Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, November 1, 2018

Rais Magufuli: Sina mpango wa kutoa pesa kwa ajili ya katiba mpya

adv1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli amewataka watu wanaotegemea atoe pesa kwa ajili ya kukaa vikao kujadili masuala ya kubadilisha katiba ya nchi waache kwa sababu hana mpango wala hategemei kutoa pesa kwa ajili hiyo.

Amesema kwa wale wenye fedha wanaotaka kusaidia mpango huo wampatie ili akamalizie mradi wa kujenga reli mpya ya kisasa ya Stiegler’s Gorge.

Ameyasema hayo leo Alhamis Novemba Mosi  alipokuwa akizungumza na washiriki wa kongamano la kuijadili hali ya siasa na uchumi wa nchi lililojumuisha maprofesa na viongozi kutoka katika sekta mbalimbali za serikali na Jeshi, lililofanyika ukumbi wa Nkrumah katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Rais Magufuli amesema amekuwa akipata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali kuhusu kubadilisha Katiba mpya wasidhani hajui umuhimu wake ila kwa sasa hana pesa za kufanya hivyo.

“Sitegemei kutoa hela kwa ajili ya watu kwenda kujadili masuala ya kubadili katiba kama watu wana hizo hela watupe tukamalizie mradi wa Stieglers George,” amesema.

Rais Magufuli amesema hali ya uchumi ya nchi kwa sasa inakuwa kwa asilimia saba na  na Tanzania ni miongoni mwa nchi Tano za afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi na mambo yakienda kama yalivyo pangwa itaendeleakukuwa na atasimamia hili ili ikue zaidi ya hapa.

“Nchi yetu ilifika katika hatua  kubwa sana ya rushwa na ndiyo maana  niliamua kujipa kazi kubwa ya kutumbua majipu kwa sababu nilitaka kufikisha nchi sehemu nzuri pamoja na changamoto zake niliapa lazima tutafika tu.

“Katika mambo makubwa ya msingi ni lazima tuyasimamie kwa pamoja kama watanzania bila kujali itikadi zetu za kisiasa na vyama na tusikubali kutumiwa,”amesisistiza Magufuli.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )