Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, November 11, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 30

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA
               
“Dada yako yupo njiani analetwa hapa. Haki ya Mungu usipo nieleza ukweli Ethan ninakwenda kumuua mbele yako, sinto jali wewe ni mtu ninaye mpenda au laa. Ila nilazima nitamuua”
Camila alizungumza kwa msisitizo na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa, kiasi cha kuzidi kumchukia Camila. Hazikupita hata dakika tano dada Mery akaingizwa ndani humu, akasukumizwa chini huku mikono yake ikiwa imefungwa na kamba.
“Ethan ni wapi lilipo boksi jeusi?”   
Camila alizungumza huku akikabidhiwa bastola na mmoja wa walinzi wake. Camila akaielekeza bastola hiyo  kweye paja la dada Mery.
“Wifi”
Dada Mery aliita huku akijaribu kuangaza angaza ilipo simama Camila. Mlio wa risasi ukanifanya nilie kwa nguvu sana, kwani risasi hiyo imempiga dada Mery kwenye japa la mguu wake wa kulia na kumfanya agaregare chini kwa maumivu makali sana.

ENDELEA
Machozi mengi yakazidi kunimwagika machoni mwangu, hasira yangu ikazidi kupanda hadi ikafikia kiwango nikaanza kumwagikwa na makamasi puani mwangu. Sikuamini kama Camila ninaye ishi naye siku zote na kumchukulia kama mtu wa maana kwangu, kumbe ana roho mbaya sana.
“Sema boksi lipo wapi?”
Camila alizungumza kwa hasira huku akiwa amemuelekezea dada Mery bastola ya kichwani. Kilio cha dada Mery kikazidi kunipagawisha kabisa, kwani kila jinsi anavyo lia ndivyo jinsi damu inavyo mwagika kwenye kidonda chake.
“Nipo tayari kuwasaidia kuhakikisha kwamba tunalipata hilo boksi”
 
“Zungumza wapi?”
Gafla mlango wa kuingilia humu ndani ukavunjwa. Akasimama Ethan mlangoni huku kucha za vidoleni mwake zikiwa zimechongoka kwa sentimita kadhaa. Walinzi wa Camila wakaanza kumshambulia kwa kumpiga risasi mfululizo  ila hapakuwa na risasi hata mmoja ambayo iliweza kumdhuru Ethan. Risasi zilivyo waisha, Ethan kwa kasi ya ajabu akaanza kuwaua walinzi hawa wa Camila huku akiwachomoa miayo yao jambo lililo mfanya Camila kuogopa sana hadi haja ndogo ikaanza kumwagika. Ndani ya sekunde kadhaa walinzi wote wa Camila wakawa chini huku wakiwa tayari ni marehemu. Ethan akaanza kumfwata Camila aliye zidi kurudi nyuma nyuma hadi akafika ukutani na kukosa sehemu ya kwenda. Ethan akanitazama usoni mwangu huku akisubiria amri ya kufanya kama ni kumuua Camila au laa.
 
Nikamuita kwa ishara ya macho Ethan, akanifungulia kamba na pingu nilizo kuwa nimefungwa, kwa haraka nikamuwahi dada Mery chini alipo kaa. Nikataka kumfungua kitambaa chake ila nilivyo angalia maiti hizi nikaona hakuna haja ya kumfungua kitambaa chake. Nikamuacha na kuanza kutembea hadi alipo Camila.
“Nilikuambia kwamba sinto kusamehe kwa kuitoa siri yangu.”
Nilizungumza huku nikimkazia macho Camila usoni mwake.
“Sikujua kwamba nipo na jini. Ni hivi kuanzia hivi sasa hivi mimi na wewe basi kwenye kila jambo, si mahusiano na wala si kwa mambo mengine. Umenielewa?”
 
Camila akatingisha kichwa akimaanisha amenielewa. Ving’ora vya gari za polisi vinavyo kuja katika eneo hili vikanifanya nimtazame Ethan mwenzangu ambaye tayari amesha fanya mauaji makubwa sana.
“Ondoka na dada yangu”
“Na wewe?”
“Nahitaji kuwepo hapa hapa, sitaki kukimbia na kuwa mtu anaye tafutwa”
Ethan akanitazma ausoni mwangu, kwa haraka akanirudisha kwneye kiti changu, akanifunga kama nilivyo kuwa nimefungwa hapo awali. Akamshikisha Camila bastola na kumsimamisha mbele yangu na kuninyooshea.
 
“Unafanya nini?”
“Utaona”
Ethan baada ya kufanya anacho kifanya, akamkumbatia dada Mery na kuondoka naye katika eneo hili. Polisi wakaingia ndani humu huku wakiwa na silaha. Polisi wote wakabaki wakiwa wameshikwa na bumbuwazi kubwa sana, kwa haraka wakamuwahi Camila na kumpokonya bastola aliyo nielekezea.
“Ethan upo salama?”
Askari mmoja aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu. Askari hawa wakaanza kunifungua pingu pamoja na kamba, sehemu ambalo alikuwepo dada Mery kuna mwili wa mlinzi mmoja. Camila kila anacho ulizwa na askari hawa juu ya hichi kilicho tokea hapa anashindwa kuzungumza. 
 
Nikatolewa nje na madaktari wa kitengo hichi cha polisi wakaanza kunishuhulikia jeraha lililopo mgongoni mwangu huku wote wakiwa na shauku ya kuhitaji kunihoji maswali. Sikuweza kuwaona wazazi wa Camila katika eneo hili zaidi ya watu wengine.
“Mumejuaje nipo hapa?”
Nilimuuliza mmoja wa askari anaye nishuhulikia jeraha langu.
“Tulipigiwa simu na mama Camila, akisema kwamba mtoto wake amekuteka na amesikia milio ya risasi ikitokea huku”
“Mama?”       
“Ndio, ilikuwaje hadi imekuwa hivi?”
Nikashusha pumzi sana huku nikifiria usaliti alio ufanya mama Camila kwa mwanaye. Nikawaona wazazi wa Camila wakimkimbilia mtoto wao aliye wekwa chini ya ulinzi mkali wa askari.
 
“Una uhakika mama yake ndio aliye piga simu kwenu?”
“Asilimia mia moja”
Nikamtazama Camila jinsi anavyo kumbatiwa na wazazi wake. Kitu kinacho nishangaza ni kulia kwa mama yake, jambo lililo nifanya nijiulize swali kama aliamua kumsaliti mwanaye sasa hivi kwa nini ameamua kulia. Camila akaingizwa kwenye moja ya gari la askari. Baba Camila akaonekana kuzungumza na askari hao ila hapakuwa na askari ambaye anamsikiliza na kila askari anafwata sheria za nchi zinavyo kwenda. Hata kama wewe ni mtoto wa kiongozi, ukifanya makosa ni lazima watakukamata. Mama Camila akaanza kutembea huku akitufwata kwa kasi katika eneo hili ninalo patiwa matibabu.
 
“Ethan ni nini ulicho kifanya eheee?”
Mama Camila alizungumza kwa ukali sana huku akinitazama usoni mwangu.
“Mwanao ndio aliye niteka mimi na kunisababishia majeraha mgongoni mwangu”
Mama Camila akanizaba kofi zito la shavuni mwangu na kuwafanya askari wa kike walio karibu na eneo hili kumzuia, kwani kufanya hivyo navyo ni kuvunja sheria.
“Ole wako mwanangu afungwe nitahakikisha na wewe unafungwa”
 
Mama Camila alizungumza kwa hasira sana huku akiondolewa katika eneo hili. Hapa ndipo nikatambua kwamba mchezo wote wa kupiga simu ameufanya Ethan, jini mwenye uwezo wa kujibadilisha kila aina ya mtu amtakaye yeye. Nilipo maliza kupatiwa matibabu na mimi nikaingizwa kwenye gari la polisi na safari ya kuelekea makao makuu ya polisi ikaanza. Ukimya ndani ya gari hili umetawala kiasi cha kunifanya nizidi kusongwa na mawazo kichwani mwangu. Mahusiano yangu na Camila yamebadilika sana na kuzalisha uaduia mkubwa sana. Mipango  yote ambayo tulikuwa tumeipanga kwenye maisha yetu pale tutakapo ingia kwenye ndoa, ndio tayari imesha vurugika.
 
Nikafika katika kituoa cha polisi na kukuta kundi kubwa la waandishi wa habari wakitusubiria hadi nikajikuta nikishangaa na kujiuliza wametokea wapi hawa. Wandishi wa habari wakandelea kufanya kazi  yao ya kuchukua kila tukio linalo endelea huku wengine wakiwa na shahuku ya kunihoji ila polisi waliwazuia na nikafanikiwa kuingia ndani ya jengo hili kubwa lenye gorofa zaidi ya thelathini. Nikaingizwa kwenye chumba cha mahojiano na kuachwa peke yangu. Nikaanza kukumbuka tukio la Ethan jinsi alivyo kuwa akiwaua walinzi hao na mbaya zaidi amewachomoa chomoa mioyo yao.
 
‘Ethan’
Niliita kimoyo moyo, baada ya sekunde kadhaa Ethan akakaa kwenye kiti kilichopo mbele yangu na tumetenganishwa na meza tu.
‘Vipi dada yangu yupo sehemu salama?’
‘Ndio nimemuweka sehemu salama kabisa, na kidonda chake kimepona’
‘Camila je?’
‘Bado unamkumbuka huyo mpuuzi?’
‘Hapana, ila nataka kufahamu kwamba yupo wapi?’
‘Yupo kwenye chumba cha mahojiano’
‘Ni kitu gani ambacho kimempata hadi kuwa vile?’
‘Ni hasira tu ndio imepelekea yeye kuwa vile’
‘Mmmm sasa hii kesi si ataibeba yeye?’
‘Nakusikiliza wewe, kama unahitaji apotelee jela, nipo tayari hii kesi kumgeuzia yeye?’
 
Nikaka kimya huku nikimtazama Ethan usoni mwake. Uzuri mazungumzo yetu hakuna binadamu yoyote anaye yasikia. Nikasimama kwenye kiti na kuanza kuzunguka ndani ya chumba hichi huku nikitafakari ni kitu gani nimjibu Ethan. Nikakumbuka maisha ya nyuma ambayo tuliishi na Camila, maisha ambayo kila mmoja alikuwa akituzungumzia sisi. Nikakumbuka kipindi cha utoto jinsi alivyo kuwa akinitetea shule kutokana na ubaguzi wa rangi ulivyo kuwa kipindi hicho.
‘Fanya mamuzi sahihi’
Ethan alizungumza huku akiwa amesimama nyuma yangu.
‘Mbeleni hato kuja kunidhuru?’
‘Ni ngumu sana kuzungumzia vitu vya mbeleni, kwani dunia hubadilika kila kukicha’
‘Iue kesi kwa upande wake’
‘Sawa nitambambikia kesi daktari aliye kufanyia upasuaji huko nyuma.’
 
‘Kwani hukumuua?’
‘Yupo hai, utaona nitakacho kifanya, na hata ukiiulizwa maswali hakikisha kwamba unamtetea Camila kwamba bastola aliishika kwa ajili ya kujitetea mara baada ya kukuta dokta akiwaua walinzi wake kwa kuwachomoa mioyo yao’
‘Hilo linaweza kukubalika kweli?’
‘Ndio linakubalika, huku mimi nitatengeneza ushahidi wote na kila jambo litakwenda vizuri sawa’
‘Sawa’
Ethan akanishika bega kisha akapotea katika eneo hili. Mlango ukafunguliwa na akaingia mzee mmoja wa makamo. Mzee huyu akakaa kwenye kiti alicho kuwa amekalia Ethan.
“Habari yako bwana Ethan”
Alisalimia huku akinitazama usoni mwangu. Taratibu nikarudi na kukaa kwenye kiti nilicho kuwa nimekalia.
“Nahitaji kufahamu ni kitu gani kilitokea?”
“Wapi?”
 
“Kwenye eneo la tukio?”
Nikakaa kimya kwa sekunde kadha huku nikiwa nimeinamisha kichwa changu chini. Nikamtazama mzee huyu.
“Nilipo toka hospitalini leo asubuhi, nilielekea nyumbani kwa wakwe zangu. Nikiwa pale jina langu lilitajwa na magaidi, nina imani kwamba utakuwa umeona video ile”
“Ndio nimeiona”
“Nilichanganyikiwa kwa kweli, na niliingia chumbani kwa Camila kwa muda kidogo. Baba yake aliingia chumbani mule akihitaji ufafanuzi juu ya boksi hilo jeusi ambalo kwa kweli mimi  silifahamu”
Nilizungumza kwa upole sana huku nikimtazama mzee huyu usoni mwake.
 
“Baada ya kutoka nje nikiwa ndani ya gari, Camila naye aliingia. Ila baada ya muda kidogo alitoka na kuelekea ndani”
“Kwa nini alitoka?”
“Tulipishana kauli za kimapenzi”
“Kauli gani hizo?”
“Mzee mahusiano yangu na Camila si ya kuhojiwa, kwani wewe na mke wako hamkuwahi kugombana?”
“Sawa, endelea”
Walinzi walinizunguka huku wakiwa wamenishikia bastola, wakaniamrisha kutoka ndani ya gari. Mmoja wao akanipiga mtama na nikaanguka chini. Wakanifunga pingu na kunipeleka katika ile nyumba ya pembeni mulipo nipata. Mlinzi mmoja alinipiga sana huku akinilazimisha kunihoji ni wapi lilipo hilo boksi jeusi, ila sikuweza kumjibu chochote zaidi ya kuendelea kunipiga”
 
“Ilikuwaje walinzi walikufa?”
“Daktari aliingia ndani ya chumba hicho kwa kuvunja mlango, sijui alikuwa na nguvu za aina gani. Walinzi walijaribu kumshambulia kwa risasi, ila cha kushangaza hakufa. Alianza kuwatoa mioyo yao mmoja baada ya mwengine. Hadi anaingia Camila pale alikuta watu wote wapo chini, akashika moja ya bastola huku akijaribu kumshambulia dokta yule kwa maana alikuwa katika hatua za kuniua mimi kwa kunitoa moyo”
“Unataka kusema kwamba Camila hausiki na chochote?”
“Atahusikaje na tukio hilo ikiwa yeye ndio alikuja kuniokoa”
“Kwa nini ulikamatwa na walinzi wao?”
“Hilo sio swala langu, ungemuuliza mgombea uraisi, ni kwa nini walinzi wake walinikamata”
 
“Unakumbuka chochote juu ya daktari?”
“Ndio baada ya kuwaua wale walinzi, alinipasua hapo nyuma ya mgongo wangu, sikujua anatafuta nini ila kabla hajamaliza anacho kifanya ndipo Camila alipo tokea”
“Tunashukuru”
“Nipo tayari kuondoka?”
“Tutakufahamisha mara mahojiano yetu yatakapo kishwa”
Mzee huyu akatoka chumbani humu na kuniacha peke yangu. Ethan akarudi tena na kuiweka miguu yake juu ya meza huku akitabasamu sana.
“Ethan rafiki yangu naomba kitu kimoja”
“Kitu gani?”
“Namuhitaji nimuoe dada yako”
“Merry au dada yangu yupi?”
“Huyo huyo, sikuwahi kufahamu kama ni mzuri kiasi kile”
Nikamtazama Ethan huku nikiwa nimemkazia macho.
“Sawa ni wewe na yeye mimi sipo hapo”
“Nashukuru”
Ethan akaondoka na kuniacha peke yangu, mlango ukafunguliwa, akaingia mwanasheria wa kampuni huku akiwa ameongozana na mzee ambaye alikuwa ananihoji maswali. Nikaruhusiwa kuondoka eneo hili. 
 
“Pole sana bosi”
“Nashukuru”
Tukatoka nje na kukutana na kundi la waandishi wa habari ambao wanamuhoji Camila na wazazi wake. Waandishi wa habari walipo niona mimi wakakimbilia wote kwangu na wakanizingira huku kila mmoja akihitaji kunihoji swali lake. Sikuwajibu kitu chochote hawa waandishi wa habari, nikatembea hadi walipo simama Camila na wazazi wake.
 
“Mumenionyesha uhalisia halisi wa familia yenu nawashukuru sawa. Ila CAMILA kuanzia hivi sasa sahau kama kuna mwanaume ulisha wahi kumpenda anayeitwa Ethan. Na mzee ninatoa asilimia zangu za mchango nilizo kuchangia kwenye kampeni zako tusijuane kuanzia hivi sasa. Asanteni”
Mara baada ya kuzungumza maneno hayo huku mwanasheria wangu akiwa amesimama nyuma yangu tukaondoka eneo hili na kumuacha Camilia akiangua kilio kizito sana ambacho sikuhitaji kukijali kwani alicho kua anakitafuta kwangu tayari amesha kipata.

==>>ITAENDELEA KESHO
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )