Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, November 12, 2018

Msemaji wa Jeshi la Magereza: Lulu Michael Bado Ni Mfungwa

Msemaji wa Jeshi la Magereza, Amina Kavirondo, ametoa ufafanuzi juu ya kuachiwa huru kwa muigizaji Elizabeth Michael 'Lulu' ambaye inasemekana amemaliza hukumu ya kifungo chake, akisema kwamba Lulu bado ni mfungwa.

Msemaji huyo amesema kwamba utaratibu wa mfungwa yeyote anayemaliza kifungo chake lazima ufuatwe kwanza, ndipo aachiwe rasmi na Jeshi la Magereza, na ndipo anaweza kuwa huru na maisha yake.

“Taratibu nafikiri zinaeleweka, anakuwa bado ni mfungwa, na anapokuwa na kifungo hicho cha nje kuna taratibu zake, akimaliza basi kuna taratibu kama mfungwa yeyote, hata kama ni maarufu. Kile ambacho Lulu atafanyiwa ndicho atakachofanyiwa mfungwa mwingine yeyote, 'treatment' yetu ni sawa na wafungwa wengine," amesema.

"Kama hatukutangaza wakati wafungwa wengine wanatoka hata yeye hatutatangaza, na hakutakuwa na upendeleo, na mwenyewe anajua anatakiwa afanye nini, yule ni mfungwa kama wengine, hawezi kumaliza akaondokea kule kule”, ameongeza Amina Kavirondo.

Muigizaji huyo anatarajiwa kumaliza kifungo chake mwezi huu, baada ya kubadilishiwa hukumu kutokana na msamaha wa Rais na kupewa kifungo cha nje, kwa kesi ya mauji bila kukusudia iliyokuwa ikimkabili hapo awali, ambapo alihukumiwa miaka miwili jela.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )