Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, November 17, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 152 na 153 )

adv1

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA

Nilizungumza huku nikimkabidhi Martin magazine iliyo salia, kisha taratibu nikanyanyuka kutoka katika eneo hili nilipo jificha huku bastola yangu nikiwa nimeinyoosha kwa juu. Nikamuona Yemi akiwa amehishikiliwa na wanajeshi hawa wa Kimarekanani ambao idadi yao kwa haraka haraka inaweza kufika mia moja.
“Muachieni mke wangu, nipo tayari kujisalimisha mikononi mwenu”
Taratibu wakamuachi Yemi aliye anza kutembea kwa mwendo wa taratibu akija eneo hili nilipo, na mimi nikaanza kutembea kwa mwendo wa taratibu huku nikiwatazama wanajeshi hawa walio ninyooshea mitutu ya bunduki zao na endapo nitafanya kosa lolote wataniua mimi na Yemi jambo ambalo sihitaji litoke mbele ya macho yangu.
       
ENDELEA   
Tukakutana na Yemi katikati, akanitazama usoni mwangu huku machozi yakimwagika.
“Nenda”
Nilizungumza kwa sauti ya upole iliyo jaa simanzi ndani yake.
“Kwani nini umefanya hivi mume wangu?”
“Hakuna jinsi ya kufanya mke wangu nenda, nenda tafadhali”
Niliendelea kuzungumza kwa huzuni ila kwa msisitizo kidogo, Yemi hakuwa na ubishi zaidi ya kuazidi kusonga mbele hadi sehemua lipo jificha Martin. Nikasimama futi sita kutoka alipo simama mkuu huyu wa jeshi.
“Muacheni mke wangu na mlinzi wangu waondoke hili eneo”
“Usijali hatuwezi kuwagusa”
“Niahidini?”
“Waruhusu waondoke”
“Martin ondoka na shemeji yako”
Nilizungumza kwa sauti ya juu, nikageuka nyuma nikamuona Martin akinyanyuka sehemu hiyo, akamshika Yemi mkono aliye zidisha kulia kwa uchungu kwani ninaimani kwamba hawezi kwenda kuniona tena kwenye maisha yake.
“DANYYYYYYYYY”
Yemi alilia kwa uchungu sana huku Martina akiw ana kazi ya kumkimbiza kuelekea katika chumba tulicho ingilia. Nilipo hakikisha wameingia kwenye chumba hicho nikageuka mbele na kumtazama mkuu huyu wa jeshi. Wakaichukua bastola yangu na kunifunga pingu, za mikononi pamoja na nyororo ngumu na ndefu kiasi kwenye miguu yangu. Wanajeshi hawa wakaanza kunikimbiza mkuku mkuku hadi kwenye moja ya ndege ya kijeshi, wakangiza huku nikiwa katika ulinzi mkali sana. Wakaniingiza katika chumba kilicho tengenezwa na nondo ngumu, kisha wakakinga kwa nje. Mkuu wao akanisogelea huku akiwa ameshika simu mkononi mwake.
“Muheshimiwa raisi nimeweza kumpata Dany”
Nikasoma jina la mkuu huyu kwenye mfuko wa shati lake na kugundua kwamba anaitwa Josephat D.R
“Kama ulivvyo niagiza mkuu wangu, nitahakikisha ninamfikisha Marekani baada ya masaa machache na mke wake nimeagiza vijana wanakwenda kumuua na hawawezi kutoka mikononi mwetu”
Nilitamani kukata pingu hizi kwa hasira ila sina uwezo wala nguvu ya kufanya hivyo kwani sikutegemea kwamba hawa jamaa wanaweza kunisaliti na kwenda kinyume na makubaliano ambayo tumeyaweka kuhusiana na mke wangu pamoja na mlinzi wangu ambaye nina imani kwamba nimemuacha katika mazingira magumu sana.
“Malaya mkubwa wewe”
Nilijikuta nikitukana kwa hasira na kumfanya mkuu huyu kucheka kwa kejeli. Akaondoka huku simu yake akiwa ameishika mkononi mwake na ninaimani kwamba alikuwa anarekodi video. Ndege hii ya kijeshi ambayo ipo tofauti kabisa na ndege za abiria, kwani haina siti hata moja. Wanajeshi wakakaka kwenye mizigo iliyopo humu ndani, na taratibu ndege hii ikafungwa na nikasikia mlio wa injini ya ndege hii zikianza kuwashwa.
Moyoni mwangu nikajikuta nikianza kujilaumu kwa kuweza kufanya maamuzi ya kujiamini na kushindwa kumsikiliza meja ambaye kwa haraka haraka ni sawa na baba yangu. Hadi sasa hivi wala sielewi wanajeshi wangu wa Boko haramu wamekwamia wapi kwani hadi sasa hivi sijasikia shambulizi hata moja.
Hadi ndege ikapaa hewani hapa ndipo nikajikuta nikikata tamaa kabisa. Taratibu nikajikuta nikikaa chini huku machozi ya hasira yakinimiminika usoni mwangu. Sijajua kifo changu kinakwenda kuwa cha aina gani, kwani ni nimeweza kuwaua wanajeshi wengi wa Marekani hususani makomandoo wao ambao  waliwaagiza kwa ajili ya kunisaka mimi.
“Kazi nzuri”
Nilimsikia meja akizungumza na simu yake ya mkononi. Akasimama na kunisogelea sehemu nilipo.
“Una habari?”
Aliniuliza kwa dharau huku akiwa ameinama, nikanyanyua uso wangu na kumtazama huku nikizidi kujawa na hasira.
“Kambi yako ya boko Haramu hadi sasa hivi ipo PUUUUUUUUUUUUU……!!”               
Maneno ya mwanajeshi huyu yakanifanya nisimame kwa haraka huku nikiwa nimeshikwa na mshangao mkubwa kwani kuondoka kwangu ninaimani kwamba kumeleta matatizo makubwa sana.
“Sasa hivi hakuna Boko Haramu, wala Boko njemaaa. Umepoteza Dany, wewe anza kusali sala yako ya mwisho kwani ukifika Marekani ni kunyongwaaaaa tuu”
“Krgahaaaaaaaaaaaaaaaa”
Nililia kwa hasira huku nikijaribu kuitoa mikono yangu nje ya hizi nondo huli nijaribu kumshika mkuu huyu wa jeshi hili la Wamarekani, ila sikuweza kumshika na alicho kifanya ni kurudi nyuma yangu kwa hatua chake akaviweka vidole vyake gumba kichwani mwake na kuchezesha vidole vyake vilivyo salia huku ulimi wake akiutoa nje, ishara ambayo ni kejeli kubwa sana juu yangu na ananizomea kwa kunidharau.
“Dany huna cha kufanya sasa, umefuliaa baba”
“Siwezi kufa kabla sijalipiza kisasi kwa wale walio nifanyia mabaya. Usijiingize kwenye vita ambayo haikuhusu kwa mana utakufa pasipo sababu ya msingi”
Nilizungumza kwa sauti nzito sana huku nikimtazama mwanajeshi huyu, akazungumza neno moja ambalo sikulielewa na kuwafanya wanajeshi wake wote kucheka kwa dharau sana.
“Huna njia ya kutokea Dany, tena muheshimiwa raisi anakusubiria kwa hamu sana”
“Nashukuru”
Nilijibu kwa upole wa kuigiza ila moyomi mwangu nimejawa na hasira moja kali sana. Mkuu wao huyu akarudi sehemu yake, akafungua begi dogo, akatoa laptop na kurudi sehemu nilipo, akafungua laptop hii na kuanza kuminya minya batani zake.
“Ninawasiliana na raisi moja kwamoja nina imani atafurahi kukutana na wewe”
Jamaa alizungumza huku akiwa ameishika laptop. Baada ya kufanya anacho kifanya akageuza laptop ussawa wangu huku akiwa amesimama mbele yangu. Nikamona raisi bwana Donald Bush akiwa amekaa kwenye kiti chake cha uraisi
“Muheshimiwa raisi nilihiji kukutumia video kukuambia kwamba nimemkamata Dany ila nikaona tuwasiliane moja kwa moja tukiwa tunaonana”
“Waoooo nimemuona, habari yako Dany”
“Mkuu pia nina habari mpya”
“Niambie tu”
Raisi alizungumza huku  akiwa amejawa na furaha sana.
“Hadi ninavyo zungumza hivi sasa ni kwamba kambi ya Boko Haramu imefumuliwa kisawa sawa na wanajeshi wetu”
“Kweli?”
“Ndio muheshimiwa raisi japo sijapata ripoti ya kukamatwa kwa mke wake”
“Ila vijana si uliwaagiza?”
“Ndio niliwagiza”
“Kwa sasa nipo kwenye Air Foce One ninaelekea Urusi hakikisheni mukimfikisha Marekani munamueka chini ya ulinzi hadi nitakapo rudi.”
“Sawa sawa mkuu”
“Ngoja mara moja, mke wangu njoo hapa uone kitu”
Nikaiona sura ya Hawa, ambaye baada ya kuniona mimi akaonekana kushangaa sana na kustuka. Raisi akambusu Hawa shavuni mwake.
“Nakupenda sana mke wangu”
“Ninakupenda pia mke wangu”
“Sajenti tutaonana Marekani baada ya siku mbili”
“Shukranu muheshimiwa raisi”
Mawasiliano haya kwa njia ya video kati ya raisi Donald Bush pamoja na Sajent Josephat yakaishia hapo, akaifunga laptop yake na kurudi kukaa kwenye sehemua lipo kuwa amekaa huku akiwa na tanasamu pana sana.                       
‘Lazima niwaue wote’
Nilizungumza hukku nikiwatazama wajeshi hawa kwa macho makali sana. Masaa yakazidi kusonga mbele, gafla kitu kizito kikasikika kikiipiga hii ndege na kuifanya kuyumba. Wanajeshi walio jiegesha kupata usingizi wakajikuta wakikurupuka kutoka kwenye usingizi.
Wanajeshi wote wakajikuta wakishika bunduki zao na kuwa makini sana. Hadi sasa hivi sielewi ni kitu gani kinacho endelea. Kishindo kingine kikasikika na hichi kikashinda hata kishindo cha kwanza. Mlango wa pembeni wa hii ndege ukang’ofolewa na kusababisha upepo mwingi sana kuingia ndani ya hii ndege. Wanajeshi ambao wamesimama kizembe zembe walijikuta wakivutwa nje na upepo huu amba una nguvu kubwa sana.
“Fungeni mikanda haraka”
Sajenti alizungumza na kuwafanya wanajeshi wengine wanao pambana kukaa vizuri kuwenye viti vyao kuhakikisha kwamba wanaifunga mikanda ya sehemu walizo kali.
Gafla hali ya hawa ndani ya hii ndege ikazidi kuwa nzito hii ni baada ya kuingizwa bomu dogo la gesi inayo fanya watu kumwagikwa na machozi. Ukungu mwingi ukatawala ndani ya hii ndege, nikasikia milio ya risasi na vilio vya wanajeshi wa Kimarekani hadi mimi mwenyewe nikajikuta nikichangayikiwa kwani hili shambulizi hadi sasa hivi sijui limefanywa na nani.
“Huyu hapa”
Nilisikia watu wakizungumza, kufuli nje ya kibanda hichi cha chumba likavunjwa kwa kupigwa risasi kadhaa. Kwa haraka nikavalishwa kifaa maalumu kichwani kwangu cha kuzuia kuivuta gesi hii ambayo inamnyong’onyeza mtu.
“Jenero Peter”
Mtu huyu anaye sumbuka kunifungua pingu za mikoni alizungumza
“Ndio ndio”
“Upo salama muheshimiwa”
Jamaa huyu akafanikiwa kufungua pingu za mikono yangu, kisha akafungu mnyororo nilio  fungwa miguuni mwangu.
“Ongozana nasi muheshimiwa”
“Nyinyi ni kina nani?”
Niliuliza kwa sauti ya juu kwa maana upepeo unao zidi kuingia ndani ya hii ndege unazimeza saiti zrtu kiraisi sana.
“Utanifahamu tu jenero, ongozana nami”
“Samahani ninaomba silaha yako”
Jamaa huyu bila ya kipingamizi akanikabidhi bastola yake, taratibu nikajikaza kutembea huku mku mkono moja nikishika sehemu ili nisianguke, nikafika hadi sehemu alipo kaa Sajenti Josephat, nikamkuta akiwa anaugulia maumivu ya risasi alizo pigwa mguuni mwake.
“Nilikuambiaa nitatokaa”
Nilizungumza huku nikimtazama jinsi anavyo pata shida ya kuupelekea mkono wake kwenye bastola yake iliyo angukia pembeni, ila hana ngungu ya kufanya hivyo.
“Nisalimie huko ulipo kuwa unahitaji kunipelekea”
“Malay……….”
Hakumalizia sentensi yake nikampiga risasi mbili za kichwa kisha nikamrudishia jamaa huyu batola yake, kisha akaniomba nisimame mbele yake akanikimbatia kwa nguvu na kujikunga mkanda ulio tufunga viunoni mwetu, akanikabidhi.
“Jenero nishikilie kisawa sawa”   
“Sawa”
“Moja, mbili, tatu”
Jamaa huyu akaruka pamoja na mimi, huku wezake wawil walitufwatia kwa nyuma. Tukaanza kwenda chini huku tumetanguliza vichwa vyetu jambo lililo niongopesa sana, ila nikajikausha kimya nisionekane muoga sana kwani mchezo huu ni mara ya pili sasa unajirudia kwenye maisha yangu na mara ya kwanza nilifanya nikiwa katika opareheni ya kwenda kuvamia kundi la Al-Shabab nchini Somalia.
Jama huyu wala sikujua amefanya nini, tukajikuta tumegeuka tu na kuanza kuanguliza miguu yetu, nikaanza kuona ndege nyingine ikiwa chini yetu.
“Tunatua juu ya hiyo ndege iandae miguu yako jenero”
Jamaa huyu alizungumza, na kujikuta nikijianda kwa tukio hili ambalo litatokea baada ya muda mfupi sana. Tukatua juu ya ndege hii, japo kuna upepo mwingi sana, ila huyu jamaa nina imani ana mafunzo makubwa sana kwenye hili analo lifanya, laiti kama ningekuwa peke yangu basi ni muda mwini sana ningekuwa nimesha kufa. 

Wezake wawili nao wakatua juu ya hii ndege inayo endelea kwenda. Kuna sehemu mbele yetu ikafunguka taratibu na tukaingia kwa pamoja ndani ya hii ndege huku jamaa hawa wawili wakifwatia na sehemu hii ikajifunga. Jaamaa akafungua mkanda alio nifunga kiunoni mwangu, kisha akavuaa vifaa maalumu vya kuzuia gesi. Nikabaki nikiwashangaa kwani wana asili ya Kimarekani. Nikavua na mimi huku nikiendelea kuwashangaa.
“Tunaomba utufwate”
Nikaanza kuwafwata huku tukitembea kwenye kordo ndefu ya hii ndege inayo onekena ni ya kifahari kwa maana hakuna hata abiri mmoja zaidi ya wahudumu wakike. Tukaingia kwenye moja ya chumba sikuamini macho yangu baada ya kukutana na meja wa Kimarekani ambaye alitokea kunipenda sana kwa kipindi nilipo kuwa kambini kwake nchini Somalia.
   
AISIIIII……….U KILL ME 153
“Meja”   
“Karibu sana rafiki yangu Dany”
“Asante sana meja”
Nilijikuta nikizungumza huku furaha kubw aikiwa imenitawala sana usoni mwangu. Tukakumbatia kwa sekunde kadhaa kisha tukaachiana.
“Pole sana kwa matatizo yaliyo kupata”
“Nashukuru sana”
“Naombeni mutuachie chumba”
Meja akawaambia wanajeshi wake hawa, wakatoka ndani ya chumba hichi na kutuacha wawili. Meja akanikaribisha kukaa kwenye sofa lilipo pembeni yangu.
“Mke wako pamoja na mlinzi wako hadi sasa ninavyo zungumza wapo salama”
“Kweli meja?”
“Asilimia mia moja na kwa sasa wapo kwenye ndege wakielekea visiwa vya Madagasca na huko tunawekukaa kwa muda wa siku kadhaa ili kujipanga upya katika hili jambo lililo jitokeza”
“Ninaweza kuwasiliana nao?”
“Yaa unaweza”
Meja akafungua laptop iliyopo mezani kisha akaanza kuminya minya batani baada ya muda kidogo akanigeuzia. Sikuamini macho yangu baada ya kumuona Yemi akiwa katika hali ya usalama, tukajikuta tukishindwa kuzungumza kwa muda na machozi yakaanza kutumwagika taratibu taratibu.
“Yemi”
“Ndio mume wangu……upo hai kweli?”
“Ndio mke wangu nipo hai”
“Tumesaidiwa na watu ambao wala hatuwajui mume wangu vipi wewe?”
Yemi alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Hao ni rafiki zangu mke wangu”
“Kweli mume wangu?”
“Ndio na kwa sasa wanawapeleka Madagascar, tutaonana huko kwa masaa kadhaa”
“Ohoo asante Mungu kwa kutuepusha na kifo kwa maana nilisha kata tamaa kabisa”
“Ni kweli mume wangu”
“Muambie mtoto naye atangana nasi Madagascar, kazi ya kumkomboa imesha kamilika”
Meja alizungumza na kunifanya nizidi kujawa na furaha.
“Dany ni nani huyo anaye zungumza?”
“Ni rafiki yangu, anasema mtoto wetu yupo salama salmini”
“Kweli?”
“Ndio mke wangu”
“Ohooo asante Mungu naomba nimsalimie”
Yemi alizungumza kwa furaha, nikaigeuza Laptop sehemu alipo kaa meja.
“Habari yako shemeji yangu”
“Salama shemeji yangu, yaani sijui hata niseme nini, umebadilisha giza kuwa mwanga kwenye maisha yetu na mume wangu. Yaani ninakushukuru sana Meja”
“Ni jukumu langu kuwasaidia nyinyi kwa manaa mume onewa katika hili”
“Kweli shemiji yangu, yaani nina rudia tena na kusema Mungu akubariki wewe na watu wako”
“Amen tutaonana Madagascar”
“Asante”
Meja akanigeuzia laptop, tukatazamana na Yemi laiti ingekuwa tupo karibu basi tungekumbatiana kwa furaha sana.
“Natamani kukuona hata sasa hivi mume wangu”
“Usijali mke wangu tutaonana hapo”
“Nakupenda sana mume wangu kuliko kitu chochote kwenye maisha yangu”
“Ninakuopenda pia mke wangu”
Tukamaliza kuagana na Yemi na kukata mawasiliano haya kwa njia ya kuonana.
“Mapenzi yenu yananikumbusha mbali sana, kipindi nilipo kuwa kikazi nje ya Marekani, nilikuwa ninazungumza hivyo na marehemu mke wangu, ila ndio hivyo yalitokea yakutokea kama nilivyo kueleza na sikuwa na jinsi ya kufanya tena”
Meja alizungumza kwa sauti ya unyonge kiasi. Nikabaki nikimtazama usoni mwake kwa haraka haraka anaonekana ni mtu ambaye bado anaishi na upendo wa mke wake hadi leo akiwa katika uzee wake.
“Kwa nini umeamua kunisaidia?”
“Nilijua tu utaniuliza swali hilo mara baada ya kufika hapa”
“Ndio kwa maana maisha yangu nilisha yatoa kwa ajili ya kufa, maisha yangu nilisha yaweka mikononi mwa Mungu wangu kwani nilisha tambua kwamba siwezi kufanikiwa kutoka mikononi mwa watu walio nisaliti”
“Hilo ndio lilinifanya nikusaidie, sipendi usaliti kwenye maisha yangu na wala sipendi mtu msaliti kwa sababu usaliti ulinifanya maisha yangu niishi pasipo mwanamke ninaye mpenda, kisa kazi yangu ambayo kwa sasa nimesha iacha nimeamua kuachana na maswala ya jeshi”
“Umeacha kazi!!?”
“Ndio nimeacha kazi na nimeamua kumiliki jeshi dogo la vijana wangu ambao niliwafundisha mambo mengi na wana ujuzi mkubwa kuliko hata wanajeshi waliomo ndani ya nchi yangu na ninaimani kwamba umeweza kushuhudia kazi walio ifanya”
“Ndio nimeshuhudia, yaani kila kitu walicho kifanya hadi sasa hivi ninahisi ni ndoto ambayo dijui yaani imeishaje ishaje?”
“Hahahaaa sio ndoto rafiki yangu. Raisi wetu aliamua kukusaliti isitoshe akamchukua mwanamke ambaye unampenda kwenye maisha yako japo uliamua kufanya mabadiliko ya moyo wako ila Hawa ulimpenda si kweli?”
“Ndio nilimpenda ila kwa sasa siwezi kufanya hivyo kwa maana amenisaliti sasa sijajua ni kitu gani amepewa na raisi huyo?”
“Raisi amekuwa akiiendesha serikali ya Marekani kwa ubinafsi sana, na hapa ninavyo kuambia ni kwamba amemuacha mke wake kwa ajili ya Hawa”
“Hilo ninalitambua na Hawa ndio alimshauri raisi kuweza kumuacha mke wake haraka iwezekanavyo”
“Dany unatakiwa kufanya kitu katika hili, huwezi kuwaacha waishi kwa amani, namna hiyo ikiwa tayari amesha haribu mfumo wako mzima wa jeshi ambalo liliweza kufwata sheria yako pasipo kipingamizi cha ina yoyote”
“Kweli meja nitahakikisha ninaishangaza dunia katika hili”
“Katika hilo nina imani kwamba utanisaidia kwa asilimi mia moja kwa maana ninahitaji kuiongoza Marekani, ninahitaji Marekani iwe mpya iwe na nguvu, na isiongozwe na raisi anaye sikiliza mawazo ya mwanamke ambaye ni ninaweza kumfananisha na Malaya na amemucha mwanamke ambaye tunamtambua kikatiba”
“Unahitaji kuwa raisi?”
“Ndio”
“Hilo wazo nimepewa ni mke wa raisi mama Donald Bush, mimi ndio mtu wa pekee ambaye aliweza kuniamini na kuniomba niweze  kumpindua mume wake kwa njia ya ina yoyote na nihakikishe kwamba ninaichukua nchi”
“Ila kumbuka kwamba nchi yako ni kubwa na utampindua kwa namna gani?”
“Hakuna njia nyingine zaidi ya kumuu”
“Na baada ya kumuua inchi itachukuliwa na makamu wa raisi ambaye ataongoza nchi hadi kwenye uchaguzi mkuu?”
“Ndio kwa sasa tumebakisha miaka miwili hadi kuufikia uchaguzi mkuu, miaka hiyo inanitosha sana kujitengenezea jina katika chama cha siasa na nafasi ya kuiongoza nchi ninayo kwa maana jeshi zima linanipenda na kuniheshimu na uzuri kwamba wanatambua mchango wangu katika kupambana na maswala makubwa ya kigaidi duniani. “
“Kama ni hivyo nitakusaidia katika hilo”
“Kwa nini na wewe usiiongoze Tanzaian?”
“Ahahaaa hapana sijafikiria kabisa kuwa mwanasiana, hivi unahisi hii sura ni nani anaye weza kuipenda na kuniona nikiwa ni raisi wa Tania”
“Mbona Godwin aliongoza Tania na alikuwa ni gaidi?”
“Tazama mwisho wake ulivyo kuwa mbaya, nikifanikiwa kumuua K2 basi nitaachana na kila jambo na nitakwenda kuishi mbali sana Afrika nikiwa na familia yangu”
“Sawa niwazo tu nilikupa”
“Nashukuru, ila muda unaweza kuamua  sijui”
Tukajikuta tukifurahi sana na Meja huyu. Safari ikachukua masaa kadhaa tukafanikiwa kufika nchini Madagascar, kitendo cha kushuka kwenye ndege hii, nikaingia kwenye gari ya kifahari pamoja na meja, kisha vijana wake wakiingia katika gari nyingine mbili ambazo zimeliweka gari letu katikati.
“Hii nchi ninaipenda sana ndio maana nikaamua kuja kujenga huku”
“Marekani una nyumba?”
“Ndio ninazo nyingine, Dany mimi ni bilioner japo huwa sipendi sana watu kuweza kufahamu wala nchi yangu kufahamu, ila utajiri wangu unaweza kufika hata dola bilioni kumi”
“Mmmmmm upo mbali sana”
“Yaa nina vijana wachache wa ulinzi binafsi na ninawalipa pesa nzuri sana”
“Utajiri huo uliupata wapi?”
“Kwa marehemu baba yangu na mama yangu, wao walikuwa mabilioner wa enzi hizo, na mimi nilikuwa mtoto wa pekee kwenye famili yao, ila kwa kipindi kile sikuweza kupenda kabisa maswala ya biashara na ndoto yangu kubwa ilikuwa ni kuja kuwa mwanajeshi na ndicho nilicho kifanya hadi kufikisha uzee wangu huu”
Tuliendelea kuzunugumza mambo mengi hadi tukafanikiwa kufika katika jumba kubwa la kifahari, hari zote zikakaguliwa getini na kuruhusiwa kuingia ndani.
“Karibu Dany hapa ndio nyumbani kwangu”
“Shukrani mzee umejitahidi sana?”
“Kidogo kidogo tu”
Tukashuka kwenye magari na kuanza kuingia ndani huku nikiwa nimeongozana na meja. Tukaingia sebleni na kumkuta Yemi na Martin wakiwa wamekaa. Yemi kwa haraka akasimama na kunikimbilia tukakumbatia kwa furaha huku tukinyonyana midogo yetu.
“Mmmmmm”
Meja alikohoa kidogo tukajikuta tukiachiana na Yemi na kumtazama.
“Karibuni sana hapa ni kwangu na mujisikie kama mupo nyumbani”
“Tunashukuru sana meja. Yemi kutana na meja huyu ni rafiki yangu ambaye yeye ndio ametupa msaada wote huu”
“Shukrani sana meja kwa msaada wako”
“Usijali, shemeji yangu”
“Meja huyu ni…..”
“Aahaa Dany unataka kunitambulisha shemeji yangu wakati ninamfahamu”
Meja alizungumza kwa utani na tukajikuta tukicheka sana. Ikanibidi kumtambulisha Martin kwa meja.
“Martin nimepata taarifa zako kwamba upo vizuri, uliwasumbua sana vijana wangu hadi kuweza kukuweka sawa”
“Hapana mkuu, nilikuwa ninafanya kazi yangu kumlinda mke wa mkuu”
“Kweli natambua huwa najua walinzi binafsi ni ngumu sana kuweza kumuelewa mtu tofauti na bosi wako. Ila Dany hapo umepata mtu muaminifu sana laiti ingekuwa ni mwengine basi mke na yeye sasa hivi wangekuwa wamesha kufa”
“Ni kweli”
“Jamani tupate chakula kwanza na mambo mengine yataendelea”
Meja alizungumza, tukakaribishwa mezani na wafanyakazi wake wa ndati, tukala chakula taratibu huku meja akiendelea kutusimulia mambo mengi ya maisha yake ya nyuma.
“Kweli ninawashauri Dany na Yemi kabla ya kufanya chochote kesho fungeni ndoa, tule tusherekee maisha yanasonga. Na yamebaki masaa machache sana kwa kijana wenu kuweza kufika nchini hapa”
“Ohoo sijui niseme nini shemeji, mimi nipo tayari kufunga ndoa hata sasa hivi?”
“Mchungaji tutampata wapi?”
“Dany wewe tatizo lako ni mchungaji au ndo, kama ni mchungaji hata kesho tunaweza kumleta hapa na ndoa ikafungwa, yaani ndoa yeni haitaji mashabiki, ni sisi sisi hapa tunahudhuria baada ya hapo ratiba nyingine zinafwata”
“Sawa hakuna tabu”
Baada ya kupata chakula, tukaonyeshwa chumba chetu huku Martin na yeye akikabidhiwa chumba chake. Kitendo cha kuingia ndani humu, tukajikuta tukivua nguo zetu haraka haraka na kubakiwa kama tulivyo zaliwa.
Nikaanza...
“Nipe mume wangu”   
..... taratibu nikamshusha Yemi huku sote tukimwagikwa na jasho jingi.
“Ninakupenda sana mume wangu, yaani kwao nimefika kwa raha hisi sidhani kama kuna mwanaume anaweza kunishawishi ili niwe naye”
“Wewe ndio mwanamke wa mwisho kwenye maisha yangu, nakupenda sana Yemi wangu”
“Nakupenda pia mume wangu”
Nikamnyanyua Yemi kwa nguvu na kuanza kumbeba na taratibu tukaingia bafuni, na kuanza kuoga, hatkuchukua muda mrefu sana tukamaliza na kutoka, huku tukuwa tumevaa mavazi maalumu tuliyo yakuta humu bafuni.
“Yaani kesho natamani haya ifike sasa hivi, yaani nitafurahi sana mwanangu akiwepo kwenye harusi yetu”
“Nina imani matatizo sasa yataisha, japo nina kazi ndogo ya kuikamilisha ila ikiisha hiyo nataka sisi na mtoto wetu tukaishi maisha mbali kabisa na Afrika”
“Wapi unataka twende tuishi?”
“Popote ili mradi tuondoke kwenye ardhi ya bara la Afrika kwa maana watu wake wame……”
Mlango ukagongwa taratibu, nikakatisha sentensi yangu, nikaanza kutembea hadi mlangoni, nikafungua na kumkuta meja akiwa amesimama, kwa ishara ikaniita.
“Mke wangu ninakuja”
Nilizungumza huku nikitoka na kuufunga mlango huu, tukatembea hatua kadhaa kutoka mlangoni.
“Dany kuna tatizo limejitokeza”
“Tatizo gani meja”
“Mtoto wenu amefariki kwa kuuwawa”
Mwili mzima nikahisi ukizizima kwa kupoteza nguvu, macho yakanitoka kwani taarifa hii kwangu ni nzito ila ninaweza kuihimili, ila sijuia Yemi mke wangu kama anaweza kuihimili taarifa isitoshe nimemuacha akiwa katika furaha kubwa sana ya kuifikiria ndoa yetu tuliyo panga kuifunga kesho.                                                                                          ITAENDELEA
“Haya sasa furaha imeingia shubiri, usikose sheemu inayo fwata ya kisa hichi cha kusisimua”
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )