Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, November 5, 2018

Bunge Kuanza Kesho Jumanne

Mkutano wa 13 wa Bunge utaanza kesho, huku miswada ya sheria mitano ikitarajiwa kusomwa kwa mara ya kwanza ikiwemo wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2018.

Spika wa Bunge, Job Ndugai  leo amesema miswada mingine ni wa maji na usafi wa mazingira, marekebisho ya sheria mbalimbali namba nne wa mwaka 2018, muswada wa mamlaka ya hali ya hewa wa mwaka 2018 na wa mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa nchi kavu.

"Pia kuna muswada wa sheria za huduma ndogo za fedha wa mwaka 2018 ambao utasomwa katika hatua zake zote. Hati ya dharura ya mheshimiwa Rais nimeshaipokea na kamati ya uongozi imeridhia kusomwa katika hatua zake zote," alisema.

Aidha, alisema wabunge wanne watakula kiapo kesho ambao wote ni wa CCM,  Thimotheo Mzava (Korogwe Vijijini), Mwita Waitara (Ukonga), Julias Kalanga (Monduli) na Zuberi Kuchauka (Liwale).

Alisema pia katika mkutano huo mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa mwaka 2019/20 utajadiliwa na sehemu kubwa mijadala itajikita katika mpango huo.

Ndugai aliongeza kuwa, maswali 125 yataulizwa na ya papo kwa waziri mkuu yatakuwa 16.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )