Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, November 27, 2018

TFS Yawasimamisha Kazi Watumishi 11 Kutekeleza Majukumu Yao

Kashfa ya uhujumu uchumi imetajwa kuwa chanzo cha  watumishi 11 wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kusimamishwa kazi huku wengine wakifikishwa mahakamani.

Taarifa iliyotolewa  Jumatatu Novemba 26, 2018 na mkuu wa kitengo cha mawasiliano Wizara ya Maliasili na Utalii, Dirona Makaya amesema watumishi hao wamesimamishwa kazi kufuatia operesheni maalumu iliyofanyika kwenye vijiji na misitu na kubaini uvunwaji haramu wa miti aina ya Mkurungu.

TFS imezuia biashara ya mti wa Mkurungu kwa matumizi ya ndani au kusafirishwa nje ya nchi hadi taarifa rasmi itakapotolewa.

‘’Kufuatia uchunguzi uliofanywa, gari moja lilikamatwa likiwa na mbao 382 za mti wa Mkurungu na kuzuiliwa kwa uchunguzi ambapo watuhumiwa wawili walikamatwa,’’ amesema Makaya.

Amesema mbao 825 zilikamatwa zikisafirishwa kwa treni katika  stesheni ya Usule, Shinyanga na watuhumiwa sita  ambao ni watumishi wa reli wamekamatwa  kwa mahojiano.

Hata hivyo, majina na vyeo vya watumishi hao havikuwekwa wazi kwenye taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza mamlaka hiyo kwa kusirikiana na Kikosi cha Kuzuia Ujangili  (NTAP) wamezuia halmashauri kuendesha biashara ya miti bila idhini ya mamlaka husika.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )