Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi, ameeleza kukerwa na vitendo vya ushoga na kuwaagiza viongozi wa dini ya Kiislamu kupambana navyo.Mufti alisema hayo jana katika Baraza la Maulid lilifanyika kitaifa mjini Korogwe, mkoani Tanga.
Akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani
Jafo, ambaye alimwakilisha Rais John Magufuli kuhutubia baraza hilo, Mufti Zuber, akiwaagiza mashekhe wote
nchini kusimamia kwa makini kuhusu kupiga vita tabia ya ushoga kwa
kuwa inadhalilisha na ni dhambi kubwa kwa Mungu.
Aliwasisitiza viongozi hao wa dini kusimamia kwa makini kupiga vita suala
la ushoga.
Mufti alisema masheikh kote nchini wasimamie vita dhidi ya ushoga bila kuona aibu na kushirikiana na serikali kuhakikisha ushoga nchini haupati nafasi.
Mufti aliiomba serikali kuwaahidia katika vita dhidi ya ushoga ili kukinusuru kizazi cha vijana kisiharibiwe na ushoga.
Mufti aliiomba serikali kuwaahidia katika vita dhidi ya ushoga ili kukinusuru kizazi cha vijana kisiharibiwe na ushoga.
Aidha waislamu wameshauriwa kutumia muda wao katika kujadili masuala
yenye tija kwa waumini wao na taifa kwa ujumla badala ya kuendekeza
migogoro ambayo hatima yake ni kurudisha nyuma jitihada za kumcha Mungu na maendeleo kwa ujumla.
Hayo yalisemwa na Waziri Jafo
na kusisitiza kuwa msimamo wa serikali ni pamoja na kuhakikisha maadili yanalindwa na kwamba haitakuwa tayari kuruhusu vitendo vyenye kwenda kinyume cha msimamo huo.
Aidha, alisema suala la uadilifu ni moja ya ajenda za serikali ya
awamu ya sasa kwamba limetumika pia katika kusimamia rasilimali
fedha na kukusanya kodi, jambo alilolieleza kuwa limefanya kuwapo kwa
maendeleo makubwa kwa miaka mitatu.
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi
==>>... << BOFYA HAPA Kui Install>>
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )