Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, December 27, 2018

Bondia Francis Cheka Afunguka Baada ya Kupewa Kipigo Kizito na Dullah Mbabe

adv1
Bondia Francis Cheka amekubali yaishe kwa Abdallah Pazi (Dullah Mbabe)  baada ya kuchapwa kwa Knock Out raundi ya sita ya pambano lililokuwa la raundi 12 la kuwania ubingwa wa mabara wa WBF kwenye uzani wa super middle.
 
"Sijui kilichotokea,  Nilijikuta tu niko chini raundi ya sita na sikuendelea tena na pambano, " alisema Cheka.
 
Katika pambano hilo lililopigwa kwenye ukumbi wa PTA, Sabasaba mashabiki wa Cheka waliduwazwa na kipigo hicho.
 
"Sina namna zaidi ya kukubaliana na matokeo, Nimepigwa kihalali, sijui nilipatwa na nini kwani sikuwa natembea ulingoni,  Muda mwingi nilicheza kwenye kamba wakati si kawaida Yangu,.
 
Cheka alidai kipigo chake hakijasababishwa na umri au kiwango chake kushuka isipokuwa mpinzani wake alimuotea tu na kushinda.
 
"Hadi sasa sijui nimepotezaje pambano hilo, lakini pamoja na kupoteza siwezi kustaafu ngumi kwa sasa, " alisema.
 
Hata hivyo Dullah Mbabe ametamba kwamba kipigo hicho kwa Cheka si cha kubahatisha alijiandaa kumnyamazisha bondia huyo bingwa wa zamani wa dunia wa WBF.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )