Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, November 1, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 23

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA 
 Kabla sijamjibu kocha simu yake ikaingia meseji. Nikaa kimya huku nikimtazama kocha anavyo soma meseji hiyo. Akashusha pumzi huku akinikabidhi simu simu yake ili niisome meseji hiyo.
‘Shule haito husika kwa chochote kwenye swala la mshahara wako wa ukocha, malezi na matumizi ya timu yako la sivyo jiudhuru ukocha tumuachie huyu mpumbavu timu tuoneka kama ataweza kuiongoza. Bili ya hotelini, leo ndio itakuwa siku yenu ya mwisho kukaa, nimeisitisha na muthithubutu kurudisha miguu yenu kwenye hiyo hoteli sawa Robert’
“Kocha ni nani huyu?”
“Mwalimu mkuu wenu”
Nikajikuta nikiachia msunyo mkali sana kwani sijui ni kitu gani mwalimu mkuu huyu anakifikiria kwenye ufahamu wake wa akili hadi kuamua kumshinikiza kocha kuacha ufundishaji wa timu hii.

ENDELEA
“Usijali, nakuomba usimueleze mchezaji yoyote kuhusiana na hili swala. Ngoja niwasiliane na dada yangu ili aweze kushuhulika na hili swala”
“Sawa”
“Ila ushindi wowote utakao patikana asilimia hamsini itakuwa yangu na zifwatazazo zitakuwa kwa ajili ya timu na hakuna hata asilimia itakayo ingia kwenye akaunti ya shule umenielewa?”
“Nimekuelewa”
Tukaingia kwenye gari na nikakaa kwenye siti aliyo kaa Frenando.
“Vipo kocha anasemaje?”   
“Ngoja tutazungumza tukipata muda”
“Sawa”
 
Nikatoa simu yangu mfukoni na kuingiza namba ya dada Mery kisha nikampigia. Simu yake ikaanza kuita na baada ya muda kidogo ikapokelewa.
“Ethan”
“Naimbie dada yangu”
“Safi, nasikia upo kwenye kiosi cha timu ya shule yako”
“Ndio dada. Upo wapi?”
“Mimi ndio ninajiandaa kutoka hospitalini hapa. Vipi?”
“Kuna jambo moja nahitaji kukuomba unisaidie”
“Zungumza tu mdogo wangu”
“Nahitaji uniwekee oda kwenye hoteli nzuri, nina idadi ya wachezaji ishirini na mbii pamoja na kocha mmoja”
“Ahaa sawa hilo halina shida kuna la ziada?”
“Hapana ni hilo tu, ila hoteli iwe ya kimichezo, viwepo viwanja vya michezo”
“Sawa sawa, nimekuelewa ndani ya dakika tano nitakupatia jibu lako”
 
“Poa”
Nikakata simu kisha nikasimama katikati ya basi hili, wachezaji wezangu wote wakanitazama.
“Naomba tusikilizane ndugu zangu”
“Kunzia hivi tunavyo toka hivi sasa. Hatuto rudi kwenye hoteli hiyo. Moja ni kutokana na maswala ya usalama wetu kwani kwa tukio la jana nina imani kila mmoja wetu emekuwa ni mtu mwenye wasiwasi na mashaka. Tumeamua kutafuta hoteli nyingine kwa garama zangu, na kila huduma ambayo timu kama timu itahitaji basi nipo tayari kugaramia”
Wachezaji wezangu wote wakapiga makofi na kushangilia
“Ngoja niwaeleza kitu kimoja. Ninawapenda sana”
“Hata sisi tunakupenda kapteni”
“Tunakwenda kupambana na tuhakikishe kwamba tunashinda sawa jamani”
“Sawa”
 
Wachezaji walitikia na mmoja wao akianzisha nyingo za kushangilia. Gari likafurika kwa shangwe huku kila mchezaki akipata munkari wa kwenda kucheza mechi iliyopo mbele yetu. Simu yangu ikaanza kuita, nikaipokea kuiweka sikio la upande wa kuhosto huku na nikiziba sikio la upande wa kulia ili niweze kumsikiliza dada Mery atazungumza kitu gani.
“Mbona makelele?”
“Utawaweza wachezaji, niambie umefanikiwa?”
“Ndio nimefanikiwa kupata hoteli moja ila ipo nje ya mji, ina kila sifa ulizo zihitaji”
“Hembu nitumie picha zake”
“Sawa, mechi munaanza kucheza saa ngapi?”
“Mida ya saa kumi na moja jioni”
“Ahaa sawa, nitafanikiwa kuiwahi kwa maana hivi sasa ninaelekea kwenye hiyo hoteli na wamehitaji kulipwa dola elfu ishirini na tano kwa siku”
“Sawa hilo halina tatizo, kikubwa iangalie na kama ipo vizuri muambie muhasibu atoe pesa hiyo kwenye akaunti yangu”
“Poa”
 
“Vipi mama?”
“Yupo vizuri hapa anategemea kuangalia mechi yenu”
“Poa badae basi”
“Poa”
Nikakata simu na kuzisubiria picha za hoteli hiyo. Baada ya muda kidogo picha hizo zikaingia kwenye simu yangu, nikamuonyesha Frenando.
“Duu hapa pazuri kaka”
“Eti ehee?”
“Yaa hapa pazuri kuliko hata pale”
“Poa poa”
Tukafika katika uwanja mkubwa wa mpira wa Olympiastadion Berlin ambao ndio shuhuli za ufunguzi wa kombe hili zinafanyika. Uwanja huu unaingiza mashabiki zaidi ya 74,475 kwa wakati mmoja. Basi letu likasimama katika eneo maalumu na sikuamini macho yangu baada ya kukuta idadi kubwa ya mashabiki ambao ni watu wazima wakiwa wamekusanyika kuipoke timu yetu. Waandishi wa habari ambao ni wengi sana wakaendelea kupiga picha mbalimbali huku wengine wakirekodi kila kinacho endelea. Tukashuka hutu nikuwa tumevaa makoti ya jezi zetu za shule.
 
“Ethan Klopp, Ethan Klopp”
Baadhi ya waandishi wa habari waliniita kwa ajili ya mahojiano. Nikasimama na wakanizunguka huku wakiniwekea vinasa sauti karibu na mdomo wangu.
“Kwanza poleni sana kwa kile kilicho tokea kwa kocha wenu”
“Tunashukuru sana”
“Je mumejiandaaje kwa mechi ya leo pasipo kuwa na kocha mkuu”
“Mimi na wachezaji wezangu tumejiandaa vizuri sana na nina imani kwamba tutawapa mashabiki wetu kitu kizuri kile wanacho kitarajia kutoka kwetu”
 
“Nimepata habari ya chini ya kapeti, ni kweli shule imejitoa katika kuihudumia timu kutokana na tukio la kukosekana kocha mkuu?”
Nikaka kimya huku nikimtazama muandishi huyu, nikatabasamu kidogo.
“Hapana ni uongo mtu. Kama shule ingejitoa katika kuhudumia timu basi leo hii tusinge kuwepo hapa”
“Mbona kuna hii meseji hapa imetoka kwa mwalimu mkuu wako, alininitumia na kudhibitisha kwamba shule imekata huduma zote juu ya timu yenu?”
“Kwa mimi hilo sifahamu na sina maoni juu ya hilo”
“Je mutafanikiwa kushinda kwa mbinu za kocha msaidizi?”
“Kija kitu ni mipango. Asanteni”
 
Nikaanza kuondoka na wakaanza kunifwata ila wakazuiwa na askari wanao imaeisha ulinzi katika eneo hili. Tukaingia kwenye vyumba vya kubadilishia mazoezi na kukuta jezi zetu zikiwa zimepangwa vizuri kila mtu kwenye sehemi yake. Tukabadilisha nguo, zetu na kuvaa jezi hizi na viatu.
‘Ethan’
Niliisikia sauti ya Ethan mwenzangu, nikaangaza macho ndani ya chumba hichi ila sikuweza kumuona.
‘Upo wapi?’
‘Siwezi kujitokeza kwenye kundi hili la watu’
‘Vipi?’
‘Leo jitahidi kwani timu pinzani ina mikakati mizito dhidi yenu na inaweza kuwa moja njia ya kuwadhalilisha’
 
‘Kutudhalilisha tena?’
‘Ndio’
‘Kivipi?’
‘Mutakwenda uwanjani utajionea’
‘Unanipa presha rafiki yangu’
‘Usijali’
‘Ethan’
Ethan hakuitika na ukimya ukatawala ndani ya nafsi yangu. Nikaendelea kumtazama kocha jinsi anavyo endelea kupanga mipango yake ya jinsi gani tuweze kucheza.
“Hei mbona unaonekana kama huna raha?”
Frenando aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.
“Hakuna ninawazia tu mechi”
“Usiwaze sana, tunakwenda kuwafunga hawa wajinga”
“Nakuomba usiruhusu goli Frenando”
“Usijali kaka”
 
Tukaendelea kukaa ndani ya chumba chetu hichi, tukisubiria maonyesho kadhaa yaweza kumalizika uwanjani. Saa kumi na moja kasoro kumi tukatoka ndani ya chumba chetu cha michezo na kuelekea katika mlango wa kutokea. Wachezaji wengi wa shule hii kutoka Italy ni warefu na wana miili mkubwa kiasi cha kuwafanya baadhi ya wachezaji wezangu kujawa na hofo. 

Kama timu kapteni nikaka mbele ya mstari huku nuyuma yangu akinifwatia Frenando na wengineo. Kocha msaidizi na madaktari wa timu wakatangulia uwanjani. Refa na wasaidizi wake wawili, wakasimama mbele kabisa na ilipo timu saa kumi na moja kasoro tano tukaanza kutembea na kutoka uwanjani humu. Uwanja mzima umejaa mashabiki wengi sana na katika maisha yangu sijawahi kucheza mpira kwenye wingi wa mashabiki wengi kama hawa.
 
‘Ehhh Mungu nisaidie’
Nilizungumza huku mapigo ya moyo yakiniende kasi. Hata mimi mwenyewe wasiwasi mwingi umenijaa moyoni mwangu. Tukapanga mstari mmoja, na sisi kama wenyeji, tukaanza kuwapa mikono marefa kisha tukafwatia wachezaji wa timu pinzani. Kila mchezaji ninaye mtazama naona ananizidishia wasiwai mwingi san. Baada ya kuwamaliza kuwapa mikono wapinzani wezetu, nikawaita wachezaji wezengu na kukusanyika duara moja.
 
“Hei jamani hawa wana ukuwa tu wa miili ila nina imani tunakwenda kushinda sawa”
“Sawa kapteni”
“Kapteni tayari kule”
Mchezaji mmoja alizungumza huku huku akinionyesha sehemu walipo simama marefarii. Nikakimbilia katika eneo hilo na kukuana na kapteni wa timu pinzani. Refarii akatuonyesha shilingi yenye pande mbili huku akituomba kila mmoja achague upande wake.
“Kichwa”
Nilizungumza huku nikimtazama refa, akairusha shilingi hiyo juu kisha akaibana na viganja vyake. Kwa bahati timu yangu inaanzia upande wa mashariki mwa uwanja huku tukupeleka mashambulizi kaskazini mwa uwanja.
 
“Asante”
Nilizungumza huku tukibadilishan nembo za shule na mpinzani wangu. Tukawa marefarii mikono pamoja na wasaidizi wao na kwa ishara nikawaomba timu yangu tuelekee upande wa mashariki. Tukapiga picha ya pamoja na kila mchezaji akatawanyika upande wake huku mimi nikisimama peke yangu katikati ya uwanja nikiwa na mpira kwa ajili ya kuanzisha mpira huu. Refarii akatazama saa yake ya mkononi na ilipo timia saa kimi na moja kamii akapiga kipenga cha kuanzisha mpira. 

 Nikampigia Pilo na taratibu tukaanza mchezo huu huku wapinzani wetu wakitufwata kwa kasi, kwa bahati mbaya mchezaji mwezetu mmoja akapokonywa mpira. Wapinzani wezetu wakimbia kwa kasi kuelekea golini kwetu na mmoja wao akapige shuti moja kubwa sana, Frenando akajaribu kulifwata kwenye pembe ya goli, ila akashindwa kuuzuia kwa mkono mmoja na mpira ukaingia nyavuni.
 
Robo ya uwanja wakanyanyuka na kushangilia, nikatazama saa kubwa hapa uwanjani ndio kwanza ni dakika ya pili. Nikastuka mara baaya kuwana mabeki wakiwa wamemzunguka Frenando, kwa haraka nikakimbilia hadi golini na kumkuta Frenando akilia kwa uchungu huku akiwa ameshika kiganja cha mkono wake wa kulia. Nikamvua gloves ya mkono huo, kidole kimoja cha mwisho cha Frenando kimefunjika jambo ambalo ni pigo kubwa kwetu kwani ndio kipa tegemezi naninaye muamini. Refarii akafika eneo hili huku madaktari wetu nao wakifika wakaanza kumpa Frenando huduma ya kwanza.
 
“Siwezi kuendelea”
Frenando alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake, jambo lililo nifanya na mimi machozi kunilengea lenga usoni mwangu. Nikatazama nje ya uwanja na kumuona kipa namba mbili akijiandaa na kipa huyu udhaifu wake mkubwa ni kunyaka mipira ya chini, huwa hajiwezi kabisa kuruka chini. 
 
‘Ethan upo wapi?’
Nilimuita Ethan mwezangu ila hakuweza kuitikia, nikajiona kwenye tv kubwa la hapa uwanjani jinsi nilivyo jawa na wasiwasi mwingi sana. Frenando akatolewa uwanjani hapa kwa kigari maalumu na kukimbizwa hospiyalini kwa matibabu zaidi. Akaingia kipa namba mbili anaye itwa Antoniyo Jr.
“Hakikisha huonyeshi udhaifu wako sawa”
Nilizungmza na kipa huyu huku nikimtazama usoni mwake.
“Sawa kapteni.”
 
Tukaanza mpira kwa kasi sana huku nikijitahidi kupeleka mashambulizi mbele, ila zaidi ya wachezaji wanne wananikaba mimi peke yangu na kunifanya nipate wakati mgumu wa kumiliki mpira hata kwa sekunde kumi. Kila nilivyo jaribu kutoa pasi kwa Pilo, hakuweza naye kutembea kwani kuna benki mmoja mkubwa anamzuia. Katika maisha yangu ya mpira leo ndio siku ambayo ninajihisi kukata tamaa mwanzo tu mwa mechi. 

Wachezaji wezangu hapo katikati ya uwanja wamepoteana kabisa, kwani wachezaji wanao cheza kati wa timu pinzani wana uwezo mkubwa, kwanza kumiliki mpira na pili kupiga chenga. Dakika ya kumi na tisa tukafunga goli la pili, tena kipa alipigiwa shoti lililo mchanganya akaruka upande mwengine na mpira ukaingia upande mwengine.
 
‘Ethan nisaidie, nipe uwezo basi rafiki yangu’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiwatazama wachezaji wa timu pinzani wakishangilia goli hilo. Kwa dakika hizi kumi na tisa za hapa awali wachezaji wezangu wote wamechoka na wamechoka na wanaonekana kukata tamaa kabisa. Tukaanza tena mpira huku nikijitahidi kukimbia kidogo na mpira na kupiga katika goli la wapinzani, ila mipira yangu haikuweza kufika kwani mabeki ni mahiri kwa kuzuia mipira ya juu. 

Dakika ya ishiri na mbili tukafungwa goli la tatu. Dakika ya ishirini na nane tukafungwa goli la nne. Dakika ta arubaini na tano tukafungwa goli la tano ambalo liliyafanya machozi yangu kushindwa kujizuia na kuanza kutiririka machoni mwangu kwani mchezaji wa timu pinzani aliwapiga chenga mabeki wanne na akampiga tobo kiba na kufunga goli hili na kwa dharau ya ajabu akaanza kupiga piga kifua chake kwamba sisi na mashabiki wetu hatuna chochote mbele yao.

==>>ITAENDELEA KESHO
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )