Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, November 8, 2018

BREAKING: Mahakama Yaamuru Freeman Mbowe Akamatwe....Wakili wa Msigwa ajitoa

adv1
Wakili Jamhuri Johnson, anayemtetea Mchungaji Peter Msigwa, katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi tisa wa Chadema, ametangaza kujiondoa kumtetea kwa madai ya kutorishishwa na mwenendo wa kesi hiyo unavyoendeshwa.

Wakili Johnson ametangaza uamuzi huo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Alhamisi Novemba 8, mara baada ya upande wa mashtaka kumaliza kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.

Akitangaza kujitoa kumtetea Msigwa, wakili Johnson amedai haridhishwi na mwenendo wa kesi hiyo jinsi unavyoendeshwa.

Amedai kwa miaka 20 ya uwakili wake, hajawahi kuona kesi inaendeshwa kama inavyoendeshwa hiyo.

Awali, washtakiwa hao wamesomewa maelezo ya awali huku washtakiwa hao wakigoma kujibu lolote wakidai wakili wao hayupo.

Mdhamini wa Ester Matiko ameieleza Mahakama kuwa mshtakiwa amepata ziara ya kibunge na yuko nchini Burundi pamoja na kuwasilisha vielelezo ikiwamo tiketi ya ndege.

Mdhamini wa mshtakiwa wa kwanza, Freeman Mbowe, ameieleza mahakama kuwa bado yuko nje ya nchi kwa ajili ya matibabu.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimb amesema sababu za wadhamini wa washtakiwa hao kutofika mahakamani hazina msingi wowote na kwamba kwa maana hiyo ni sawa na washtakiwa wameruka dhamana.

Amesema vielelezo alivyowasilisha mdhamini wa Matiko ambaye ni mbunge wa Tarime Mjini, havina mashiko kwa sababu ni barua tu ya Katibu wa Bunge kumruhusu kusafiri.

Wakili Nchimbi amesema washtakiwa hao wako nje kwa dhamana na masharti maalum na kwamba kwa kuwa Bunge na Mahakama ni mihimili tofauti, basi barua hiyo ya Katibu wa Bunge haiwezi kuwa sababu ya kutohudhuria kesi yake.

Wakili Nchimbi ameiomba mahakama iamuru washtakiwa hao wakamatwe na wafikishwe mahakamani wajieleze ni kwa nini wasifutiwe dhamana.

Mbowe anadaiwa amekwenda kutibiwa nje ya nchi, jambo ambalo pia limeibua utata wa nchi alikokwenda kutibiwa kwa kuwa taarifa za awali kwa mujibu wa kumbukumbu za Mahakama, alidaiwa kwenda kutibiwa Afrika Kusini lakini leo mdhamini wake amedai amekwenda kutibiwa Dubai.

Mdhamini huyo alipoulizwa na Hakimu Wilbard Mashauri anayesikiliza kesi hiyo kuhusu taarifa za kutibiwa Afrika Kusini, alikana kuwa yeye hakusema hivyo.

Hakimu Mashauri alipombana kuwa kwa hiyo mara ya kwanza alitaja kuwa mshtakiwa amekwenda kutibiwa nchi gani, alisema yeye alieleza tu kuwa alisafirishwa kwenda kutibiwa nje ya nchi na alikuwa hajajua ni nchi gani na kwamba jana ndio alithibitisha ni Dubai.

Alipotakiwa kutoa vielelezo kuwa mshtakiwa huyo amekwenda kutibiwa hakuwa navyo na badala yake amesema mshtakiwa mwenyewe atakuja kuvitoa akirudi.

Hakimu Mashauri baada ya kusikiliza hoja hizoameamuaru wabunge hao wakamatwe na kufikishwa mahakamani kwa kukiuka masharti ya dhamana zao.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )