Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, December 12, 2018

Amuua kaka yake kwa mganga wa kienyeji Kisha na Yeye Ajinyonga

adv1
Watu wawili wamefariki dunia Mkoani Morogoro baada ya mtu aliyedaiwa kuwa na ugonjwa wa akili kumuua ndugu yake na kisha yeye mwenyewe kujinyonga walipokuwa kwa mganga wa kienyeji kwaajili ya kupata matibabu.
 
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi wa Polisi Wilbord Mtafungwa amesema kuwa tukio hilo limetokea desemba 1, 2018 baada ya Lucian Kigolo (54) ambaye anamatatizo ya akili kumshambulia kaka yake Gerald Kigolo(60) kwa kumpiga na kitu kizito kichwani.

Aidha Kamanda huyo amesema baada ya kutenda tukio hilo, mtu huyo aliamua kujinyonga kwa kutumia kamba  nyumbani kwa mganga wa kienyeji ambaye ametambulika kwa jina la Luka Paulo (50), ambapo katika tukio hilo Jeshi la Polisi linamshikilia mganga huyo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )