Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, November 30, 2018

Mhadhiri Aliyesema Chuo Kikuu UDSM Kimekithiri Kwa Rushwa ya Ngono Aitwa Kuhojiwa

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Vicensia Shule ameitwa kwenye kamati ya maadili ya chuo hicho kuhojiwa leo Ijumaa, Novemba 30, 2018 mchana kuhusiana na taarifa yake aliyoitoa kwenye mtandao wa Twitter akimuomba Rais Dkt. John Magufuli kuingilia kati kukithiri kwa rushwa ya ngono chuoni hapo.

Kupitia mtandao wa Twitter, Vicensia aliandika;  "Baba @MagufuliJP umeingia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kufungua maktaba ya kisasa. Rushwa ya ngono imekithiri mno UDSM. Nilitamani nikupokee kwa bango langu ila ulinzi wako umenifanya ninyamae. Nasubiri kusikia toka kwako maana naamini wateule wako ni waadilifu watakwambia ukweli." 

Jana Alhamisi jioni aliandika kwenye Twitter kwamba amepigiwa simu na kutakiwa kufika mbele ya Kamati ya Maadili  UDSM.

"“My good people, a quick update. Leo Alhamisi 29 Nov jioni nimepigiwa simu kuitwa kwenye Kamati ya Maadili siku ya Ijumaa 30 Nov mchana. Nasubiri mwaliko rasmi kwa maandishi. For our dear sexual violence survivors, we are almost there, we will win, big time! #IStandWithDrShule,” 
Aliandika
Ingawa hakueleza ni rushwa ya aina gani iliyokithiri,  lakini katika  baadhi ya vyuo vikuu vingi kumekuwepo na tatizo la wahadhiri  kuwarubuni wanafunzi kwa rushwa ya ngono ili wawafaulishe na pindi wanapogoma hupigwa sup, carryover.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )