Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, December 20, 2018

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 176 na 177 )

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  

Wanajeshi wawili wakasimama nyuma ya mzee huyu huku wakiwa wamemshikilia mtu aliye valishwa kigunia cheusi kichwani mwake. Wanajeshi hawa wakamvua mtu huyo, moyo ukanistuka, mapigo ya moyo yakaanza kwenda kasi huku jasho jingi likinimwagika usoni mwangu, kwani mtu waliye mkamata ni Yemi msicha ambaye hadi leo ninaishi na upendo wake moyoni mwangu na pete yake ya ndo bado ipo kidoleni mwangu, mzee huyu akasogea pembeni taratibu na hapo ndipo nikaona tumbo la Yemi ambalo limevimba kidogo, ikiashiria kwamba ni mwanamke mjamzito.
“Huyu ni mke wako wa ndoa, ni mjamzito sasa. Chagua kati ya mke na mtoto au kujisalimisha mbele ya jeshi la Kimarekani”
Sikujibu kitu chochote zaidi ya kutetemeka mwili mzima, maumivu ya moyo ninayo yasikia kusema kweli hayana mfano, kwani nilimuacha Yemi aende akaishia maisha yake salama salimin kwani ninatambua maisha yangu ni maisha ya hatari sana kwa kila ninaye ingia naye kwenye mahusiano ya kimapenzi.
   
ENDELEA
Nikajiikuta nikiifunika lapto hii taratibu huku nikimtazama Livna usoni mwake.
“Wanahitaji nini?”   
“Wamemkamata Yemi”
“Mmmmmm, Ester wamepata vipi mawasiliano nasi?”
“Waliniomba kupitia mtandoa nilio  post video zile”
“Wamefahamu ni wapi tulipo?”
 
“Hapana, hawajaweza kufahamu”
“Muda mwengine usiwakubalie pasipo kunifahamisha mimi kwanza”
“Sawa mkuu”
“Dany twende”
Livna alizungumza huku tukirudi kwenye chumba tulipo waancha Erick na wezake. Kila aliye nitazama nina imana anahisi kwamba kuna kitu ambacho kimetokea.
“Mkuu vipi?”   
Martin aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.
“Kuna tatizo limetokea”
Livna alizungumza huku akiwatazama kwenye nyuso zao.
“Tatizo gani?”
Winy naye aliuliza huku akiwa amejawa na shauku ya kuhitaji kufahamu ni kitu gani ambacho kimetokea.
“Yemi amekamatwa na Wamarekani, wanamlazimisha Dany kujisalimisha mikononi mwao la sivyo wanamuua Yemi na mbaya zaidi ni kwamba Yemi ni mjamzito”
“Oooohooo Mungu wangu!!”
Babyanka alizungumza huku akinitazama kwa macho yaliyo jaa masikitiko mengi.
 
“Hii ni vita, siwezi kujisalimisha mikononi mwao. Sihitaji kuonyesha udhaifu kisa mke na mtoto. Nilisha itoa sadaka famili yangu, mke wangu pamoja na mwanangu. Ninahitaji kuionyesha Marekani kwamba nina weza kufanya kitu”
“Sasa mkuu utaifanya nini Marekani ikiwa hatuna uwezo  wa kwenda kupambana nao, isitoshe wana vifaa vingi vya kivita, wana majeshi makubwa sana. Tuna fanyaje hapo?”
“Uwezo wa kumpiga Mmarekani tunao, tutampiga kwa silaha zao wao wenyewe”
Livna alizungumza kwa msisitizo huku  akinitazama usoni mwangu.
“Sasa mutaipiga Marekani na Yemi akiwa ndani yake?”
“Hatuna jinsi Babyanka, wanatulazimisha kufanya hivyo”
“Ila kuna kitu pia ninakifikiria?”
“Kitu gani Livna?”
 
“Nina mifumo mizima ya kuendeshea mabomu ya nyuklina yaliyopo Korea Kusini, munaonaje tukatumia mabomu hayo tukaipiga Marekani, na sisi tukajiweka pembeni pale watakapo anza kufumuana kwa maana Korea Kusini na Marekani ni sawa na panya na paka”
Sote tukamtazama Livna huku tukiwa tunashangaaa, hadi yeye mwneyewe akajistukia.
“Maana yangu sio mbaya kuzungumza hivyo, ila ninacho kisema hapa ni kuangalia ni jinsi gani sisi tunaweza kumuokoa Yemi pamoja na kiumbe elicho kuwa nacho tumboni na nina imani kwamba Yemi hayupo Marekani,  yupo Afrika hii hii”
Livna alizidi kunyoosha maelezo yake.
“Sasa Wakorea Kusini hawato tugeukia sisi?”
“Hapana, kila kitu tunacheza na code za kijeshi zinazo weza kuruhusu mabomu hayo kweza kushambulia Marekani na nina imani kwamba hakuna siku hata moja Mmarekani akakaa meza moja na Mkorea Kusini”
“Basi kama ni hivyo inabidi tufanye hili na tutazame ni nini kitakacho tokea”
“Jamani sio kama nina pinga hayo maamuzi, ila inabidi kujua ni wapi alipo Yemi, tumuokoe yeye na mtoto wake aliyopo tumboni?”
 
“Sawa Babyanka hilo halina shida vijana wangu watalishuhulikia kikamilifu”
“Hapo sawa, kwa maana mwenzenu nina roho ndogo sana kuona mwanamke mwenzangu tena mjamzito anaingia kwenye matatizo”
“K2 je?”
“Winy K2 huyo kwa sasa anapambana na aibu aliyo ipata, hadi akikaa sawa sisi tutakuwa tumesha maliza hili swala”
“Poa”
“Ila nina wazo”
Martin alizungumza na kutufanya sote tumtazame.
“Munaonaje Dany ukazungumza tena na Wamarekani ili kuwatishia kumuachia Yemi kabla ya wewe hujachukua maamuzi mazito kwa maana hili tunalo kwenda kulifanya ni vita ya tatu ya Dunia”
“Kweli hata mimi naunga mkono hilo swala. Dany hembu hili swala tuliweke mezani jamani na tulifikirie kwa umakini. Kuna wamama, kuna watoto wadogo, hawa wote ni mabilioni wa watu katika hizi nchi mbili. Je watakwenda kufa kwa ajili ya Yemi?”
 
Babyanka naye alizungumza huku akitutazama usoni mimi na Livna ambao tayari tumesha amua kufanya maamuzi magumu.
“Hilo nalo neno”
Winy naye akatilia ujazo wa maoni, jambo lililo tufanya mimi na Livna kutazamana.
“Basi hilo tuliweke ni Plan B, haya sasa tufikirieni Plan A, tutamuokoa vipi Yemi, na sasa hivi Wamarekani wana hasira kuliko kitu chochote wakimshika mmoja wetu hapa ninaimani kwamba hato pona”
Livna alizungumza na kufanya ukimya wa zaidi ya dakika mbili kutawala katika eneo hili.
“Na isitoshe Dany hawezi kujisalimisha mikononi mwao”
“Tukijua ni wapi alipo Yemi alipo mimi nitakwenda kumuokoa”
Martin alizungumza.
 
“Acha kutafuta kifo kisicho na sababu Martin”
“Hata nikifa sababu ipo, nitakuwa nimekufa nikijaribu kumuokoa mke wa mkuu wangu isitoshe hata kwenye harusi niliwasimamia mimi”
“Hakuna kitu kujaribu hapa ni kufanya”
“Martin unakumbuka namba yoyote ya meja?”
“Meja ndio nani?”
Livna aliuliza huku akinitazama usoni mwangu.
“Alikuwa ni mkuu wa kambi ya jeshi nchini Somalia, ni rafiki yangu na yeye ndio aliye andaa harusi yangu na Yemi”
“Una muamini, kwa maana hawa watu hawaaminiki kabisa”
“Alinisaidia katika mengi hata kuniokoa mikononi mwa Wamarekani walivyo nikamata kwa mara yangu ya kwanza”
“Ndio ninakumbuka namba yake ya mkononi alisha wahi kunipatia”
“Livna unaweza kuniazima simu ambayo nilimpigia nayo K2?”
“Ndio”
“Ninaomba unisaidie”
Livna akatoa simu yake mfukoni na kunikabidhi. Martin akaanza kunitajia namba moja baada ya nyingine. Nikaipiga namba hii huku nikiiweka simu hii sikioni mwangu, taratibu ikaanza kuita, baada ya sekunde kadhaa kikapokelewa.
 
“Haloo”
Niliisikia sauti ya Meja, nikameza fumba la mate huku nikishusha pumzi taratibu.
“Habari yako meja”
“Dany”
“Ndio meja”
“Habari za masiku”
“Salama”
“Aissee Dany nimejaribu kukutafuta siku zote sijakupata. Ninaiona kazi yako jinsi ilivyo kwenda vizuri”
“Nimejitahidi kwa kiasi chake meja”
“Sio kwa kiasi chake, umfanya kazi nzuri sana Dany, sikutegaema kama unaweza kuwa na roho ya ujasiri kiasi hicho”
“Shukrani sana meja, ila ninatatizo”
“Tatizo gani?”
“Yemi amekamatwa na Wamarekani”
“Ila Yemi si ulisha achana naye, yeye wa nini tena?”
“Ana ujauzito wangu na pia ni mke wangu wa ndoa. Bado nina mpenda na pete yake ninayo”
 
Ukimya wa sekunde ukatawala
“Sasa Dany unahitaji hapo nikusaidiaje rafiki yangu”
Meja alizungumza kwa sauti ya chini sana.
“Ninakuomba unisaidie kumpata mke wangu. Wamarekani wakimuua, basi hali ya dunia itakwenda kubadilika meja. Wewe ndio mtu wa pekee unaye weza kuzuia hali ya dunia kutochafuka, kama ilivyo anza kuchafuka kwa Wamarekani”
“Sawa nitaomba unipigie baada ya lisaa moja tutafute ni wapi alipo”
“Ninashukuru sana Meja”
“Ila upo wapi?”
“Usijali meja nitakuambia ni wapi nilipo baada ya hiyo kazi kuisha”
“Sawa”
Nikakata simu na kumrudishia Livna simu yake.
“Tuna lisaa moja la kusubira kuweza kupata jibu ni wapi Yemi alipo”
“Kwa hiyo nisiwaambie wasichana wangu kuto kufanya chochote?”
“Wakae tayari”
“Sawa”
“Samahani. Dany wakae tayari katika nini?”
“Katika vita, kama walimuweza Osama mwaka 2002, hawato niweza mimi”
 
Baada ya kumaliaza kuzungumza maneno haya nikasimama na kuanza kueleka mlangoni, Livna akaanza kunifwata kwa nyuma huku akiwa ameongozana na Martin.
“Dany huyu mtu unamuamini sana kwa maana kumbuka kwamba Wamarekani wana uzalendo mkubwa na nchi yao na isitoshe amelitumiakia jeshi lake kwa muda mrefu?”
“Akienenda kinyume nami ninamuua”
“Ila kweli mkuu alicho kizungumza Livna”
“Nimesema meja akinisaliti, nitamuua. Kuna swali?”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiwa nimejawa na hasira ambayo haiitaji kusikia maswali ya mtu yoyote. Martin akatingisha kichwa akionyesha kwamba hana swali jengine, nikarudi chumbani kwangu huku nikiwa nimeongozana na Livna na Martin alirudi katika chumba tulichokuwepo mara baada ya kuona sipo sawa. Livna akaufunga mlango kwa ndani na kunisukumia kitandani, kisha akanikalia kiunoni mwangu huku akinitazama.
 
“Hivi umemua kunisaidia kutoka moyoni mwako?”
“Ndio Dany, ninakuomba uniamini sana, nimefanya hili swala kutoka moyoni mwangu sinto weza kukusaliti hadi kufa kwangu”
Baada ya Livna kuzungumza maneno haya akaanza kuninyonya midomo yangu taratibu, nikakishika kiuno chake na kuanza kukiminya minya.
Hisia za mapenzi zikaanza kutupanda huku kila mmoja akiwa na hamu ya kupata burudani hii, japo tupo katikati ya matatizo makubwa. Tukavuana nguo zetu, pasipo hata kuandaana sana

Baada ya kumaliza Livna alishuka kitandani, akaanza kutembea kueleka bafuni huku akipepesuka sana. Nikashuka kitandani na kumfwata kwa nyuma, nikamsaidia kumshika mkono na kuingia naye bafuni, tukaoga kwa pamoja na kutoka humu, kila mtu akavaa nguo zake yeye mwenyewe kama desturi ya waafrika tukimaliza kufanya tendo la ndoa kila mmoja anavaa nguo zake japo mwanzo tunajifanya kuvuana nguo.
“Lisaa moja litakuwa tayari ehee?”
“Yaa inabidi nimpigie”
“Chukua simu”
Livna akanipigia simu, nikampigia meja, simu ikaita baada ya muda ikapokelwa.
 
“Dany”
“Ndio”
“Sijafanikiwa kufahamu ni wapi Yemi alipo, kwani unahitaji kufanya nini?”
Nikajikuta nikisimama huku nikimtazama Livna usoni mwake.
“Halooo”
“Meja  niambie ukweli hujampata kabisa Yemi?”
“Niambie kwanza ni nini unataa kukifanya kwa Wamarekani nami nitakuwa tayari kukusaidia kumpata mke wako”
Upande mmoja wa roho yangu inaniambia nisimuambie meja mpango ninao kwenda kuufanya juu ya nchi yake pendwa aliyo itumikia kwa miaka mingi katika kitengo cha jeshi. Ila upande wa pili wa roho yangu unanishawishi kumueleza mpango mzima ili mradi anisaidie kumpata mke wangu wa ndoa mwenye ujauzito unao sadikika kwamba ni wangu.

AISIIIII……….U KILL ME 177

“Meja ukimpata Yemi nitakuambia ni nini ambacho nimekipanga, ila kwa sasa sinto weza kukuambia hilo. Samahani sana”
Baada ya kumaliza kuzungumza hivi nikakata simu na kumtazama Livna.
“Anahitaji nimueleze ni nini nitakacho kwenda kukifanya kwa Mmarekani”
“Ni vizuri ulivyo kataa kumuambia, ila ngoja wasichana wangu wanaweza kufanya kazi ya kumtafuta Yemi. Twende kwenye chumba cha mawasiliano”
Tukaongozana na Livna hadi kwenye chumba hichi cha mawasiliano, akamuita Ester pamoja na wasichana wengine wawili.
 
“Umeweza kumpata Yemi alipo?”
“Bado mkuu”
“Na haukujua  video ile waliyo hitaji kuzungumza na Dany ilitokea wapi?”
“Yaa nao waliweza kufunga mitambo yao na hatujajua ni wapi walipo”
“Wapigieni tena nizungumze nao”
“Dany”
“Naomba wafanye hivyo”
Livna akanitazama kwa muda usoni mwangu.
“Sawa”
Livna alizungumza, akamkabidhi Ester kazi kuwasiliana na mkuu wa jeshi la Marekani.
“Njoo kwenye chumba hichi”
Tukaingia kwenye chumba hichi ambacho kuna Tv kubwa tatu. Livna akawasha Tv moja ya katikati. Baada ya muda kidogo ikamuonyesha mkuu wa jeshi niliye zungumza naye masaa machache nyuma.
 
“Una masaa machache ambayo unaweza kujisalimisha mikononi mwa vikosi vya Marekani”
“Mzee sijakuja kukuomba wala sijakuja kukubembeleza. Ninakuamrisha ndani ya dakika kumi na tano muachie mke wangu. La sivyo  wananchi wa nchi yako watakwenda kulia kilio cha kusaga meno kwa kile ambacho kinakwenda kutokea”
Tv hii ikagawanyika katika picha mbili huku moja ikimuonyesha mkuu huyu wa jeshi na nyingine ikiwaonyesha viongozi walio kaa kwenye meza moja kubwa.
“Dany unazungumza na makamo wa raisi wa Marekani. Thomas Sound”
Nikaka kimya huku nikimtazama kiongozi huyu, ambaye sio mara yangu ya kwanza kumuona.
 
“Tunahitaji kuingia makubaliano nawe je upo tayari”
Nikamtazama Livna aliye simama pembeni na yeye haonekani kwenye hii Tv. Livna akatingisha kichwa kukubaliana na anacho kizungumza makamu huyu wa raisi aliye ichukua nafasi ya raisi Donald Bush niliye idhibitishia dunia kwamba mimi ndio niliye muua.
“Zungumza”
“Tunahitaji kumuachia mke wako, endapo pale utakapo jisalimisha mikononi mwa serikali yangu ya Marekani”
“Akili zenu ni moja, munazungumza kitu kimoja. Sasa nimewaambia ndani ya dakika kumi na tano ninahitaji mumuachie mke wangu. Zikipita kunzia hivi sasa. Mamilioni ya Wamarekani itakwenda kuwalaumu kwa maamuizi ya kijinga unayo yafanya na hao watu wako walio kuzunguka.”
“Mpumbavu wewe ni nani anaye kupa ruhusa ya kumuita raisi wetu mpumbavu”
Mzee mmoja alizungumza kwa sauti ya kukwaruza sana, huku hasira ikiwa inaonyesha dhairi kwamba imempanda.
“Munadakika kumi na tano”
Nikanyanyuka kwenye kiti nilicho kikalia, na Livna akazima tv hii.
“Dakika hizo kumi na tano una mpango wa kufanya nini?”
“Ninahitaji kutumia mpango ambao ulihitaji sisi kuweza kuufunya”
“Kutumia silaha za Korea Kusini kumshambulia Mmarekani?”
“Ndio”
“Ngoja kwanza, tulipua visima vyake kumi vya nyuklia, nina imani kwamba itakuwa ni fundisho kubwa kwao”
 
“Sawa waite vijana wako wanao weza kuifanya hiyo kazi”
Livna akatoka katika chumba hichi, hazikupita hata dakika mbili akarudi akiwa amongozana na wasichana watatu akiwemo na Ester, akawalezea ni nini wanatakiwa kufanya. Kazi ikaanza mara mmoja, ndani ya dakika kumi, wakawa wamefanikiwa kufahamu namba za siri ambazo zinaweza kutumika katika kulipua visima vya kuzalshia mabomu ya nyuklia ambayo duniani yanasifika kwa uhatari wa hali ya juu.
“Ukihitaji kulipua unaminya batani hii”
Ester alizungumza huku akinikabidhi laptop aliyokuwa anafanyia kazi.
“Nikiminya vinalipuka kwa muda mmoja?”
“Ndio kwa pamoja vinalipuka”
“Shukrani binti, wapigieni tena”
“Ila dakika kumi na tano bado hazijafika”
“Zimebaki ngapi?”
“Dakika tatu”
Livna alizungumza huku akitazama saa iliyopo ukutani mwake.
“Hizi tv si zinaweza kuonyesha chaneli kama BBC, CNN?”
“Ndio”
“Ziwasheni”
Livna akawasha tv hizi mbili na kuweka sauti ya chini sana ambayo haitoweza kuingiliana kabisa na mazungumzo ambayo ninakwenda kuyafanya na viongozi wa Marekani. Zilipo timia dakika kumi na tano Tv hii ninayo itumia kufanya mawasiliano Wamarekani ikawashwa na kuwakuta wakiwa kwenye kikao chao.
 
“Dakika kumi na tano nina imani zimesha fika, je munamuachia Yemi au hamumuachii?”
Makamu wa raisi pamoja na mkuu wa jeshi wakaka kimya kwani wao ndio wahusika wakubwa ninao zungumza nao.
“Munamuachia Yemi au hamumuachiii?”
“Hivi huyu nguruwe anajimini nini hadi kututisha kiasi hichi”
“Waziri wa ulinzi nyamaza”
Makamu wa raisi alizungumza kwa ukali huku akimtazama mzee huyo. Taratibu mkono wangu nikausogeza kwenye batani hii  ya kulipulia visima hivi vya nyuklia.
“Dany”
Makamo wa raisi alizungumza na kunifanya nisitishe zoezi la kuminya batani hii.
“Tutamuachia Yemi ila kwa makubaliano ya kubadilishana”
“Kubadilishana na nani?”
“Tunamuhitaji mke wa raisi, bi Hawa”
“Hawa alikuwa ni mpenzi wangu, raisi wenu alinipokonya na kuhitaji kuniua. Nina imani nyinyi nyote muliweza kujua ni mchango gani niliutoa kwa ajili ya kuliondoa kundi la Al-Shaba. Ila serikali yenu ikanigeuka na kuhitaji kunia, kisa raisi wenu amemchukua mpenzi wangu. Sasa makubaliano hayo musahau, Sawa”
Viongozi wote wakaka kimya huku wote wakinitazama usoni mwangu.
 
“Ninawauliza kwa dakika ya mwisho je mutamuachia Yemi na kuwapa maelekezo ni wapi apelekwe au?”
“Nchi yangu haiingii makubaliano na gaidi, ninakuhakikishia kwamba tutakutafuta, iwe ni angani au nchi kavu nilazima serikali yangu ikutafute na kukuua”
“Sawa tuanze kutafutana sasa”
Nikaminya batani ambayo nimeelekezwa na Ester. Nikawatazama viongozi  hawa wa Wamarekani huku nikitabasamu. Nikamuona msichana mmoja akimsogezea makamu wa raisi, akaonekana kustuka sana, kwa ishara akamuomba kijana mmoja kuwasha Tv kubwa iliyopo nyuma ya kiti chake. Nikataupia macho yangu kwenye Tv ya pembeni. Vituo vya habari vikaanza kuonyesha taarifa ya dharura inayo husiana na milipuko ya visima ya nyuklia.
“Huo ndio mwanzo, mukishindwa kumuachia, kitakacho fwata ni mara kumi ya hicho mulicho  kiona hapo”
Nikanyanyuka kwneye hiti hichi huku nikiwaachia mtihani mkubwa viongozi hawa wa kimarekani. Tv zikazima na tikatoka katika chumba hichi.
 
“Ester hakikisheni ulinzi unaimarishwa, kwa maana tumesha ingia kwenye vita”
“Sawa mkuu”
Tukaondoka katika eneo hili. Sikuzungumza kitu chochote zaidi tulipo ingia kwenye chumba ambacho wasichana wadogo wenye umari wa miaka mitano kwenda juu wanafundishwa jinsi ya kupambana.
“Hawa watoto wazuri”
Watoto hawa wakasimama kwenye mistari minne iliyo nyooka, wakatoa heshima yao kwa kuinamisha vichwa vyao chini. Livna akaipokea heshima hiyo kwa kuinamisha kichwa chake na yeye chini, kisha akawaruhusu waendelee na mazoezi yao.
“Yaa sasa hawa wakifikia miaka kumi na tano tunaaza kuwakabidhi kazi nchini mbali mbali”
“Kwa hiyo maisha yao yote wanaishi kujifunza kupambana?”
“Yaaa wanaishi kwa kupambana”
Simu ya Livna ikaita, akaitoa mfukoni akaitazama kisha akanikabidhi na kukuta namba ya meja ndio inayo piga. Taratibu nikaipokea na kuiweka sikioni.
“Dany wewe ndio umehusika katika kulipua visima vya nyuklia?”
 
Meja aliniuliza huku akiwa na wasiwasi mwingi sana.
“Kwa nini unaniuliza hivyo?”
“Kama ni wewe Dany kwa nini unahusisha matatizo kwa raia ambao hawana hatia yoyote. Kumbuka nina dhamira yangu ya kwenda kuiongoza Marekani, ninahitaji kuwa raisi wa hiyo nchi. Ni kwa nini umefanya hiyvo?”
“Meja unazungumza na kunishutumu mimi bure, kwa nini?”
“Dany nimepata taarifa kutika Washinton D.C na wewe ndio umehusika katika ulipuaji wa visima vya nyuklia, kama upo karibu na Tv hembu tazama ni jinsi gani raia walivyo fariki”
“Kosa sio langu, kosa ni la viongozi wa nchi yako. Ni hivi waambie kwamba wamuachie Yemi la sivyo kabla ya giza halijatawala anga, nitakwenda kuigeuza Marekani magodauni kama walivyo fanya kwa nchi za Iraque na Pakistani”
Nikakata simu na kumrudishia Livna. Baadhi ya watoto wakabaki wakiwa wananitazama kwa macho ya kunishangaa hadi nikajisikia aibu kwa kuzungumza vitu vizito mbele yao.
Nikatoka chumbani humu huku Livna naye akinifwata kwa nyuma. Tukarudi katika chumba cha mawasiliano na kuingia kwenye chumba chenye Tv. Nikawasha tv hizi na kuangalia taarifa za habari. Nikaona uharibifu mkubwa wa majengo, ulio fwanya na visima hivi vya nyuklia ambavyo nimevilipua.
“Mmmmm”    
 
Livna aliguna huku akitazama taarifa hizi.
“Nini?”
“Tuwapigie tena na kuwapa onyo, wamuachie Yemi”
“Acha kwanza walie lie, hembu mpigie K2”
“K2 utamuua kwa presha bwana”
“Lengo letu ni wafe. Wakati wao umeisha sasa niwakati wangu kuwaendesha umefika”
“So unahitaji kuhack kamera zao”
“Hapana ninahitaji kuzungumza naye kwa video call kama tulivyo fanya kwa Wamarekani”
“Sawa”
Livna akatoka chumbani humu. Nikabaki nikitazama taarifa hizi za habari, nikaona jinsi watu wengi walivyo fariki kwa milipuko wa visima hivi vya nyuklia.
‘Mungu ninakuomba unisamehee kwa maana hawakujua walitendalo’
 
Nilizungumza kimoyo moyo, mlango ukafunguliwa na akaingia Livna na wasichana wake wa mara ya kwanza huku kila mmoja akiwa na laptop yake mkononi mwake.
“Tumesha mpigia K2 anakusubiria uwashe Tv hiyo ya kati.”
Nikachukua rimoti  iliyopo pembeni yangu na kuisha tv hii. Nikamuona K2 akiwa amekaa kweye kiti cha ofisini kwake huku nyuma yake kukiwa na nembo ya taifa, ya mwanaume na mwanamke na imetawaliwa na rangi ya kijani.
“Nina imani umeona kilicho wapata Wamarekani, je upo tayari na wewe nikupige?”
K2 akaka kimya huku akinitazama, nikaitazama midomo yake jinsi inavyo cheza cheza kwa hasira kali.
“Usiteteshe midomo yako K2, je unahitaji na wewe nikubamize?”
“Huyo malaya ndio amekupa nguvu ya kuwa jeuri mbele yangu si ndio?”
Hata kabla sijazungumza chochote Livna akasimama nyuma yangu.
“Malaya mimi au wewe?”
“Wewe ndio malaya, umenisaliti kwa ajili ya huyo msen**”
“Hahahaaa, hivi unajua hichi kikundi ni wapi kilipo tokea au una ropoka?”
 
“Mbwa wewe, ninajipanga nikija ninakutumbua tumbua na hao panya wako”
“Nyooo jaribu uone, wewe mwenyewe unanijua mimi ni nani. Tena usinifanye nikabadilisha mawazo yangu nikakufwata wewe. Bado nina hasira ya vijana wangu wawili ulio watoa sadaka. Yaani laiti ingekuwa si kuijua vizuri Tannia, ningekubamiza kenge wewe”
Livna na K2 wakarushiana maneno ya kike, nikamzuia Livna, akaondoka nyuma yangu huku akiwa amenuna kwa hasira kali.
“K2 unatambua fika kwamba sina woga juu yako kwa maana ninakujua kinaga ubaga. Nina damu ya raisi mmoja mikononi mwangu, sasa hivi sihitaji kukuua ukiwa ni raisi, achia madaraka basi.”
“Siwezi kuachia madaraka kwamwe, si wewe wala si viongozi wa kisiasa wanao nilazimisha mimi kuachia madaraka. Nitahakikisha kwamba ninakuua”
“Na wewe unanitisha, K2 achia madaraka na mkabidhi waziri wako mkuu madaraka ambaye hukuona thamani yake ukahitaji nimuue.”
 
“Kenge wewe tena ngoja”
K2 kwa ishara akamuita mlinzi wake mmoja, akamnong’oneza, kisha mlinzi huyu akaondoka. Tukaka kimya huku tukitazamana na K2,  huku nikisubiria kuona ni nini atafanya. Baada ya muda akaingizwa Lucy aliye chakaa kwa mateso makali. K2 akamshika kichwa Lucy na kukilaza kwa lazima kwenye meza. Akamnyooshea mkono mlinzi wake, akachomoa bastola na kukabidhi, K2 akaiweka bastola hii kwenye sikio la Lucy huku akinitazama kwa macho makali.
“Ninamuua huyu malaya wako uliye mtoa bikra na kukukaribisha nchini kwangu, sasa utajua kwamba nina uwezo wa kukufanya wewe chochote.”
Baada ya K2 kuzungumza maneno hayo, pasipo na huruma akafyatua risasi iliyo ingia sikioni mwa Lucy na kusababisha damu nyingi kusambaa kwenye meza yake jambo lililo nifanya nifumbe macho yangu kwa hasira kali na kujikuta nikijilaumu  ni kwa nini nimemuacha K2 hai kipindi nilipo pata nafasi ya kumuua.
 
ITAENDELEA
‘Haya sasa K2 amemua Lucy mbele ya Dany ambaye kwa sasa anaogopwa Duniani kote hii ni kutokana na watu walio simama nyuma yake wakihakikisha wanamsaidia. Je Dany atamfanya nini K2? Usikose sehemu inayo fwata ya hadi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )