Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, November 21, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 35

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA
Nikashusha pumzi taratibu, nikamsogelea mwana sheria na kumtaza usoni mwake.
“Hii ni vita ambayo tumesha ianzisha. Ni lazima damu za watu ziweze kumwagika. Nahitaji kuwa pamoja nawe kwenye kila jambo”
“Usijali mkuu, baba yako alinipa jukumu la kukuangalia nami nitakuangalia hadi mwisho wa maisha yangu”
“Sawa nashukuru kusikia hivyo. Huyo mwana mama tunamfanyaje?”
“Kwa sasa ngoja tumtafute kwanza mamam mzazi. Tukisha mpata tunamgeukia na yeye”
“Nashukuru”
“Huyu mzee mkuu tunamfanya nini?”
Kijana mmoja aliniuliza huku akinitazama usoni mwake. Nikamuonyesha ishara ya kuchinja, kijana huyu akachomoa bastoka yake na kumpiga risasi nne za kifua mzee huyu na kumfanya afe hapo hapo.
           
ENDELEA           
“Hakikisheni kwamba mwili wake hauonikani sehemu yoyote katika dunia hii. Ikiwezekana mumuingize kwenye pipa la tindikali”
Nilizungumza huku nikiwatazama vijana hawa.
“Sawa mkuu”
“Kitu kingine, naamini kwamba leo hii mimi na nyinyi ndio tumeonana. Naomba haya mambo yabaki humu ndani, juu ya nguvu zangu mulizo zishuhudia pia liwe jambo la siri sawa”
“Sawa mkuu, kati yetu hakuna mtu ambaye anatatoa siri yoyote. Tuamini katika hilo”
“Nafurahi na ninashukuru kusikia hivyo”
Mara baada ya kuzungumza hivyo nikaagana na vijana hawa. Kijana aliye kuja kutupokea akatuto na kutupeleka hadi sehemu ilipo helicopter tulio.
 
“Ninawategemea katika hii kazi”
“Usijali mkuu, tutaifanya katika muda mfupi snaa na kwa umakini wa hali ya juu kisha tutakueletea ripoti”
“Sawa”
Akafungua mlango wa helicopter hii, nikawa wa kwanza kupanda kisha akapanda mwanasheri. Mlango ukafungwa kisha rubani wetu taratibu akawasha helicopter hii na safari ya kurudi hotelini ikaanza. Ukimya ukatawala ndani ya helicopter hii, huku mwanasheria akionekana kujawa na mawazo mengi sana.
 
“Unawaza nini mzee?”       
“Nawaza jinsi ulivyo mnyanyua yule mzee na kiti chake hadi sasa hivi ninakosa jibu?”
“Hahaa usijali katika hilo, nina uwezo binafsi ambao Mungu amenijali”
“Kweli, Mungu ashukuriwe katika hilo”
“Wale vijana una waamini?”
“Asilimia mia moja wala usiwe na mashaka nao mkuu”
“Sawa, sinto penda kutokee matatizo kwenye hii kazi”
“Usijali”
 
Tukafika hotelini majira ya saa saba usiku. Nikashuka kisha mwanasheria akaondoke na kurudi kwake. Nikafika kwenye mlango wa chumba changu, nikaminya kengele, nikaisikia sauti ya Camila akiniuliza ni nani, nikaguna kidogo na baada ya sekunde tano mlango ukafunguliwa. Camila alipo     niona akanikumbatia kwa furaha sana
“Umenipa hofu mwenzako”
“Kweli?”
“Ndio, nimeshindwa hata kulala”
“Pole mpenzi wangu, ninamshukuru Mungu nimefanikiwa kulimaliza jambo lililo nipeleka kule”
“Vipi umemuona mzee?”
“Yaa nilimuona, amebananishwa kidogo na ametaja ni sehemu gani alipo mama yangu”
“Duuu sasa mama utampataje?”
 
“Kuna watu nimewakabidhi kazi ya kwenda kumleta, nina imani kwamba watafanikisha kumleta akiwa salama”
“Yupo nchi gani?”
“Tanzania”
“Ahaaa sawa mume wangu, twende bafuni tukaoge”
Camila alizungumza huku akinishika kiuno kwa nyuma. Tukaingia bafuni, akanivua nguo zangu zote kisha naye akavua nguo hizi za kulalia. Tukaoga kisha tukarudi chumbani, kutoka na uchovu nilio nao, sikuweza kufanya kitu chochote na usingizi uliwahi kunipitia. 

Asubuhi na mapema nikawahi kuamka na kumuacha Camila akiwa amelala, nikavaa nguo zangu za mazoezi kisha niakelekea uwanjani. Nikaanza kufanya mazoezi peke yangu hata kabla ya wachezaji wezangu. Baada ya nusu saa wachezaji wezangu wakajumuika nami katika kufanya mazoezi. Jinsi ninavyo cheza leo, kumewafanya wachezaji wezangu kunisifia kwani jana sikuwa sawa kabisa. Kocha akatupa mipango ya jinsi gani tunatakiwa kucheza mechi yatu ya kesho, kwani hadis asa hivi tunaongoza kundi letu kwa pointi sita.
“Tunatakiwa kushinda kila mechi iliyopo mbele yetu. Ethan nahisi hili ninalo kwenda kuzungumza sio jambo zuri kidogo, ila naomba ulivumilie kwa leo tu”
“Zungumza tu kocha”
“Leo naomba usifanye     chochote na bibie, asije akakumaliza nguvu sawa”
Mimi na wachezaji wezangu tukajikuta tukicheka huku tukimtazama kocha.
 
“Kweli vile, ninalo lizungumza lina maana Ethan”
“Usijali kocha”
“Haya sasa ni muda wa kupata kifungua kinywa”
Tukaondoka uwanjani hapa na kurudi eneo la hotelini, tukamkuta Camila akisiaidiana na wafanyakazi wa hapa katika kuandaa vifungua kinywa. Camila alipo niona akanifwata kunilaki, akanikumbatia pasipo kujali kama nina jasho liilo nilowanisha nguo zangu zote.
“Vipi, umecheza vizuri?”
“Ndio mke wangu na kesho nitafunga magoli kwa ajili yako”
“Kweli mume wangu?”
“Ndio”
“Utanifungia magoli mangapi?”
“Kama sita hivi”
“Huuhuhu, sita?”
“Ndio, kwani nashindwa?”
“Hamna hushindwi mume wangu, ila inabidi ufanye kazi kubwa. Tena leo inabidi nikubanie nisikupe utamu”
Camila alizungumza kwa kuninong’oneza sikioni mwangu na kunifanya nitabasamu.
 
“Sawa mama”
“Mbona umeitikia kinyonge?”
“Hamna mke wangu, mbona sijaitikia kinyonge”
“Kweli?”
“Ndio mke wangu”
“Nimeandaa kifungua kinywa kwa ajili yako, twende ukanywe.”
“Sawa”
Tukaa kwenye meza yetu pamoja na rafiki yangu Frenando. Tukapata kifungua kinywa kisha tukarudi mavyumbani mwetu.  Siku nzima hii ya leo, kocha alikaa nasi karibu sana huku akituhimiza sana tusipoteze mchezo ulipo mbele yetu kwani ana malengo makubwa sana nasi kwa maisha ya baadaye ya soka.
                                                                                                            ***   
Siku ya mechi ikawadia, tukaingia kwenye basi letu maalumu kwa timu hii kisha safari ya kuondoka nje ya mji ikaanza huku tukipewa usindikizaji wa gari mbili za polisi. Moja ipo mbele ya basi letu huku nyingine ipo nyuma ya basi letu. Daktari wa timu akampa Camila nafasi ya kuwa msaidizi wake, hivyo naye amejuimuika kuungana nasi katika basi hili.
“Utaimudu kazi ya udokta?”
“Ndio, kwa nini nishindwe”
“Hahaaa haya mwaya”
“Tena ukianguka wewe, nitakufwata na kukuhudumia hadi upone”
“Haya bwana mke wangu, ngoja nizungumze na wachezaji wangu”
 
Nikanyanyuka kwenye siti yanguna kusimama katikati ya basi. Wachezaji wezangu wote wakanitazama.
“Ni siku nyingine, tunakwenda kupambana, tukiwa pamoja. Ninawaomba tucheze kwa umoja, na tuhakishe tunashinda. Ninawategemea sana na kwa pamoja tutashinda sawa”
“Sawa kapteni”
Wachezaji wezangu waliitikia kwa pamoja kisha safari ikaendelea. Hadi kufika uwanjani, ilitugarimu masaa mawili. Tukashuka na kuwakuta waandishi wa habari pamoja na mashabiki wakiwa tayaru kwa kutupokea. Waandishi walipo niona ninashuka kwenye gari huku nikiwa na Camila, wakapiga shangwe ambayo hakika sikuitaraji. 
 
“Ethan na Camila tunawapenda”
Ni maneno yaliyo sikika katika kundi moja kubwa la wamashabiki wa kike. Nikagairi kuelekea ndani na kuwafwata mashabiki wangu hao huku walinzi na askari wakiwa wametangulia mbele yetu. Nikaanza hukuchua kalamu ya kila mshabiki, wapo wengine walihitaji niweke saini yangu kwenye mikono yao huku wegine wakihitaji niweke saini kwenye tisheti zao walizo zifanya. Camila naye aliweka saini kwa mashabiki wake wanao muomba kufanya hivyo.
 
“Ethan muda sasa umefika”
Mlinzi mmoja alizungumza pembeni yangu. Nikawapungia mkono na kuanza kuongozana na walinzi huku nikiwa nimeshika Camila mkono. Tukaingia katika chumba chetu cha kubadilishia nguo.
“Camila naomba clipbandeji”
“Ya nini mume wangu?”
“Nahitaji kujifunga kwenye mguu wa kulia, nahisi kama nyayo kidogo inavuta vuta kwa chini”
“Sawa”
Camila akaanza kunifunga mguu wangu kulia.
“Kaza kidogo”
 
Camila alafanya kama nilivyo mueleza. Akanivisha soksi, nikavua koti langu pamoja na suruali hii ya mazoezi niliyo ivaa, kisha nikavaa jezi yangu, ambayo mgongoni imeandikwa namba sana pamoja na jina langu. Kocha akaanza kupiga piga makofi, ikiwa ni ishara ya kutunyamazisha. Baada ya sekuende kadhaa kila mmoja akanyamaza na kumsikiliza kocha ni kitu gani ambacho anahitaji kuzungumza.
“Naamini kwamba kila mmoja anatambua nafasi yake si ndio”
“Ndio kocha”
“Kasi, na mashuti ya mbali ndio mchezo wa leo. Wamezoea kutuona tunacheza mchezo wa pasi fupi fupi, kumbukeni wezetu wana nguvu, wana kasi pia. Hivyo ni lazima tuweze kukubaliana na mwendo kasi wao la sivyo tutachemsha leo sawa”
 
“Sawa sawa kocha”
“Ethan, Pinto ninawategemea. Hakikisheni kwamba munayengeneza mfumo mzuri wa kushirikiana. Katikati, Chris na wezako hakikisheni hamtawaliwi. Chukueni mipira nyuma kisha muipeleke mbele sawa”
“Sawa sawa kocha”
“Tunadakika tano kabla ya kuingia uwanjani. Munaweza kuendelea na shuhuli zenu”
“Kocha suti ya leo imekutoa?”
Nilimtania kocha na kumfanya acheke kidogo.
“Nashukuru capten”
Camila taratibu akanifunga kitambaa cha ukapten katika mkono wangu wa kushoto.
“Hakikisha unaongoza timu na inashinda, sihitaji ushindwe mume wangu sawa”
“Sawa mke wangu
 
Camila akanipiga busu la mdomoni. Nikamuachia, kisha yeye na benchi la ufundi wakaanza kutoka katika chumba hichi. Taratibu tukaanza kutoka katika chumba chetu na kuelekea katika mlango wa kutokea, huku makaera man wakiwa makini sana kuhakikisha kwamba wana turekodi vizuri. Nikakonyeza kamera moja ambayo inanichukua kwa ukaribu sana usoni mwangu.  Refarii na wazaidizi wake wakasimama mbele yangu, katoto kamoja ka kike kaliko valia jezi ya timu yetu kakanipa mkono na nikakashika.
“Unaitwa nani?”
Nilimuuliza huku nikiwa nimeinama.
“Camila Alexander Diaz”
Kalinijibu kwa ufasaha kabisa huku akitabasamu sana.
“Kweli?”
“Ndio”
 
Nikatabasamu kisha nikasimama wima. Tukapewa ishara ya kuanza kuingia uwanjani. Taratibu tukaanza kutembea hadi uwanjani, uwanja huu una mashabiki wengi sana ambao wengi wao wameshika wabango yanayo nikaribisha tena uwanjani. Tukajipanga mstari mmoja ulio nyooka huku Camila Alexander Diazi akiwa amesima mbele yangu. Ukapigwa wimbo wa taifa wa timu ya Spain kisha ukapigwa wimbow a taifa wa nchi hii ya Ujerumani. Tukabadilsiahana bendera na kapteni wa timu ya wapinzani. Leo hii timu yangu inaanza katika goli Kaskazini mwa uwanja huu. Kila timu ikazunguka nusu duara katikati ya uwanja huu na tukapewa dakika moja ya ukimya kwa kuwakumbuka waalimu wa shule ya Camila walio chinjwa na kundi la kigaidi huko barania Afrika liitwalo Al-Shabab.
 
Dakika moja ilipo kwisha, filimbi ikapigwa na refarii, kisha wachezaji tukatawanyika, kila mtu akasimama katika nafasi yake. Wapinzani wezetu wakaanzisha mpira huu, huku wakionekana kuumiliki sana mpira huu. Hatukuchoka katika kuutafuta mpira ambao wapinzani watu wana umiliki kwa kupigiana pasi zinazo fika kwa kila anaye kusudiwa kupewa mpria.
Wapinzani wetu wakafanya shambulizi moja kali sana, ila Frenando akafanikiwa kuunyaka mpira huo. Frenando akaupiga mpira mbele.

 Lukas akautuliza vizuri kifuani mwake kishaa kauweka chini, akanitazama nilipo na kupiga pasi ndefu iliyo anza kuambaa ambaa hewani, nikaanza kukimbia kuelekea kwa wapinzani wangu, huku kila mara nikiutazama mpira huu. Wachezaj wawili ninao kimbizana nao hawakusita katika kuutazama mpira huo. Kitendo cha mpira kutufikia tulipo, nikauunganisha kwa shuti kali ambao liliambaa hewani kwa sekunde kadhaa na kugonga mwamba wa juu wa wapinzani, kisha mpira ukatoka nje. Uwanja mzima ulisimama na kushangilia kwani kama mpira huo ungeingia golini basi lingekuwa ni goli moja la kihistoria katika machuano haya.
 
Inadi ya wachezaji wanao nikaba kwa timu pinzani ikaongezeka, wakaanza kunikaba wachezaji wanne wanne jambo lililo nifanya nianze kuuona mchezo mgumu kwa upande wangu, kwani kila mpira ambao ninaletewa na wachezaji wezangu, siumiliki hata kwa sekunde nyingi wanakuwa wananipokonya. Kipindi cha kwanza kikaisha pasipo kufungana 
 
“Pole mume wangu”
Camila alizungumza huku akitembea pembeni yangu.
“Ndio mpira mpenzi wangu”
Nilizungumza huku tukiingia ndani ya chumba chetu. Kila mchezaji uso wake umetawaliwa na kuchoka, kwani mtandange huu ni wa kukata na shoka, yaani ni bora hata na mechi ya kwanza tulo cheza kwani tulifungwa na tulikuwa na hamasa ya kutafuta goli, ila mechi hii, karibia wachezaji wa timu pinzani wanakaba na wanaonekana hawana hata hamu ya kutafuta goli na itakuwa ni furaha yao wakiona tunagawana pointi.
 
ITAENDELEA   
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )