Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, November 23, 2018

Breaking News: Freeman Mbowe, Ester Matiko Wafutiwa Dhamana.... Sasa Kupelekwa Rumande

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu (DSM) imewafutia dhamana leo 23/11/2018, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Mbunge wa Bunda Mjini (CHADEMA) Ester Matiko kwa kukiuka masharti ya dhamana.

Uamuzi huo umetolewa leo asubuhi Novemba 23, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.

Akitoa uamuzi huo dhidi ya Mbowe na Matiko, Hakimu Mashauri amesema, kitendo cha washtakiwa hao kutokufika mahakamani bila ya kuwa na sababu za msingi ni kudharau amri za Mahakama kwa makusudi.

Akitoa uamuzi kuhusu mshtakiwa Mbowe, Hakimu Mashauri amesema, sababu zilizotolewa na mdhamini wake Novemba Mosi mwaka huu kuwa mshtakiwa huyo aliugua ghafla na kupelekwa nje ya nchi akiwa mahututi huku Wakili wake Peter Kibatala akieleza kuwa alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu si za kweli kwa sababu zinakinzana na taarifa alizotoa mshtakiwa mwenyewe.

Amesema, Mbowe katika maelezo yake alieleza kuwa alisafiri nchini Oktoba 28 mwaka huu kuelekea Washngton DC kuhudhuri mkutano wa Oktoba 30 na kwamba Oktoba 31, usiku alipotaka kusafiri kurejea nchini kwa ajili ya kesi hiyo iliyopangwa kuwepo Novemba Mosi, mwaka huu alishambuliwa na ugonjwa wa ghafla.

Alieleza kulingana na ugonjwa wake, madaktari waliokuwa wakimtibu, walimshauri asisafiri umbali mrefu kwa ndege lakini hata hivyo hati yake ya kusafiria inaonesha alisafiri umbali mwingine mrefu kwa kwenda Marekani kwa ndege na kitu kinachoonyesha kwamba alikuwa anadharau amri za mahakama kwa makusudi kwa sababu amezungumza mambo ya uongo.

Pia alisema licha ya Mbowe kueleza kuwa alitakiwa kupumzika, lakini nyaraka yake ya matibabu ilionesha kuwa Novemba 8, mwaka huu ndio alipata matibabu katika nchi za Falme za Kiarabu nchini Dubai, wakati akijua alitakiwa kufika mahakamani.

"Haiingii akilini kwamba daktari alizuia mshitakiwa kuruka na ndege kutokana na ugonjwa wake lakini aliweza kwenda Ubelgiji ambako alikaa kuanzia Novemba Mosi hadi 6, mwaka huu na kusafiri tena kwenda Dubai kwa ajili ya matibabu," alisema Hakimu Mashauri.

Akitoa uamuzi kuhusu Matiko, Hakimu Mashauri amesema nchi yetu inaongozwa na sheria na sheria inamtaka mshitakiwa akikabiliwa na makosa ya jinai pamoja na vyeo vyao bado wanatakiwa kuwepo mahakamani.

Amesema maelezo aliyoyatoa mshitakiwa kwanini asifutiwe dhamana hayakidhi matakwa ya yeye kushindwa kuhudhuria mahakamani na wanaleta dharau.

"Mahakama imeamua kuwa mshitakiwa wa kwanza na wa tano (Mbowe na Matiko), dhamana yao imefutwa," alisema.

Baada ya uamuzi huo wakili Kibatala alitoa taarifa kwa kuieleza mahakama kuwa wataukatia rufaa uamuzi huo Mahakama Kuu na kudai kuwa hawapo tayari kuendelea na usikilizwaji wa ushahidi wa kesi hiyo kwa leo.


Hata hivyo, Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi aliiomba mahakama kutupilia mbali ombi la wakili Kibatala la kutaka kesi hiyo iharishwe kwa kuwa hoja zilizowasilishwa na wakili Kibatala za kuomba ahirisho zinakosa msingi wa kisheria na hata kiutaratibu.

Nchimbi alidai kuwa hoja hiyo kimsingi haina mashiko, na kuhusu kukata rufaa Mahakama imekwishatoa maamuzi kutokana na mwenendo wa Shauri hilo.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )