Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, November 2, 2018

Rais Magufuli Asema CCM hawakutaka amteue Dk. Bashiru Ally kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho

Rais  John Magufuli amesema kuna viongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao hawakutaka amteue Dk. Bashiru Ally kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho.

Amesema moja ya hoja ya viongozi hao ni kuwa msomi huyo alikuwa anadaiwa kuwa mwanachama wa Chama cha Wananchi (CUF).
 
Rais Magufuli aliyasema hayo jana wakati wa kongamano la Hali ya Uchumi na Siasa nchini lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi, wasomi, wanasiasa na viongozi wa dini.

Rais Magufuli alisema Dk. Bashiru alipigwa vita na wanachama wa CCM kupewa nafasi hiyo, lakini aliamua kumteua.

"Hata Dk. Bashiru Ally wakati namleta CCM, alipigwa vita sana na wanaCCM, wakasema huyu ni mwanachama wa chama cha CUF," Rais Magufuli alisema na kuongeza:

"Ndiyo nawaeleza ukweli, hali ilivyokuwa wakati wa kumteua Dk. Bashiru. Na mimi nikasema nataka mtu wa CUF wa namna hii aje CCM. CCM hao hao hawakutaka mabadiliko na palikuwa na 'ka-syndicate' (kikundi cha watu waliokubaliana kuungana kufanya jambo) fulani. Na ndiyo maana namshukuru huyu mwanaCUF kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kunisaidia kufanya kazi nzuri ndani ya chama."

Dk. Bashiru ambaye alikuwa mhadhiri wa sayansi ya siasa katika chuo hicho, aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Mei 29, mwaka huu, akichukua mikoba ya Abdulrahman Kinana aliyestaafu.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )