Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, November 7, 2018

Serikali kuja na mfuko mpya wa bima ya afya kwa Wanajeshi

adv1
Kufuatia malalamiko ya huduma za tiba kutokidhi mahitaji halisi kwa wanajeshi, Serikali imesema inakamilisha taratibu ili kupata ridhaa ya kuanzisha mfuko mpya wa bima za afya kwa ajili yao.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Waziri wa Ulinzi Dkt Hussein Mwinyi akijibu swali la Mbunge wa Rashid Kuachua ambaye alihoji kuwepo kwa malalamiko ya wanajeshi juu ya kutounganishwa kwenye mpango wa bima ya afya.

Akijibu swali hilo Waziri wa Ulinzi Dkt Hussein Mwinyi amekiri kuwepo kwa malalamiko ya huduma ya tiba katika hospitali za jeshi na kuongeza hivi karibuni wataanza mfumo huo.

“Ni kweli kuwa yapo matatizo juu ya huduma za tiba kwenye hospitali za jeshi kunakosababishwa na gharama ya fedha kutokana na hayo mapungufu serikali inamalizia taratibu ili kupata ridhaa ya kuwa na bima kwa ajiili ya jeshi la ulinzi la Tanzania.” Amesema Waziri Mwinyi

Aidha Waziri Mwinyi amesema “mfuko huo wa jeshi hautaleta mgongano wa kimaslahi baina yake na mfuko wa taifa na lengo kubwa ni kuendelea kuimarisha jeshi letu.”
 
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )