Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, November 3, 2018

Sakata la Zitto lamuibua Lema, sasa kuitisha mkutano wa dharula wa wabunge wote

adv1
Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema amewataka wabunge kuandaa mkutano maalum utakaojadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi kwa sasa kwa kile alichokidai kuwa hiyo ni haki yao ya kisiasa.

Ameyasema hayo jijini Arusha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa ataitisha mkutano wa dharula utakaohusisha wabunge ili kujadili mambo mbalimbali.

Lema amependekeza kuanzishwa kwa tume huru ya uchunguzi ili kuchunguza taarifa ya mauaji iliyotolewa na jeshi la polisi na kuleta mkanganyiko dhidi ya taarifa iliyotolewa na mbunge Zitto Kabwe.

“Mkutano wa dharula uitwe Dar es salaam au Dodoma, na wabunge wote tukutane ili tutafute njia sahihi ya kupigania haki zetu za mikutano, na hatawakizuia ila iwe chanzo cha kuheshimu katiba. Hatuwezi kuendelea kuishi hivi.” Amesema Lema

Aidha, amesema kuwa Zitto amesema watu waliokufa ni wengi, idadi ya watu waliokufa ndiyo kinachopingwa na anachopendekeza kiwepo chombo cha mbadala cha uchunguzi ili ijulikane nani mkweli kati ya  Zitto, Polisi au Mbunge wa jimbo lile Mwilima.
 
Zitto Kabwe jana  alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa makosa matatu ya uchochezi, ambapo aliachiwa kwa dhamana na kesi yake itasikilizwa novemba 12 mwaka huu.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )