Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, November 8, 2018

Rais Magufuli Ashiriki Ibada Na Kutoa Heshima Za Mwisho Kwa Marehemu Mercy Anna Mengi

adv1
Rais  John Magufuli na mkewe Mama Janeth leo wameshiriki ibada ya kuuaga mwili wa aliyekuwa mke wa Dkt. Reginald Mengi, ambaye ni mmoja wa waanzilishi wa Makampuni ya IPP, Mama Mercy Anna Mengi,  katika Kanisa la Azania Front Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kuuaga mwili huo, Rais Magufuli amesema: “Ushuhuda uliotolewa hapa na waumini mbalimbali, nina hakika Mama Mercy Anna Mengi ni mtu ambaye alimpenda Mungu na alimtegemea Mungu, na nina uhakika Mungu atamsamehe dhambi alizonazo ili aweze kupumzika kwa amani.”

Kwa upande wake, Askofu wa Kanisa la Kiinjili na Kiluteri Tanzania (KKKT)  Dayosisi na Mashariki na Pwani, Askofu Alex Malasusa, amewataka watu waendelee kumuombea mama huyo ambaye alifariki dunia Oktoba 31 mwaka huu.

Akizungumza katika ibada maalum  kanisani hapo, ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa, Askofu Malasusa alinukuu neno la Biblia kutoka Paulo 4 mstari 13 hadi 14 na Paulo 5 mstari 1 hadi 2.

“Jambo kubwa na la maana kwetu sisi ni kuwa na uhakika kwa Mungu kwa kushika mapenzi yake, na hata katika hili tuyakubali mapenzi yake kama inavyosema sala yake, ili tuendelee kuishi kwa mapenzi yake.

“Mungu ameweka siri kubwa kwenye suala la kifo, hata sisi wachungaji Mungu ametuficha, ni siri yake yeye mwenyewe Mungu.  Niwaombe ndugu na jamaa tuendelee kujiweka karibu na yeye ili kila mtu afikie tamanio la kwenda mbinguni,” amesema Dkt Malasusa.

Mbali na Rais Magufuli, miongoni mwa viongozi wengine walioshiriki ibada hiyo ni Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mercy alifariki nchini Afrika Kusini ambapo alikuwa akipatiwa matibabu katika Hosptali ya Mediclinic Morningside ya Johannesburg.

Ibada hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam, ilianza majira ya saa sita mchana na kuongozwa na Askofu Malasusa akisaidiwa na Chadiel Luiza.

Mama Mengi atakumbukwa kama mmoja ya waanzilishi wa makampuni ya IPP ambayo inamiliki vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo EATV, EA Radio, ITV, NIPASHE, The Guardian, Radio One, na Capital Radio.

Mwili wake utasafirishwa hadi Machame, Moshi, kwa ajili ya maziko Jumamosi Novemba 10, 2018.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )