Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, November 27, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 162 na 163 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   

Lucy akanibusu mdomoni mwangu, hakuwajali walinzi wake, nikaingia ndani ya gari na kutoka katika hili eneo. Safari ya kuelekea posta ikaanza, cha kumshukuru Mungu usiku huu barabarani hakuna foleni ya magari, ikanichukua muda mchache sana kufika karibu kabisa na makao makuu ya  NSS, kitengo ambacho nilikitumikia kwa zaidi ya mikaa mitano na ninalitambu vizuri hili jengo kwani limejaa kamera nyingi za ulinzi(CCTV CAMERA).
‘Lazima niiingie humu ndani’   
Nilizungumza huku nikilitazama jengo hili lililo refu kwenda juu, kish taratibu nikashuka kwenye gari na kuanza kutembea kwa kujiamini nikielekea katika geti la kuingia gorofa hili ambapo kuna askari wa NSS wasio pungua watano na wana bunduki za moto pamoja na mbwa wakubwa wakali wenye uwezo wa kumrarua binadamu dakika chache pale watakapo pewa amri ya kufanya hivyo.
   
ENDELEA
Nikaiweka kofia yangu vizuri huku nikiishusha usawa ambao sio rahisi kwa mtu kuweza kuiona sura yangu vizuri. Taratibu nikajikuta nikipunguza mwendo wa hatu zangu baada ya kuuona mlinzi mmoja akinifwata huku ameshika bundiki yake mkononi.
“Habari yako kiongozi”   
Nilimsalimia mlinzi huyu anaye onekana kuwa makini sana katika kunitazama usoni mwangu.
“Unahitaji nini usiku wote huu?”
“Gari yangu kidogo imepata itilafu sasa nikaona niombe msaada wenu hapa kwenu”
“Unahisi hapa ni kwa fundi magari”
“Hapana kiongozi, nimeona niombe msaada”
“Anataka nini huyo?”
Mlinzi mmoja aliuliza huku akitutizama.
“Eti anahitaji msaada gari lake limeharibika”
“Anazingua hembu mpeleke mahala husika huyo”
“Twende huku”
Jamaa alizungumza huku akianza kuongoza mbele.
“Ahaa gari langu lipo kule!!” 
   
Nilizungumza huku  nikijifanya ninashangaa.
“Wewe twende huku”
Mlinzi huyu alizungumza, sikuwa na ujanja zaidi ya kumfwata kwa nyuma.
“Ingia hapo”
Mlimzi huyu alifungua mlango wa moja ya chumba ambacho kwa kukichungulia ndani kina maboksi mengi.
“Samahani mkuu, ila huku sipo nilipo kuwa nina pahitaji kwenda”
“Ingia bwana”
Jamaa huyu alifoka, kwa macho ya haraka nikatazama kamera za hili eneo nikaziona zimeelekea upande mwengine.
“Tena uvu……”
Sikumpa nafasi mlizi huyu ya kumalizia maneno yake. Nikamtandika ngumi kadhaa za shingo kisha nikamvutia ndani ya chumba hichi na kuufunga mlango. Nikamvunja mlinzi huyu shingo yake, nilipo hakikisha roho yake imeacha mwili, nikaanza kumvua nguo zake na kumuacha na nguo zake za ndani.
 
Nikavua nguo zangu nilizo ziva ana kwa haraka nikaanza kuvaa nguo zake, nikachukua maboksi kadhaa ambayo yana uzito kiasi na sikujua yana vitu gani ndani, nikayaweka juu ya mwili wa huyu  jamaa na kumficha na hata kama kuna mtu ataingia ndani ya hichi chumba basi hatoweza kumuona kirahisi.
Nikaivaa kofia yake vizuri kisha nikavaa na kitambulisho chake pamoja na bunduki yake, nikatoka humu chumbani, kisha nikaanza kuelekea getini walipo wezake huku kofia nikiiweka sawa usoni mwangu.
“Vipi umemuweka?”
Jamaa aliye zungumza mara ya kwanza alionge huku akinitazama.
 
“Ndio ndio”
Nilijitahidi kuiingia sauti ya jamaa niliye muua kwani kitu ambacho katika kikosi hichi cha NSS, ni udhaifu mkubwa ni juu ya askari wake kujuana kisura.
“Pombe zake zikimuishia asubuhi tutamuachia”
“Sawa”
Nikapita getini humu na kuanza kuelekea ndani na kuwaacha askari hawa wakiendelea kusimulia story wanazo zijua wao wenyewe. Nikaingia kwenye lifti na taratibu nikaanza kwenda juu, nilipo hakikisha nimefika katika gorofa husika nikatoka kwenye hii lifti na kwa kutumi kitambulisho cha jamaa niliye muua nikafanikiwa kufungua mlango wa kioo ulipo mbele yangu na kuingia kwenye ofisi hii yenye wafanya kazi wengi sana. Kitu ambacho hadi sasa hivi kinanishangaza ni kwa hawa watu kuto weza kunitambua kabisa, japo kofia imeficha sura yangu kiasi ila wameshindwa kabisa kufanya hivyo.
 
Nikatazama mandhari ya eneo hili nikaona chumba cha mahojiano, nikatembea kwa kijiamini hadi katika chumba hichi, nikafungua mlango na kuingia ndani.
“Habari”
Nilimsalimia mlinzi niliye mkuta mlangoni”
“Salama”
Nikamuona waziri mkuu pamoja na askari wengine wa hapa NSS wakiwa wamesimama katika moja ya kioo kikubwa huku Babyanka akiwa ameikunja mikono yake akifwatilia mazungumzo hayo kwa umakini mkubwa sana.
 
‘Hawa wameshindwa kunifahamu, ila Babyanka sidhani kama atashindwa kunifahamu’
Nilizungumza kimoyo huku nikianza kusonga mbele, nikafanikiwa kusimama nyuma ya moja ya askari, nikamuona Samweli jinsi anavyo endelea kupatiwa mateso makali na askari wawili walio shika vifaa maalumu vya mateso huku wakizidi kumlazimisha Erick kuzungumza ukweli wa kwa nini yupo nchini Tanzania.
“Zungumza ukweli ni nani aliye kuagizaa la sivyo tunakuua?”
Sauti ya ilisikika kutoka kwenye spika ndogo zilizopo katika hili eneo.
“Hahaahahaaaa………!! Kufaaa ni jambo la kawaida kwa kila binadamu ukiniua mimi leo kesho nawe pia utakufa”
Martin alizungumza kwa dharaua na kumfanya jamaa huyo aliye muuliza swali kumpiga ngumi ya shavu.
 
“Hakuna njia nyingine ya kumuhoji huyu mtu?”
Waziri mkuu alizungumza huku akimtazama Babyanka.
“Kusema kweli mkuu kila njia tumejaribu ila kusema kweli imeshindikana”
Babyanka alizungumza huku akiishusha mikono yake chini.
“Mchomeni sindano ya sumu afe anatupotezea muda”
“Mkuu”
“Nimesema mchomeni sindano ya sumu kwani kuna serikali itakuja kudai kifo chake na kama itajitokeza serikali itakayo dai kifo cha huyu gaidi basi hiyo ndio  itakuwa imemfuga gaidi Dany”
Waziri mkuu alizungumza kwa msisitizo huku akimtazama Babyanka usoni mwake.
“Sawa mkuu nimekuelewa”   
“Sasa hivi mchomeni sindano ya sumu ninahitaji kuona jinsi anayo kufa”
 
“Munamtaka Dany?”
Martin alizungumza na kuwafanya watu wote hum ndani kustuka na kumfanya hata waziri mkuu kumtazama Martin.
“Ndio seme yupo wapi?”
“Nitawaambia ni wapi alipo ila ni kwa masharti yafwatayo”
“Zungumza hayo masharti yako?”
“Kwanza ninahitaji miniachie huru, pili nahitaji raisi wenu afe”
“Shenzi shenzi kabisa, raisi wetu afe yeye ni nani?”
Waziri kuu alifoka huku akiingia ndani ya chumba cha mahojiano na mateso.
“Choma choma sindano ya sumu kabisa, anacheza na maisha ya raisi wetu”
Babyanka kwa haraka kapita mbele yangu, alipo fika kwenye mlango wa kuingilia katika chumba hicho akasita na kunigeukia na kunitazama kwa sekunde kadhaa.
 
“Nipe sindano nimchome mwenyewe”
Kelele za waziri mkuu zikamfanya Babyanka kugairi kunitazama, na kuingia ndani kumzuia waziri mkuu kuto kumuua Martin.
“Mkuu huyu anafahamu ni wapi Dany alipo na tukimtumia huyu tunaweza kumpata Dany kirahisi.”
“Sasa swala la raisi wetu kufa, anajua raisi wetu ni nani, anajua ana heshima gani kwetu ehee”
“Tunajua hilo muheshimiwa ila ombi lake la pili hatuto weza kulishushulikia”
“Munaraisi au muna gaidi, munahisi Dany ni gaidi ila si gaidi. Nani katika hichi chumba anajua kwamba raisi wenu aliiua familia ya Dany kwa kuwachinja hadi mtoto wake mchanga eheeee?”
Martin alizungumza huku machozi yakimtoka, waziri mkuu na Babyanka wote wakajikuta wakisitisha mazungumzo yao na kumtazama Martin.
 
“Nitakufa kwa ajili ya Dany, musipo niua leo basi siku nyingine zinazo kuja nitakufa na raisi wenu”
“Unazungumza nini wewe mshenzi?”
“Umenisikia muheshimiwa waziri mkuu na usijiingize kwenye vita hii kwa maana utakuf…….”
Waziri mkuu akampiga ngumi ya shavu Martina na kuwafanya jamaa walio kuwa wakimuhoji Martin kumshikilia wakimzuia.
“Njooeni mumtoe muheshimiwa”
Babyanka alizungumza kwa haraka nikaingia huku nikiwa nimeongozana na askari wengine tulio kuwa nje ya chuma hichi. Nikamtazama Martin kwa bahati nzuri macho yetu yakakutana, taratibu Martin akatabasamu kwa maana yeye ndio anaye nijua vizuri hata niwe katika muonekano wa namna gani.
“Wewe hembu vua kofia yako?”
Babyanka alizungumza huku akinitazama kwa macho makali. Kwa haraka sana, kwa kutumia kitako cha bunduki hii nikaanza kuwapiga askari nikio ongozana nao kuingia katika chumba hichi, jambo lilo mshangaza waziri mkuu na Babyanka. 
 
Babyanka akahitaji kutoa bastola yake kiunoni ila akajikuta akishindwa kufanya chochote kwani bunduki yangu tayari nimesha ielekeza kichwani mwa waziri mkuu. Jamaa hawa walio kuwa wanamuhoji Martin wote nao wakajikuta wakishindwa kufanya chochote, huku askari nilio wapiga kwa kitako cha bunduli wapo chini wamepoteza fahamu. Taratibu nikavua kofia yangu na kuwafanya wote mimacho yakiwatoka kwa kunishangaa, ni sawa mtu akakutana na yule asiye mpenda katika wakati ambao hajategemea kabisa kukutana naye.
“Mfungueni”
Nilitoa kali moja iliyo mfanya jamaa kutoa fungoa ya pingu mfukoni mwake na kumfungua Martina haraka sana kwani nina imani kwamba wote wanaijua historia yangu, na huwa nikizungumza mara moja sirudii mara ya pili. Martin akasimama taratibu huku akijinyoosha viungo vya mwili wake.
“Dany huyo hapo mkamateni sasa”
Martin alizungumza huku akiichomoa bastola ya Babyanka kiunoni mwake.
 
“Dogo vaa nguo za mmoja wapo hiyo ndio njia rahisi ya kutoka hapa”
“Sawa mkuu”
Kwa haraka Martin akaanza kuvua nguo zake kisha akamvuaa askari mmoja aliye lala chini akiugulia maumivu. Akazivaa nguo za askari huyo na watu wote ndani ya hichi chumba wanatazama kila kitu kinacho endelea kwani maisha ya mkuu wao yapo mikononi mwao kwani kosa moja kifo cha waziri mkuu kitakacho pelekea hata ugeni wa raisi Donald Bush kusitishwa.
“Wewe kum** umenipiga sana”
Martin alizungumza huku akimpiga jamaa mmoja aliye kuwa akimhoji, teke la tumbo na kumfanya jamaa huyo kuanguka chini hiku akigumia kwa maumivi. Akamtandika mateke mfululizo ya tumbo hadi jamaa akaanza kutapia damu mdomoni mwake.
“Kumbe  vinaume eheee”
“Oya dogo muda wa kuondoka sasa”
“Sasa hawa tunawaacha hai?”
“Usiwaue”
 
“Sawa mkuu”
“Sasa sikieni, sihitaji kuwaua wala sihitaji kua mtu wenu. Mzee utaniongoza kutoka humu ndani, na wewe Babyanka utaniongoza pia. Martin naomba kofia yangu”
Martin akaiokota kofia yangu na kunikabidhi.
“Martin”
“Naam”
“Walaze”
Kwa haraka Martina akaanza kuwashambulia walinzi walio ndani ya hichi chumba na wote akawazimisha. Nikaishusha bunduki yangu taratibu huku nikimtazama waziri mkuu jinsi anvyo tetemeka kwa woga mwingi.
“Twendeni”
Martina akawatazama askari hawa alio washambuli, wote wamezimia hata watu walio kuwa wanamuhoji nao wamezimia. Tukatoka katika chumba hichi huku waziri mkuu na Babyanka wakiwa wametangulia mbele kwa jinsi tunavyo tembea hakuna hata mfanyakazi ambaye anaweza kustuka kwa kwamba tumewatekea viongozi wao.
 
“Madam madam”
Dada mmoja alizungumza huku akimfwata Babyanka na mkononi mwake ameshika karatasi.
“Simama”
Nilizungumza kwa sauti ya chini na kumfanya Babyanka na waziri mkuu kusimama huku wakimtazama msichana huyu anaye tembea kwa haraka kufika hapa tulipo simama.
“Kuna simu kutoka kwa raisi”
“Niunganishe naye kwenye simu yangu ya mkononi”
“Sawa”
Tukaendelea kutembea kueleke kwenye lifti, taratibu tukaingia kwenye lifti na kuanza kushuka chini.
“Dany kwa nini unafanya hivi?”
“Kimya pokea simu ya raisi wako na weka loud speker”
Babyanka akatoa simu yake mfukoni na kuipokea na kufanya kama nilicho muambia.
“Ndio madam raisi”
“Mumefanikiwa kufahamu ni wapi Dany alipo?”
“Hapana madam ila tunaendelea kulishuhulikia”
“Si upo na waziri mkuu?”
 
“Ndio?”
“Mpatie simu”
Babyanka akampatia waziri mkuu simu akabaki akiwa ameishika huku mwili ukimtetemeka.
“Muheshimiwa raisi”
“Waziri mkuu nimepata picha inaonyesha Dany ameingia katika nyumba ya mwanao na kwa sasa walinzi wangu wamemshikilia binti yako kwa mahojiano zaidi kwa maana inaonyesha ana mahusiano mazuri na Dany, labda tunaweza kumtumia binti yako kumkamata Dany sawa waziri mkuu?”
Waziri mkuu akaka kimya huku mwili ukiendelea kumtetemeka kwa woga sana.
“Waziri mkuu”
“Nd……iiiiooo muheshimiwa raisi”
“Umenielewa nilicho kizungumza?”
“Ndi…oo madam raisi”
“Mbona unazungumza kwa wasiwasi mwingi vipi?”
Nikamkazia jicho kali waziri mkuu na kujikuta akiirudisha simu kwa Babyanka pasipo kujibu chochote kwani kuropoka kwake kunaweza kukawa mwisho wa maisha yake hapa duniani.
 
AISIIIII……….U KILL ME 163 

“Haloo”   
Niliisikia sauti ya K2 akizungumza kwenye hii simu hii ni baada ya kuona swali alilo muuliza waziri mkuu limekosa jibu.
“Samahani muheshimiwa raisi naona waziri mkuu amestuka kwa kusikia taarifa hiyo ya mwanaye kuwa kuhisika na kumuhifadhi Dany”
“Sawa basi akiwa sawa nitaomba kuzungumza naye”
“Sawa muheshimiwa raisi”
“Na mutakuwa munatakiwa kunijulisha kila kitu  kinacho endelea baada ya nusu saa”
“Sawa muheshimiwa raisi”
Babyanka akakata simu na kuirudisha mfukoni mwake huku akihema, taratibu lifti ikafunguka na tukaanza kutoka ndani ya lifti hii, iliyo fika chini kabisa ya ardhi ambapo kuna maegesho maalimu ya magari. Tukaingia kwenye moja ya gari huku Babyanka akiwa ndio dereva.
 
“Tunaelekea wapi?”
“Toka kwanza kwenye hili jengo”
“Ila Dany hili jambo unalo lifanya ni hatari sana kumteka waziri mkuu pamoja na mimi mkuu wa NSS”
“Hatari eheee?”
Nilizungumza huku nikiwa nimekaa siti ya pembeni huku  waziri mkuu akiwa amekaa siti ya nyuma pamoja na Martin. Babyanka hakuzungumza kitu chochote kwani tayari tumefika katika geti la kutoka katika jengo hili taratibu akafungua dirisha, mlinzi wa geti alipo muona ni bosi wake, akarusu geti kufungulia na tuokaondoka.
“Dany tunaelekea wapi?”
“Sehemu salama ni kwako”
“Kwangu unahisi kwamba utashindwa kukamatwa”
“Najua kuna kamera nyingi ila jambo la muhumu ni kuhakikisha kwamba kila kamera iliyo tegwa nyumbani kwako unaizima”
 
“Yaani siamini kama Dany umebadilika kiasi hichi, kwa nini lakini umekuwa muuaji, gaidi?”
Babyanka alizungumza kwa msisitizo huku akinitazama usoni mwangu. Sikumjibu kitu chochote zaidi ya kukaa kimya ukweli wa kila kitu kilicho tokea kwenye maisha yangu anakijua kwa asilimia kadhaa.
“Unaelekea wapi huku?”
Nilimuuliza Babyanka baada ya kumuona anaelekea sehemu nyingine ambayo ni tofauti na sehemu ninayo ifahamu ilipokuwa nyumba yake ambaye alipewa zawadi na raisi aloye pita madarakani.
“Ninaelekea nyumbani kwangu”
“Kwako?”
“Ndio ulihisi nitakuwa ninaishi kwenye nyumba ile ile?”
“Ukifanya makosa yoyote Babyanka nitakuu wewe na huyu mzee hapa”
“Sawa”
 
Tukaelekea tegeta na gari likasimama kwenye moja ya nyumba yenye uzio wa ukuta na geti kubwa, hatukumaliza hata sekunde mbili geti hili likafunguka, tukaingia kwenye eneo la hili nyumba ambayo ni ndogo kiasi, baada ya gari kusimama nikawa mtu wa kwanza kushuka ndani ya gari hili, niksihika bunduki yangu vizuri huku nikitazama eneo la hii nyumba, sikuona dalili  yoyote ya mtu, nikazunguka upande wa dereva na kwa ishara nikamruhusu Babyanka kushuka huku nikiwa nimenyooshea bunduki hii, taratibu Babyanka akashuka akashuka huku mikono yake ikiwa juu. Martin naye akashuka huku akiwa amemnyooshea waziri mkuu bunduki.
Nikiwa ninashangaa kuangalia kitendo cha Martin kuhakikisha kwamba waziri mkuu hafanyi jambo lolote nikastukia teke kali kwenye mikono yangu na bunduki niliyo ishika ikaangukia pembeni. Babyanka akanipiga teke la kifua lililo nirudisha nyuma kidogo ila nikajiweka sawa, Martin akahitaji kuingilia ili swala ila kwa ishara ya mkono nikamuzuia asiingilie hili swala.
Nikajiweka sawa huku nikimtazama Babyanka aliye kunja ngumi za mikono yake huku akiivuta juu kidogo suruali yake ya jinzi ambayo imembana kidogo.
 
Babyanka akaanza kunifwata kwa kasi huku akirusha ngumi ambazo nikaanza kuzizuia kwa mikono yangu, kwani hata mimi mwenyewe kwenye swala la kupigana nipo vizuri sana. Nilipo  ona mashambulizi ya Babyanka yamekuwa makali sana na nimechoka kuyazuia, ikanilazimu na mimi kuanza kujibu mashambulizi hayo kwa haraka kadri nilivyo weza. Uzuri ni kwamba ninamfahamu vizuri Babyanka na tulisha wahi kuwa walinzi wa raisi aliye pita madarakani na tulisha yatoa maisha yetu kwa ajili ya kumlinda raisi huyo ambaye mwisho wa siku alinisaliti kwa kufwata amri ya dada yake K2.
Nikajirusha hewani na kuvurumisha teke langu kwa kumguu wa kulia lililo mpiga Babyanka mabegani mwake na kumuangusha chini.
“Sihitaji kukua ila ukihitaji kukua, nitafanya hivyo”
Nilizungumza huku nikimtazama Babyanka akisimama huku akijiweka sawa mikono yake. Babyanka akajaribu kurusha teke ila nikalizuia hewani kwa teke lililo mfanya ayumbe kwani matarajio yaliyo yatarajia kwa teke lake yameenda tofauti kabisa. Nikamtazama mguu wake wa kulia ambao nimemzuia teka lake nikaona akiutingisha tingisha kuuweka sawa kwani nina imani ameumia kwa kiasi fulani.
 
“Babyanka acha hichi unacho taka kukifanya”
“Siwezi kuwa msaliti kwa ajili ya nchi yangu”
“Unahisi mimi ni msaliti wa hii nchi?”
“Wewe ni msaliti na nilazima nikuue”
“Usiingilie matatizo ambayo hayakuhusu wewe kuingilia”
“Kazi yangu ni kulinda viongozi wa nchi hii”
“Kulinda viongozi ambao hawahitaji kulindwa, viongozi  ambao wameweza kuitekeza familia yangu. Hembu funguka Babyanka utakufa bure, kufa kwa ajili ya vitu vya maana na si kufa kwa ajili ya watu wasio na maana yoyote”
“Siwezi kufwata maneno yako”
Babyanaka baada ya kumaliza kuzungumza maneno yake, akaanza kunishambulia tena. Sikuwa na jinsi zaidi ya kuanza kupigana naye kana kwamba ninapigana na mwanaume mwenzangu. Kila Babyanka alipo jaribu kunishambuli akajikuta akishindwa kabisa kunihimili kwani nimecharukwa na nina uwezo mkubwa sana kuliko yeye. Nikahakikisha  kwamba ninampiga Babyaka hadi mwili ukamlegea kabisa na kulala chini. 
 
“Mmmmmm”
Martin aliguna huku akimtazama Babyanka jinsi anavyo mwagikwa na damu mdomoni mwake.
“Wakistukia hili ni lazima wata itafuta simu ya huyu malaya”
Nilizungumza huku nikihema kwani shuhuli ya kumdhibiti Babyanka nayo sio ndogo.
“Ngoja nichukue simu yake”
“Hapana muangalie huyo mzee”
Nilizungumza huku nikimsogelea Babyanka, nikachuchumaa na kuanza kumpapasa mifukoni mwake, nikaitoa simu yake hata kabla sijasimama simu ya Babyanka ikaita na kuona namba inayo andikwa imeandikwa ‘Madam President’. Nikaitazama simu hii kwa umakini mkubwa kisha nikikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.
“Nusu saa limepita Babyanka mumefikia wapi?”
“Mbona unawasiwasi muheshimiwa raisi?”
Nilizungumza kwa sauti yangu ya asilia ambayo nina imani kwamba K2 anaifahamu vizuri sana.
 
“DANYYYY…….!!!!”
“Ninaimani utakuwa umeshangazwa na uwepo wangu karibu na vibaraka wako ulio wajaza sumu ya kunichukia mimi si ndio?”
“Mwanaharamu wewe ni nani aliye kupa ujasiri wa ku…kkuuu..uuu”
“Kufanyeje……? Unapatwa na kigugumizi ikiwa una mamia ya walinzi walio kulinda hapo ikulu. K2, ohooo samahani. Muheshimiwa raisi hili swala ukishirikisha walinzi wako nitahakikisha kwamba Babyanka na waziri mkuu wako wote maisha yao ninayaondoa kwa kuwaua kinyama sana na vifo vyao vitakuwa mikononi mwako”
Nilizungumza kwa msisitizo jambo ambalo nina imani kwamba linampa wasiwasi mkubwa K2, nikaweka simu hii loudspeaker ila sote tulipo hapa tuweze kumsikia muheshimiwa raisi K2.
“Dany unahisi kumua waziri mkuu na Babyanka vifo vyao vitakuwa na hasara kwangu, umekosea baba na nitahakikisha kwamba ninakuwinda hadi mwisho wa pumzi yangu”
 
“Unaniwinda ila tambua ya kwamba mimi ndio nitakuwa mtu wa mwisho kuweza kuikatisha pumzi yako na hapo ndipo nami nitakuwa radhi kuingia katika mikono ya hii serikali”
“Hahahahaaaaaaa…..ohoo Mungu wangu Dany unahisi wewe peke yako unaweza kupambana na maelfu ya wanajeshi nilio nao eheee?”
K2 alizungumza kwa dharau kubwa sana hadi waziri mkuu akashangaa. Taratibu nikasimama huku nikiendelea kumtazama Babyanka jinsi alivyo lala chini akiugulia muamivu kwani kipigo nilicho mpiga ni kipigo cha kumnyong’onyeza na si kumuua.
“Unatumia jeshi kulinda mauvo yako ya kumchinja mama yangu, kumchinja dada yangu, kumchinja mwanangu, kumchinja mama wa mwanangu eheee?”
“Yaaa niliwaua kuhakikisha kwamba unaijisikia maumivu ya ujinga wako ulio jaribu kuifanya mbele yangu. Kumbuka kwamba nilikuambia kwamba sisi ndio wenye nchi na nilikuahidi kukuonyesha na ndio nimekuonyesha sasa wewe waue tu huyu waziri mkuu na Babyanka na wala usihisi kwa kuwatumia hao nitasitisha uovu wangu kwako”
 
Simu ikakatwa taratibu nikamuona waziri mkuu akikaa chini huku akionekana haonekani kushangaa sana kwa kile alicho kisikia.
“Mwenye masikio haambiwi sikia mwenye macho haambiwi ona.”
Nilizungumza huku nikimnyanyua Babyanka chini alipo lala na nina imani kwamba amesikia kila kitu kinacho endelea.
“K2, K2, K2 mshenzi mkubwa weweee”
Waziri mkuu alizungumza huku akilia kwa uchungu. Nikafungua mlango wa gari siti ya nyuma na kumkalisha Babyanka.
“Huyu mzee vipi!!?”
Martin aliuliza huku akimtazama mzee huyu jinsi anavyo lalamika chini alipo kaa.
“Muache amesha elewa nchi yake inaenda vipi”
Nilizungumza huku nikiiokota bunduki yangu.
“Dany”
Babyanka aliniita kwa sauti ya upole. Nikamsogelea karibu alipo kaa kwa ajili ya kumsikiliza kitu anacho hitaji kukizungumza.
 
“Samahani”
“Kwa kipi?”
“Kwa hili lililo jitokeza”
“Ulikuwa unafanya kazi yako, sikulaumu katika hilo”
“Siamini kama K2 anahusika na kifo cha mama yako, alikuwa mwalimu wangu mzuri sana”
“Nashukuru kwa kuweza kusikia kwa masikio yako wewe mwenyewe. Je upo tayari kuungana nami?”
“Nipo tayari”
Babyanka alizungumza kisha akatema damu kidogo, nikamtazama waziri mkuu. Taratibu akanyanyuka huku Martin akiendelea kuwa makini naye.
“Mzee upo tayari kwa hili, kwa maana raisi wako haioni thamani yako. Je nikuue kama alivyo sema raisi wako kwamba kifo chako kwake hakina thamani”
Taratibu nikamuona waziri akipiga magoti chini huku akilia kwa uchungu. Taratibu akanishika miguu yangu huku akiniomba msamaha”
 
“Nisameheeeee”
Alizungumza huku akiendelea kulia.
Nikamnyanyua waziri mkuu huku nikimtazama usoni mwake.
“Nina imani mwanao Lucy yupo mikononi mwa K2 na ninakuambia kwamba hayupo salama, anaweza kumfanya chochote ili mradi mimi nijisalimishe, ili hayo yote yanaweza kwenda tofauti pale tu utakapo amua kuungana nami”
 
“Nipo tayari, nipo tayari”
Waziri mkuu alizungumza huku akinitazama usoni mwangu kwa macho yalio jaa uwekundu wa machozi yanayo endelea kumwagika usoni mwake.
“Dany eneo hili sio salama tena na nina imani kwamba NSS, wamepewa kazi ya kunitafuta na wakija kunipata hapa basi hata wewe utakuwa umekamatwa”
“Twendeni shambani kwangu”
Waziri mkuu alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Ni wapi?”
“Bagamoyo ndani ndani, sidhani kama huko kuna mtu anaweza kuja au kufahamu kwamba tupo huko”
“Hatuwezi kutumia gari hili tena”
Babyanka alizungumza kwa sauti ya upole huku akiwa ameinama.
“Tunaweza kupata gari lolote?”
“Lipo gari langu moja ni jipya kabisa nimelinini wiki  iliyo pita nina imani linaweza kutupeleka huko”
 
“Twende tukachukue funguo”
Nilizungumza huku nikimpa mkono Babyanka akaushika na taratibu tukaanza kutembea kuelekea ndani kwenye nyumba yake hii, akaniomba nitoe funguo chini ya kapeti, na nikafanya hivyo na kumkabidhi funguo. Moja kwa moja tukaelekea hadi chumbani kwake, Babyanka akachukau funguo kwenye droo ya dressing table yake.
“Unajisikiaje?”
Nilizungumza huku nikimtazama Babyanka usoni mwake.
“Najisikia maumivu kwenye mbavu na tumboni”
“Utakuwa umepata itilafu kidogo, ila utakaa sawa”
“Yaaa, hembu fungua hilo kabati la nguo”
“Kuna nini?”
“Kuna begi lina silaha”
Nikafungua kabati hili na kukuta begi kubwa jeusi, nikalitoa na kulibeba mkononi tukatoka humu ndani na kuifunga nyumba yake. Moja kwa moja tukaelekea nyuma ya nyumba hii ambapo kuna maegesho ya magari. Babyanka akanionyesha gari husika tukaingia ndani, ya hili gari na taratibu nikaliwasha gari hili na kuliweka sawa na kuanza kuelekea getini. 
 
“Magari yangu yote yana kifaa maalumu nilicho funga kwa chini, hayawezi kunadwa na rada wala satelaiti popote niendapo”
“Kwa nini umefunga kifaa hicho?”
“Niliamua tu kufunga kwa usalama wangu binafsi”
Waziri mkuu na Martin wakaingia ndani ya gari hili aina ya Toyota TX. Taratibu geti likafunguka nikaanza kutoa gari hili taratibu. Kabla hata sijakunja kona ya kuingia barabarani gari zipatazao nne kutoka katika kitengo cha NSS, nikaziona zikija kwa kasi jambo lililo nifanya nianze kufikiria kwa haraka ni kitu gani ninaweza kukifanya ili kuhakikisha kwamba ninawakimbia askari hawa wa kikosi cha NSS, mabao tayari wamesha gundua kwamba mkuu wao pamoja na waziri mkuu wapo mikononi mwangu jambo ambalo nina imani wanaamini kwamba ni hatari kwao.
 
 ITAENDELEA
“Haya sasa Babyanka na Waziri mkuu wameungana na Dany kuhakikisha kwamba wanamtoa madarakanni raisi K2 je umoja wao utadumu. Usikose sehemu inayo fwata ya hadi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )