Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, November 24, 2018

Msemaji Mkuu wa Serikali: Miaka 3 ya JPM Imechagiza Mageuzi Katika Sekta ya Anga

Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli ndani ya miaka mitatu imeweza kuleta ukombozi katika sekta ya anga kwa lengo la kuchagiza mageuzi katika sekta hiyo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi wakati wa kipindi cha Morning Talk cha redio Ebony Fm Mjini Iringa.

Dkt. Abbasi amesema kuwa Rais Dkt. Magufuli amekuwa akitekeleza yale yote aliyoyaahidi ambapo mpaka sasa anaendelea kutekeleza aliyoyaahidi katika sekta ya anga.

"Mpaka sasa nchi yetu inandege tatu aina ya Bombadia na Dreamliner moja na pia mwezi Desemba tunaleta AIRBUS mbili ili kuendeleza na kuchagiza mageuzi katika sekta ya Anga" amefafanua Dkt. Abbasi.

Aidha, Dkt. Abbasi anaongeza kuwa "Leo hii Shirika letu la ndege limeongeza idadi ya abiria wanaotumia usafiri huo kwa mwezi kutoka 4000 hadi kufikia 36000".

Akizungumzia kuhusu Ujenzi wa Reli ya Kisasa unaoendelea, Dkt Abbasi amesema kuwa, kufikia mwaka 2019 Desemba kipande cha reli cha kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro kitakuwa kimekamilika na treni ya kwanza ya umeme itatoka Dar es Salaam kwenda Morogoro.

Vile vile Dkt. Abbasi amebainisha kuwa Serikali imeanzisha mfumo wa kuleta mbolea na baadhi ya pembejeo kwa pamoja ili kuweza kusaidia kupunguza gharama na kusaidia maendeleo katika sekta ya kilimo.

"Wakulima waendelee kufanya kazi katika maeneo yako kwani Serikali inafanyia kazi changamoto zote ikiwamo ya masoko kwa lengo la kusaidia maendeleo katika sekta hiyo muhimu kwa Watanzania" ameongeza Dkt. Abbasi.

Mbali na hayo Dkt. Abbasi amesema kuwa kwa sasa Serikali ipo katika hatua kubwa ya kujenga nchi kwa kusimamia utekelezaji wa miradi mbali mbali mikubwa ya maendeleo ikiwemo Mradi wa Kamuzalisha Umeme wa Stieglers.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )