Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, November 23, 2018

Nikki wa Pili: Afande Sele Anaufahamu Mdomo

Msanii wa muziki Bongo, Nikki wa Pili amejibu madai ya Afande Sele kuwa kundi la Weusi lilishinda tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA) kwa vile ni Wachaga.

Nikki ameeleza kuwa Afande Sele anaeleza hayo kutokana ana ufahamu mdogo kuhusu kundi hlo kwa upande wa muziki. 

==>>Hiki ni kile alichoandika kwenye ukurasa wake wa Instagram;

"Afande anasema, Weusi tulipata tuzo za kili kwa sababu sisi ni Wachaga, Tuzo za kili kwa usiku mmoja zilikuwa na zaidi ya kategori 30. Ukisema labda kwa miaka mitatu ni tuzo 90....hapo karibuni 99% ya washindi sio wachaga.

"Hivyo ukisema uchaga ni kigezo inamaanisha huna ufahamu dhidi ya tuzo au una ufahamu mdogo, any way nikawaida ya binadamu kuwa na ufahamu mdogo.

"Kuhusu redio Weusi tumepigwa na kushika chati ya redio zote tanzania na hata za nje kama Mtv, trace, citizen nakadhalika, ukisema tunabebwa na redio moja pia, inamaanisha huna ufahamu mzuri juu ya weusi, so ni tatizo lile lile la ufahamu mdogo.

Hapa sijakujibu isije tafsirika vibaya, bali nimefanya uchambuzi wa mpangilio wa mawazo yako, uchambuzi unanionesha yamepangwa katika ufahamu mdogo."
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )