Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, November 8, 2018

Mfumuko Wa Bei Wa Taifa Umepungua Kwa Asilimia 3.2

adv1
Na.Alex Sonna,Dodoma
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetoa taarifa ya mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka unaoishia Oktoba, mwaka huu, umepungua hadi asilimia 3.2 kutoka 3.4 kwa mwaka unaoishia Septemba, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Makazi na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo,amesma kuwa kupungua huko kuna maanisha kwamba kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma imepungua.

Aidha Mkurugenzi huyo amesema kuwa hiyo inamanisha kuwa mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka unaoishia Oktoba mwaka huu, imepungua ukilingansiha na kazi iliyokuwe kwa mwaka unaoishia Septemba, mwaka huu.

“Mfumuko wa Bei wa Taifa unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi nchini,” amesema Bw.Kwesigabo

Hata hivyo amesema kuwa  kupungua kwa Mfumuko wa Bei ya Taifa kwa mwaka unaoishia Oktoba, mwaka huu, kumechangiwa hasa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa kipindi kinachoishia Oktoba, mwaka huu, ukilinganansiaha bei za Oktoba mwaka jana.

Kwesigabo amesema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Oktoba, mwaka huu, umepungua hadi asilimia 1.2 kutoka asilimia 2.0 ilivyokuwa Setptemba, mwaka huu.

Amezitaja baadhi ya bidhaa za chakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwezi Oktoba katika mwaka huu ni pamoja na mchele kwa asilimia 3.8.

Nyingine ni mahindi kwa asilimia 21.8, unga wa mahindi kwa asilimia 11.6, unga wa mtama kwa asilimia 5.1, unga wa muhogo kwa asilimia 14.1, maharage kwa asilimia 3.0, mihogo mibichi kwa asilimia 5.9, viazi vitamu kwa asilimia 2.1, migimbi kwa asilimia 23.2 na ndizi za kupika kwa asilimia 11.6.

Amesema hali ya Mfumuko wa Bei kwa bidhaa katika Nchi za Afrika Mashariki (EAC) unaonesha kwamba Kenya mfumuko wake wa bei kwa mwaka unaoishia Oktoba mwaka huu, umepungua hadi asilimia 5.53 kutoka 5.70 kwa mwaka unaoishia mwezi Septemba, mwaka huu.

Kwa upande wa nchi ya Uganda, mfumuko wa bei kwa mwaka unaoishia Oktoba, mwaka huu umepungua hadi asilimia 3.0 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka unaishia Setptemba, mwaka huu.

“Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ni taasisi ya Umma iliyoanzishwa kwa sheria ya takwimu ya mwaka 2015. Kwa mujibu wa sheria hiyo, NBS imepewa mamlaka ya kutoa, kusimamia na kuratibu upatikanaji wa takawimu rasmi nchini,” alisema.

Mkurugenzi amesema kuwa Takwimu hizo ni pamoja na takwimu za Mfumuko wa Bei kwa ajili ya matumizi ya serikali na wadau wa takwimu nchini.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )