Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, November 14, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 148 na 149 )

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA 
      
“Na nimekuwa msaliti kwa wale walio kuwa wamenituma kwa ajili yako wewe, na laiti ningeihitaji kuwaua wewe na baba yako pasinge kuwa na mtu wa kunizuia kufanya hivyo. Ila wao walisaliti na ndio maana nikawa na nyinyi, ndio maana ninahitaji kuhakikisha ninalipa kisasi kabla sijaingia ndani ya hii ardhi. Nitaleta mwanao mikononi mwako, na kuanzia hapo nitakuwa tayari kufa na kuifwata familia yangu kule ilipo elekea ambayo K2 amehusika katika kuwaua”
Nilizungumza kwa hasira na sauti ya ukali huku nikiwa nimemtazama Yemi usoni mwake, jambo lililo pelekea kuzungumza maneno ambayo sikuyatarajia kuyazungumza mbele ya Yemi siku hata mmoja kwenye maisha yangu.
   
ENDELEA   
“Kifo changu hakito kuwa na thamani kwa mtu yoyote, maisha yangu yalisha haribika tangu nikiwa kijana mzuri ambate laiti kama ningekuwa nimetulia leo hii nisinge kuwa hapa na kuingia katika mikasa kama hii ambayo unaiona. Nimeteseka, nimegangaika, bado napigana kuhakikisha kwamba ninalipa kisasi kwa wale ambao  wameiteketeza familia yangu”
Nilizungumza huku machozi yakinitoka usoni mwangu.
“Najua nitakufa, Marekani inaniwinda mimi, Tanzania inaniwinda mimi, nilazima nitakufa mke wangu, mimi sio mwanaume wa kunipenda kwa maana sina gerentii ya maisha yangu”       
“Hapana Peter usizungumze hivyo, ninakupenda”
“Ninanjua unanipenda ila maisha yangu ni ya hatari, sina makazi maalumu Yemi, siwezi kusema ninaweza kuanzisha familia ambayo inaweza kuingia matatizoni kisa mimi. Hembu tazama familia yangu iliuwawa kwa kuchinjwa, tazama mwanao kwa sasa ametekwa kwa ajili yangu, bado unihisi kwamba mimi ni mwanaume sahihi kwenye maisha yako?”
Kwa haraka Yemi akanisogelea na kunikumbatia kwa nguvu huku akimwagikwa na machozi usoni mwake.
“Peter wewe ndio mwanaume wa ndoto zangu, nina kuahidi tutakuwa pamoja kufa na kupona, ninakupenda sana, ninakuhitaji kwenye maisha yangu wewe ndio baba wa wanangu. Lolote litakalo tokea nipo pamoja na wewe, kamwe sinto jali ni nani anaye kuwinda anaye kutafuta ila nitahakikisha kwamba ninakuwa na wewe mume wangu”
Maeno ya Yemi yakazidi kunisisimua mwili wangu, taratibu tukaachiana huku tukitazamana.
“Ninatakiwa kulishuhulikia swala la mtoto, ninakuomba utulie na nitajua nitakacho fanya”
“Kwani mume wangu hao walio mshikilia ni kina nani?”
“Aliye mshikilia ni mtu mmoja na ananguvu kubwa sana kwenye huu ulimwengu”
“Ni nani huyu mume wangu?”
“Ni raisi Donald Bush, ni raisi wa Marekani?”
Yemi akaonekana kustuka kidogo, mstuko wake ninatambua unatokkana na mtu niliye mtajia.
“Kwenye hiyo vita ni lazima na mimi nipigane kufa na kupona”
Yemi alizungumza kwa msisitizo huku akinitazama usoni mwangu.
“Kwa nini?”
“Nilijua kwamba huyo mshenzi atakuwa ameacha kuiandama famili yangu kumbe bado anendelea kuiandama ni lazima nimuue”
Yemi alizungumza kwa msisitizo na kuzidi kunishangaza.
“Ni kitu gani ambacho unakifahamu dhini ya Donald Bush?”   
Yemi akaka kimya kwa muda huku akionekana kufikiria jambo fulani kichwani mwake.
“Niambie mke wangu?”   
“Donald Bush alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mama yangu, kabla mama hajakutana na baba yangu, baada ya wawili hao kuachana chuo kila mmoja kuendelea na maisha yake, mama aliweza kumpata baba. Basi Donald alijaribu sana kumrudisha mama mikononi mwake, ila mama alisha mpenda baba yangu, mwisho wa siku katika kugombania msichana na kupambana na baba, alimchoma mama kisu cha tumbo kisha akamchoma na baba kisu cha tumbo, sikuweza kufanya chochote nilipo shuhudia tukio hilo kutokana mimi nilikuwa bado mdogo mdogo. Mama alifariki ila baba aliweza kubaki hai. Baada ya kupona ndipo baba alipo anza harakati za kutengeneza jeshi lake hadi leo unaona jeshi limekuwa kubwa kama hivi”
“Baba alijaribu kulipiza kisasi?”
“Waliwindana sana, hadi baba amefariki hakuweza kufanikiwa kumpata, na wala mimi sikujishuhulisha na maswala ya kulipiza kisasi kwani niliamua kuishi maisha ya usalama na ya amani. Ila kwa hapa alipo fika, amefikia pabaya sana, ni lazima nimshuhulikie”
“Yemi”
“Bee”
“Una nipenda?”
“Ndio ninakuependa mume wangu, zaidi ya unavyo fikiria”
“Una niamini?”
“Ndio mume wangu”
“Ninakuomba hili swala nilishuhulike mimi peke yangu, sihitaji wakuguse wewe”
“Dan……ahaa Peter”
“Ukipenda kuniita Dany pi unaweza kuniita mke wangu hakuna haja tena ya kuficha uhalisia wangu kwako ikiwa unafahamu kila kitu”
“Sawa mume wangu. Ila kumbuka kwamba mimi na wewe ni mke na mume na tunatakiwa kushirikiana ili kumkomboa mtoto wetu?”
“Natambua hilo ila ninakuahidi mtoto atarudi, na nitakuacha hapa na utaweza kusimamia madaraka yote ya kijeshi na amri ya mwisho watapokea kutoka kwako sawa mke wangu”
“Dany mimi na jeshi wapi na wapi?”
“Najua unaweza, na ninatambua utafanya. Huu sio wakati wa kurudi nyuma mke wangu, huu ni wakati wa kupambana sawa”
“Sawa mume wangu”
“Ngoja nielekee nje sasa”
Nikambusu Yemi usoni mwake kisha nikashuka kitandani, nikaanza kueleka nje huku nikiwa nimeishia simu ya Yemi mkononi mwangu.
“Habari ya asubuhi jenero”   
Martin alinisalimia mara baada ya kutoka chumbani kwangu na kumkuta akiwa amesimama sebleni akinisubiria.
“Salama tu, kuna lipi jpya?”
“Hakuna jipya ila wanajeshi wanaisubiria hotuba yako kwa hamu sana”
“Usijali majira ya saa nne nitawahutubia, ila kwa sasa muambie meja aje ofisini kwangu nina mazungumzo naye”
“Sawa mkuu”
Tulizungumza huku tukitembea, Martin akaeleke kumuita meja na mimi nikaelekea ofisini kwangu. Nikaingia ofisini kwangu, na kukaa kwenye kiti changu huku mawazo mengi yakiendelea kunitawala kichwani mwangu. Hisia zangu za kukataa mtoto wa Yemi kuishia mbali nasi kumbe zilikuwa sahihi kabisa. Mlango ukafunguliwa akaingia meja, akanipigia saluti kwa ishara nikamruhusu kukaa kwenye kiti kinacho tazamana nami.
“Jenero mbona unaonekana huna furaha kabisa?”
“Kuna tatizo ila hili ni binafsi sana, sitaki kulihusisha jeshi kwani sihitaji mtu yoyote aumie tena kwa ajili yangu”
“Tatizo gani jenero”
“Mtoto wangu wa kufika amekamatwa na Wamarekani”
“Mtoto wako wa kufikia!!?”
Meja aliniuliza huku akiwa amenitazama usoni mwangu.
“Ndio, mtoto wa Yemi amekamatwa na raisi wa Marekanani na ananishinikiza mimi kwenda kufanya mabadililo naye la sivyo atamuu”
“Mke wako anatambua hilo?”
“Yeye ndio alikuwa wa kwanza kuweza kulitambua hilo swala”
“Duuuu”
Meja alizungumza huku akishusha pumzi nyingi kwani hili swala ni zito sana na linahatarisha maisha yangu na usalama wa hili jeshi kwa asilimia tisini, kwani nimesha anza kuona jinsi mchango wangu ulivyo mkubwa kwneye hii chini.
“Yaani hapa kichwa changu kina niuma, mke wangu ana kazi ya kulia tuuuu, yaani ninashindwa kabisa nifanyaje, na nimekwama kusema kweli meja wangu”
“Unaonaje hiyo kazi tukawapa vijana wetu wakaifanya?”
“Hapana Mmarekani akiwa kwake ana mbinu nyingi sana za kuwakamata, na hiyo inaweza kupeleka vijana wetu wakapoteza maisha kwa swala ambalo haliwahusu”
“Ila jenero kumbuka kwamba hapa huyu ni mjukuu wa muasisi wa hili kundi, ni lazima damu yake ipiganiwe kwa garama yoyote”
“Hilo ni kweli ila sinto hitaji iwe hivyo”
“Sasa hapo tunafanya nini jenero wangu?”
Sijui meja, yaani natamani kwenda kuifanya hii kazi ila sinto rudi, hawa watu zaidi ya laki mbili wataongozwa na nani?”
Sote tukajikuta tukikaa kimya huku tukikuna vichwa vyatu.
“Nimekumbuka kuna watu wanaweza utuusaidia”
Maje alizungumza na kunifanya nimtazame usoni mwake.
“Kitu gani?”
“Kuna kundi moja la majasusi lipo Mosscow nchini Urusi, hilo lina mtandao mkubwa sana hadi ndani ya serikali ya Marekani, kwa kuwatumia hao mtoto anaweza kurudishwa akiwa salama Salmin na kikubwa ambcho kinatakiwa ni kuweka pesa mezani”
“Unaweza kuwasiliana nao hata sasa hivi?”
“Ndio ninaweza mkuu”
“Wasiliano nao basi tujue tunafanyaje”
Meja akatoa simu yake mfukoni akaminya minya batani za simu yake na kuiweka sikioni. Meja akaanza kuzungumza na mtu huyo.
“Ndio tulipata msiba wa mzee jana ndio tumemzika”
“Tunashukuru, ila kuna tatizo moja kubwa sana”
“Mjukuu wa mzee ameshikiliwa na serikali ya Marekani, wanamshinikiza mkuu wetu mpya aweze kujisalimisha mikononi mwao na watamuua nina imani wakimkamata”
Kwa ishara ninakumuomba meja kuweka simu yake loudspeaker.
“Mumepata mkuu mpya?”
“Ndio tnaye mkuu mpya ni mkwe wa mzee”
“Yule jamaa bishoo bishoo”
“Hapana huyu wa sasa ni komandoo, naamini umesikia jinsi tulivyo mtandika mmarekani na jeshi la Nigeria, yote nimatunda yake”
“Kama ni yeye aliye ongoza basi mumepata kichwa hapo”
“Yaaa, sasa anahiyaji hii uparesheni muifanye nyinyi, je mutaweza?”
“Hakuna jambo linalo shindikana hata kama mukihitaji tumuangamize huyo aliye mshikilia tunaweza kufanya”
“Basi zungumza naye huyu hapa”
“Habari yako ndugu”
Ilinibidi nianze kuzungumza mimi.
“Salama jenero hongera kwa ushindi wako wa jana, dunia nzima inalia kwa kile mulicho kifanya ila kwetu sisi ni furaha kwa maana tumepata wasaidizi wetu kwenye hii na Mmarekani”
“Ninashukuru sana, kitu ninacho kihitaji munifanyie ni kuhakikisha mwanangu anarudi mikononi mwangu nyinyi niambieni ni kiasi gani cha pesa mutahitaji ili kumkomboa mtoto wangu”
“Kwa sasa kaka sihitaji pesa yako, ngoja tuifanye kazi ikikamilika basi nitakuambia ni kiasi gani ambacho tunahitaji na pia nitahitaji ushirikiano wetu, kwani vita yetu sote ni dhidi ya Marekani”
Maneno ya huyu kiongozi wa kikundi cha kijasusi yakanifariji snaa moyoni mwangu na kujikuta nikishusha pumzi huku  nikitokea kuwaamini sana katika utendaji wao wa kazi japo sikuwahi kuwaona nah ii ndio mara yangu ya kwanza kuwasikia.

AISIIIII……….U KILL ME 149

“Nimekuelewa ndugu na mutachukua muda gani kuweza kukamilisha zoezi la kumuokoa mwanangu?”
“Masaa kumi na mbili kuanzia hivi sasa, tupatie picha ya mwanao kisha tunajua tunaanzia wapi?”
“Poa poo tutakutumia baada ya muda mfupi”
“Sawa mkuu”
Nikakata simu na kumrudishia meja simu yake huku usoni mwangu nikiwa nimejawa na tabasamu pana kiasi kwani nimepata njia ya matumaini.
“Naomba ukaniitie mke wangu”   
“Sawa jenero”
Meja akatoka ofisini kwangu na kuniacha nikiwa ninatafakari njia ya pili enepo majasusi hawa watashindwa kabisa kumukoa mtoto wa Yemi. Haukupita muda sana mlango ukafunguliwa akaingia meja pamoja na Yemi ambeye usoni mwake amapoteza furaha kabisa. Taratibu Yemi akaka kwenye kiti alichokuwa amekali na meja na kumfanya meja kusimama.
“Mke wangu tuepata njia ya kumuokoa mtoto”   
“Njia gani mume wangu?”   
Nikatamzama meja na kumpa ishara ya kuelezea mpango mzima tulio upanga na majasusi wa Urusi.
“Muna waamini?”   
“Ndio nina waamini wamefanya kazi nyingi pia na marehemu baba yako, na kupitia baba yako mimi niliweza kuwafahamu”
Meja alizungumza kwa kujiamini  sana.
“Sasa wanataka kiasi gani?”
“Hawaitahi kiasi chochote kwa sasa hadi kazi itakapo kamilika, ila wamehitaji picha ya mtoto wetu”
“Tuwapatie kama ndio hivyo?”
Yemi alizungumza kwa sauti iliyo jaa upole ndani yake huku akinitazama usoni mwangu.
“Sawa meja unaweza kufanya hilo”
“Naomba simu, kuna picha niliyo tumiwa whatsapp wiki iliyo pita nia imani itakuw andio nzuri”
Nikamkabidhi simu Yemia akaanza kuitafuta picha hiyo kisha akanigeuzia simu niitazame picha hiyo.
“Inafaa. Meja chukua simu hiyo umtumie jamaa”
“Sawa jenero”
Meja akachukua simu ya Yemi, akatoka humu ofisini. Taratibu nikasimama na kumsogelea Yemi ambaye hana furaha kabisa kwenye uso wake. Taratibu nikamnyanyua huku nikimkumbatia tararibu pasipo kuzungumza kitu chochote.
“Dany mume wangu ninakupenda sana”
“Ninakupenda pia mke wangu”
“Nikuulize kitu?”
“Niulize”
“Kama ingekuwa hujasalitiawa na watu walio kuwa wamekuagiza ni kweli ungetuua?”
Swali la Yemi likanifanya nikae kimya kwa sekunde kadhaa huku nikifikiria kile nilicho kifanya kwa baba Hawa na kundi lake la Al-Shabab.
“Nisinge weza kufanya hivyo?”
“Kwa nini?”
Yemi alizungumza huku akijitoa mikononi mwangu taratibu na kunitazama usoni mwangu kwa macho ya mshangao kidogo.
“Ninakupenda, na mulinipenda na kuniamini, hata kama wasinge kuwa wamenisaliti kama ulivyo sema ila ukarimu wenu ungeyayusha maagizo yote niliyo kuwa nimepewa dhidi yenu”
“Nashukuru sana mume wangu kwa hilo kwa mana umesha tambua ukweli ni kwamba ulikuwa unatumiwa kulipiza kisasi cha watu wengine ikiwa wao wamekaa kwenye sehemu zao salama salimini”
“Usijali mke wangu, ndio manaa ninahitaji jeshi la baba yako kwa sasa lifanye kazi za faida, na zilizo njema na si kwa kuwaumiza wananchi wasio na uwezo wa kijeshi”
“Ni kweli unatakiwa kufanya mabadiliko mume wangu wewe ni kijana na wengi walipo kwenye hili kundi ni vijana wezako wape maisha ambayo kila mmoja atakupenda na kukuheshimu zaidi ya hapa wanavyo kuheshimu”
“Asante mke wangu kwa ushauri wako”
Mlango ukagongwa kwa nje taratibu nikamuachia Yemi na kumkaribisha mtu anaye bisha hodi. Akaingia Martin akiwa ameshika faili.
“Muheshimiwa nimekuandalia hotoba kama hotojali unaweza kuipitia”
Martin alizungumza huku akikabidhi faili hili alilo kuja nalo ofisini kwangu.
“Shukrani”
Nilizungumza huku  nikilichukua faili hili na kulifunua, nikaanza kupitia mwanzo wa hii hotuba, nikamtazama Martin kisha nikatabsamau kwani kile alicho kiandika ni kama vile alikuwa kwenye akili yangu kwani niliahidi kuhutubia wanajeshi wangu kwa ushindi tulio upata ila kwa haya matatizo niliyo kutana nayo asubuhi ya leo kichwa changu chote kimepagawa na sijui ni kitu gani ninaweza kukifanya.
“Umefanya jambo zuri Marti, waambie wanajeshi baada ya nusu saa nitakuwa uwanjani kwa ajili ya kuwahutubia”
“Sawa”
Akaingia meja, Martin akatoka na kutuacha ofisini.
“Nimesha mtumia mkuu”
“Amesemaje?”
“Ameomba nimpigie azungumze na wewe”
“Mpigie”
Nilizungumza huku nikizunguka meza hii na kukaa kwenye kiti changu, meja akapiga simu kwa mkuu wa kikosi cha majasusi kisha akanikabidhi.
“Ndio kaka”
“Tumeipata picha ya mwanao, na upelelezi tulio ufanya hadi hivi sasa, mwanao ameshikiliwa katika ikulu ya Marekani na sehemu hiyo inahitaji nguvu ya ziada kuweza kuingia hapo ikulu”
“Ohoo Mungu wangu”
Nilizungumza huku nikishusha pumzi nyingi, jambo lililo mfanya Yemi kunitazama kwa macho ya mshangao huku  akiwa na shauku ya kuhitaji kuni kitu gani kinacho endelea.
“Ni pagumu sana kuweza kuingia ndani ya ikulu ya Marekani, kwani sasa hivi ulinzi wake umebadilika kwa asilima mia moja, na kufanya hivyo inaweza kuepela vijana wangu wengi kupoteza maisha”
“Hamna mtu ndani ya ikulu ambaye anaweza kuifanya hiyo kazi?”
“Yupo ila nimewasiliana naye inavyo onyesha ni kwamba hato weza kufanya hivyo kwani mtoto wenu yupo chini ya ulinzi wa askari wa raisi na nikatika chumba cha siri”
“Naomba unipe dakika kumi na tano nitakupigia”
“Sawa kaka”
Nikakata simu huku nikiwa nimepiteza furaha kabisa kwenye uso wangu.
“Mume wangu naomba uniambie ni kitu gani ambacho kimempata mwanangu?”
“Yupo ndani ya ikulu ya Marekani na yupo katika chumba cha siri”
“Ohoo Mungu wangu, sa…sasa wamesemaje hao watu?”
Nikamtazama Yemi usoni mwake kwa sekunde kadhaa huku nikitafakari ni kitu gani ninacho weza kukifanya.
“Mkuu hili jambo linahitaji tuandae kikosi cha kwenda kuifanya hivyo kazi?”
“Sio kwenye ikulu ya Marekani, hakuna hata mmoja ambaye anaweza kutoka salama”
“Acha tu iwe hivyo mkuu?”
“Meja kufanya hivyo pia mwanangu ninamuweka katika hali ya hatari, unahisi wamarekani wataacha kumua endapo sisi tukienda kuwavamia?”
Maneno yangu yakamfanya meja kukaa kimya kwa sekunde kadhaa huku akinitazma usoni mwangu, Yemi hakusema kitu chochote zaidi ya kuinama chini huku kiganja cha mkono wake wa kulia kikiwa na kazi ya kuziba uso wake moja kw amoja nikatambua kwamba analia.
“Ila tuna makomandoo ambao tukiwatuma nina uhakika wanaweza kuifanya hii kazi ikaenda sawa sawa”
“Meja naomba unipe muda wa kulifikiria hili na mke wangu”
“Sawa mkuu”
Meja akatoka ofisi humu na kutuacha na Yemi. Nikaanza kusikia kilio cha Yemi kwa sauti ya chini, kadri muda ulivyo zidi kwenda ndivo jinsi alivyo zidisha kulia kwa sauti.
“Mke wangu”
Nilizungumza kwa sauti iliyo jaa majonzi huku nikinyanyuka kwenye kiti changu, nikamnyanyua Yemi kweye kiti alicho kali na kumkumbatia kwa mara nyingine.
“Mke wangu nitahakikisha  kwamba ninamleta mwanao nyumbani sawa”
“Kivipi Dany hembu tazama, tazama mwanangu sasa hivi yupo ikulu ya hao mashetani, hivi kweli mwanangu atarudi jamani?”
Yemi aliendelea kuzungumza huku akilia kwa uchungu.
“Atarudi mke wangu mimi ndio ninaye kuahidi, nitahakikisha kwamba anarudi”
Niliendelea kumfariji Yemi hadi akapungumza kulia kwa uchungu, alipo maliza nikamuomba akae kwenye kiti, nikachukua faili mezani alilo niletea Martin, nikambusu Yemi kwenye paji la uso wake kisha nikatoka ofisini humu. Tukaanza kuongozan ana Martin hadi kwenye kiwanja kikubwa, nikawakuta wanajeshi wengi wakiwa wamesimama kwenye mistari iliyo nyooka vizuri.
“Muheshumiwa kila kitu kipo salama”
Meja alizungumza huku akinitazama usoni mwangu, nikawatazama wanajeshi hawa wanao nisubiria mimi kwa muda sasa, nisha taratibu nikasogelea sehemu yenye kipaza sauti huku Martin akisimama nyuma yangu. Nikaka kwa takribani dakika tano huku ninawatazama wanajeshi hawa, kichwa changu kusema kweli hakipo sawa. Usoni mwangu inanijia picha ya mtoto wa Yemi, kilio cha Yemi ninakisikia masikioni mwangu.
“Mkuu mbona kimya”
Martin alininong’onezaa kwa sauti ya chini.
“Ehee!!”
“Ipo kimya mkuu watu wanasubiria uzungumze kwa sasa”
“Sawa sawa”
Nikasha pumzi nyingi hadi ikasikika kwenye kipaza sauti kilicho wekwa mbele yangu. Nikanyoosha mkono wangu wa kulia juu huku nikiwa nimekunja ngumi.
“Bokoooo Haramuuuuu”
Wanajeshi wote wakaitikia kwa shangwem jambo lililo nipa ujasiri kidogo wa kuzungumza.
“Jana ilikuwa ni siku ndefu kwetu sote, nina imani wengi wenu mumeamka mukiwa na uchovu na kuchoka kwa namna moja ama nyingine. Tuliweza kumsindikiza mzee wetu katika nyumba yake ya milele, na pia tuliweza kuwapiga Wamarekani pamoja na jeshi la serikali la hapa Nigeria”
“Huu ni mwanzo mzuri katika uongozi wangu, mwanzo ambao nitahiji uende hivi hivi hadi pale mauiti yatakapo nichukia. Sipendi kuona damu ya hata mmoja wenu ina mwagika, yale mauaji yaliyo fanywa na raisi wa Tanzania, K2 siwezi kuyaacha yapite hivi hivi. Ni lazima na mimi nilipe kwa ubaya wake alio ufanya.”
“Jana tuliwaweza kuwazuia wavamizi wetu, ial tukumbuke ni lazima wavamizi wetu watajipanga na kurudi dhidi yetu. Ninacho waomba mukifanye, tuhakikishe kwamba tunajiandaa kwa lolote ambalo litajitokeza mbele yetu, nilazima tuhakishe tunakuwa ni kundi bora kama ilivyo kwa Al-quida”
Nikaka kimya huku nikifikiria niwaeleze juu ya kutekwa kwa mtoto wa Yemi ila nikajukuta nikijikataza mimi mwenyewe kuzungumzia jambo hilo.
“Ninaandaa mpango mzuri na viongozi wa juu, nitahakisha kwamba kila mwanajeshi anakuwa na gerentii ya maisha yeke na familia yake. Kila mwanajeshi nitahakikisha kwamba familia yake inapatiwa huduma nzuri kuanzia afya, malezi, na chakula.”
Wanajeshi wote wakashangilia na kunifanya nitabasamu.
“Mimi ni kijana mwenzenu ninaweza kuifanya kazi yoyote ambayo nyinyi munaweza kuifanya nitawaomba kama kuna wasaliti katikati ya hili jeshi basi waondoke mapema iwezekanavyo kwani sinto muonea huruma mtu ambaye ni msaliti, nitahakikisha kwamba anakufa mbele ya watu wengine kwa kupigwa risasi zisizo na idadi. Ninawatakia asubihi njema”
Baada ya kumaliza kuzungumza maneno hayo nikashuka kwenye jukwaa hil na kuwaacha wanajeshi wakinipigia makofi.
“Mkuu nimepata simu kutoka Urusi”
“Jamaa wanasemaje?”
“Wanaomba wazungumze nawe”
“Wapigie”
Nilizungumza na meja huku tukiendelea kutembea kurudi ofisi kwangu. Meja akapiga simu baada ya muda akanipatia simu yake na kunikabidhi.
“Ndio ndugu”
“Tumepata tatizo”
“Tatizo gani?”
“Mtu ambaye tulikuwa tunawasiliana naye kuweza kutupa maelekezo ndani ya ikulu ya Marekani amekamatwa na hivi sasa anahojiwa ili kuweza kutoa ushirikiano wa sisi kukamatwa”
“Nyinyi kwani mupo wapi?”
“Watu wangu wapo Marekani ila wanajiandaa kuondoka nchini hamo. Kwa hiyo ninahitaji kukuambia kwamba kazi uliyo tupa hatutoweza kuifanya kabisa. Samahani kwa hilo ndugu”
Nikabaki kimywa kwa sekunde kadhaa, huku nikiwa nimesimama, nikakata simu na kukabidhi meja simu yake.
“Hii kazi nitaifanya mimi mwenyewe, ninakuomba uniandalie usafiri ambao utanifikisha nchini Marekani kisiri pasipo mke wangu kujua wala serikali ya Marekani kufahamu.”
“Jene……”
“Meja fanya hivyo, hiyo ni amri na si ombi”
Nilizungumza kwa sauti nzito huku nikimtazama meja usoni mwake na kumfanya atingishe kichwa kukubaliana kwa kile nilicho kizungumza kwani hata akikataa hawezi kupinga maamuzi yangu kwani mimi ndio mkubwa wake wa kazi japo kiumri yeye ndio mkubwa.                                                                                                                                                  ITAENDELEA
“Haya sasa Dany anaingiza mzigoni mwenyewe, watu alio wapia dili mambo yamewashinda, je atafanikiwa kufika nchini Marekani. Usikose shemu inayo fwata ya story hii ya kusisimua.”
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )