Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, November 30, 2018

Breaking News: Mahakama Kuu Yatupilia Mbali Mapingamizi Ya Serikali....Rufaa Ya Mbowe Kusikilizwa Saa Nane Mchana

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali pingamizi za serikali za kuzuia rufaa ya dhamana iliyokatwa na Mwenyekiti wa Chadema Mh.Freeman Mbowe na Esther Matiko isisikilizwe na hivyo imeamua kusikiliza rufaa hiyo leo saa nane mchana.

Mbowe, ambaye pia ni Mbunge wa Hai, sawa na Matiko wa Tarime Mjini, wamekata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam chini ya hati ya dharura wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Kisutu kuwafutia dhamana katika kesi ya jinai inayowakabili mahakamani hapo.

Walifutiwa dhamana na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, anayesikiliza kesi hiyo Novemba 23 kutokana na maombi ya upande wa mashtaka yaliyodai wameshindwa kuhudhuria mahakamani wakati kesi yao ilipopangwa kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali bila sababu za msingi.

Endelea Kuwa nasi
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )