Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, November 25, 2018

Ajali ya Mashua yaua Watu 30 Ziwa Victoria Uganda

Watu 30 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 40 wameokolewa baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama jana Jumamosi Novemba 24, 2018 katika Ziwa Victoria nchini Uganda.

Hata hivyo, polisi nchini Uganda wamesema kuna uwezekano idadi hiyo ikaongezeka hasa kutokana na idadi ya abiria waliokuwemo kwenye boti hiyo kutojulikana.

Msemaji wa polisi nchini humo, Emilian Kayima amesema kikosi cha uokoaji kinaendelea na operesheni ya uokoaji

Amesema hadi sasa haijafahamika kilichosababisha kuzama kwa boti hiyo.

Boti hiyo iliyokuwa na watu waliokuwa wanakwenda kwenye sherehe ilipata ajali katika kaunti ndogo ya Mpatta wilaya ya Mukono.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )