Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, November 14, 2018

Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lakabidhiwa rasmi Kiwanda cha Korosho cha Buko

adv1

Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) leo limekabidhiwa rasmi kiwanda cha kubangua korosho cha Buko kilichopo mkoani Lindi  tayari kwa kuanza kupokea na kubangua korosho.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku mbili baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli kutangaza kwamba Serikali itanunua korosho za wakulima.

Makabidhiano hayo yamefanyika kati ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi na Kanali Rajabu Mabele na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wa mkoa huo pamoja na mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) Adam Kamana.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kiwanda hicho, Kanali Mabele amesema wanaanza na tathmini kabla ya kuingia kwenye kazi rasmi.

“Tunafanya tathmini, nia yetu ni kukiboresha katika kiwango cha juu ili kuweza kutekeleza maelekezo ambayo ametoa mheshimiwa Rais ili kwenda na mwendo ambao anautaka yeye,” alisema Kanali Mabele.

Kuhusu ulinzi wa maghala ya korosho amesema ulishaanza kufanyika na  ulifanywa kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama kama alivyoagiza Rais John Magufuli.

“Tumefika pale kusaidiana na vyombo ambavyo vipo katika ulinzi wa maghala yote ambayo yako mkoa wa Lindi pamoja na mikoa mingine ambayo imetajwa,” alisema Kanali Mabele

Naye mwakilishi wa TADB, Adam Kamana amesema wakulima wamekuwa wakinyanyasika kwa muda mrefu na hata Serikali inapoweka viwanda vinakufa ili zao hilo lisafirishwe kwenda nje bila kubanguliwa.

“Katika mnyororo mzima wa mazao lazima tujifunze kutouza malighafi kutoka shambani, sasa mheshimiwa Rais ameliona ametoa agizo, tuko hapa tumeshaanza kutembea, benki ya kilimo tunatembea na wakulima Tanzania nzima tumekuja kutii agizao.”

Kuhusu suala la malipo amesema fedha tayari ipo na ana uhakika wakulima wataanza kulipwa kesho Alhamisi kwani rais amewatuma kununua korosho kwa bei ya Sh 3,300 kwa kilo.

“Tumekuja kwa kusema ukweli pesa tuko nayo iko kwenye system zetu zote, ipo benki ya kilimo hapa ninavyoongea hata tukiongea baadaye kuna kikosi kazi kitakuwa kinafanya kazi baada ya muda huu ili kuangalia utaratibu upi tuufuate kuwalipa wakulima.’’
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )