Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, November 12, 2018

Nape Alianzisha Bungeni Kuhusu Korosho....Naibu Waziri Amtuliza

Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ameitaka Serikali kutoa majibu ni wapi zitapatikana fedha za kuchangia elimu mkoani Lindi ikiwa korosho hazijauzwa.

Nape ameuliza swali hilo bungeni leo Jumatatu Novemba 12, 2018 akisema yaliyotokea kwenye korosho yanajulikana.

"Mheshimiwa mwenyekiti, sisi mkoa wa Lindi tukikubaliana kukata Sh30 kwa kilo ya korosho ili kuchangia elimu na mwaka jana katika jimbo langu pekee zilipatikana zaidi Sh 400 milioni lakini yaliyotokea sote tunajua, je nini mkakati wa serikali katika hilo," amehoji Nape

Akijibu swali hilo ni vizuri Naibu Waziri TAMISEMI, Josephat Kandege amesema; "Nape tusubiri, najua unatamani korosho zinunuliwe, lakini vile ambavyo tulipanga viende kwenye maendeleo lazima viendelee"
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )