Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, November 1, 2018

Polisi wafanya upekuzi nyumbani kwa Zitto Kabwe

adv1
Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi Kinondoni limefanya upekuzi nyumbani kwa Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe.

Jebra Kambole, wakili wa mbunge huyo wa Kigoma Mjini amesema kuwa upekuzi huo umefanyika Masaki jijini hapa, nyumbani kwa mbunge huyo.

Jana  asubuhi Zitto alikamatwa na polisi akiwa nyumbani kwake na kupeleka katika Kituo cha polisi Oysterbay ambako alihojiwa kwa saa tatu na kuhamishiwa kituo kikuu cha polisi.

Kambole amesema baada ya mteja wake kupelekwa kituo kikuu cha polisi, hakulala hapo alihamishiwa kituo kingine kilichopo Mburahati ambako aliondolewa leo asubuhi na kurudishwa kituo cha polisi Oysterbay.

“Leo asubuhi mteja wangu aliongozana na polisi hadi nyumbani kwake Masaki kwa ajili ya kufanya upekuzi kisha akarudishwa kwenye kituo cha Oysterbay,” amesema.

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )