Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, November 4, 2018

Watalii MASHOGA Kutimuliwa Nchini

Waziri wa Mali Asili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla, ameweka wazi juu ya mpango wa kuwarudisha kwao watalii watakaoingia nchini, ambao watabainika kuwa wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Kigwangalla ameweka wazi msimamo huo kupitia ukurasa wake wa Twitter alipokuwa akijibizana na wafuasi wake ambao walikuwa wakijaribu kumuonya kuhusu kuingilia kati suala la 'ushoga' kuwa litaathiri utalii wa nchi.

Waziri Kigwangalla amesema kwamba watu hao watarudishwa kwao wakiwa uwanja wa ndege mara tu baada ya kutua.

"Machoko hawatoingia hapa, wataishia airport na kurudishwa walikotoka"-Ameandika Kigwangalla
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )