Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, November 23, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 36


ILIPOISHIA
Inadi ya wachezaji wanao nikaba kwa timu pinzani ikaongezeka, wakaanza kunikaba wachezaji wanne wanne jambo lililo nifanya nianze kuuona mchezo mgumu kwa upande wangu, kwani kila mpira ambao ninaletewa na wachezaji wezangu, siumiliki hata kwa sekunde nyingi wanakuwa wananipokonya. Kipindi cha kwanza kikaisha pasipo kufungana
“Pole mume wangu”
Camila alizungumza huku akitembea pembeni yangu.
“Ndio mpira mpenzi wangu”   
Nilizungumza huku tukiingia ndani ya chumba chetu. Kila mchezaji uso wake umetawaliwa na kuchoka, kwani mtandange huu ni wa kukata na shoka, yaani ni bora hata na mechi ya kwanza tulo cheza kwani tulifungwa na tulikuwa na hamasa ya kutafuta goli, ila mechi hii, karibia wachezaji wa timu pinzani wanakaba na wanaonekana hawana hata hamu ya kutafuta goli na itakuwa ni furaha yao wakiona tunagawana pointi.
                   
ENDELEA   
“Mumecheza vizuri. Ila wapinzani wetu hawajaweza kutupa nafasi ya kufunga. Munachotakiwa kufanya hivi sana ni kuhakikisha kwamba viungo wa katikati munapanda na nyinyi wafungaji, wakipanda viungo kwenda kushambulia nyinyi munarudi kuwa viongo”
 
Kocha alizungumza huku akitutazama.
“Ndio mfumo gani tena huo kocha?”
Mchezaji mmoja aliuliza huku akimtazama kocha usoni mwake.
“Ni ZigZag. Wapinzani wote macho yao yapo kwa Ethan na Pinto. Wanawafanya wanashindwa kumiliki mpira. Mawinga wa pembeni, hakikisheni sasa hivi nyinyi ndio munakuwa munaongoza jaramba za kufunga. Safu ya mabeki, nanyi hakikisheni kwamba hapiti mshambiliaji yoyote wa upinzani. Mumenielewa?”
 
“Tumekupata kocha”
Baada ya kumaliza kutibiwa majeraha madogo madogo yakiwemo kubwanwa na misuli, tukaanza kurudi uwanjani.
“Mume wangu leo umeshikika”
Camila alizungumza kwa sauti ya chini huku tukitembea kwa pamoja.
“Yaani wee acha tu, wanakaba kama nyuki. Tena mtazame yule mchezaji namba sita uwanjani. Yaani kama nimepokonya mwanamke. Yaani nikigusa mpira tu huyu hapa miguuni”
“Hahaaaa acha hizo mume wangu. Nenda kanifungie goli bwana nifurahie”
“Sawa mke wangu”
“Nitakunyima na leo pia”
 
Maneno ya Camila yakanifanya nitabasamu tu huku nikiingia uwanjani na yeye akielekea kwenye eneo la benchi la ufundi. Wachezaji wote tukakamilika uwanjani, refaa akaanzisha mpira, huku wachezaji wa timu zote mbili tukionyesha haya ya kuhitaji kufunga goli. Kama vile kocha alivyo tuelekeza ndivyo tulivyo anza kucheza na kuwachanganya wapinzani wetu ambao muda wote macho yao yalikuwa kwangu na Pinto. Kazi yetu ikawa ni kuwakusanya upande mmoja wapinzani wetu, kisha mipira tunawapasia Alex na Lukas. 
 
Ndani ya dakika kumi na tano za kwanza tukafanikiwa kupata goli la kuongoza ambalo amelifunga Lukasa, kwa kuunganisha pasi nzuri aliyo pewa na Rodguize kiungo wetu wa katikati. Furaha ikatawala uwanja mzima huku kila mtu akiwa amejawa na furaha kubwa sana.
“Wamachanganyikiwa, ni mwendo wa kuongeza kasi ya mashambulizi”
 
Niliwaambiwa wachezaji wezangu, huku tukiwa tumekusanyika duara moja, muda wa kushangilia. Tukatawanyika na mpira ukaanza tena, wapinzani wetu wakaanza kuelewa mfumo wetu, wakapunguza mazoea ya kutukaba mimi na Pinto na walicho kifanya ni kunza kujigawa mmoja mmoja kwa kila mchezaji wa timu yetu.
“Kampeni mchezo umebadilika tunafanyaje?”
Alex aliniuliza huku tukisubiria beki wetu apige mpira mbele.
“Turudini kwenye mfumo watu wa kawaida”
“Utasaidia?”
“Hatuna jinsi, hakikisha munalinda goli”
“Sawa”
 
Maagizo niliyo yatoa yakaanza kumfikia mchezaji mmoja baada ya mwengine, nikafanikiwa kupata mpira, nikautuliza chini, mchezaji ambaye leo amenikamia kuhakikisha sing’ari uwanjani, akanifwata kwa kasi, nikamtazama kwa macho yakumkazia, akajaribu kunyosha mguu ili kuuchukua mpira, nikauvuta mpira kwa nyum kidogo na kuufanya mguu wake upoteze muelekeo, nikaupitosha mpira katikati ya miguu yake, japo alijaribu kuibana ila akashindwa. 

Akajaribu kunipiga kikumbo nisimpite, ila nikamkwepa kisha nikaanza kukimbia na mpira pembezoni mwa chaki nyepe. Wakaongezeka na kuwa wachezaji wa nne huku wote wanaonekana kujawa na uchu wa kunipokonya mpira.
 
Nikaubana mpira katikati ya miguu yangu, nikaurusha juu kidogo na ukampita beki mmoja, nikauwahi kabla ya mchezaji mwengine kuuchukua, naye nikamfanya kama mwenzie. 

Nikatika kama ninaupiga mpura, ila nikausogeza kidogo pembeni na kumfanya beki mmoja kupitiliza huku akiserereka kana kwamba ameanguka na pikipiki. Nikaanza kuichezesha miguu yangu huku nikimtazama beki aliye salia, nikaukanyaga mpira na mguu wangu mmoja kisha nikazunguka nao na nikampita beki huyu akiwa amesimama pasipo hata kuthubutu kunyoosha mkono wake. Uwanja mzima ukafurika kwa shangwe, nikalitazama goli na kumuna kipa akiwa amesimama upande huu ninao tokea. 

Nikausogeza mpira kwa mbele kidogo kisha nikaachia shuti moja kali sana na kuufanya mpira uzunguke zunguke hewani, na ukaingia katika kona ya juu ya goli, japo kipa alijaribu kwa kadri awezavyo kuruka ili autoe ila akashindwa kabisa. Shangwe zikafumuka uwanja msimza. Nikaanza kukimbia kuelekea katika benchi la ufundi huku nikimyooshea Camila kidole. Nilipo mkaribia Camila akanikumabia kwa furaha huku kocha na wachezaji wengine wote nao wakinikumbatia.
“Kwa ajili yako mke wangu”
Nilizungumza kwa sauti huku nikiendelea kukumbatiwa. Camila akashindwa hata kuzungumza kitu na kubaki akimwagikwa na machozi tu.
 
Tukarudi unawanjani huku jina langu likiibwa na mashabiki wote. Mpira ukaanza tena huku wapinzani wetu wakiwa wamechanganyikiwa kabisa, kwani goli nililo lifunga hakika limeingia kwenye rekodi ya magoli bora katika michuano hii.
Hadi tunafika dakika ya mwisho, goli ni mbili bila. Tukaanza kuepeana mikono na wapinzai wetu, japo tumewafunga ila kwenye kundi letu wao ndio wanatufwatiwa nyuma tetu. Tukawaaga mashabiki wetu huku waandishi wa habari wakiwa makini katika kuniwinda ili kunihoji maswali mawili matatu. Nikaitwa na waandishi wa habari wawili na nikasimama katika eneo maalumu ya kuhojiwa huku nikiwa na Frendando.
 
“Kwanza hongereni sana kwa ushindi huu mzuri”
“Tunashukuru sana”
“Ethan unajisikiaje kufunga goli moja zuri sana ambali hakika hadi sasa hivi sijapata la kufananisha nalo?”
“Ahaa….ni furaha kwa kweli, unajua wapinzani wetu ni wazuri sana. Kipindi cha pili hawakunipa nafasi ya kufunga basi kipindi cha pili nikaapiza kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba ninafunga na kweli nimefunga. Ninamshukuru sana Mungu kwa hilo”
 
“Hongera sana hii ni zawadi ya goli bora kwa mechi ya leo”
Muandishi huyu alinipa kiboksi ambacho ndani kina kiatu kidogo cha dhahabu.
“Nashukuru sana”
“Frenando Alemedo, hongera sana kwa kuto ruhusu goli kuingia nyavuni kwako”
“Nashukuru”
“Nini siri yako ya kunyaka kila mkwaju ambao walikuwa wakiutuma wapinzani wako na isitoshe ndio umerudi kutoka kwenye majareha?”
“Kila kitu ni kijituma na mazoezi, nilijitahidi kuhakikisha kwamba ninakuwa kipa bora na basi nitakuwa kipa bora kwenye hii michuano”
“Hongera sana na wewe umepata zawadi yako ya mchezaji bora wa mechi kutoka SuperSport”
 
“Tunashukuru”
“Hata tutwatakie siku njema”
“Asanteni”
Tukaondoka katika eneo hili na nikamkuta Camila akinisubiria, akanipoke zawadi yangu niliyo pesa kisha akanipiga busu la mdomoni na kuwafanya wa wapiga picha kila mmoja kujitahidi kupiga picha kadri ya uwezo wake. Tukarudi katika vyumba vya kubadilishia nguo. Kila mmchezaji hakusita kunipongea kwa juhudi niliyo ionyesha.
“Unajua nini Ethan”
“Mmmm….”
Muna ule yule beki alivyo kwua akiserereka, nilifumba macho kwa kweki, kwa maana ile miguu laiti kama ingekupata basi sasa hivi tungekuwa tunazungumza mambo mengine kwa kweli”
 
“Yaa na nilijua tu kwamba akili zake zitaishia pale, unajua ameserereka hadi ameacha alama uwanjani, kang’oa kabisa nyasi”
“Hahaaaaa…..”
Furaha ikazidi kutawala ndani ya chumba chetu hichi. Tukavaa track suit zeu kisha tukaelekea eneo lilipo basi letu tukapanda na kuanza safari ya kurudi kambini.
“Mume wangu ona ona”
Camil alizungumza huku akionionyesha jinsi goli langu linavyo rudiwa kurushwa kwenye kituo cha SuperSport 3. Nikaendelea kujitazama kwenye simu hii ya Camila, hakika kitu nilicho kifanya kwa mabeki hawa kitaandika histori kubwa sana kwenye maisha yangu.
“Wanalifananisha goli langu na Ronaldinho yule wa Braziel”
Nilizungumza huku nikimuonyesha kocha matangazo haya ya moja kwamoja tunayo yatazama kupitia simu ya Camila.
“Duu, na wanasema kwamba ni zaidi ya goli lake”
Nilizungumza kwa furaha.
 
“Ni historia umeandika, sasa usivimbe kichwa. Hakikisha kwamba unazidi kuishangaza dunia kwa mambo mengine mengi sana.  Sawa”
“Sawa kocha”
Tukafanikiwa kufika hotelini salama salmin. Tukaingia kwenye vyumba vyetu. Mimi na Camila tukaanza kuoga kwa pamoja. Kutokana na hisia kali zilizopo kati yetu, tukashindwa kujizuia hisia zetu na kujikuta tukizama kwenye mahaba mazito ambayo kila mmoja alijitahidi kuhakikisha kwamba ana mridhisha mwenzake kwa kiwango cha juu. Tukamaliza mzunguko huu na tukajilza kwenye sinki hili la kuogea.
“Baby”       
“Mmmmm”
“Una mpango gani na maisha yako ya mpira ya baadae?”
“Nitainia kwenye timu yoyote kubwa ambayo itanihitaji”
“Kama?”
 
“Liverpool, Real Madrid”
“Unaipenda sana Liverpool?”
“Yaa nina ipenda, ila kama watanihitaji kwa dau kubwa basi nitakubali kuungana nao?”
“Inabidi unifanye niwe wakala wako”
“Haahaaa”
“Ndio mume wangu, kila kitu kiwe kwa ajili ya familia yetu. Lazima nikusimamie kwenye kila jambo zuri ambalo badae litatufanya tuishi maisha mazuri”
“Usijali mke wangu, nina imani kwamba kuna mawakala wengi watajitokeza. Mbaya sina msimamizi, baba alisha fariki na aliniacha katika wakati mgumu kiasi wa kusimamia kampuni zake. Kwa hiyo nahitaji mtu makini katika maisha yangu ya soka”
“Sawa mume wangu, kama utapenda utaniweka mimi?”
“Nitalifikiria hilo, il aje siku ukiwa mjamzito kweli utaweza kusafiria masafa ya mbali kuingia mikataba na timu kubwa kubwa?”
 
“Kwani mume wangu mimba nina ibeba mwaka mzima. Tutapanga mpango madhubuti na tena mume wangu, tufanye jambo juu ya hili sawa. Maliza masomo yako nami nimalize yangu kisha tutaendelea na biashara yetu ya mpira huu wa miguu”
“Sawa tuombe Mungu”
“Timu ambayo itataka kukunununua, ni lazima ikulipe paund dola laki tano mshabara wa wiki”
“Mmmm mke wangu, unataka nikawe mbuzi wa albadili huko kwenye timu za watu?”
“Kwa nini?”
“Msaada wangu kwenye timu ni lazima uwe mkubwa kutokana kile wanacho nilipa”
“Mungu atakujalia Mume wangu”
“Kweli na utafanikiwa tu mume wangu”
“Haya”
 
Tukamaliza kuoga, tuvaa nguo za kushindia kwa usiku huu. Tukajumuika na wachezaji wezangu katika kupata chakula cha usiku. Tukiwa katika eneo hili tukaanza kuwaona walinzi wa baba Camila wakiingizana humu ndani jambo lililo tufanya watu wote humu kupatwa na mshangao. Tukawaona wazazi wa Camila ambao kwa kipindi hichi ni maarufu sana hapa Ujerumani, hii ni kutokana na nafasi ya kiti cha uraisi anacho kigombania baba yake.
Mimi na Camila tukanyanyuka na kuwakaribisha kwa furaha sana.
“Tumewafanyia suprize”   
Baba Camila alizungumza huku akinisalimia kwa kunipa mkono.

“Tunashukuru sana, karibuni sana wazazi wetu”
“Asanteni”
Tukakaa nao katika meza tuliyo kuwa tumeketi.
“Kwa goli ambalo Ethan umefunga leo, yaani nilisime hapana. Nilazima nije nikuangalie vizuri mwanangu. Heee hapana kwa kweli”
Mama Camila alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana.
“Nashukuru sana mama. Kumbe mama na wewe huwa unatazama mpira ehee?”
“Yaani toka ulipo anaza kucheza wewe, nikaanza kupenda mpira. Unakumbuka ile siku ambayo Camila alitaka kujirusha gorofani?”
 
“Ndio ndio nakumbuka mama?”
“Sasa siku ile ndio nilipenda kutazama mpira, hakika nina mkwe ambaye anatufanya kila muda tujisikie amani katika mioyo yetu”
“Nashukuru sana mama”
“Kocha wenu yupo wapi?”
“Yule kule”
Nikamuita kocha kwa ishara, akasimama na kutufwata eneo hili tulio kaa.
“Hongera sana kwa wachezaji wako ulivyo waanda. Yaani wanatupa buruni moja nzuri sana”
“Nashukuru sana mkuu”
“Nikipata nafasi, nitapendekeza uinoe timu ya taifa na hii mashine yako hapa nayo iwepo katika timu yako ya Taifa”
Maneno ya baba Camila yakanistua kidoo, kwani katika maisha yangu yote ya kuishia hapa Ujerumani, sijawahi kufikiria kuichezea timu ya taifa ya nchi hii japo nina uraia wa hapa Ujerumani. Nchi yangu mimi ni Tanzania na mimi ni Mtanzania na kamwe sinto isaliti Tanzania hususani katika maswala ya mpira ninao cheza.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )