Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, November 10, 2018

Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Ataka Mashoga Wasitengwe

Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba mkoani Kagera, Desiderius Rwoma amekemea vitendo vya ushoga na kutaka wanaofanya dhambi hiyo wasitengwe na kubaguliwa badala yake wasaidiwe na kuonyeshwa ubaya wa wanachofanya.

Amesema kumvumilia mkosefu yeyote haina maana ya kumuunga mkono na kuwa ushoga ni dhambi na laana na watu wenye tabia hiyo wanahitaji msaada wa matibabu na huduma za kisaikolojia.

Katika mahubiri yake leo katika siku ya wanaume wa Jimbo Katoliki kwenye kanisa la Bikra Maria Mama wa Huruma, Askofu Rwoma ametaka uwepo wa sheria za kudhibiti vitendo vya ushoga.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )