Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, November 1, 2018

Lowassa Akwama Kumuona Zitto Kabwe Polisi

adv1
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa amezuiwa kumuona kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe anayeshikiliwa na polisi tangu jana Oktoba 31, 2018.

Msaidizi wa waziri mkuu huyo wa zamani, Aboubakary Liongo amesema kuwa  leo Alhamisi Novemba Mosi, 2018 saa 9 Alasiri Lowassa alikwenda kumuona Zitto kutaka kujua hatima yake, kwani wako pamoja naye kuhakikisha haki inatendeka, lakini akaelezwa kuwa muda wa kumuona umeshapita.

Baada ya kufika kituoni hapo, msaidizi wa Lowassa alikwenda kuomba kibali cha kumuona Zitto lakini alielezwa kuwa muda umekwisha, ambapo Lowassa amenukuliwa akisema, “Huyu ni kiongozi mwenzetu huku upinzani lazima tushikamane kukabiliana na lolote lililo mbele yetu, tunahitaji kuwa kitu kimoja kuliko wakati mwingine wowote".

Zitto yupo kituo cha polisi Mburahati ambako amepelekwa leo  akitokea kituo cha Osterbay
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )