Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, December 4, 2018

Afisa Uvuvi Ilemela Mbaroni Kwa Rushwa Ya Mil.1.5

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Mwanza inamshikilia ofisa uvuvi wa manispaa ya Ilemela, Williadius Buberwa (33) kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh. milioni 1.5.

Imeelezwa kuwa kitendo hicho ni kinyume na kifungu cha 15(1) cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Desemba 4, 2018 naibu mkuu wa Takukuru mkoani Mwanza, Emmanuel Stenga amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani muda wowote leo.

Stenga amesema  mtuhumiwa huyo alifanya doria isiyo rasmi katika eneo la Tunza wilayani Ilemela Oktoba 25, 2018 kwenye boti ya mfanyabiashara huyo na kukuta ana vibali vyote.

Stenga amesema mtuhumiwa aliweka kikwazo, kuzuia samaki kushushwa na kutishia kuwataifisha endapo asingepewa fedha.

“Aliomba rushwa ya Sh 2milioni ila mfanyabiashara huyo aliomba kiwango kipungue na kufika  Sh1.5milioni. Alipopewa fedha ndio akaruhusu mzigo kupakiwa kwenye gari,” amesema Stenga.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )