Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, December 20, 2018

Abdallah Mtolea Kapita Bila Kupingwa....Mkurugenzi Kamtangaza Kuwa Mbunge Temeke

adv1
Abdallah Mtolea, aliyepitishwa na CCM kuwania Ubunge wa Temeke,  leo Alhamisi Desemba 20, 2018 amepita bila kupingwa baada ya wagombea waliokuwa wamechukua fomu kuwania nafasi hiyo  kukosa sifa.

Mtolea aliyekuwa mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CUF hadi Novemba 2018 alipojiunga na CCM na kupitishwa kuwania ubunge, leo Alhamisi Desemba 20, 2018 ametangazwa na msimamizi wa uchaguzi, Lusubilo Mwakabibi kuwa mshindi.

Kifungu cha 45 (2) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, na kile cha 44 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, vinasema endapo mgombea aliyeteuliwa katika uchaguzi ni mmoja tu, mgombea huyo atahesabika amechaguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )