Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, November 14, 2018

Watalii 10,000 kutoka China kuja kuitembelea Tanzania mwakani

adv1
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesaini makubaliano na kampuni ya Touchroad International Group ya China kwa ajili ya kusafirisha watalii 10,000 kutoka jiji la Shanghai kutembelea Tanzania mwaka 2019 kwa kutumia ndege Maalum (chartered flights).

Makubaliano hayo yalisainiwa sambamba na mikutano ya kutangaza utalii katika soko la China- Tourism Roadshow katika miji mitano ya China iliyoanza katika jiji la Shanghai tarehe 12 Novemba 2018.

Mikutano hiyo ni matokeo ya jitihada za Ubalozi wa Tanzania nchini China kwa kushirikiana na TTB ambapo katika mkutano wa kwanza uliofunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki, washiriki mbalimbali zaidi ya 200 walijitokeza wakiwemo makampuni ya utalii (tour operators), mawakala wa usafirishaji (travel agents), mashirika ya ndege (airlines), na vyombo vya habari.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii, Bi. Devotha Mdachi alitoa mada maalum kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania pamoja na fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii. Aidha, makampuni ya utalii kutoka Tanzania yalipata fursa ya kuelezea packages zao za utalii mahsusi kwa soko la China. Kadhalika, Shirika la Ndege la Tanzania lilitumia fursa hiyo kutangaza juu ya mpango wake wa kuanza safari za moja kwa moja kutoka Tanzania hadi China katika mji wa Guangzhou mwezi Februari 2019.

Mikutano ya kutangaza utalii itaendelea kufanyika katika miji mingine ikiwa ni pamoja na Guangzhou tarehe 14 Novemba 2018, Hong Kong tarehe 16 Novemba 2018, Chengdu tarehe 19 Novemba 2018 na Beijing tarehe 20 Novemba 2018.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, 13 Novemba 2018
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )