Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, November 19, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 154 na 155 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
Nilizungumza huku nikitoka na kuufunga mlango huu, tukatembea hatua kadhaa kutoka mlangoni.
“Dany kuna tatizo limejitokeza”   
“Tatizo gani meja”
“Mtoto wenu amefariki kwa kuuwawa”
Mwili mzima nikahisi ukizizima kwa kupoteza nguvu, macho yakanitoka kwani taarifa hii kwangu ni nzito ila ninaweza kuihimili, ila sijuia Yemi mke wangu kama anaweza kuihimili taarifa isitoshe nimemuacha akiwa katika furaha kubwa sana ya kuifikiria ndoa yetu tuliyo panga kuifunga kesho.   

ENDELEA           
Ukimya ukatawala kati yetu mimi na Meja, nikajikuta nikiwa nimeshika na kigugumizi kizito kabisa, sijui hata nizungumze kitu gani.
“Walipo kuwa wanakuja huku wamevamiwa na watu wasio julikana njiani, yeye na watu wangu wawili walio kuwa wakimleta haku wameuwawa”
Nikahisi jasho likinimwagika mgongoni.
“Nimeagiza vijana wangu kuweza kufwatilia na kujua ni nani ambaye ameweza kuhusina na mauaji haya”
 
“Hapo meja unahisi atakuwa ni nani kama sio raisi Donald Bush, kwa maana huyu mtoto ndio alikuwa ni shabaha yake ya kuweza kunipata mimi na ameshindwa kunipata na amaemua kulipiza kwa mtoto”
“Majibu kamili Dany tutapata vijana wangu watakapo niletea taarifa?”
“Meja samahani ninakuomba hili niweze kulishuhulikia na liwe ni jambo la siri kati yangu mimi na wewe sihitaji Yemi kwa sasa aweze  kujua hili swala”
“Sawa itakuwa ni siri kwa sasa ila kulishuhulikia hili Dany, kwa sasa ni hatari tulia kwanza upumzike na mke wako hili swala     vijana wangu watalishuhulikia”
 
“Hapana meja hii ni vita yangu, vita inayo garimu maisha hadi ya vijana wako kwa ajili yangu, ninakuomba niimalizie hii vita ilipo fikia sasa hivi hata nikifa basi najua nitakufa kwa ajili ya kuitafuta haki ya moyo wangu. Tafadhali meja ninakuomba”
Nilizungumza kwa msisitizo huku machozi yakinilenga lenga usoni mwangu. Meja akanitazama kwa sekunde kadhaa, mlio wa simu ukamstua na akaitoa simu yake mfukoni na kuipokea.
“Ndio”
“Ipelekeni hospitali”
“Sawa”
Meja akaka simu na kunitazama.
“Miili ya marehemu wanaiepeleka hospitali sasa hivi, ikiwemo mwili wa mtoto wenu”
“Nahitaji kwenda kuiona tafadhali ninakuomba uniruhusu katika hilo”
 
“Sawa jiandea, ndani ya chumba chenu ndani ya kabati kuna suti ninaimani utazipenda”
“Shukrani meja”
Nikarudi chumbani na kumkuta Yemi akiwa amesimama mbele ya kioo huku akiweka mapozi kadhaa huku akiwa ameshika kiuno chake.
“Mume wangu kesho yaani nitatembea kimadoido kama hivi”
Yemi alizungumza na kuanza kutembea kama wanavyo tembea mamisi wakiwa majukwaani. Nikajitahidi kutabasamu kwani sihitaji Yemi kugundua ukweli unao endelea.
“Mke wangu umependeza ukitembea hivyo?”
“Asante sana mume wangu sasa na wewe inabidi nikufundishe mwendo wa kutembea kwenye harusi yetu sawa mume wangu”
 
Furaha aliyo nayo Yemi kusema kweli laiti akigundua kwamba mwanae amefariki sijui atakuwa katika hali gani kusema kweli.
“Njoo njoo mume wangu tuanze kutembea”
Yemi alizungumza hukua kinishika mkono, nikakubali kufanya hivyo, maumivu ninayo yapata moyoni mwangu kusema kweli hayana kipimo. Yemi akaanza kunifundisha kutembea taratibu, lengo langu ni kumfurahisha kwa muda kidogo ili niweze kumuaga kuondoka katike eneo hili.
“Mke wangu kuna sehemu nahitaji kwenda na meja mara moja”
Nilizungumza huku nikitabasamu nikihakikisha kwamba Yemi hawezi kuona utofauti wowote ambao nipo nao kwenye moyo wangu.
“Unakwenda wapi mume wangu?”
“Kuna baadhi ya vitu vya arusi anahitaji kwenda kunionyesha, mke wangu vitu vingine inabidi kukufanyia suprize usinifanye nivizungumzee”
“Mmmm jamani mume wangu wala hatujakaa sana”
“Mke wangu kuna zawadi nzuri sana ninakwenda kuitafuta”
“Zawadi gani?”
“Mmmmm mke wangu itakuwa ni suprize sawa”
“Haya mume wangu naamini ukija utamkuta mtoto wetu amesha fika”
 
Maeno ya Yemi bado kidogo yanimwage machozi ila nikaikuta nikitabasamu tu.
“Ndio, meja ameniambia kwenyeh hili kabati hapa kuna suti ngoja niangalie kwa maana ana nisubiria”
“Sawa mume wangu”
Nikatoa suti nyeusi ambayo ina kila kitu kuanzia tai hadi shati, nikaanza kuvaa kwa haraka, Yemi akanisaidia kunifunga tai hii. Nikamshika kidole cha shahada cha mkono wake wa kushoto nikakitazama kwa umakini.
“Nini mume wangu”
“Naangalia ni pete gani ambayo inaweza kukupendeza mke wangu”
“Yoyote mume wangu kikubwa ni upendo wangu mkubwa nilio kuwa nao kwako”
 
“Nashukuru kwa kunipenda mke wangu”
Nilizungumza kisha taartibu nikamkumbatia Yemi huku bado nikizidi kupata maumivu mengi moyoni mwangu.
“Haya nenda sasa mume wangu usije ukachelewa”
“Sawa mke wangu”
Nikarudia tena kumbusu Yemi kisha nikatoka chumbani humu, nikakutana na meja akinisubiria kwenye kordo. Moja kwa moja tukaelekea kwenye gari ambazo zimendaliwa tayari. Msafara wa gari mbili hizi ukaanza huku kwenye gari nikiwa nimejawa na mawazo mengi kichwnai mwake. Hatukuchukua muda mrefu tukafika kwenye moja ya hospitali kubwa, tukashuka na kupokelewa na mtu mmoja ambaye yupo chini ya meja.
“Wamejeruhiwa vibaya sana kwa risasi”
“Gari je?”
 
“Gari zipo sehemu ya tukio lilipo tokea polisi wanaendelea na uchunguzi”
“Kipindi munafika katika eneo la tukio waandishi wa habari walikuwa wamefika?”
“Hapana meja ila watu kadhaa ndio walikuwa wameanza kufika eneo la tukio”
“Wahusika mumeweza kuwajua?”
“Tunaongeza juhudi katika kuwafwatilia na ninaimani kwamba tukiwafahamu tutawashuhulikia”
Tukafika katika chumba cha kuhifadhia maiti, maiti ya kwanza kuonyeshwa ni mtoto wa Yemi ambaye nilimuona picha yake kwenye simu ya mama yake. Ni mtoto mzuri sana kisura japo ni wa kiume ila ni mzuri sana na amebarikiwa kuchukua sura ya mama yake.
“Ni kijana mdogo sana”   
Meja alizungumza huku akimtazama mtoto wa Yemi.
“Yaaa, kifo chake kipo mikononi mwangu”
 
“Hapana Dany, tumejitahidi kadri ya uwezo wetu ila waliweza kutuwahi?”
“Najua meja, ila ukweli ni kwamba huyu mtoto hakustahili kufa, ni lazima nifanye jambo kabla ya kumzika huyu mtoto”
“Vijana wangu wanaendelea kufwatilia wakipata muhusika basi tutajua ni kitu gani cha kufanya”
“Na Yemi nyumbani anasubiria kumuona mwanaye tutafanyeje katika hili?”
Meja akashusha pumzi nyingi huku akinitazama usoni mwangu.
“Tutatakiwa kutumia akili kubwa sana katika hili”
“Akili gani?”
“Mimi nitajua cha kumueleza nina imani ananiamini sana”
“Tujartibu katika hilo, ila sidhani kama harusi itafungwa kabla ya kumuona mwanaye”
 
“Kila jambo niachie mimi Dany”
“Mkuu tumepata sehemu ya wahusika ambao wamesababisha mauji ya watu wetu”
“Mume weza kuwafahamu ni watu wan chi gani?”
“Hapana mkuu ila tumeweza kufahamu ni wapi gari lao lilipo”
Kijana huyu wa kimarekani alizungumza na meja.
“Twende tukawavamie sasa hivi”
Nilizungumza huku nikimtazama meja usoni mwake.
“Dany……”
“Meja usinichukulie kama mgeni wa heshima ninaimani unaijua. Suti hii niliyo ivaa isinifanye nibadilike uahalisia wangu. Mimi nimefuzu mafunzo mengi ya kijeshi unajua niliweza kuiangusha kambi ya Al-Shabab na wewe ulishuhudia juhudi zangu nilizo zifaya. Tafadhali meja ninakuomba uniruhusu katika hili”
 
Nilizugumza huku machozi ya hasira yakinimwagika usoni mwangu, japo ni aibu mwanaume kulia mbele ya mwanaume mwenzake, ila kwangu sikuhitaji kulitilia maanani.
 
“Sawa Dany mpatie bastola”
Meja alimuambia kijana wake, akanikabidhi bastola nikaichomeka kiunoni mwake kisha tukatoka hapa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.
Safari ya kuelekea katika sehemu walipo jificha watu walio husika na kifo cha mototo wa Yemi ikaanza. Tukafanikiwa kufika katika jengo moja, tukawakuta vijana wengine wa meja wakiwa wamesha imarisha ulinzi wa kuingia katika eneo hili. Vijana wa meja wakaanza kutuonyesha ramani ya jengo hili kupitia laptop.
“Ndani ya jengo kuna watu sita na hao ndio walio weza kufanya mauaji mkuu”
“Hakikisheni kwamba tunawakamata wakiwa hai”
“Sawa mkuu”
 
Vijana wa meja wakaanza kusonga mbele huku mimi na meja pamoja na mlinzi wake mmoja tukibaki kwenye gari.
“Nahitaji kuingia ndani meje”
“Dany tulia nina waamini vijana wangu, nina uhakika watakwenda kukamilisha hii kazi kiumakini sana.”
“Sawa meja”
Vijana hawakuchukua muda sana wakatupa ishara ya sisi kuweza kuingia ndani, kwa haraka tukakimbilia ndani na kukuta kundi la vijana likiwa limewekwa chini ya ulinzi.
“Muna uhakika kwamba hawa ndio wamefanya mauaji?”
Meja alizungumza huku akiwatazama vijana hawa wa kiafrika, nyuso zao zinaonyesha kwamba hawana uwezo kabisa wa kufanya tukio ambalo wamelifanya.
 
“Ndio mkuu hawa ndio wa husika. Wana silaha za kutosha sana”
Nikachomoa bastola na kuvututa mmoja wa hawa kijana.
“Ni nani aliye waagiza?”
Nilizungumza kwa sauti nzito huku nikimtazama kijana huyu usoni mwake.
“Sijui unacho zungumza”
Kijana huyu alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake. Kwa taaluma yangu ya kuwafahamu watu nikajua kabisa kwamba huyu kijana ananidanganya. Nikampiga kwa kitako cha bastola hii kwenye sikio lake na kumfanya jamaa huyu akianguka chini na kulia kwa uchungu.
“Dany huyo hana la kuzungumza, vijana wenyewe hawa ninawaona kama wavuta bangi”
 
“Hapana meja wanatutania hawa. NINIANI ALIYE KUAGIZAAAA”
“Sijui mimi maisha yangu ya shida sifahamu ni kitu gani unacho kizungumza”
“Sioni sababu ya nyinyi kuishi”
Nikampiga risasi ya kichwa kina huyu nikamgeukia kijana wa pili naye nikampiga risasi ya kichwa pasipo kuwa na huruma ya aina yoyote. Nikampiga risasi kijana wa tatu, kabla sijampiga risasi kijana wa nne akaniomba nimsamehe kwani anakwenda kuzungumza ukweli.
“Nazungumza nazungumza ukweli”
“Ni nani aliye watuma”
“Ni madam”
“Madam madam gani?”
“Madam Hawa, mke wa raisi wa Marekani”
Meja akanitazama kwa macho ya mshangao, kwani sote hapa tunamfahamu vizuri Hawa kwani alikuwa ni msichana mwema sana kipindi nipo naye.
 
 AISIIIII……….U KILL ME 155

“Hawa, Hawa ndio alio waagiza?”   
Niliendelea kuwauliza kwa sauti ya ukali huku nikimtazama kijana huyu aliye toboa siri ambayo tayari imesha wagarimu wezake watatu uhai wao.
“Ndio, alitumbia kwamba tumue mtoto mara baada ya kufika hapa Madagascar”
“Alijuaje kama mtoto anakuja hapa Madagascar?”
“Sijui, sisi tulipewa kazi na tumeikamilisha mkuu”
Kijana huyu alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.
 
“Meja nina imani kuna mtu anatoboa siri katika hili”
“Nitalifanyia upelelezi wakimya kimya kuhakikisha kwamba ninamfahamu ni nani ambaye alitoboa siri katika hili”
“Nina ombi jengine meja”
“Ombi gani?”
“Ninaihitaji kwenda Mosscow Urusi”
“Mossow?”
“Ndio meje, sina muda wa kupoteza katika hili kwa maana raisi wa Marekanai hadi sasa ninavyo zungumza yupo inchini Urusi na nina imani kwamba hiyo ndio nafasi yangu ya pekee kwa mimi kuweza kumuaa Donald Bush pamoja na Hawa kwani siwezi kumsamehe katika hili alilo lifanya”
 
“Dany kumbuka ulinzi ambao umeimarishwa katika eneo hilo unalo taka kwenda ni mkubwa sana na kuna watu makini sana. Huto toka kabisa endapo utakwenda”
“Hilo kwangu sijalishi meja, hii ndio kazi yangu ya mwisho. Ninakuomba unipe baraka zako za mwisho”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama meja usoni mwake. Akaanza kutoka katika hichi chumba ambacho tayari tumeweza kugundua ukweli wa wahusika walio sababisha tukio la mauaji la mtoto wa Yemi.
“Meja najua hili  ambalo  ninakwenda kulifanya hata kwako litakuwa na nafasi kubwa, ninakuomba niweze kwenda kuifanya hii kazi sinto weza kukaa hapa na kuendelea kuyaona machozi ya Yemi yakimwagika mbele yangu na nikiwa sina msaada wowote kwake ikiwa mimi ndio nimepelekea matatizo haya yote kwa mwanae”
“Unahisi ni kwa nini Hawa amemua kufanya mauaji ya mtoto wa Yemi?”
 
“Meja ukiniuliza hivyo utakuwa unakosea kwa maana mimi na wewe sote tupo hapa na isitoshe walifahamu vipi kama mtoto anakuja Madagascar na hadi akauwawa hapa?”
Meja akakaa kimya kwa muda kisha akanishika bega la mkono wangu wa kushoto.
“Ninakuruhusu Dany katika hili ninajua ni mangapi ambayo yaliweza kukupata katika maisha yako na yote hayo yametokea kwa dhuluma na husda za watu walio kuzunguka. Ninakuomba hakikisha kwamba unakuwa hai kwa manaa bado hujamalizana na K2”
“Shukrani meja kwa kuligundua hilo”
“Yaa ninajua ni kitu gani ambacho kipo ndani ya moyo wako”
“Ninakuomba niondoke pasipo mke wangu kuweza kufahamu”
 
“Hapana Dany hilo linaweza kuwa kosa kubwa sana litakalo kugarimu kwenye maisha yako yote”
“Kivipi meja, kwa maana hii ni kazi ambayo ninatakiwa kuifanya kikamilifu”
“Ngoja kwanza nifwatilie leo kwamba raisi wa Marekani atakaa kwa muda gani Urusi kisha tutapanga mapango mzima wa mauaji yake na wewe ndio utayakamilisha kwa mkono wako wewe mwenyewe”
“Sawa meja”
“Maandalizi ya harusi yaendelee kama kawaida, jikaze kiume na mke wako asifahamu kitu chochote hii itabaku kuwa siri kati yangu mimi na wewe”
 
“Nimekuelewa”
“Mkuu”
Mmoja wa vijana wa meja alizungumza huku akifika katika eneo hili tulilo  simama.
“Ndio”
“Kuna hichi kitu unatakiwa kukiona hapa”
Jamaa huyu akamkabidhi meja simu aina ya iphone six, akatazama kwa muda kisha uso wake kidogo ukaonekana kujawa na tabasamu pana usoni mwake.
“Dany kazi yako nina imani itakuwa raisi sana”
“Kwa nini?”
“Baada ya siku mbili raisi Donald na mke wake wanaelekea nchini Tanania kwa ziara yasiku mbili na mwenyeji wao atakuwa ni raisi K2 na hii ni taarifa kutoka ikulu ya Marekani”
Meja akanikabidhi simu aliyo ishika, nikasoma maelezo haya yanayo onyesha ziara hii ya raisi Donald Bush pamoja na Mke wake.
 
Furaha ikaanza kutawala moyoni mwangu kwani kazi hii inakwenda kuwa raisi kwangu kwani ninaifahamu Tanzania vizuri sana kuliko hata nchi yoyote ambayo nimeweza kwenda.
“Tuelekee madukani sasa kutafuta pete ya mke wangu”
Nilizungumza kwa sauti iliyo jaa msisitizo, meja akakubaliana nami. Tukaondoka eneo hili, siku nzima hii tukaitumia katika kufanya manunuzi ya harusi ambayo itahudhuriwa na watu wachache sana ila ni harusi ya kifahari sana. Nikamnunulia Yemi pete ya dhahabu yenye garama kubwa sana, pamoja pia nikamnunulia na mkufu wenye thamani kubwa sana.
“Dany”
 
“Ndio meja”
“Nimeweza kukutana na vijana wengi, na nimefundisha vijana wengi ila sijawahi kuona kijana mwenye kipaji kama wewe”
“Kipaji cha nini meja?”
“Laiti ingekuwa ni mtu mwengine wa kawaida kawaida tu ambaye aliamua kuingia jeshi kwa ugumu wake wa maisha basi hadi sasa hivi sidhani kama angekuwa hai hapa duniani”
“Una maanisha nini kuzungumza hivyo meja?”
“Nina maanisha kwamba umepitia maisha magumu ambayo hata mimi na uzee huu sikuweza kuyaptia. Umeweza kuimili mikiki mikiki mingi sana kwenye haya maisha, ninakuomba sasa hakikisha kwamba unaimaliza hii kazi, hakikisha hawa watu watatu wanafia kwenye mikono yako. Chochote kitakacho tikea nipo nyuma yako nitakusaidia, iwe kifedha, kimali au hata kuyagarimu maisha yangu basi ninaweza kufanyaa hivyo”
 
Meja alizungumza kwa msisitizo huku tukiwa ndani ya gari tunarudi katika jumba la meja.
“Ninashukuru sana meja, natambua baada ya hii kazi dunia nzima itakuwa inanitafuta mimi”
“Hilo nitalifanyia uangalizi kikubwa ni kumuoa Yemi na kunza maisha yenu mapya mbali sana na Afrika”
“Sawa meja.”   
Tukafanikiwa kufika nyumbani salama salim, nikamkuta Yemi akiwa amekaa sebeleni pamoja na Martin anatazama filamu. Yemi akanifwata na kunikumbatia kwa furaha sana, akanipokea begi kubwa kiasi ambalo lina gauni lake la harusi pamoja na vitu kadhaa. Tukaelekea chumbani kwetu na akanza kufungua begi hili huku furaha ikiwa imemtawala sana.
 
“Waooooo mume wangu umejuaje kama ninapenda magauni ya aina hii”
Yemi alizungumza kwa furaha sana huku akililaza gauni hili kitanani.
“Yaani mume wangu umejuaje ninapenda magauni ya aina hii”
“Kweli?”
“Yaa kweli yaani hata kwenye mitindo yangu ninayo buni huwa ninajisikia furaha kuunda magauni ya aina hii, ngoja kwanza mbona kama lina chata ya kampuni yangu”
Yemi alizungumza huku akichukua kikaratasi kidogo na kukisoma
“Mume wangu ni kampuni yangu kumbe bidhaa zangu zinafika hadi huku”
“Yaaa, alafu wala sikujua nilipo kuwa ninanunua”
Furaha ya Yemi ikazidi kutawala baada ya kutoa pete mbili za ndoa ambazo tutavishana wakati wa kuoana siku ya kesho.
“Yaani mume wangu natamani hata ndoa yetu tufinge hata sasa hivi ili tuwe mume na mke”
 
“Usijali mke wangu, Mungu ni mwema kesho itafika kikubwa ni ulinzi wake”
“Amen, vipi umemuuliza shemeji juu ya safari ya mwanangu?”
“Yaa nilimuuliza ila kidogo ndege yake ilipata itilafu ikawabidi kutua nchini Senegal, kwa matengenezo zaidi”
Nilizungumza uongo huku nikifahamu kila kitu kinacho endelea
“Ahaaa, kwa nini sasa wasipande ndege nyigine ili mwanangu awahi”
“Kwa ajili ya usalama, si vizuri kwa mtoto kupanda ndege nyingine, kwa maana nina imani watakuwa wanafwatiliwa si unajua kwamba ametolewa mikononimwa Wamarekani ambao hawahitaji kushindwa na lolote”
“Kweli, ila akiwahi sawa asipo wahi pia sawa, kikubwa yupo salama”
 
“Ni kweli mke wangu. Jaribu basi gaini nione kama nimepatia kununua au laa”
Nilizungumza huku nikijaribu kujenga tabasamu  usoni mwangu, Yemi akaanza kuvua nguo alizo vaa kisha akavaa gauni hili, nikamsaidia kufunga kamba ndefu  zilizopo nyuma ya hili gauni. Kusema kweli sijakosea katika kuchagua gauni hili kwa maana limependeza sana Yemi.
“Yaani kama ulinijaribisha mume wangu, hujakosea kabisa”
“Yaa ila ni mali ya kampuni yako nina imani kwamba watakuwa wametengeneza mahususi kwa ajili yako”
“Ni kweli yaani natamani hata kualika marafiki zangu kuja kusherekea hii harusi yangu ila ndio hivyo ni ngumu, umehitaji iwe harusi ya watu wachache”
 
“Ni kweli mke wangu ila ulihitaji kuwaalia kina nani?”
“Ahaa hata tukisema tuwaalike, hawawezi kufika muda umesha kwenda. Ila kuna rafiki yangu mmoja ningetamani sana awepo kwenye harusi yangu sema nimepoteza mawasiliano naye”
“Anaitwa nani?”
“Hawa yaani huyo kipindi tunasoma tulipanga kualikana kwenye harusi zetu sema ndio hivyo maisha yameingiliana”
‘Laiti ungejua alicho kifanya Hawa wala usinge zungumza hivyo mke wangu’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikimtazama Yemi usoni mwake. Nikamvalisha mkufu  nilio mnunulia na kumfanya azidi kujawa na furaha.
“Mke wangu nina kuja mara moja”
“Unaenda wapi?”
“Kuzungumza na meja”
“Njoo unisaidie kufungua hivi vijikamba huku mgongoni”
Nikafanya kama alivyo niagiza Yemi, nikamfungua vimikanda vya hili gauni kisha nikatoka humu chumbani, nikamkuta meja akiwa amekaa sebleni na Martin wakiendelea kuzungumza  mambo mawili matatu.
 
“Meja ninakuomba”
Taratibu meja akasimama na kunifwata sehemu nilipo simama.
“Nimezungumzana na mke wangu, na nimemueleza kwamba ndege walio yapanda watu wako imeharibika na imetua nchini Segegal, ili kutia msisitizo zaidi katika hili ninakuomba umueleze hivyo na uwaambie kwamba ndege inaendelea kufanyiwa marekebisho na hawawezi kupanda ndege nyingine kwa ajili ya usalama na msako wanao ufanya Wamarekani”
“Hilo halina shida, ila anaonekana kuhisi chochote?”
“Hapana, ana furaha tu ya kujiandaa na harusi yetu”
 
“Sawa nimekuelewa, hapa nimekodisha hoteli moja ipo kwenye kisiwa cha pembeni na hapo ndipo ndipo itakapo fanyika harusi yenu”
“Meja mbona umeingia garama kubwa sana katika hili?”
“Dany ukiachilia mbali kwamba wewe ni rafiki yangu wa karibu, ila ni sawa na mwanangu, sina mtoto wa kuweza kumfanyia haya yote na isitoshe nina miliki kiasi kikubwa sana cha pesa, kwa hiyo hilo wala lisikumize kichwa”
“Ila meja kuna mambo mengine unanifanyia hadi najihisi aibu kwa manaa naona sina uwezo wa kufanya na mimi mwenyewe”
“Uwezo unao na ninajua kwamba una utajiri mkubwa sana wa baba yako ila bado hujauweka mikononi mwako”
“Unafahamu chochote kuhusiana na baba yangu?”
“Ndio nina fahamu mengi sana kuhusiana na familia yako, niliamua kufwatilia familia yako baada ya kuweza kukufahamu”
 
“Umegundua kitu gani kwa maana hadi dakika ya mwisho K2 aliniambia kwamba familia yangu ipo hai na yeye ndio mtu wa pekee ambaye anafahamu ni wapi familia yangu ilipo?”
“Hapana amekudanganya na yeye ndio muhusika mkuu wa mauaji ya famili yako na kikosi chake cha wasichana anacho kimiliki, ninakuhakikishia kwamba nitakwenda kukivunja siku si nyingi”
“Shukrani sana meja”
“Karibu tutazame filamu”
Meja alizungumza hukua kielekea kwenye sofa, nikaitazama filamu hiyo, ila kutokana si mpenzi sana wa kutazama filamu ikanibidi kuwaaga na kurudi chumbani. 
 
“Dany kusema kweli ninakupenda, ninakupenda kutoka moyoni mwangu. Sijui ni kwa nini nilishindwa kukufahamu siku zote za maisha yangu”
Yemi alizungumza huku akinifwata sehemu nilipo simama, akanikumbatia huku mikono yake akiiweka begani mwangu.
“Ninakupenda pia mke wangu, kila jambo linakuja na wakati wake. Kuna wakati wa furaha na wakati wa kulia, wakati wa kupata na wakati wa kupoteza, kwa hiyo kila kitu mke wangu kinakuja kwa mpango wa Mungu”
“Amen mume wangu, ila leo naona neo la Mungu lipo moyoni mwako au ndio harusi?”
Yemi alizungumza katika hali ya utani, nikajikuta nikicheka tu, nikamnyanyua taratibu na kuanza kumzungusha ili mradi nitengeneze furaha ambayo hato weza kunistukia au kustuka kama kuna jambo lolote baya ambalo linaendelea.
“Utaniangusha bwanaaaa Danyyyyy nishusheeee nahisi kizunguzunguuuu mwenziooo”
“Badooo”
Niliendelea kuzungumza huku nikiendelea kumzungusha Yemi, kisha tukajirusha kitandani huku sote tukiwa tumetawaliwa na furaha kubwa sana.
 
“Sijawahi kufurahi na mwanamke kwa namna hii, nina imani kwamba wewe ndio mke wangu sahihi”
“Kweli mume wangu?”
“Ndio mke wangu, yaani ninajisikia furaha sana kuwa nawe”
“Hata mimi mume wangu, ila ninaomba nikuulize swali?”
“Ni ulize tu mke wangu?”
“Mimi ni mwanake wa ngapi kwako?”
Swali la Yemi likanifanya nigune kimoyo moyo kwa maana nina mlolongo wa wasichana wengi ambao nilitembea nao, na laiti nikimjibu idadi kamili ya wasichana nilio tembea nao kimwili nina unakika kwamba ni lazima Yemi atapata wasiwasi na mimi.
 
“Mbona kimya mume wangu, wewe nijibu tu, kama mimi ni wa pili au watatu?”
‘Hata kwenye thelathini bora haupo’
Nilijibu kimoyo moyo huku nikimtazama Yemi usoni mwake.
“Wewe ni wa tatu?”
“Kweli mume wangu?”
Nilijikaza kujibu uongo kwa Yemi
“Ndio”
“Nakupenda, nakupenda, nakupenda sana mume wangu. Wewe ni mwanaume wa pili na utakuwa ni mwanamke wa mwisho kwenye maisha yangu”
 
“Asante mke wangu”
Siku hii ikatawaliwa na furaha, hadi tunaingia kitandani kulala furaha imetawala. Asubuhi na mapema, wasichana maalumu wanao shuhulika na maswala ya urembo wakafika katika jumba hili la meja na wakaanza kumshuhulikia Yemi. Na mimi nikaletewa kinyozi mmoja ambaye meja ameniambia yupo vizuri katika unyooaji nywele kwa wanaume.
Shamra shamra za harusi hii hazikumuacha nyuma Martin kijana wangu aliye bahatika kutoka mikononi mwa jeshi la Marekani ambao wameteketeza kambi nzima ya boko haramu. Martin ndio msimamizi wa harausi kwa upande wangu huku Yemi naye akiwa na msimamizi wa kike ambaye aliletwa na meja.
 
Tukatumie helicopter kuelekea katika kisiwa kidogo ambacho kina hoteli moja tu ya kufahari, tukafanikiwa kufika salama katika hoteli hii ambayo tumekuta umeandaliwa vizuri sana na ulinzi mkali wa vijana wa meja unaendelea kuimarishwa kila kona.
Wahuzuriaji wa harusi hii ni watu wachache sana ambao hawazidi hata kumi na wote wanaonekana ni matajiri wakubwa sana kwani ni marafiki wa meja. Mchungaji hakuwa na mahubiri marefu juu yetu alicho kifanya ni kuingia katika ibada ya kufungisha ndoa hii. Tukavishana pete na Yemi na kuwafanya watu wote kufurahia. Tukakumbatia kwa nguvu na Yemi huku kila mmoja akiwa amejawa na furaha kubwa sana. Gafla kipande kimoja cha goroa la hoteli hii kikalipuka kwa bomu jambo lililo wafanya walinzi wote wa meja kukimbilia katika eneo tulipo na kuanza kututoa katika eneo hili kwa haraka sana kwani hatujui ni nani ambaye amefanya shumbulizi hili.
 
ITAENDELEA
“Haya sasa harusi imeingia dosari furaha ya Dany na mkewe imakatishwa na mlipuko huo ambao hakuna anaye jua ni nani amesababisha, usikose shemu inayo fwata ya kisa hichi cha kusisimu”
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )