Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, December 3, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 166 na 167 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
   
“DAANY?”
“Waziri mkuu, na mkuu wa NSS hukuona thamani yao hata ta nikiwaua kwako ilikuwa ni POA tuu, sasa huyu mume wako nitamuua kama nilivyo fanya kwa waziri mkuu wako”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiichomoa bastola yangu moja kiunoni mwangu na kuielekeza kwenye kichwa cha mzee huyu aliye zidi kutetemeka hadi mikojo ikaanza kulowanisha suruali yake.
“Dany Dany ninakuomba, ninakuomba mpenzi wangu usimuue huyo mwanaumee tafadhalii…………………!!”
K2 alizungumza kwa sauti iliyo jaa woga na majonzi hapa ndipo nikagundua udhaifu wa K2 upo kwa huyu mkuu wa polisi ambaye kwa muonekano wa nje ni mbaya mbaya tu na sijui amempa nini K2 hadi leo hii analia kwa ajili yake.
   
ENDELEA   
“Hahaaaa muheshimiwa raisi unaniitaje mimi leo?”
“Dany nipo na wageni ninakuomba hili swala tulizungumze wawili nipo tayari kuonana na wewe na niambie chochote nitafanya tafadhali Dany”
K2 alizungumza kwa sauti iliyo jaa majonzi na kunibembeleza sana.
‘Huu ni mtego’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikimtazama mzee huyu.
“Utaniambia muda na wapi tunaweza kuonana ila una lisaa moja mbele. Andaa sanda yako kwani sinto kwenda kukuacha hai”
Nikasikia mihemo ya K2 jinsi anavyo ishusha kwenye simu yake.
“Naomba masaa mawili”
“Basi utaongeza hili. Hakikisha kwamba unatangaza kujiudhuru hadharani ili nikikuua ufe kama K2 na si raisi K2”
“Sawa Dany nimekuelewa”
Nikata simu na kumtazama mzee huyu.
“Mfunge pingu na tuondoke”
“Sawa mkuu”
“Hakikisha unawavua askari watatu nguo zao, zitatusaidia”
“Usijali mkuu”
Nikaanza kurudi kwenye gari, nikafungua mlango na kuingia kwenye gari, Babyanka akaingia ndani ya gari huku akishusha pumzi nyingi.
 “Hatuna raisi kwa kweli”
“Mulimchagua kwa kura zenu”
“Amesemaje?”
“Nimemuambia kwamba atafute sehemu tuonane na nimemuomba masaa mawili ili tuweze kuonana”
“Hivi unahisi kwamba K2 ni mjinga wa kukubali kuonana nawe kirahisi namna hiyo?”
 
“Nimemuambia atangaze kujiudhuru nafasi ya raisi ndani ya masaa mawili ya jayo, pasipo kufanya hivyo huyu mzee nina muua”
Nilizungumza huku tukiondoka eneo hili kwa kasi sana, kwani hatuna tulicho kibakisha.
“K2 umeanza naye mahisiano lini ikiwa ana mume wake?”
Nilimuuliza mzee huyu huku nikizidi kuongeza mwendo kasi wa gari hili.
“N…….ii..i.i.i aa…aaal….i….li…taka”
“Zungumza vizuri wewe”
Martin alizungumza kwa ukali huku akimtandika ngumi ya mbavu mkuu huyu wa polisi na kumfanya atoe kilio cha maumivu makali sana.
“Alinitaka yeye mwenyewee”
“Umempa nini hadi ana kupapatikia hivi, au ulimla m***?”
“Weee Dany swali gani hilo?”
“Babyanka unashangaa kwa raii wako kufanya
 
“Wewe umejuaje?”
“Tuachane na hayo”
“Au na wewe umesha a kwa maana kipindi kile nilikuwa siwaelewi elewi”   
“Tunaelekea wapi Babyanka tuachane na hayo mazungumzo”
“Kwanza zima simu ya huyo mzee toa laini na itupe la sivyo kufwatiliwa ni lazima”
Nikamkabidhi Babyanka simu yamzee huyu, akatoa betri pamoja na laini kisha akaitupa. Kunja kushoto”
Babyanka alizungumza na kunifanya nipunguze mwendo kasi wa gari na kukunja kushoto.
“Tunaelekea wapi?”
“Tukipite barabara hii kukamatwa ni lazima”
“Sawa”
Tukazidi kusonga mbele huku tukihakikisha kwamba tunaweza kufika jijini Dar es Salaam pasipo kukamatwa na mtu yoyote. 
 
“Kuna rafiki yangu maeneo ya hapo Tegeta inabidi tufike kwake”
“Anafanya kazi gani?”
“Alikuwa NSS, ila alikuja kuacha na kuunda kikosi chake cha ulinzi”
“Ulinzi gani?”
“Hawa walinzi walnao linda kwneye makampuni binafs”
Babyanka alizungumza huku akitoa simu yake mfukoni, akaminya minya batani na kumpigia rafiki yake huyo.
“Winy upo wapi mama?”
“Nipo karibu na getini kwako”
“Sawa dakika moja tu nitakuwa hapo”
Babyanka alizungumza kisha akakata simu
“Utasimama kwenye nyumba ile pale”
Taratibu nikapunguza mwendo kasi wa gari hadi kwenye geti la jumba hili la kifahari, nikasimama getini taratibu geti hili kubwa likafunguliwa, nikaingiza gari hili ndani na kulisimamisha nyuma ya gari jengine.
 
“Nisubirini”
Babyanka alizungumza huku akishuka kwenye gari hili. Akazungumza na dada mmoja mrefu mweusi kiasi na ana umbo jembaba kidogo. Taratibu nigemgeukia mzee huyu aliye kaa siti ya nyuma na Martin. Nikamtazama vizuri kuanzia usoni mwake hadi kifuania mwake, kisha nikajikuta nikitabasamu.
“Mzee una nifahamu mimi?”
Mzee huyu akatingisha kichwa akionyesha kunifahamu.
“Unanifahamu mimi kama nani?”
“Ehee?”
“Mzee wangu unaelewa maswali yangu mbona unajifanya huelewi”
Kabla mzee huyu kunijibu kitu chochote Babyanka akagonga kidogo kioo cha upande wangu, taratibu nikashuha kioo.
“Unaweza kushuka”
Taratibu nikashuka, dada huyu alipo nitazama akaonekena kushangaa sana.
 
“Ulihisi ninakutania Winy”
“Yaa nilihisi unanitania kwa manaa wewe ndio ulikuwa unaongoza jaramba la kumkamata Dany ila leo hii upon aye yaani siamini”
“Ndio uamini. Dany huyu ni rafiki yangu wa damu kabisa, anaitwa Winy. Winy huyu ni Dany”
“Nashukuru kukufahamu Dany”
Winy alizungumza kwa furaha huku akinipa mkono, taratibu nikaupokea mkono wake huku nikiutingisha kidogo.
“Asante Winy”
“Yupo na kijana wake pamoja na fala mmoja hivi tumemkamata njiani”
“Waambie washuke”
Nikaonyesha ishara ambayo nina imani kwamba Martin anaifahamu, akashuka kwenye gari huku bunduki yake akiwa ameishia vizuri. Akatufwata shehemu tulipo akasalimiana na Winy, kisha akafungua mlango na kumtoa mkuu wa Polisi.
“Wewe fala ulihisi sinto kupata eheee?”
Winy alizungumza huku akianza kumfwata mzee huyu jambo lililo tushangaza wote hapa. Akamsukumia mkuu wa polisi kwenye gari huku akilikunja shati la mzee huyu maeneo ya kifuani mwake.
“Ulihisi sinto kupata mjinga wewe”
“Vipi shosti?”
“Huyu mzee jana amemlaza ndani mdogo wangu, na akakataa asitolewe dhamana”
“Kwa nini usiniambie?”
“Nilijaribu kukupigia sikukupata hewani”
Winy akamtandika makofi mawali mazito mzee huyu hadi machozi yakaanza kumlenga lenga.
“Sasa leo umeingia mikononi mwangu, utaona sasa kama humu utatoka kwa dhamana”
“Huyu dada anaonekana na ni mbabe?”
Martin alizungumza kwa sauti ya chini chini huku tukimtazama Winy.
 
“Anaonekana hapendi ujinga”
“Ila yupo vizuri”
“Umemtamani nini?”
“Yaa ingekuwa sio haya matatizo ningemtokea”
“Acha uhuni, tufanye kazi”
“Sawa bosi”
“Jamani samahani kwa kuweza kumshuhulikia mtu wenu ila kwa upande wangu pia ni mtu ambaye nina muwinda”
“Usijali”
“Kuna chumba tunaweza kumfungia”
“Martin chukua uangalizi wa hilo”
“Sawa”
Martin akamshika mzee huyu na kuanza kuongozana na Winy, wakazunguka nyuma ya jumba hili. Baada ya dakika kadhaa Martin na Winy wakarudi sehemu walipo tuacha mimi na Babyanka, akatukaribisha ndani.
 
“Karibuni kwangu jamani, japo kupo kimya ila karibuni sana”
“Unaishi peke yako hapa?”
“Nipo na mdogo wangu wa kiume ambaye kwa sasa yupo polisi kwa ajili ya huyo mjinga muliye kuja”
“Shukrani”
“Eheee nielezeni mipango yenu kwa maana nina hamu ya kurudi kwenye game, kwa maana ni siku nyingi sijaua mtu”
“Shosti mbona una haraka”
“Yaani ulivyo niambia kwamba umekuja na Dany, ki** changu kimenicheza yaani nikia mtu n** zeto huwa zinaniisha”
Tukabaki tukitazamana na Martin kwa mshangao.
“Jamani musinione ninazungumza sana ila huo  ndio ukweli”
“Mumzoee ndio alivyo”
“Sawa”
Nikaanza kumuelezea Winy mpango wa kumuua K2 na kwa sasa nisubiria hotuba yake kwenye Tv ya kujiudhuru, kisha nionane naye.
 
“K2 hawezi kufanya hivyo hata siku moja”
“Ninatambua ila mwanaume tuliye mshika ni kama roho yake”
“Roho ya K2 sio huyo mwanume, na atamtumia mwanaume huyo kukua. K2 ana watu ana jeshi, ana mazagazaga ya kila aina”
Winy alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Dany nilikuambia kwamba K2 hawezi kujisalimisha kwa ajili ya huyo mkuu wapolisi. Ameigiza kupagawa ili mradi uingie kwenye kumi na nane zake kwa maana kila kitu ambacho amekifanya amekukosa”
“Mkuu hapo ninashauri tungekaa kwa muda, K2 asipo jiudhuru basi mpango umefeli na huyu mzee tunamuua kama tulivyo waua askari wake”
 
“Sawa, ila kuna watu bado nipo nao kichwani?”
“Kama nani?”
“Hawa na raisi Donald Bush”
“Unataka kumuua Donald Bush!!!?”
Winy alizungumza huku akinishangaa kwani mtu ninaye mzungumzia analindwa zaidi ya anavyo lindwa K2.
“Ndio”
“Mmmmm Dany una kazi wewe”
“Huo ndio mpango ulio nileta Tanzania, baada ya hapo nitaondoka Tanzania na hata nikifa basi nitakuwa sija jinsi na nitakufa kihaki”
“Winy unatambua kwamba Donald Bush atalala wapi?”
“Hapana sijafahamu bado, ila ngoja nimuulize mtu”
“Sawa”
Winy akachukua simu yake iliyopo kwenye meza ya Tv, akampigia mtu anaye hitaji kuzungumza naye.
“Baby”
 
“Nimekumis jamani”
“Ohoo ndio munampeleka raisi Donald hotelini?”
“Hoteli gani?”
“Ahaa baada ya hapo?”
“Hadi ziara yake iishe?”
“Mmmm haya jamani mpenzi wangu, hapa k** yangu inahitaji
“Nakupenda mume wangu”
“Kazi njema. Mwaaaaa”
Winy akakata simu huku akiachia msunyo mkali sana na kuing’ong’a simu yake.
“Mijiwanaume mingine ni usalama wataifa ila mijimbea kama nini”
“Kwa nini?”
“Alikuwa na haja gani ya kuniambia kwamba wanampeleka raisi Serea Hoteli”
“Amesaidia kutufahamisha”
“Yaaa. Ehee mutaingiaje Serena kwa maana inalindwa kuliko hata ikulu?”
Sote tukakaa kimya huku tukitazamana kwa maana hili jambo ni gumu sana.
“Tanzania hivi hakuna njia za chini ya ardhi?”
Martin alituuliza hukua kitutazama kwenye nyuso zetu.
“Barabara za chini hakuna”
Winy akawahi kujibu maswali.
“Hapana sio barabara za chini, anamaanisha mabomba makubwa nayayo pitisha maji machafu”
“Hayo yapo, tena tukitumia mabomba hayo tutafika Serena Hoteli pasipo wasiwasi wa aina yoyote.”
 
Babyanka alizungumza kwa msitizo. Kabla ya mtu yoyote kuzungumza kitu chochotea, taarifa ya dharura(Breaking News) ikakatisha mziki unao onekana kwenye chanel ya Tv kubwa iliyopo humu sebleni. Macho yangu yalipo  muona raisi K2 amesimama kwenye sehemu maalumu ya raisi anayo hutubia taifa kupitia vyombo vya habari ikanifanya taratibu kuichukua rimoti iliyopo mezani na kuongeza sauti kwenye hii Tv ili niweze kusikia kwa kile ambacho K2 anakwenda kukizungumza kwa taifa la Tanzania kwa maana nilimpa chaguo la kuachia madaraka kama vile alivyo nipa chaguo hilo mimi kipindi nilipo kuwa jeneral katika kundi la kigaidi la Boko Haramu.

AISIIIII……….U KILL ME 167
“Habari zenu Watanania, matumaini yangu ninaimani kwamba mutakuwa muwazima buheri wa afya. Tumeweza kumpokea raisi wa Marekanai kwa shangwe na vifijo nina imani kwamba ziara yake ya siku mbili hizi  kwetu itakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa letu”
K2 akakaa kimya huku akionekana kutafakari kitu. Sote sebleni tukabaki tukiwa kimya huku tukimtazama K2 kupitia hii Tv.
“Tunashukuru Mungu, kwamba ulinzi umezidi kuimarishwa katika maeneo yote ya nchi. Na nikiwa kama raisi wa Tanzaa nitahakikisha kwamba ninamkamata huyu gaidi Dany. Nina ahidi kwamba kabla ya kupambazuka nitakuwa nimemshika mikononi mwangu. Ninacho waomba Waanzania ni kuhakikisha munatoa taarifa ya kupatikana kwa Dany kupitia simu namba 0657072588.  Nasi jeshi langu nitahakikisha kwamba tunafika sehemu ya tukio na kumkamata Dany, kwa maana hatuwezi kuona mtu mmoja anasumbua serikali hii ikiwa, nchi yetu ni nchi ya amani na upendo.”
 
Nikazima Tv na kuwageukia wezangu, wote macho yao yapo usoni mwangu kwani kile nilicho kuwa nimekitegemea ni tofauti na hichi ninacho kiona hapa.
“Nilisema”
Winy alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Mkuu ni nini tutafanya ikiwa muhusika bado anaamini nguvu aliyo nayo inaweza kutuangusha.”
“Muacheni kwanza”
Babyanka alizungumza baada ya kuniona nimekodoa macho yangu sehemu moja hata pasipo kuzungusha sura yangu. Kila ninacho kifikiria akilini mwangu ninaona hakifai kabisa.
“Ninawazo”   
 
Winy alizungumza, na kunifanya taratibu nimtazame huku nikiwa sina matumaini ya kufanya chochote kwa wakati huu.
“Munaonaje tukafanya pigo kwa K2”   
“Pigo gani?”
“K2 ukiachilia huyu mzee, ila ana mtoto wake”
“Unahisi mtoto wake ni rahisi kumpata kwa muda huu?”
Babyanka alizungumza huku akimtazama Babyanka.
“Hata kwa siku zijazo?”       
“Unahisi siku zote hizo tutaendelea kuwa huru kama sasa hivi?”
“Hapa kwangu kupo salama, hakuna anaye weza kuwakamata”
“Mkuu niruhusu nimchinje yule mzee”
Macho yakanitoka na kubaki nikiwa nimemtazama Martin.
“Kumchinja!!?”
Babyanka akauliza naye akiwa ameshikwa na bumbuwazi.
“Ndio, anamuita gaidi bosi wangu, ili aone kwamba sisi ni magaidi kichwa cha huyu mzee inabidi kipelekwe kama zawadi kwake. Jinsi atakavyo kasirika sisi kwetu ndio itakuwa ni udhaifu mkubwa wa kuweza kumpata kirahisi”
“Ila swala la kuchinja jamani hilo ni kubwa?”
“Hilo nitalifanya mimi mwenyewe kama bosi ataniruhusu”
“Dany zungumza kitu?”
 Babyanka aliniambia kwani muda wote nilibaki kimya huku nikimtazama usoni mwake kwani muda wote nimeshindwa kuzungumza chochote.
 
“Mchinje”
“Dany!!!!”
“Ndio fanya hivyo Martin na kichwa chake niletee hapa”
“Hilo ni jambo jema. Usiogope Babyanka”
Winy alizungumza huku  akitoka sebleni hapa na Martin na kutuacha mimi na Babyanka.
“Dany hili  munalo taka kulifanya litazidi kuhatarisha usalama wako”
“Unahisi nipo salama?”
“Najua haupo salama ila…..”
“Ila nini, hivi unatambua ni jinsi familia yangu ilivyo kufa?”
Babyanka akaka kimya huku akinitazama usoni mwangu.
“Aliwaua watu wa karibu yangu kwa kuwachinja sasa na mimi nitawaua watu anao wapenda kwa kuwachinja”
Nilizungumza huku nikiiwasha Tv, sikukuta hotuba ya raisi tena zaidi ya vipindi vingine kuendelea kwenye hii Tv.
“Dany”   
Nikamgeukia Babyanka na kumtazama usoni mwake.
“Una, una…..una….”
“Nina nini?”
“Bado unanipenda?”
Tartibu nikajikuta nikiyafumba macho yangu kisha taratibu nikayafumbua na kumtazama vizuri Babyanka.
“Sina hisia za mapenzi moyoni mwangu”
 
Kabla Babyanka hajazungumza kitu chochote Martin na Winy wakaingia huku wakiwa na boksi kubwa. Walilo lizungushia mfuko wa rambo, wakaliweka mezani, taratibu nikalisogelea boksi hili na kulitazama vizuri. Japo mimi ninaroho ya kikatili na swala la kumuua mtu ni kawaida, ila kusema kweli  kwa hichi walicho kifanya kwa huyu mzee ni ukatili ulio pitiliza kwani kichwa chake wakekichinja kama kuku aliye chinjwa, ila kilicho nizidisha kuniogopesa ni jinsi walivyo kikata kata kwa kitu chenye makali makubwa.
“Mbona mume mkata kata hivi?”
“Aliteta tabu ikabidi nimtandike mapanga kadhaa kichwani”
Winy alijibu kwa kujiamini sana, hadi mwili ukanisisimka kwa woga mkali. Babynka wala hakuhitaji kuusogelea hili boksi.
“Haya tutalifikisha vipi kwa muhusika?”
“Tutalipeleka mkuu”
“Ikulu!!?”
“Hapana sio ikulu, hapa cha kufanya ni kupiga simu kwenye namba husika aliyo itangaza K2 kisha tutajidai kama tumekuona kwenye eneo tutakalo hilo eneo  sasa hapo utaandika ujumbe ambao wewe utamfikia K2 huko alipo”
Nikamtazama Martin jinsi anavyo zungumza kisha nikatingisha kichwa changu kwa kukubaliana naye.
 
“Naomba karatasi”
Winy akachuka moja ya daftari na kalamu vilivyopo kwenye moja ya meza yenye computer ndogo kisha akanikabidhi. Nikachana moja ya karatasi kwenye hili daftari kisha taratibu nikaka kwenye sofa na kuanza kufikiria cha kuandika.
“Mkuu acha tujiandae kuna zile nguo za polisi naamini zitatusaidia”
“Sawa”
Martin na Winy wakatoka sebleni hapa.
‘HUU NI MWANZO TU, HUWEZI KUNIUA HADI NIHAKIKISHE NINAKUUA, ILA USIPO ANGALIA WATU WAKO WOTE WAKARIBU YAKO WATAKUFA KIFO KAMA HICHI. DANY’
Baada ya kuyaandika maneno hayo nikasimama na kuikunja taratibu karatasi yenye maandishi, taratibu nikalisogelea boksi lenye kichwa cha mume wa K2 kisha nikaidumbukiza huku nikiwa nimeikunja vizuri sana.
Winy na Martin wakarudi wakiwa wamevalia mavazi ya askri ambao tuliwaua.
“Ila yana damu ila yataufaa hivi hivi”
Winy alizungumza huku akinitazama.
“Mwili wake mumeuweka wapi?”
“Mwili wake upo kule kule stoo”
“Twende tukauone”
 
Nilumuambia Martin, lengo la kutoka sebleni hapa si kwenda kuuona mwili huo pekee, ila lengo kubwa ni kuhakikisha kwamba ninazungumza na Martin juu ya huu mpango. Tukaiingia kwenye chumba alichokuwa ameingizwa mkuu wa polisi. Nikaukuta mwili wake ikiwa imelazwa chini huku damu nyingu zikiwa zimesambaa kwenye sakafu.
“Unatakiwa kuwa makini na huyu mwanamke”
“Sawa mkuu”
“Tusimuamini moja kwa moja, ikiawa hatujui ni wapi tulipo tokea, na amekubali kirahisi rahisi kuingia kwenye huu mpango. Ukiona anaenenda kinyume nasi muue”
“Usijali mkuu nitalifanya hilo”
“Kitu kingine kama ni mtu anaye elekeweka hakikisha unaosha rungu ili asiondoke mikononi mwetu”

“Sawa mkuu nitahakikisha ninampa mambo ya kina Jonyyyy”
Martina alizungumza huku akiwa ametabasamu kwa furaha kubwa sana.
“Hakikisha humpi nafasi  ya kuwa mbali nawe, kosa moja ua asirudie kosa jengine itatugarimu na wakikukamata sasa hivi watakuua, hawato kupa hata nafasi ya kukuhoji kwani tayari umesha kuwa most wanted kama mimi”
Nilizungumza kwa sauti ya chini sana huku nikimtazama Martin machoni mwake.
 
“Sawa mkuu”
Tukatoka ndani ya chumba hichi na kurudi sebleni na kuwakuta Babyanka na Winy wakiwa wanelekezana kitu kwenye hii computer iliyopo hapa sebleni.
“Tayari bibie tuondoke”
“Ngoja ninamuelekeza Babyanka jinsi ya kuweza kutuona kila tunapo kwenda kupitia satelaiti”
“Haito kuwa hatari kwetu?”
“Hapana, pia katika hichi kichwa nimechokea kifaa ambacho tutaweza kukiona kila kitakapo kwenda”
“Babyanka unaweza kufanya hayo mambo?”
“Ndio japo sio sana”
“Sawa”
Winy na Babyanka wakaelekezana kwa muda kidogo walipo hakikisha kwamba wamemaliza. Martin na Winy wakatuaga na kuondoka huku kila mmoja akiwa ana silaha yake, huku Martin akiwa amelibeba boksi lenye kichwa cha mume wa K2. Nimsogela Babynka alipo kaa, nikatazama anacho kifanya kwenye hii computer, tukawaona Winy na Martina wakingia kwenye gari jengine linalo milikiwa na Winy ana kuondoka katika hili eneo.
 
“Unahisi huu mpango utafanikiwa?”
“Mbona unakuwa na mashaka sana Babyanka upo nasi au haupo nasi?”
Ilinibid kuzungumza kwa ukali huku nikimtazama Babyanka machoni mwake. Taratibu Babyanka akasogeza kiti chake cha matairi alicho kikalia, akasimama mbele yangu huku akinitazama kwa macho malegevu.
“Nina mashaka na wewe Dany, sihitaji kukupoteza kama nilivyo kuacha mara ya kwanza ulivyo potea”
“Tupo katika kazi mapenzi tuyaweke kando kwanza, tazama wanapo elekea wezetu”
Babyanka akanibusu mdomoni mwangu kisha akarudi na kukaa kwenye kiti. Tukazidi kulifwatilia gari walilopanda Winy na Martin hadi wakafika katika daraja la Sarenda. Wakasimamisha gari pembeni, na Winy akashuka kwenye hili gari, taratibu akashuka hadi chini ya daraja na kuweka boksi hili na kwa haraka akrudi kwenye gari. 
 
“Wanafanyaje?”
“Ninahisi watakuwa wanazungumza na simu”
“Hembu vuta hiyo video karibu”
Babyanka akafanya hivyo na taratibu video ikaanza kuwajia karibu hadi tukamuona Winy akizungumza na simu, baada ya kuzungumza ancho kizungumza, akaitupa simu hiyo pembeni ya barabara na wakaondoka katika eneo hili.
“Unaweza kupata video katika hilo boksi?”
“Ndio”
“Fanya hivyo”
Ikamlazimu Babynka kutoa video inayo onyesha gari walilo panda Winy na Martin, akaonyesha video hii inayo tokea kwa juu,  inayo onyesha boksi lenye kichwa cha mume wa K2. Hazikupita hata dakika tano gari zipatazo kumi za NSS, zikafika katika eneo la daraja la Sarenda. Wakashuka na kuanza kulizunguka daraja hilo, huku kila mmoja akiwa naa silaha yake.
 
“Wamelipata boksi”
Babyanka alizungumza huku akinionyesha askari aliye lishika boksi hilo. Askari hawa wakaanza kulizunguka hili boksi huku wakionekana kuwa na woga sana.
“Kwa nini askari wako ni waoga?”
“Nahisi wanahisi hilo ni bomu”
“Watafikisha kweli mzigo huo?”
“Ngoja tuone”
Askari hawa wakaliweka bosky hilo katitaki ya barabara na magari yao wakayaweka umbali kidogo kutoka sehemu lilipo boski. Tukawaona askari wawili wakiwa wamevalia mavazi maalumu ya kutegulia mabomu wakianza kulisogela boski hilo taratibu.
“Umeandika huo ujumbe umfikie raisi?”
“Hapana”
“Watausoma na tulicho kifanya ni kazi bure”
“Sio kazi bure ngoja tuone”
Askari hao wakalisogelea boksi na taratibu wakalifungua, wote wakaonekana kustuka hadi mmoja wao akaanguka chini.
Askari wengine walio kaa umbali kidogo wakaonekana kuwa makini huku wakiwatazama wezao. Askari aliye anguka chini akasimama tarataibu na kuonyesha ishara iliyo wafanya wezake kusogea taratibu. Kila askari aliye tazama ndani ya boksi hilo akaonekana kustuka sana.
“Tunaweza kusikia wanacho kizungumza?”
“Hapana hatujatega vinasa sauti”
“Sawa”
 
Tukamuona askari mmoja akizungumza na simu, baada ya muda kidogo akakata simu hiyo na kurudi eneo lilipo  boksi. Babyanka akamtazama askari huyo anavyo zungumza na wezake, kisha Babyanka akanigeukia na kunitazama.
“Anazungumza nini jamaa?”
“Amewaambia wezake waimarishe ulinzi kwa maana raisi amehitaji kufika eneo la tukio”
“Umejuaje?”
“Nimetazama mdomo wake jinsi unavyo zungumza na nimeweza kulijua hilo. Umesahau kama nina uwezo mkubwa wa kufahamu jinsi mtu anavyo zungumza hata kama hajatoa sauti”
“Nakumbuka”
“Niamini basi katika nililo kuambia”
“Poa”
Baada ya dakika kumi na tano, gari nne nyeusi zenye bendera ya rasi pamoja na bendera ndogo ya nchi hii, zikafika katike eneo la tukio. Wakashuka walinzi wote, walipo  hakikisha usalama upo vizuri akashuka K2, aliye anza kutembea kwa kasi kuelekea sehemu lilipo boksi lenye kichwa cha mume wake.
 
“Laiti kama wangeweka bomu basi hii ingekuwa shabaha yangu ya pekee kuhakikisha kwamba K2 anakufa”
“Ni kweli, ila kama mtu mmoja simuoni katika walinzi wake ikiwa wasichana wengine nimewaona”
“Nani?”
“Livna Livba”
Hata kabla sijatazama vizuri, mlango wa hapa sebleni ukafunguliwa. Sote tukajikuta tukigeuka nyuma, tukamuona Martin akiingia humu ndani ila uso wake ukivuja damu na ametulia sana, akaingia na Winy naye jicho moja limemvimba, nikaishika bunduki yangu vizuri huku nikipiga hatua moja mbele. Martin akatingisha kichwa akiashiria kunikataza kusogea mbele kwani kufanya hivyo inaweza kuwa hatari kwangu, kwani sifahamu ni nani aliyopo nyuma  yao.

 ITAENDELEA
“Haya sasa Winy na Martin wamepata walicho kipata huko watokapo na K2 amefika sehemu husika lilipo boksi lenye kichwa cha mume wake. Je nini kitampata baada ya kukiona kichwa chiho.? Usikose sehemu inayo fwata ya hadi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )