Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, November 21, 2018

Kilichoendelea Leo Mahakamani Katika Kesi ya Wema Sepetu

Upelelezi wa kesi inayomkabili mcheza filamu, Wema Sepetu katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu bado haujakamilika.

Hayo yameelezwa Leo Novemba 21 na Wakili wa Serikali Jenifer Masuri wakati kesi hiyo ilipotajwa mbele ya Hakimu Mkazi, Mwita Kasonde.

Wema alipanda kizimbani saa 3:30 asubuhi na kushuka kizimbani hapo saa 3:32 asubuhi.

Akiwa kizimbani hapo, wakili Masuri aliieleza mahakama kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa upelelezi wake bado haujakamilika.

Hivyo akaiomba mahakama iipangie tarehe nyingine ya kuitaja ili kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika ama la.

Baada ya wakili huyo kueleza hayo, Wakili wa Wema, Ruben Simwanza alidai kuwa hana pingamizi.

Hakimu Masonde baada ya kusikiliza Maelezo hayo aliiahirisha kesi hiyo hadi Desemba 12, mwaka huu.

Msanii huyo alipofikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza alitakiwa kutoweka video zinazohusiana na ngono wala Maneno yoyote yenye muelekeo huo katika mtandaoni wake wa kijamii wa Instagram

Mshtakiwa huyo alielezwa hayo na Hakimu Kasonde wakati akipatiwa masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja aliyesaini bondi ya Sh 10 milioni. Wema alifanikiwa kukamilisha masharti hayo ya dhamana na yupo nje.

Katika kesi hiyo Wema anadaiwa Oktoba 15, mwaka huu katika jiji la Dar es Salaam alichapisha video ya ngono na kusambaza katika mtandaoni wake wa kijamii wa Instagram.

Hata hivyo Wema baada ya kusomewa shtaka hilo alikana.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )