Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, November 25, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 37

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA
“Sasa siku ile ndio nilipenda kutazama mpira, hakika nina mkwe ambaye anatufanya kila muda tujisikie amani katika mioyo yetu”
“Nashukuru sana mama”
“Kocha wenu yupo wapi?”
“Yule kule”
Nikamuita kocha kwa ishara, akasimama na kutufwata eneo hili tulio kaa.
“Hongera sana kwa wachezaji wako ulivyo waanda. Yaani wanatupa buruni moja nzuri sana”
“Nashukuru sana mkuu”
“Nikipata nafasi, nitapendekeza uinoe timu ya taifa na hii mashine yako hapa nayo iwepo katika timu yako ya Taifa”
Maneno ya baba Camila yakanistua kidoo, kwani katika maisha yangu yote ya kuishia hapa Ujerumani, sijawahi kufikiria kuichezea timu ya taifa ya nchi hii japo nina uraia wa hapa Ujerumani. Nchi yangu mimi ni Tanzania na mimi ni Mtanzania na kamwe sinto isaliti Tanzania hususani katika maswala ya mpira ninao cheza.

ENDELEA
Nikatabasamu usoni mwangu,  ili kuficha msimamo wangu nilio nao moyoni mwangu, amboa kuutangaza kwa sasa itanigarimu sana maisha yangu katika soka.
“Nitashukuru  sana mkuu, nami nitajitahidi kuhakikisha kwamba ninaipelekea timu ya taifa katika viwango vya juu kabisa vya kimataifa vya Fifa”
“Nashukuru sana”
Kocha na baba Camila wakamaliza kusalimiana na kisha kocha akarudi kukaa katika kite chetu.
“Tunaweza kupata muda wa kuzungumza nanyi wawili?”
Mama Camil alizungumza huku akitutazama usoni mwetu.
“Ndio hakuna tatizo mama yangu”
“Basi twendeni tukazungumze”
Nilizungumza huku nikimtazama mama Camila usoni mwake. Tukaondoka eneo hili na kuingia kwenye moja ya ofisi iliyo andaliwa kwa ajili yetu. Tukaingia watu wa nne na walinzi wote wakabaki nje. Ukimya wa sekunde kadhaa ukatawala katika eneo hili huku mimi na Camila tukiwa tunawatazama.
“Nina imani kwamba mumebakisha mwaka mmoja kabla hamjafikisha kiwango cha miaka kumi na nane si ndio?”
 
“Ndio ndio baba”
Niliitika wa unyonge, kwani mazungumzo ambayo naamini yanazungumzwa hapa ni muhimu sana.
“Na munapenda sana?”
“Ndio mama”
“Labda nichukue muda mwengine Ethan, kwa niaba ya familia yangu, ninakuomba unisamehe sana kwa yale yaliyo jitokeza kati yako wewe na Camila pamoja na familia nzima. Hakika tulishindwa kumzuia mtoto wetu, akafanya jambo la kipumbavu  ambalo hadi leo hii, linaniumiza sana”
“Musijali wazazi wangu, ninaelewa hilo na tulisha lizungumza, tuacha yaliyo pita tutazame haya taliyopo mbele yetu”
 
“Nafurahi kusikia hivyo”
“Mimi na baba yenu, niliona kuna umuhimu endapo mukifikisha miaka kumi na nane muvishane pete ya uchumba, kisha nyinyi mutapanga ni muda gani munaweza kuoana”
Jambo hili kidogo likatufanya tustuke kwani tangu tuanze mahusiano yetu hatukuwahi kuketi chini na wazazi hawa na kuzungumzia lolote kuhusiana mapenzi yetu.
“Sawa sisi hili halina tatizo wazazi wangu. Nipo tayari kumuoa Camila kwa garama ya aina yoyote mutakayo nitajia”
 
“Hapana, unayo yafanya kwenye maisha ya famili hii ni garama tosha. Nakukabidhi mwanangu. Kumbuka ni mtoto wetu wa pekee, hatuna mwengine hata wa kusingizia na wala hakujawahi kuwazia kama tutapata mwenzake.”
“Musijali, tambueni kwamba nafanya kila jambo kwa ajili ya Camila. Ninaandaa familia bora kwa ajili yake, ninawahakikishia kwamba mtoto wenu yupo katika mikono salama. Mikono ambayo hakuna ambaye ataweza kuichafua””
“Asante sana mwanangu Ethan. Kuna jambo jengine nilizungumza na baba yako hapa akalipitisha. Kama unavyo fahamu tupo kwenye kipindi cha uchaguzi. Kila anaye gombani kiti hichi anafanya analo weza kuhakikisha kwamba anapata nafasi ya kuwa raisi. Nikiwa kama kampeni meneja wa baba yenu, nilikuwa nina pendekeza Ethan uweze kufanya tangazo moja la kumsaidia baba yako ili katika uchaguzi huu aweze kushinda?”
“Hili halina tabu mama, nakumbuka Camila nilisha kuambia hili si kweli?”
“Yaa kweli uliniambia”
“Hilo halina tatizo, nyinyi andaeni tu tangazo na nitalifanya kwa moja mmoja”
 
“Tunashukuru sana”
“Endapo Mungu akinijalia kuingia ikulu, nitakurudishia kiasi ulicho wekeza japo si kwa siku moja basi hata taratibu taratibu kwa maana nina imani kwamba wewe ni mfanya biashara, umetoa kiasi hicho kwenye makampuni yako kuhakikisha kwamba mambo kwa upande wangu yanakwenda vizuri nami nitalipa fadhila kwa kuyapunguzia makampuni yako kodi”
“Nashukuru sana baba”
Nilizungumza huku nikiwa nimejawa  na furaha kwani katika vitu ambavyo ninavichukia katika biashara  nikulipa kodi kubwa serikalini.
“Kesho Ethan muna ratiba gani na kocha wako?”
Mama Camila aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.
“Kesho nahisi tutapumzika tukisubiria mzunguko wa mtaano”
“Sawa, basi kesho tutatuma walinzi waje wawachukue na wawalete studio uweze kutengeza tangazo la kempeni”
“Usijali mama yangu”
 
“Na mimi mama nahitaji kuwemo kwenye tangazo hilo”
“Sawa tutaangalia kama muandishi wa tangazo atakupatia nafasi basi nawe utakuwepo”
“Nashukuru mama”
Tukazungumza mazungomzo mengi sana na mipango yetu ya baadae kisha wazazi wa Camila wakaagana na wachezaji wa timu yetu kisha wakaondoka. Nikamueleza kocha juu ya ombi nililo ombwa la kwenda kutengeneza tangazo la kampeni, kocha hakuwa na kinyongo na jambo hilo zaidi alichi kihitaji niweze kuwa makini. Nilipo maliza kuzungumza na kocha nikaingia chumbani na kumkuta Camila akiwa amejilaza kitandani kama alivyo zaliwa. Nikamtazama kwa muda huku nikimmezea mate ya uchu, taratibu nikavua nguo zangu kisha nami nikapanda kitandani. Nikaanza kumpapasa mapajani mwake.
 
“Jamani Ethan tulale bwana”
“Nina hamu na wewe bwana mke wangu”
“Mmmmm…..”
Camila alinung’unika kwa sauti iliyo jaa mahaba. Kabla sijafanya kitu chochote, simu yangu ikaanza kuita, nikashuka kitandani na kuichukua juu ya meza. Nikaitazama namba hii ya mwanasheria wa kampuni zangu, kisha nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.
“Ndio mwanasheri?”
“Nina habari nzuri kidogo japo sio sana”
“Nimabie ni habari gani?”
“Vijana wamesha fika nchini Tanzania, na wapo kwenye hicho kijiji, na hivi sasa wapo kwenye hicho kijiji na wanafanya upelelezi wa kufahamu ni wapi alipo mama yako”
“Ohooo asante Mungu, naomba unifahamishe kila kitu kinacho endelea sawa”
 
“Sawa mkuu, kila kitu nitakujulisha hata kwa meseji”
“Nashukuru”
Nikakata simu huku moyo wangu, ukiwa ametawaliwa na furaha sana.
“Kuna nini mume wangu?”
“Wanakaribia kumpata mama yangu?”
“Kweli?”
“Ndio mke wangu”
Camila akanikumbatia kwa nguvu huku naye akionekana kujawa na furaha juu ya hili swala hili.
“Nina hamu ya kumuona mama yangu mkwe”
“Mungu ni mwema atasaidia kwa kweli”
Camila akanionyesha picha za mama zilizipo kwenye simu ambazo zinamuonyesha alivyo tekwa.
                                                                                                               ***
Asubuhi na mapema tukaingia katika helicopter maalumu iliyo agizwa kuja kutuchukua hapa hotelini. Tukaelekea katika mji wa FrankFurt ambapo ndipo ilipo kambi ya kampeni ya baba Camila. Tukapokelewa na mama Camila na moja kwa moja tukaelekea katika studio kubwa za televishon ambayo ni mali ya babu Camila aliye kuwa raisi kabla ya raisi wa hivi sasa ambaye naye muda wake unakwenda kuisha.
“Mke wangu nahisi kijimoyo kina nidunda dunda?”
Nilizungumza kwa sauti ya chini huku nikimnong’oneza Camila sikioni mwake.
 
“Usiogope mume wangu jiamini”
“Mmmmm, unajua sijawahi kufanya vitu kama hivi na jua kila mtu ana ujuzi sehemu yake”
“Haahaa, hembu vuta pumzi kwa nguvu kisha iachie taratibu”
Nikafanya kama Camil alivyo nieelekeza.
“Unajisikiaje?”
“Kidogo nafufuu”
“Ethan kunata na Gibson, huyu ndio muongozaji wa kutengeneza tangazo hili. Gibson nina imani sina haja ya kukutambulisha huyu ni mkwe wangu”
“Usijali madam, ninamtambua sana Ethan”
“Nashukuru, sas anaomba uweze kumpatia maelezo ya jinsi gani atakavyo weza kuanza kulicheza tangazo”
“Sawa”
 
“Jikaze mume wangu”
Camila aliniambia kwa kunikongoneza. Nikamjibu kwa kutingisha kichwa, tukaingia katika moja ya chumba ambacho kina wadada dada wengi pamoja na nguo nyingi za kubadilishia. Eneo hili la ukumbi ni kubwa sana na limegawanyishwa katika vyumba vyumba kadhaa. Gibson akanipatia kitabu kidogo. Wadada wote humu ndani, dhairi wanaonekana kuna na hamu hata ya kunigusa, ila kutokana tupo kazini hakuna aliye thubutu kunisogelea.
“Maelezo kwa ufupi yaliyomo ndani ya hicho kitabu, yanaelezea jinsi unavyo takiwa kuigiza ukiwa mtaani, unakimbia na mpira miguuni. Unalikuta hili kundi la wadada, unawauliza kwamba wanajua nani ni kiongozi mzuri wa kumchagua. Wadada hawa watakuwa wanashangaa shangaa, utavua begi lako mgongoni, utatoa bando la vipeperushi na kuwakabidhi mmoja baada ya mwengine na watakuwa wanakuzunguka huku wanakushika shika mwilini mwako. Hadi hapo umenielewa Ethan?”
 
“Ndio nimekuelewa, endelea”
“Utaachana na wadada hao na utaendelea kukimbia na mpira, mbele kidogo utakutaa na Camila akiwa anahangaika kuliweka sawa sawa tambaa kubwa lenye picha ya mgombea uraisi. Utakacho fanya wewe utarudi nyuma kidogo kisha utapiga suti kali, mpira utagonga katika sehemu ya tambara hilo iliyo jikunja kisha taratibu tambara hilo litafunguka na kuonyesha picha vizuri ya mgombe uraisi, mutalitazama kisha mutasema maneo ya kumchagua mgombea uraisi, sawa”
“Sawa”
“Hapo nywele zako zitatengenezwa kidogo na utafanyiwa makeup”
“Poa poa”
“Make anzeni kumshuhulikia Ethan, ninakwenda kumuelekeza Camila. Endelea kusoma taratibu ili uweze kuelewa, sawa?”
 
“Sawa”
Wadada waanne maalumu kwa shuhuli ya kunipodoa wakaanza kazi waliyo agizwa. Nikayarudia kuyasoma maeleo hayo na nikayaelewa vizuri. Baada ya muda kadhaa wakamaliza shuhuli hiyo. Tukatoka nje ya studio hizi na kuingia mtaani na kuanza kutengeneza tangazo hilo. Nikavaa jezi zangu za michezo pamoja na kibegi kidogo kisha nikaanza kuigiza zoezi hili. Hapo awali kidogo liliniwia ugumu kuigiza, ila kadri jinsi nilivyo igiza ndivyo jinsi nilivyo jikuta nina himli tamhazo hilo. Hadi inafikama majira ya jioni tukamaliza kutengeza tangazo hili na ambalo hakika ni zuri sana.
 
“Mume wangu kuna missed call thelathini kwenye simu yako”
Camil alizungumza huku akinikabidhi simu yangu
“Zimetokea wapi?
“Sijatazama, unaweza kutazama”
Nikafungua missed call hizo na kukuta zimetoka kwa mwanasheria wa kampuni. Nikampigia, simu yake haikuita snaa ikapokelewa.
“Mkuu ulikuwa wapi?”
Mwanasheria alizungunguza huku akiwa na wasiwasi mwingi sana.
“Ohoo samahani sana mzee nilikuwa nina fanya tangazo moja hivi”
“Sawa, nina habari kutoka nchini Tanzania”
“Ehee niambie”
“Mama yako amepatika”
“Kweli?”
Niliuliza kwa shauku iliyo ambatana na furaha kubwa sana.
“Ndio amepatika, ila…….”
Mwanasheria alizungumza kwa sauti ya upole na unyonge kidogo.
 
“Ila nini?”                   
Nilimuuliza mwanasheria huku furaha yangu ambayo nilikuwa nayo ikaanza kunipotea taratibu.
“Hali yake sio nzuri, katika harakati za kumkomboa kwa bahati mbaya alipunyuliwa na risasi ya kichwani mwake na kumfanya apoteze fahamu, na ninavyo zungumza hivi sasa, wapo njiana wanakuja naye nchini humu”
Nikajikuta nikinyon’gonyea na taratibu nikakaa chini na kumfanya Camila na watu wengine kunishangaa, kwa maana ni muda mchache tu wametoka kuniona nikiwa nimejawa na furaha sana

==>>ITAENDELEA KESHO
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )