Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, December 18, 2018

Breaking News: Diamond Platnumz, Rayvanyy Wafungiwa Kwa Muda Usiojulikana.....Tamasha la Wasafi Festival Lafutwa

Baraza la Sanaa nchini (Basata) limewafungia  wanamuziki  Diamond Platnumz na Rayvanny  kutojihusisha shughuli za sanaa kwa muda usiojulikana.

Taarifa ya Baraza hilo iliyotolewa leo Desemba 18, imesema limefikia uamuzi huo baada ya wasanii hao kuonyesha dharau kwa mamlaka zinazosimamia shughuli za sanaa nchini, kwa kufanya vitendo vinavyokiuka maadili.

Mbali na kuwafungia wanamuziki hao, Baraza limetangaza kukifuta kibali cha Tamasha la Wasafi Festival linaloendelea nchini.

Wimbo wa Mwanza ambao uliowaingiza matatani ulifungiwa Novemba 12.


Juzi, Basata iliahidi kutoa taarifa rasmi baada ya wasanii hao kuonekana jukwaani katika Tamasha la Wasafi jijini Mwanza wakitumbuiza wimbo huo.
 
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...