Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, November 26, 2018

Zitto Kabwe Mahakamani Tena Leo

adv1
Kesi ya jinai namba 367 ya mwaka 2018 inayomkabili Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe itaendelea leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini, anakabiliwa na mashtaka matatu likiwamo la uchochezi na kutoa taarifa za uongo kuhusu mauaji ya baadhi ya askari polisi na wananchi katika Kijiji cha Mpeta, wilayani Uvinza mkoa wa Kigoma.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu alisema wananchi wafuatilie habari hiyo kupitia vyombo vya habari na waliopo katika jiji la Dar es Salaam wafike mahakamani.

“Tunapenda kuwataarifu wananchi na wanachama wetu kuwa kesi inayomkabili Zitto itaendelea kesho hivyo tunawaomba tukutane Kisutu,” alisema Shaibu.

Alisema wanawashukuru wote waliosaidia kutoa shinikizo lililosaidia kumwachia huru ama kumpeleka mahakamani.

“Tunaamini kuwa shinikizo hilo ndilo lililosababisha Jeshi la Polisi kumpeleka kiongozi wetu mahakamani na kupata dhamana,” alisema Shaibu.

Shaibu alisema kitendo cha viongozi wa vyama vya siasa kuwa na kesi mahakamani kimeunganisha vyama vyote vya upinzani na kuondosha tofauti zao.

“Hizi kesi kadri zinavyoendelea zinatuleta pamoja tunatoa salamu za kimshikamano kwa wenzetu tuko pamoja nao katika kesi zao  CUF  na Chadema,” alisema Shaibu.

Akizungumzia suala la uvuvi Shaibu aliitaka Serikali kuwashirikisha wavuvi kwenye utungaji wa sheria, kanuni na makato pia kwenye programu zake hasa zinazowagusa wavuvi moja kwa moja ili kujua mahitaji yao.

Alisema Serikali ihakikishe inapofanya operesheni kukabiliana na uvuvi haramu wasiteketeze zana zingine ambazo si haramu kama vile mitumbwi ya wavuvi.

“Tunawaomba wavuvi watoe ushirikiano kwa serikali katika kuwabaini wanaojihusisha na uvuvi  haramu  kwakuwa maziwa na bahari vikibaki bila samaki hata wavuvi hawatakuwapo,” alisema Shaibu.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )