wa kubebe mabomu makubwa yenye uwezo wa kulipua zaidi ya ita elfu kumi kwa bomu moja.”
 
“Safi, je vikosi vya ardhi?”
“Kwenye vikosi vya ardhi mkuu tuna wanajeshi zaidi ya laki mbili, ila wajeshi elfu kumi wana mafunzo ya hali ya juu ya kikomandoo na wengine wana mafunzo ya kawaida”
“Ninahitaji zitoke ndege nne jeti na moja kubwa. Utaagiza makomandoo kumi tu, na wanajehsi wa hamsini”
“Jenero ila hiyo ni namba ndogo sana?”
“Vita ni akili na si wingi wa watu, je muna vifaa vya mawasiliano ya moja kwa moja?”
“Ndio mkuu”
“Nitahitaji kuongozana na kundi hilo la makomandoo”
“Mkuu!!”
“Nimesema andaeni vikosi, tunakwenda kupambana. Meja kamlete mke wangu”
“Sawa”
Wanajehsi hawa wakatoka chumbani hapa, nina imani kila mmoja ananishangaa kwa maamuzi yangu ya kuhitaji kuelekea kwenye mapambano haya ambayo ni hatari. Ila mimi mwenyewe ninaelewa kwamba raisi wa Marekani sasa ameamua kupambana nami.
 
“Peter kwa sasa hapana, huwezi kwenda popote mume wangu”
Yemi aliingia huku akizungumza, nyuma yake akiwa ameongozana na Meja ambaye ninaimani kwamba atakuwa amemueleza juu ya hali halisi iliyopo hivi sasa.
“Mke wangu hakuna jinsi ya kufanya ni lazima niende kupambana na vijana wangu”
“Sitaki Peter, kama ni kukuingilia katika hili basi acha nikuingilie, sinto hitaji kukupoteza na wewe, unataka mimi niishi maisha gani, unahitaji mimi niwe mkimbizi, niwe mjane si ndio”
Yemi alizungumza huku machozi yakianza kumlenga lenga, kwa ishara nikamuomba meja kutoka ofisini humu, akati amri na nikabaki na Yemi.
 
“Peter hembu angalia, hayajapita hata masaa sita tangu nimzike baba yangu, wewe nawe unataka pia nikuzike kwa nini lakini huitaji kuangalia umuhimu wako kwenye maisha yangu”
“Mke wangu hii sehemu kwa sasa sio salama, ni lazima niende nikawazuie maadui zetu huko walipo kuwa”
“Siwezi kusema kweli, ni bora kufia hapa kuliko kwenda huko unapo taka, tafadhali mume wangu, sina mtu mwengine zaidi yako wewe”
Yemi alizungumza kwa upole na machozi yakaanza kumiminika usoni mwake
“Nakupenda Peter, usiniache peke yangu, uliniahidi utaishi karibu na mimi, tunza basi ahadi yako”
Nikakaa kimya huku nikimtazama Yemi usinu mwake, taratibu nikajikuta nikimshika mkono wake wa kulia na kumsogeza karibu yangu.
 
“Nimekuelewa mke wangu sinto kwenda”
“Kweli?”
“Ndio mke wangu, ila vita ikizidi itabidi nisimame mimi kama jenero”
“Sawa mume wangu”
“Niitie meja”
Yemi akanipiga busu la mdomoni, kisha akaanza kutemba kwa haraka hadi kwenye mlango wa kuingia, akaufungua nikamkuta meja na wanajeshi wezake wakiwa wamesimama. Nikawaruhusu kuingia wote kwa ishara.
“Mkuu vikosi vipo tayari”
“Sawa”
“Wanasubiria amri yako muheshimiwa”
“Sawa wanaweza kwenda, wahikikishe wanawasiliana na wanajeshi walipo msituni wanao endesha oparesheni ya kumsaka K2”
“Sawa mkuu”
Meja akawapatia amri wajaeshi hao wanao kwenda kuhakikisha kwamba wanaangusha majeshi ya Wamarekani na jeshi la taifa hapa Nigeria.
 
“Muheshimiwa unatakiwa kuelekea katika chumba namba moja cha mawasiliano”
“Sawa”
Tukatoka chumbani hapa na moja kwa moja tukaelekea kwenye chumba hichi ambacho ndio mara yangu ya kwanza kuingia. Ukuta mkubwa wa humu ndani umefungwa Tv kubwa inayo onyesha wajaneshi hao jinsi wanavyo kwenda kupambana na kila kwenye kofia ya mwanajeshi walioenda vitani, ina kamera ndogo.
“Mumeweza kuwaona vikosi vya Wamarekani?”
“Ndio mkuu, ila bado ndege zao hatujaziona”
“Ja anga la hili eneo lina ulinzi wa kutosha?”
“Ndio jenero kuna mabomu maalumu ambayo yanaweza kuangusha ndege ya aina yoyote ambayo  inaweza kukatiza katika hili eneo”
“Basi hakikisha kwamba ndege yoyote ambayo itakuwa si ya kwetu munaiangusha”
“Sawa jenero”
Wanajeshi wetu wakazidi kusonga mbele, nikawaona wanajeshi wa kimarekani wakiwa katika vikosi vinne na wamejificha sehemu ambayo nina imani ndani ya muda walio jipangia basi wanatuvamia.
 
“Jenero tumefika sehemu ya karibu je tunaweza kushambulia”
Rubani mmoja alizungumza akiwa katika ndege yake.
“Watawanyisheni kwanza kwa risasi?”
“Mkuu!!”
“Nina maana yangu meja”
Ilibidi kumkatisha meja kwa kile anacho kishangaa.
“Fanyeni hivyo”
Marubani wakaanza kushambilia eneo walilopo wanajeshi wa Marekani na Nigeria kwa kutumia risasi za moto, jambo lililo wafanya wanajeshi hao kutawanyika huku wakishambulia ndege hizo. Uzuri wa ndege hizi zina kasi kubwa jambo ambalo ni gumu sana kwa wanajeshi wa kawaida kuweza kuzifikia katika mashambulizi.
Ndege za kijeshi za Kimarekani zikaanza kushambulia, kwani kuna sehemu zilikuwa zimejificha karibu kabisa na wanajeshi hawa walipo kuwa wamejificha.
“Tumieni mabomu sasa”   
“Sawa jenero”
“Meja umeona maana yangu. Nilihitaji kuziona hizo ndege, na kama wangetumia mabomu wale wanajeshi wasinge weza kuomba msaada, ila wametumia risasi na wanajeshi baadhi wameomba msaada kutoka kwenye hicho kikosi cha anga, kwa hiyo akili katika swala la mashambulizi ndio jambo la msingi kuliko nguvu”
 
“Nimekuelewa jenero samahani kwa hilo”
“Usijali meja”
Kwa haraka haraka unaweza kusema ni filamu moja ya kivita tunayo izungumza, ila ni uhalisia kabisa, kwani atakaye kufa kwenye mapambano hayo harudi tena duniani. Wamarekani kusema kweli wamechanganyikiwa kwani hata ndege zao za kivita zina angushwa moja baada ya nyingine kwa maana hawakujipanga vizuri na hili tulilo fanya ni shambulizi la kustukiza na nina imani litamtia presha raisi Donald Bush pamoja na Hawa ambao wamepanga kuniua na mimi sinto kubali kufa hadi nafsi zao ziweze kuonja mauti na nipo tayari hata kuanzisha vita ya tatu ya dunia, kwani Simba achezewi sharubu.
                                                                                    
AISIIIII……….U KILL ME 147

Kwa mbinu niliyo itumia haikuchukua hata lisaa, tayari tukawa tumesambaratisha mipango ya wanajeshi wa kimarekani na jeshi la serikali la hapa Nigeria.
“Jenero tumefanikiwa kuangamiza wote”
Mmoja wa marubani ambaye ndio kiongozi wa jeshi la anga alizungumza na kutufanya wote tulipo ndani ya chumba hichi kuanza kushangilia kwa furaha kwani ni ushindi ambao tumetumia akili nyingi kuliko nguvu kubwa. Taratibu Yemi akanikumbatia huku akinipiga mabusu mfululizo usoni mwangu.
“Jenero tuambie ni lini tuandae harusi yenu”
Meja alizungumza huku akiwa amejawa na tabasamu usoni.
“Mmmmmm, tutalipanga ngoja kwanza hizi sekeseke zipite”
“Sawa jenerali”
 
“Kukipambazuka nitahitaji kuzungumza na wanajeshi wote”
“Sawa jenerali”
Nikawaaga watu waliomo humu ndani ya hichi chumba, tukatoka ndani humu nikiwa nimeongozana na Yemi.
“Kusema kweli ninazidi kujisikia kwamba mimi ni mwanamke mwenye bahati sana kuwesza kupata mwanaume kama wewe, yaani nina jutia ni kwa nini nilichelewa kukufahamu mume wangu”
“Mungu atusaidie mke wangu kwa maana kwa sasa nina imani dunia mzima ni lazima itakuwa inalitafuta hili kundi na kulizungumzia”
“Usijali mume wangu, nitahakikisha ninakuunga mkono kwa kila jambo”
“Maswala ya uwanamitindo vipi?”
“Uzuri kampuni yangu inaweza kujiendesha hata kama mimi sipo karibu nao”
“Sawa mke wangu. Ila kuna kitu ambacho ninahitaji kukushauri ila sijajua kama utakubaliana nami”
“Zunngumza tu mume wangu, uzuri ni kwamba kwa sasa sisi ni kitu kimoja, japo hatujafunga ndoa ila ninaimani siku yoyote tutufunga ndoa”
 
“Kweli, ninahitaji mwanao aweze kurudi hapa Nigeria, sinto hitaji akae mbali nasi, nahitaji aanze kunizoea mimi kama baba yake mpya”
“Niwazo zuri ila hapa Nigeria ninajua atawindwa na wabaya, kwa maana ninaimani kwamba lazima serikali inafahamu kwamba baba yangu ndio muhusika mkubwa wa hili kundi”
“Nitahakikisha tunamlinda kwa hali yoyote, kwa maana kukaa kwake mbali kunanifanya nikose amani kabisa”
“Usijali mume wangu”
“Martin asante kwa kutuleta hapa nenda kapumzike”
“Sawa mkuu”
Martin akatuacha nje ya mlango wa chumba chetu, tukaingia ndani huku sote tukiwa tumechoka sana.
“Haki ya Mungu, leo imekuwa siku ndefu sana jamani”
Yemi alizungumza huku akijirusha kitandani na kulala chali. Taratibu nikaanza kuvua nguo zangu, huku nikijitazama kwenye kioo cha kabati hili.
 
“Hivi Peter hili jeshi mulilo liangamiza leo hawato rudi tena kutuvamia?”
“Kurui kutuvamia lazima watarudi tu”
Taratibu Yemia akanyanyuka na kukaa kitako huku sura yake ikonekana kujawa na wasiwasi mwingi sana.
“Usijalili mke wangu nina imani tutashinda, mtu akitufwata tunahaki ya kumpiga kwa maana tukimuacha atatupiga sisi”
“Sawa mume wangu”
“Itabidi kuomba msaada kwenye nchi ambazo zina uadui na Marekani”
“Nchi kama zipi?”
“Ya kwanza ni Urusi, hawa ninajua hawapatani kabisa na Marekani, nchi ya pili ni Korea ya Kaskazini, nitahijitahidi kukutana na wakuu wao wa nchi na nitawaleza lengo letu”
“Pia kuna nchi kama Pakistani, Iraqu pia hao unaweza kuwaomba msaada mume wangu”
 
“Yaaa najua Marekani akirudi kwa mara ya pili hato kuja kwa kujitega tega kama alivyo fanya, akija atakuja kwa kushambulia tena kwa mabomu makubwa makubwa. Anaweza hata kutumia nyuklia japo anapiga vita zisitumike duniani”
“Mungu wangu sasa kama akiamua kutumia nyukilia si tutupotea katika ulimwengu huu pasipo kutimiza malengo ya baba?”
“Usijali mke wangu, ninajua cha kufanya hilo wala wewe lisikusumbue”
“Sawa mume wangu”
Nikamshogela Yemi kitandani alipo lala. Taratibua nikaanza kumvua nguo zake huku nikimtazama usoni mwake kwa macho yaliyo jaa mahaba.
“Ujachoka mume wangu tuu…..?”
“Kwenye hili siwezi kuchoka”
“Mmmmmm jamani kwa hiyo huku hata ukiwa hoi nyang’anyang’aaa wewe huto choka kabisa kupana……”
Nikawahi kumzima mdomo Yemi kwa kutumia lipsi zangu, taratibu tukaanza kuchezesha ndimi zetu.
Tukaanza kupeana burudani , hatukutumia muda mwingi tukamaliza burudani yetu. Tukashuka kitandani na kuingia bafuni, tukaoga na kurudi chumbani hambapo hatukuwa na mazungumzo mengi sana, tukajikuta tukilala fofo.
                                                                                                    ***   
Mlio wa simu ya Yemi ukanistua kutoka usingizini, taratibu nikafumbua macho yangu na kuichukua, sikutaka kuipokea kama utaratibu tulio jiwekea, hakuna mtu ambaye anaishika simu ya mwenzake.
“Yemi, Yemi”
“Mmmmm”
“Simu yako inaita”
“Nani tena asubuhi yote hii?”
Yemi aliuliza huku akijinyanyua kidogo kitandani akaichukua simu na kuitazama kwa muda kisha akaipokea. Taratibu nikashusha kitandani, nikapiga hatua hadi kwenye dirisha, nikafungua pazia na kutazama nje. Wanajeshi wangu wanazidi kufanya mazeozi ya viongo.
“Wewe ni nani?”   
Sauti ya ukali ya Yemi ikanifanya nigeuke nyuma na kumtazama.
“Mwanangu yeye wa nini?”
Yemia lizidi kuzungumza kwa ukali na kunifanya nianze kutembea taratibu kurudi kitandani huku nikiwa sina hata nguo moja kwenye mwili wangu. Nikaanza kumuona Yemi machozi yakianza kumwagika usoni mwake.
“Mke wangu kuna nini kimetokea?”
Yemi hakunijibu zaidi ya kuendelea kulia, kwa haraka nikampokonya simu yake na kuiweka sikioni mwangu.
“Mamaa……”       
Niliisikia sauti ya mtoto mdogo wa kiume, akiita moja kwa moja nikagundua kwamba atakuwa ni mtoto wa Yemi.
“Tunahitaji Dany ajisalimishe na tumuachie mwanao”
Niliisikia sauti ya kiume ikizungumza.
“Wewe ni nani?”   
Nilizungumza kwa sauti nzito huku nikiwa nimekasirika sana.
“Ohooo Dany nashukuru kupokea simu yako”
“Nimekuuliza wewe ni nani?”
“Mimi ni rafiki yako wa muda mrefu sana. Hongera kwa kuoa”
“Nimekuuliza wewe ni nani ambaye unajaribu kuingia kwenye maisha yangu”
 
“Mimi ni Donald. Donald Bush”
Mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio sana baada ya kusikia sauti halisi ya raisi wa Marekani, kwani hapo mwanzo sauti yake ilikuwa nzito naamini alijaribu kuibadilisha ili isiweze kujulikana kirahisi.
“Unahitaji nini?
“Ninakuhitaji wewe Dany, yaani leo hii wewe ndio mkuu wa Al-Shabab wakati nilikutuma ukafanye kazi ya kuangamiza kundi hilo”
Nikatamani kufoka ila nikabaki nikiwa nimemtazama Yemi na kushindwa kuzungumza chochote kibaya kwa raisi huyu ambaye kusema kweli kwa sasa amevuka mpaka ambao sidhani kama ataweza kurudi upande wa pili alipo toka.
“Lini na wapi unahitaji nijisalimishe”
“Hahaaaa, umekuwa mnyonge sana kwa ajili ya mtoto wa mwanaume mwenzako. Tafuta wa kwako basi, usililile watoto wa wezako”
 
Nikazidi kujizuia kutokuzungumza neno baya ambalo Yemi anaweza kulisikia hapa.
“Huyo ni mwanangu, niambie ni wapi na saa ngapi utahitaji nijisalimishe mikononi mwako na umuachie mwanangu?”
“Lazima uje Marekani, na ninakupa masaa arobaini na nane, yaani siku mbili uwe umesha fika ndani ya Marekani na ukifika hapa nitakuambia ni wapi na saa ngapi utaweza kumpata mtoto ambaye si wako”
“Nimekuelewa”
Nikakata simu huku machozi ya hasira yakinilenga lenga usoni mwangu huku kifua changu kikianza kuvimba kwa hasira hii.
“Mwanangu wamemteka”
Yemi alizungumza huku akiendelea kulia kwa uchungu. Nikaichukua suruali yangu iliyopo juu ya sofa, nikavaa kwa haraka, nikachukua tisheti ndani ya kabati na kuvaa. Nikaanza kutembea kuelekea mlangoni huku nikiwa nimeishika simu ya Yemi mkononi mwangu.
“Dany”
Yemi alinita kwa jina ambalo sikuwahi kumuambia hata siku moja. Nikajikuta nikiwa nimesimama mlangoni huku nimeshika kitasa cha mlango.
 
“Dany ndio jina lako halisi Peter?”
Nikayafumba macho yangu huku nikijaribu kupambana katika kuipunguza hasira yangu kwani ninashindwa hata kuzungumza kabisa.
“Naomba unijibuuu”
Yemi alizungumza kwa hasira na kunifanya nigeuke na kumtama kwa macho makali. Nikaanza kutembawa kwa kujiamini huku nikimfwata kitandani alipo kaa. Yemi taratibu akaanza kuudi nyuma huku akiwa na wasiwasi mwingi usoni mwake.
“Ndio ni jina langu”
Nilizungumza kwa sauti nzito huku nikijaribu kuibana pumzi yangu inayo kifanya kifua changu kupanda na kushuka kwa ajili ya hasira.
“Kwa nini ulinidanganya eheeeee?”
Yemi alizungumza huku akiendelea kulia kilio  kikali.
“Tazama sasa  mwanangu wamemteka, tazama Peter kwa nini hukuniweka wazi kwa nini hukuniweka wazi eheeeee”
Yemi alizungumza huku akianza kunipiga vibau vya mashavuni mwangu. Sikutaka kumfanya chochote zaidi ya kuendelea kumtazama na kumucha azidi kunipiga makofi yake.
 
“Wananitaka mimi na si mwano, nitahakikisha mwanao  anarudi mikononi mwako”
“Kivipi Peter, wewe ni muongo umenidanganya mimi, umemdanganya baba, umewadanganya wanajeshi w…….”
“Yemi kimya”
Nilizungumza kwa kufoka na kumfanya Yemi kutetemeka mwili mzima huku akiwa amenitola macho yake kwani nina imani hakuwahi kunifumania nikiwa katika hasira kama hii niliyo nayo hivi sasa.
“Wewe na baba yako majina munayo yatumi ni halisi, eheeeee? Muliwa kuniambia majina yenu halisi eheeee?”
Nilimfokea Yemi na kumfanya akae kimya huku machozi yakimtiririka mashavuni mwake hata sauti ya kilio nayo ikakatika.
 
“Sisi sote katika hili ni waongo, baba yako amekufa na siri yake na wewe umekaa na siri hiyo hata siku moja hhukuwahi kuniambia siri yenu ambayo nimeifahamu hata kabla ya kuja hapa Nigeria”
“Na nimekuwa msaliti kwa wale walio kuwa wamenituma kwa ajili yako wewe, na laiti ningeihitaji kuwaua wewe na baba yako pasinge kuwa na mtu wa kunizuia kufanya hivyo. Ila wao walisaliti na ndio maana nikawa na nyinyi, ndio maana ninahitaji kuhakikisha ninalipa kisasi kabla sijaingia ndani ya hii ardhi. Nitaleta mwanao mikononi mwako, na kuanzia hapo nitakuwa tayari kufa na kuifwata familia yangu kule ilipo elekea ambayo K2 amehusika katika kuwaua”
Nilizungumza kwa hasira na sauti ya ukali huku nikiwa nimemtazama Yemi usoni mwake, na jambo lililo pelekea kuzungumza maneno ambayo sikuyatarajia kuyazungumza mbele ya Yemi siku hata mmoja kwenye maisha yangu.
                                                                                     ITAENDELEA
“Haya sasa ukweli wa Dany umewekwa hadharani na Raisi Donald Bush aliye mshikilia mtoto wa Yemi je ni mbinu gani Dany ataitumia kumrudisha mtoto wa Yemi mikomoni mwake. Usikose sehemu inayo fwata.”
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )