Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, November 13, 2018

Serikali yapiga marufuku Walimu kutoa adhabu ya viboko kwa wanafunzi

Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Elimu William Ole Nasha imepiga marufuku Walimu kutoa adhabu ya viboko kwa mwanafunzi bila kibali maalum na pia amepiga marufuku Walimu kutembea na viboko.

Ole Nasha ametoa agizo hilo wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalum CCM Rose Tweve aliyetaka kujua kauli ya Serikali kwa Walimu wanaokiuka sheria za adhabu kwa Wanafunzi

“Haitakiwi vizidi viboko vinne, hairuhusiwi kwa mwalimu yeyote yule kuchapa viboko, bali ni mwalimu mkuu tu, na lazima kiombwe kibali cha kufanya hivyo, ni marufuku mwalimu yeyote kumchapa mwanafunzi kinyume na taratibu na sheria, lakini vile vile na marufuku mwalimu yoyote kutembea na viboko kwa lengo la kumchapa mwanafunzi, kwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria na hatua zitachukuliwa”, alisikika Naibu Waziri wa Elimu William Tate Ole Nasha.

Hivi karibuni kulikuwa na mjadala wa kuchapwa viboko wanafunzi baada ya mwanafunzi mmoja kufariki dunia baada ya kuchapwa viboko na mwalimu wake, akimtuhumu kuiba pochi yake ambayo baadaye aliletewa na dereva boda boda baada ya kuisahau.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )