Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, December 13, 2018

Badilisha Simu Yako na TECNO Camon 11 Mpya

TECNO, miongoni mwa kampuni bora za simu ulimwenguni imezindua rasmi TECNO camon 11 ikiwa ni  mwendelezo wa toleo la simu za TECNO camon. 

Simu za TECNO camon zimekuwa zenye ushawishi  mkubwa sana kutokana na uwezo wa kamera na muonekano wake kwa ujumla, na katika uzinduzi huo  TECNO ilitoa tamko rasmi kuhusiana na zoezi la ubadilishaji wa simu za camon kwa camon 11 mpya  ikiwa imeambatana na ofa ya GB 15 kwa miezi mitatu bure kutoka Vodacom Plc. 

Akiwa anazungumza na vyombo vya habari afisa wa mahusiano wa kampuni ya simu ya TECNO Bwana  Eric Mkomoya alisema, “TECNO camon 11 ni simu ya kwanza ya TECNO kuwa na teknolojia ya AI kwenye  kamera za pande zote mbili zenye kubeba pixel 16 mbele na 13+2 nyuma, na kioo chenye notch.  


Na muonekano wa nje wa TECNO camon 11 unaofahamika kama ‘diamond fire design’ unaifanya camon  11 kuwa simu yenye kuvutia zaidi kati ya zote. Na japokuwa ni simu ya kwanza kuzalishwa na kampuni  ya TECNO yenye teknolojia mpya katika kioo inayofahamika kama ‘notch’ lakini bado TECNO  imehakikisha inaongeza mvuto katika simu hiyo kwa umbo jembamba lenye upana wa nchi 6.2HD+ na  uwiano wa 19:9”.
Mteja akibadilisha simu ya camon x kwa camon 11 katika duka la TECNO Smart Hub Kariakoo. 
 
Alimaliza kwa kusema, “zoezi zima la ubadilishaji wa simu za TECNO camon (camon cx, camon cx air,   camon cm, camon x na x pro) linafanyika katika mikoa sita katika maduka ya TECNO yenye promosheni  ambayo ni TECNO exclusive Bus Terminal, TECNO Triple B, TECNO Exclusive CCM Babadi Arusha shop,  TECNO Exclusive China Plaza Smart Hub, TECNO Exclusive Mlimani City Smart Hub, TECNO Exclusive 
Samora Smart Hub, TECNO Exclusive Pablo Dodoma, TECNO Exclusive Mbeya Muna Shop, TECNO  Exclusive Jambo Mwanza Shop na TECNO Exclusive Tabora Shop”. 


Ofa hii ya ubadilishaji wa simu za camon kwa camon 11 litakuhitaji kufika kati ya maduka hapo juu ukiwa  na simu ya TECNO camon na mshiko kidogo ili uweze kupatiwa camon 11 mpya na ofa ya GB 15 kuanzia  sasa hadi tarehe 30 ya mwezi huu wa sikukuu za Christmas. 


Kwa maelezo zaidi tafadhali tembelea kurasa zetu katika mitandao ya kijamii.  


https://web.facebook.com/TECNOMobileTanzania/ 
https://www.instagram.com/tecnomobiletanzania/
https://bit.ly/2rm0qF1
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )