Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, November 10, 2018

Rais Magufuli Akagua Magari Ya Jeshi Yatakayosomba Korosho

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo Jumamosi, Novemba 10, 2018 amekagua magari ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kikosi cha Usafirishaji cha 95KJ.

Magari hayo yanaweza kutumika kubebea Korosho katika mikoa ya Kusini (Lindi na Mtwara) iwapo wanunuzi wa zao hilo hawatazinunua baada ya siku ya Jumatatu saa 10:00 kama alivyoagiza jana, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alitoa siku 4 kuanzia jana Ijumaa hadi Jumatatu, Novemba 12, kwa wanunuzi wote korosho kupeleka barua Ofisini kwake kuonyesha tani wanazohitaji, lini watazichukua.

Majaliwa alisema baada ya hapo hawatanunua tena korosho hizo, zaidi watafutiwa usajili wa ununuzi wa zao hilo.

Hii ni kutokana na sintofahamu kwenye minada ya zao hilo kuu la biashara Tanzania.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )